Utangulizi
► Kwanini migogoro ya kidini inatokea? Je migogoro ya kidini ni ya lazima, au inaweza kuepukika?
► Baada ya majadiliano mafupi kuhusu maswali haya, darasa litapaswa kutazama maandiko rejea yafuatayo: 1 Timotheo 3:15, Yuda 1:3; Mathayo 16:6, 12; Tito 1:9; na 1 Petro 3:15. Jadili kwa ufupi ni nini maandiko haya yana ashiria nini katika migogoro ya kidini.
Yesu alimwambia mwanamke msamaria kisimani kwamba tatizo la kuabudu kwa wasamaria lilikuwa kwamba hawakujua nani wanayemwabudu (Yohana 4:22). Ufahamu wa mwanadamu kwa Mungu ni sifa ya muhimu sana na hakika ndiyo msingi wa dini zake zote. Hakuna kosa lingine lililo dhahiri kuliko kutokuwa sahihi juu ya namna Mungu alivyo.
Inawezekana kabisa kumwabudu pasipo kuamini kitu chochote kuhusu Yeye. Kama mtu anaufahamu usio sahihi kuhusu Mungu, ataheshimu sifa ambazo Mungu hana na atashindwa kuheshimu sifa ambazo Mungu yuko nazo. Tabia binafsi za Mwenye kuabudu zitabadilika kuendana na tabia ambazo yeye anafikiri kwamba Mungu anazo.
Mtu hawezi kuweka Imani yake kwa Yesu kwa ajili ya wokovu pasipo kuamini kuamini kitu kuhusu Yesu. Kama mtu ataamini vitu visivyo sahihi kuhusu Yesu, akawa na fundisho lisilounga mkono Injili. Anaweza akaamini Injili ya uongo ambayo haiwezi kumwokoa yeye.
Kanisa lina wajibu wa kusimamia kweli. Mtume Paulo amesema kwamba kanisa ni nguzo na msingi wa kweli (1 Timotheo 3:15). Ili kusimamia kweli, Kanisa lina wajibu wa kuuelezea na kuutetea. Mtume Yuda anatuambia sisi kwamba wakati watu wanafundisha mafundisho potofu, sisi tunapaswa tu “mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu” (Yuda 1:3).
Fundisho potofu ni kama ugonjwa ambao unasambaza madhara yake (2 Timotheo 2:17). Fundisho potofu linafananishwa na chachu, ambayo hatua kwa hatua inaathiri donge la mkate (Mathayo 16:6).
Mungu anawaita wachungaji kuwa viongozi katika kutetea kweli. Paulo alimwambia Tito kwamba mchungaji anatakiwa kufundisha Neno kama lilivyofundishwa na pia kuwakemea wale wanaolipinga (Tito 1:9). Na pia akasema kwamba kwa sababu ya wapotoshaji, jumuiya nzima iliondolewa kutoka kwenye kweli (Tito 1:10-11).
Kozi hii sio kuhusu mafundisho ambayo yanagawa makanisa tofauti ya Kikristo kwenye makundi kama vile Wamethodist, Wabaptisti, au wapentekoste. Makanisa haya kiujumla yanakubali juu ya mafundisho muhimu ya kibiblia yaliyomo ndani ya Kijitabu cha Mkononi cha Fundisho nyuma ya Kozi hii. Badala yake, Kozi hii inatazama katika makundi ya kidini ambayo yanakana mafundisho ambayo ni msingi wa Imani ya Kikristo.
Katika somo hili tutajifunza njia nane muhimu ambazo wakristo wanapaswa kujiandaa kwazo kwa ajili ya kukabiliana na migogoro ya kidini.
Ni lazima wawe na:
1. Uzoefu binafsi katika Wokovu.
2. Kuwa imara katika fundisho la Kibiblia.
3. Kufahamu hatari ya makosa.
4. Kufahamu washirika wa Imani potofu.
5. Kufahamu asili ya dini za uongo.
6. Shirikisha Injili.
7. Kulionesha Kanisa kwa kielelezo.
8. Kutegemea Roho Mtakatifu.