Kukutana kwa Mara ya Kwanza
[1]Mark alikuwa Mromani Katoliki na aliwahi kuwa padre lakini aliacha upadre. Siku moja alikuwa anaaza kazi mpya. Wakati mtu yule alipokuwa namuonesha namna ya kufanya kazi, Mark aligundua kwamba alikuwa mafuasi wa Iglesia ni Cristo. Mark akasema, “Mimi namshikilia Yesu; Yeye ni Mungu wangu.” Yule mtu akamwambia kwamba Yesu sio Mungu, na kwamba mchungaji wake anaweza kuthibitisha kutoka katika Biblia kwamba Yesu alikuwa mpatanishi tu. walimuonesha Mark maandiko mengi, na akachanganyikiwa. Walimshawishi kwamba Yesu sio Mungu.
“Katika moyo wa Imani ya Kikristo ni tangazo kwamba Bwana wetu Yesu Kristo, mwana wa Mungu wa milele, alifanyika mwili kwa ajili ya wokovu wetu.”
- Willard Taylor
God, Man, and Salvation
