Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Kuishi Kikristo Kwa Vitendo
Course Description
Kozi hii hutumia kanuni za kiroho kwa utumiaji wa fedha, mahusiano, mazingira, mahusiano na serikali, haki za binadamu, na maeneo mengine ya kuishi kwa vitendo.
Introduction
Kama mkisoma kwa kikundi, mnaweza kubadilishana kusoma somo. Mnapaswa kusimama mara kwa mara kwa ajili ya mjadala wa darasa. Kiongozi wa darasa ana jukumu la kuhakikisha mjadala haupotei mbali na somo linalojadiliwa. Ni vizuri kuweka muda wa mjadala kwa kila sehemu.
Maswali ya majadiliano na shughuli za darasani zimeoneshwa kwa alama ya mshale ►. Kwa maswali ya mjadala, kiongozi wa darasa atauliza swali na kuwapa wanafunzi muda wa kujadili jibu. Ikiwa mwanafunzi mmoja kila mara anajibu kwanza au baadhi ya wanafunzi wanakaa kimya, kiongozi anaweza kuelekeza swali kwa mwanafunzi fulani.
Maandiko mengi yametumika katika kozi hii. Vipengele vya maandiko vinavyopaswa kusomwa kwa sauti darasani vitaoneshwa kwa alama ya mshale ►. Mwanafunzi mmoja ataombwa asome kwa niaba ya kikundi. Wakati mwingine, maandiko huandikwa katika mabano—for example: (1 Wakorintho 12:15). Nukuu hizo zinaunga mkono maelezo katika somo. Sio lazima kila wakati kusoma vifungu vilivyoandikwa ndani ya mabano.
Kila somo lina mazoezi yaliyoelezewa mwishoni. Mazoezi yanapaswa kukamilishwa baada ya somo na kuripotiwa kwa kiongozi wa darasa wakati wa somo linalofuata. Kama mwanafunzi hatamaliza mazoezi kwa wakati, anaweza kuyakamilisha baadae. Hata hivyo, kiongozi wa darasa anapaswa kuwasihi wanafunzi kufuata ratiba ili wajifunze mambo mengi zaidi darasani. Chati imewekwa mwishoni mwa somo kwa ajili ya kuweka rekodi ya mazoezi ambayo mwanafunzi amekamilisha.
Moja ya malengo ya somo hili ni kuwaandaa wanafunzi kuwa waalimu. Kiongozi wa darasa anapaswa kuwapa wanafunzi nafasi ya kukuza ujuzi wao wa kufundisha. Kwa mfano, kiongozi anaweza mara kwa mara kumpa mwanafunzi nafasi ya kufundisha sehemu ndogo ya somo kwa darasa.
Mwisho wa kila somo kuna sehemu inayoelekeza juu ya kushirikiana katika kikundi. Kiongozi wa darasa ataamua muda gani utumike kwa ajili ya mjadala huo. Masomo mengi yatakuwa na muda wa kutosha wa mjadala mnapoendelea kujifunza kitabu hiki.
Pia mwisho wa kila somo kuna sala fupi ya kumuomba Mungu kuwasaidia wanafunzi kuishi kweli walizojifunza. Kiongozi wa darasa anaweza kumuomba mwanafunzi mmoja asome sala hiyo kwa niaba ya darasa.
Ikiwa mwanafunzi anataka kupata cheti kutoka Shepherds Global Classroom, anapaswa kuhudhuria masomo na kukamilisha mazoezi. Fomu imewekwa mwisho wa somo kwa ajili ya kurekodi mazoezi aliyokamilisha.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.