Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Familia ya Kikristo
Course Description
Kozi hii inatoa mtazamo wa Kikristo kuhusiana na maendeleo ya binadamu kupitia hatua mbalimbali za maisha na zinatumia kanuni za kimaandiko kwa ajili ya majukumu ya kifamilia na mahusiano.
Introduction
Ufafanuzi kuhusiana na Kozi
Kozi hii inafundisha kanuni za Mungu kwa ajili ya hatua mbalimbali za kimaisha na mahusiano ya kifamilia, hasa ndoa na ukuzaji wa watoto. Kupitia mafundisho haya, wanafunzi watakuwa wamewezeshwa katika kumheshimu Mungu katika hatua yao ya sasa ya maisha na katika mahusiano yao. Watakuwa tayari kufundisha wengine kuhusu kanuni za kibiblia na jinsi ya kuwa na matumizi ya kanuni hizo. Wanafunzi watakuwa wamehamasishwa kujihusisha na kanisa lao katika kuleta mguso wa utauwa kwenye familia zilizoko kwenye ushirika wao na jamii zao.
Pamoja na mambo mengine, wanafunzi watakuwa wanajifunza kuhusu kufanya uanafunzi kwa watoto na vijana katika familia. Somo la 12, na Kazi ya kufanya ya 3 inatoa maelekezo kwa wazazi ambao wanachukua kozi hii kuwa na mpangilio wa kila siku wa kuwa na nyakati za kufanya ibada kwa ajili ya familia zao. Shepherds Global Classroom wametoa kitabu cha kufanya uanafunzi kwa familia, kiitwacho Zana za Mafundisho kwa Familia ambacho wazazi watapenda kukitumia wakati wa ibada zao za kuabudu. Kitabu hiki kiko tayari kwa ajili ya kupakuliwa kutoka shepherdsglobal.org.
Maelekezo kwa Viongozi wa Madarasa
Maswali ya kujadiliana na shughuli za ndani ya darasa zinaonyeshwa kwa alama ya ►. Kwa ajili ya maswali ya kujadiliana, kiongozi wa darasa atapaswa kuuliza swali na kuruhusu wanafunzi kujibu. Siyo lazima kwamba swali lijibiwe kwa usahihi sana wakati wa majadiliano. Mafundisho yaliyoko kwenye somo yatajibu swali hilo. Kama mwanafunzi mmoja ndiye kwa kawaida huwa anaanza kujibu kwanza, na wanafunzi wengine huwa hawajibu, kiongozi anaweza akaelekeza swali kwa mmoja wao: “Igor, ni kwa jinsi gani utaweza kujibu swali hili?”
Kila somo linamalizika kwa kuwepo na maswali mbadala ya hiari kwa ajili ya majadiliano ya kikundi. Kiongozi wa darasa anaweza akachagua ni swali gani linaloweza kujadiliwa na kikundi.
Maandiko mengi yametumiwa katika kozi hii. Vifungu ambavyo vinapaswa visomwe kwa nguvu katika darasa vinaonyeshwa kwa njia ya alama za mchoro za mshale. Kila mtu katika kikundi atapaswa alitizame andiko, wakati mwanafunzi mwingine akiwa analisoma kwa sauti. Wakati mwingine, marejeo ya Maandiko hutolewa kwenye mabano katika kifungu hicho. Kwa mfano: (Waefeso 6:1). Marejeo hayo ni kwa ajili ya kuunga mkono taarifa zilizoko kwenye maandishio. Sio lazima kusoma vifungu vilivyoko kwenye mabano kila wakati.
Majadiliano mafupi kuhusiana na mada mbili maalumu yanajumuishwa mwishoni mwa kozi hii. Mada hizi hazina uhusiano kabisa na masomo mengine yeyote na siyo masomo kamili yaliyokamilika yenyewe. Hata hivyo, ni mada muhimu kuzielewa kutokana na mtazamo wa Kikristo. Darasa linapaswa kujifunza na kujadili Kiambatanisho A kinachofuata Somo la 3 na linapaswa pia kujifunza Kiambatanisho B kufuatia Somo la 10. Mambo ya kukumbuka yametolewa mwishoni mwa masomo hayo mawili.
Kila somo linamalizikia na kazi za kufanya. Kazi za kufanya zinapaswa zimalizike na kuwakilishwa kabla ya muda wa kuanza somo linalofuata. Kama mwanafunzi hatakamilisha kazi ya kufanya, anaweza akaifanya kwa wakati mwingine. Hata hivyo, kiongozi atapaswa kuwahamasisha wanafunzi kutunza na kuendana na wakati ili waweze kujifunza zaidi kutoka darasani. Pamoja na kukamilisha kazi za kufanya kwa kila somo, wanafunzi watapaswa wasome somo linalofuata kwa ajili ya maandalizi ya darasa litakalofuata.
Kama mwanafunzi atahitaji kupata cheti cha kufuzu mafunzo kutoka Shepherds Global Classroom, atapaswa ahudhurie vipindi vyote vya darasa na amalize kufanya kazi zote zilizotolewa. Fomu imetolewa mwisho wa kozi hii kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi za kufanya zilizomalizika.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.