Kukutana kwa Mara ya Kwanza
John alikutana nao kwa mara ya kwanza alipokuwa anapita kati kati ya bustani ya mapumziko alipokuwa naelekea nyumbani kwake. Walikuwa ni vijana wawili wa kiume waliokuwa wamevaa suluali nyeusi na mashati meupe, walikuwa wamevaa vijibao vya majina. Walikuwa na hali ya urafiki na walitaka kuzungumza naye kuhusiana na dini yao. John aliwasikiliza na hakuuliza maswali mengi. Walionekana kutokea katika makanisa ya kawaida na walionekana kuongea mambo yale yale aliyoyasikia kanisani. Walisema wao wanatokea katika kanisa la Yesu Kristo la Mitume wa mwisho, ambalo pia linaitwa Momoni.