Kukutana kwa mara ya kwanza
Ethan alikuwa katika dini ya Romani Katoliki, lakini aliacha kuenda kanisani alipokuwa mtu mzima. Aliishi kwa starehe kwa miaka mingi, lakini alianza kuhisi kuwa anahitaji kujua kusudi la maisha yake haraka. Rafiki yake alimfundisha kutumia dawa za kulevya, na Ethan alihisi kuwa amepata taswira mpya ya ulimwengu na yeye mwenyewe. Alianza pia kusikia sauti zikimpatia muelekeo.