Utangulizi wa ibada ya Kikristo
Utangulizi wa ibada ya Kikristo
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Utangulizi wa ibada ya Kikristo

Author: Randall McElwain

Course Description

Kozi hii inaelezea jinsi gani kuabudu huathiri nyanja zote za maisha ya muumini na hutoa kanuni ambazo humuongoza mtu binafsi na mkutano wote mazoezi ya kuabudu.

Introduction

Kozi hii inatambulisha kanuni za kuabudu.

Kama mnasoma kama kikundi, msome kwa kuachiana. Mnapaswa muwe mnasimama kwa muda ili mpate kujadiliana. Wewe kama kiongozi wa darasa, unawajibika kutunza mjadala usihame kwenye mada ya kujifunza. Ni vizuri kutunza muda kwa kila kipindi cha mjadala.

Maswali ya mjadala na mazoezi ya darasani yanaoneshwa kwa mshale ► .

Kila unapofikia swali, waruhusu wanafunzi kujadili jibu. Jaribu kuhakikisha kwamba wanafunzi wote katika darasa wanashiriki katika mjadala. Kama ni lazima, unaweza kuwaita wanafunzi kwa majina.

Katika kipindi chote cha somo, kuna mazoezi ya darasani na kazi za nyumbani zinazohusisha kutafuta nyimbo za tenzi na korasi zinazokidhi vigezo maalum. Lengo la mazoezi haya ni kukuandaa uweze kuchagua nyimbo za ibada kwa ajili ya ibada unazoongoza.

Ikiwa kuna vitabu vya tenzi vilivyochapishwa kwa lugha yako, unaweza kuvitumia. Tovuti ya https://worshipleaderapp.com/ na programu ya simu inayoitwa “Worship Leader” zinatoa nyimbo za Kikristo kwa lugha mbalimbali. Unaweza pia kuangalia kwenye tovuti nyingine zinazochapisha maneno ya nyimbo za ibada yaliyoandikwa kwa lugha yako.

Maandiko mengi yametumika katika kozi hii. Vifungu ambavyo vitasomwa darasani pia vimeoneshwa kwa alama ya mshale ► . Tafadhali wanafunzi waitazame mistari hii na kuchukua kumbu kumbu halafu wasome katika mzunguko wa kikundi.

Kila somo linaishia na mazoezi. Mazoezi yanapaswa kukamilika na kuwasilishwa kabla ya somo jingine.

Kila somo lina mtihani, na sehemu ya mtihani ni kukariri maandiko ya Biblia. Kwa kila mwisho wa kipindi, kiongozi anaweza kurudia maswali haya pamoja na wanafunzi. Darasa linalofuata linapaswa kuanza na jaribio katika maswali haya. Mjaribio yanapaswa kufanyika bila kuangalia kitabu, kumbu kumbu zilizoandikwa, Biblia, au wanafunzi kuulizana. Majibu ya zoezi yapo kwa kiongozi kupakua kutoka Shepherds Global Classroom.

Katika Somo la 1, wanafunzi wanapangiwa mradi wa siku 30. Baada ya mradi huu kukamilika, kila mwanafunzi anapaswa kuwasilisha ripoti ya ukurasa mmoja ikifupisha walichojifunza kutokana na mradi huo. Wanafunzi hawatawasilisha taarifa nzima ya mradi.

Ikiwa mwanafunzi anataka kupata cheti kutoka Shepherds Global Classroom, anapaswa kuhudhuria vipindi vya darasa na kukamilisha mazoezi yanayotolewa. Fomu inatolewa mwishoni mwa kozi kwa ajili ya kurekodi mazoezi yaliyokamilishwa.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.