Kukutana kwa Mara ya Kwanza
Lydia alishangaa kuona watu wengi mtaani wanaenda kanisani siku ya Jumamosi. Aliwauliza majirani zake kuhusiana na hili, na wakamwambia kwamba Jumamosi ndio siku sahihi ya kuabudu. Walimuelezea kwamba Jumamosi hawafanyi biashara au hawanunui au hawafanyi yale ya kujifurahisha sana. Lydia alifikiri kwamba lazima walikuwa na dini tofauti na makanisa mengine, lakini walionekana kuamini mambo yale yale kuhusu Mung una wokovu.
