Huduma Ya Uongozi
Huduma Ya Uongozi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Huduma Ya Uongozi

Lead Writer: Stephen Gibson

Course Description

Kozi hii inahimiza tabia ya Kikristo wakati inafundisha viongozi kuongoza mashirika kupitia mchakato wa kugundua maadili, kutambua kusudi, kushirikishana maono, kuweka malengo, kupanga mkakati, kuchukua hatua, na kupitia mafanikio.

Introduction

Maelezo ya Kozi

Kozi hii imelengwa mahususi kwa ajili ya viongozi wahudumu wa Kikristo, lakini pia inatumia kanuni ambazo zinatumika kwenye wajibu wowote wa uongozi. Inaonyesha ni kwa nini Imani thabiti ndiyo msingi wa uongozi. Mtu anayetegemewa kuweza kuwa kiongozi atajifunza jinsi ya kuendeleza vipaji vyake na tabia yake na kuongeza ushawishi wake kabla hajaingia rasmi kwenye nafasi ya uongozi. Viongozi watapaswa wajifunze jinsi ya kuongoza mashirika yao kupitia mchakato wa kugundua thamani zilizopo, kutambua makusudi, kushirikishana maono, kuweka malengo, kuchukua hatua, na kutarajia mafanikio.

Maelekezo kwa ajili ya Viongozi wa Madarasa

Kumbukumbu za viongozi wa madarasa zimewekewa katika kozi nzima pamoja na maelekezo kwa ajili ya sehemu maalumu za masomo. Zimeonyeshwa kwa maandishi ya mlalo.

Maswali yanayohitajika kujadiliwa na shughuli za ndani za darasa zimeonyeshwa kwa alama ►. Kwa maswali yanayohitajika kujadiliwa, Kiongozi wa darasa atapaswa kuuliza swali na kuwapa wanafunzi mu(da wa kujadili hilo swali. Kama mwanafunzi huyo huyo kwa kawaida anakuwa mtu wa mwanzo kujibu maswali kwanza, au kama wanafunzi wengine hawapendi kuwajibika katika kujibu maswali, kiongozi anaweza kulielekeza swali moja kwa moja kwa kumlenga mwanafunzi yeyote: “Petro, unawezaje kujibu swali hili?”

Maandiko mengi yametumika katika kozi hii. Vifungu ambavyo vinapaswa visomwe kwa sauti katika darasa vimeonyeshwa kwa vichwa vya mishale. Wakati mwingine, marejeo ya maandiko yamekuwa kwenye kifungu kwa kutumia alama za mabano. Kwa mfano: (1 Wakorintho 12:15). Alama hizo ni kwa ajili ya kuunga mkono taarifa iliyoko kwenye kifungu husika. Hakuna ulazima wa kusoma aya zilizoko kwenye alama za mabano.

Mara chache kutakuwepo na mchoro wa umbo wenye kuwa na nukuu kutoka kwa baadhi ya viongozi katika historia. Wakati darasa litakapofika kwenye mchoro wa umbo lenye nukuu, kiongozi wa darasa anaweza akamtaka mwanafunzi kusoma na kuelezea hiyo nukuu. Kimsingi hatulazimiki kukubaliana na kila kitu ambacho viongozi hawa walifanya na kufundisha, lakini tunaweza kujifunza kutokana na mifano yao.

Kila somo linamalizika kwa kazi za kufanya. Kazi za kufanya zinapaswa zikamilishwe na ziwakilishwe kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa. Kama mwanafunzi hatakamilisha kazi ya kufanya iliyotolewa, anaweza akaendelea kuifanya baadaye. Hata hivyo, kiongozi anapaswa awatie wanafunzi moyo wa kuwa kwenye ratiba ili kwamba waweze kujifunza mambo mengi zaidi kutoka darasani. Kazi ya kufanya ya 3 ya kila somo inahusiana na kukariri baadhi ya pointi maalumu kutoka katika somo.

Kwenye mwanzo wa kila kipindi cha darasa mwalimu wa darasa atakusanya kazi zote zilizoandikwa za kipindi kilichopita. Kiongozi anaweza akachagua baadhi ya aya zilizoandikwa kwa ajili ya Kazi za kufanya ya 1 kwa majadiliano katika darasa. Pia mwanzoni mwa kila kipindi cha darasa, kila mwanafunzi atapaswa aandike yaliyomo kwenye kazi ya kufanya ya 3 ya somo lililopita kutoka kichwani bila kunukuu popote. Baada ya hapo darasa litapaswa kujadili kwa kifupi hizi taarifa za kukaririwa zilizoandikwa ili kuhakikisha kwamba kila mmoja anaelewa umuhimu wake.

Kama mwanafunzi atahitaji kupata cheti cha kufuzu mafunzo kutoka Shepherds Global Classroom, atapaswa ahudhurie vipindi vyote vya darasa na amalize kufanya kazi zote zilizotolewa. Fomu imetolewa mwisho wa kozi hii kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi za kufanya zilizomalizika.

Mojawapo ya kusudi kubwa la kozi hii ni kuwaanda wanafunzi waweze kuwa waalimu. Kiongozi wa darasa anapaswa kuwapa wanafunzi nafasi ya kuinua viwango vyao vya kufundisha. Kwa mfano, kiongozi wa darasa mara kwa mara atapaswa kumpa mwanafunzi nafasi ya kufundisha sehemu fupi ya somo katika darasa.

Mahubiri yaitwayo “Ubunifu wa Maono” yanafuata baada ya somo la 17. Mahubiri haya yanayohusiana na uongozi yanaweza kutumika wakati wowote kwa kipindi chote cha kozi na yanapatikana kwa ajili kuhubiri katika makanisa au kufundishia kwenye timu za uongozi.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.