Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Kitabu Cha Taasisi Za Wenyeji
Course Description
Kimsingi kitabu hiki ni mwongozo rejea wa wakufunzi, wasimamizi, na walimu wenyeji.
Introduction
Kimsingi kitabu hiki ni mwongozo rejea wa wakufunzi, wasimamizi, na walimu wenyeji. Kwa wakati mwinigine wakufunzi wanaweza kukitumia kitabu hiki, kufunzia walimu na wasimamizi katika taasisi za wenyeji. Pia kwa wakati mwingine, sehemu fulani ya somo yaweza kutumika kufunzia mada husika au kutambulisha Shepherds Global Classroom (SGC).
Kitabu chote kinaweza kufundishwa kwa muda kama wa masaa sita katika kipindi cha mafunzo. Mara kwa mara wakufunzi wanapaswa kutoa nafasi ya mijadala darasani.
Washiriki wa mafunzo wanahitajika kuwa na Biblia, na daftari la kuandika, na kupata nakala ya kitabu hiki.
Wakufunzi wanapaswa kuja na vitabu mbalimbali vya masomo ya Shepherds Global Classroom kwa ajili ya wanafunzi kuyatathmini. Darasa linahitaji ngalau nakala tatu za vitabu vya masomo tofauti ili washiriki waweze kufanya mazoezi ya kufundishana katika vikundi vya watu watatu watatu.
Wakufunzi wakimaliza kufundisha hadi Sura ya 6, washiriki wanapaswa kuangalia vitabu vya masomo ya SGC. Wanapaswa kuangalia mwelekeo wa masomo hayo ulioko mwanzoni mwa kila kitabu cha somo. Washiriki wanapaswa kujadiliana kuhusu mwelekeo na kuhakikisha wanaelewa.
Mifano na mazoezi ni muhimu kwa mafunzo. Mkufunzi anaweza kuonyesha mfano wa jinsi ya kufundisha kwa kufundisha masomo matatu katika vitabu vya masomo. Mfano utakuwa mzuri endapo kila somo litatoka katika kitabu tofauti cha somo. Kama kuna mkufunzi zaidi ya moja au baadhi ya washiriki wenye uelewa, wanaweza kufundisha baadhi ya masomo ili kuonyesha mitindo mbali mbali.
Baada ya kuangalia mfano, mshiriki wa masomo haya anahitaji kufanya mazoezi ya kufundisha kwa vitendo.
Kwa kiwango cha chini mazoezi yanaweza kupangwa hivi: Wagawe washiriki katika vikundi vya watu watatu. Kila mshiriki katika kikundi atafundisha somo kwa wenzake wawili kwa muda usiopungua dakika 30. Kila moja wa washiriki wote watatu watafanya mazoezi na kuangalia ufundishaji wa wenzake wawili katika kipindi cha dakika 90.
Namna nzuri ni kuwa na siku ya mafunzo ya ziada iliyotengwa kwa ajili ya mazoezi ya vitendo vya washiriki kukiwa na mrejesho kutoka mkufunzi na washiriki wengine. Siku ya mazoezi haya inaweza kupangwa siku ya mwisho. Washiriki wanaweza kupata muda wa ziada ili wajitayarishe.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.