Kukutana kwa Mara ya Kwanza
Kwa Kadiri Jonathan alipokuwa anaufahamu Uorthodoxy wa Mashariki, alivutiwa na namna ambavyo wamekuwa wakivumilia mateso kutoka kwa Waislamu na Wakomunisti katika nchi nyingi. Mashujaa wao sio wachungaji wa makanisa makubwa au viongozi wa muziki. Mashujaa wao ni wafia Imani. Jonathan alifikiri kwamba endapo mateso yanatakuwa makubwa kila mahali, waamini wa Uorthodoxy wa Mashariki ndio watakao vumilia.
