Mafundisho na mazoezi ya maisha Matakatifu
Mafundisho na mazoezi ya maisha Matakatifu
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Mafundisho na mazoezi ya maisha Matakatifu

Lead Writer: Randall McElwain

Course Description

Kozi hii inatoa maelezo ya kibiblia ya maisha matakatifu ambayo Mungu anatarajia na uwezesho kwa Mkristo. 

Introduction

Maelezo na maelekezo kwa viongozi wa madarasa.

Kozi hii inapima Imani na uzoefu wa maisha ya utakatifu.  Unapaswa uratibu dakika 90-120 kwa kila kikao cha darasa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi wanazopewa nje ya darasa.

Alama ► inaashiria swali linalopaswa kujadiliwa. Wakati wowote unapokuja katika hayo, uliza hayo maswali yanayokuja mbele yake, na uwaachie wanafunzi wajadili jibu lake. Jitahidi kuhakikisha kwamba wanafunzi wote darasani wanahusika katika majadiliano. Ikiwa ni lazima, waite wanafunzi kwa majina yao.

Kila tanbihi chini ya ukurasa inarejea andiko la Biblia.  Kama aya haijatolewa au hazijatolewa kutoka kwenye fungu, tafadhali wafanye wanafunzi waziangalie na wazisome wakati wa kipindi darasani. Labda iwe imeelekezwa vinginevyo, nukuu ya maandiko yanatoka katika Biblia ya English Standard Version (ESV).

Kila somo litakuwa na kazi za kufanya mbili:

(1) Insha fupi ya mada maalumu itakayotolewa. Kwa utashi wa kiongozi wa darasa, insha hii inaweza kuwa ni ya kuandikwa au inayoweza kuwakilishwa kwa mdomo.     

(2) Kazi ya kukariri maandiko. Haya yatakuwa yanapitiwa katika kila kipindi darasani. Itakapofikia mwisho wa kozi, wanafunzi watatakiwa wawe wamenukuu aya zote ziizokaririwa kwa kipindi chote cha kozi.

Kusudio mojawapo la kozi hii ni kuwaandaa wanafunzi kuwa waalimu. Kiongozi wa darasa anapaswa awape wanafunzi nafasi za kukuza vipawa vyao vya ufundishaji. Kwa mfano, kiongozi wa darasa mara moja moja anapaswa ampe mwanafunzi nafasi ya kufundisha sehemu fupi ya somo darasani.                       

Kila mwanafunzi ataandaa mpango kazi wa mwisho wa somo. Mpango kazi huu utahusisha mahubiri au masomo matatu kuhusiana na maisha ya utakatifu. Haya yanaweza kuelekezwa aidha kwenye uhalisia wa kibiblia au wa vitendo halisi vya maisha ya utakatifu. Ikiwezekana, kila mwanafunzi atapaswa kuwakilisha kila hubiri au somo alilolifanya na kuweka kumbukumbu kwa ajili ya kiongozi wa darasa.    

Kama mwanafunzi atataka apewe cheti cha kuhitimu Shepherds Global Classroom, ni lazima ahudhurie vipindi vyote na akamilishe kazi zote za kufanya. Fomu itatolewa kila mwisho wa kozi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi zote zilizomalizika.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.