Kanuni za Kutafsiri Biblia
Kanuni za Kutafsiri Biblia
Audio Course

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Kanuni za Kutafsiri Biblia

Lead Writer: Randall McElwain

Course Description

Kozi hii inafundisha kuhusu kanuni na mbinu za kufasiri Biblia ipasavyo ili kuongoza maisha na uhusiano wetu na Mungu.

Introduction

Kozi hii inatoa utangulizi wa kanuni za msingi za kutafsiri Biblia. Masomo mengi katika kozi hii yana msingi katika Kitabu maarufu, Living by the Book, cha Howard na William Hendricks. Endapo unaweza kukipata kitabu hiki, utaweza kupata mazoezi ili kufanyia kazi kanuni zinazofundishwa katika kozi, vile vile utapata majadiliano zaidi katika kila kanuni. Hata hivyo, kitabu hakihitajiki kwa ajili ya kozi. Nyenzo zote zinazohitajika zimejumuishwa katika masomo haya.

Mwanafunzi anatakiwa kusoma kila Somo kabla ya kuja darasani. Unapaswa kupanga kuwa na dakika 90-120 kwa kila kipindi, Pamoja na muda wa mazoezi nje ya darasa. Kwa sababu kozi hii ina msingi katika mazoezi ya vitendo, unaweza kupenda kugawanya somo katika vipindi zaidi ya kimoja. Hii inaweza kuwapa wanafunzi muda zaidi wa kufanya shughuli.

Masomo yanajumuisha shughuli kadhaa kwa ajili ya kutendea kazi kanuni zinazofundishwa katika somo. Ni muhimu kwamba mwanafunzi achukue muda kufanya shughuli hizi kwa umakini. Shughuli hizi zinatembea katika Maandiko mengi tofauti tofauti. Usikimbilie kumaliza somo. Kwa sababu shughuli nyingi kati ya hizi zitakuwa mpya kwa mwanafunzi, chukua muda darasani ili kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anaelewa namna ya kukamilisha shughuli hizi. Lengo la msingi si kupata jawabu fulani; lengo la msingi ni kukuza stadi katika kujifunza na kutafsiri Biblia.

Mwishoni mwa kozi hii, mwanafunzi atakuwa amesoma vifungu kadhaa vya Maandiko. Kila mwanafunzi atunze nakili zake alizoziandika wakati wa kozi katika daftari lake kwa ajili ya matumizi ya baadae. Kazi zilizofanyika katika kozi hii zitakuwa msaada kwa ajili ya kuandaa ujumbe na somo la Biblia.

Maswali ya majadiliano na shughuli za darasani zimeoneshwa kwa dondoo mshale ►. Kwa habari ya maswali ya majadiliano, wanafunzi wajadili majibu. Jaribu kuhakikisha kwamba wanafunzi wote darasani wanahusika katika majadiliano. Kama itabidi, waite wanafunzi kwa majina yao.

Kila mwanafunzi atafanyia kazi mradi wa kozi katika kipindi chote cha kozi. Baada ya Somo la 10, watawasilisha darasani au watakusanya kazi zao kwa kiongozi wa darasa. Maelekezo kwa ajili ya mawasilisho au kazi yametolewa katika sehemu ya Mazoezi ya Somo la 10.

Mazoezi mengine kadaa pia yamejumuishwa mwishoni mwa Somo la 2 na 7. Wanafunzi wamuoneshe kiongozi wa darasa kazi zilizokamilika lakini watunze nakala ya kazi zao katika shajala zao.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.