Type at least 2 characters to search
No results found for ""
Courses
Lessons
Sections
navigate open
See all results →
Tamaduni za Imani za Ulimwengu

Tamaduni za Imani za Ulimwengu

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Tamaduni za Imani za Ulimwengu

Lead Writer: Stephen Gibson

Course Description

Kozi hii inaelezea Imani za msingi na historia ya Imani potofu na tamaduni za dini 17 zilizochaguliwa, ikizilinganisha na Ukristo wa kihistoria wa Kiprotestanti na kutathmini mafundisho yao na matendo yao kupitia Biblia. Mwanafunzi ataandaliwa ili kujibu upotovu wa dini zisizo sahihi na kumlinda Mkristo kutokana na uongo au upotofu.

Introduction

Imani Potofu Ambazo Zinajifananisha na Ukristo

Dini Zisizo za Kikristo

Tamaduni Tofauti za Kikristo

Umomoni

Uhindu

Usabato

Mashahidi wa Yehova

Ubudha

Uromani Katoliki

Iglesia ni Cristo (Inglesia ni Kristo/Kanisa la Kristo)

Utao

Uorthodoxy wa Mashariki

Eastern Lightning (Mwangaza wa Mashariki)

Uislamu

Theolojia ya Mafanikio

Imani potofu ya Kiapokaliptiki

Uyudaizimu

 

 

Dini ya New Age

 

 

Dini za Asili

 

 

Voodoo

 

 

Maelezo na Mwongozo kwa ajili ya Kiongozi wa Darasa

Wakati ambapo Maandiko yameandikwa katika mabano au ndani ya andiko kuu, darasa linatakiwa kusoma maandiko hayo kabla ya kuendelea.

Masomo kuhusiana na makundi ya kidini (Somo la 3 – 19) kwa ujumla yanafuata mpangilio ulioelezewa katika mwongozo ufuatao. Masomo mawili ya kwanza ni juu ya mada maalumu.

Mwongozo huu unaelezea namna ambavyo darasa linaweza kufundishwa kwa kiwango cha juu kabisa cha ubora. Kiongozi wa darasa ni lazima atunze kiwango hiki kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatamani kupata cheti kutoka Shepherds Global Classroom. Kwa makundi mengine ambayo hayataweza kufikia mahitaji haya, mwalimu anaweza kuweka mahitaji ambayo yako ndani ya uwezo wao, na kuwapatia vyeti tofauti.

Tunatarajia kwamba kila somo linachukua masaa mawili ili kulimaliza kikamilifu. Endapo kundi linakutana kwa kipindi kifupi, somo linaweza kugawanywa katika mikutano miwili.

Mpangilio wa Shughuli za Kundi

(1) Ripoti ya Mjadala kuhusu Injili (Muda Unaokadiriwa: Dakika 20, endapo kuna ripoti kadhaa)

Wanafunzi ambao wamemaliza zoezi la mazungumzo kutoka somo la nyuma wanatakiwa kutoa taarifa. Wanachopaswa kufanya tu ni kuelezea Habari ya mazungumzo yao. Wanafunzi wengine wanaweza kutoa maoni yao kwa ajili ya matumizi ya mbeleni. Usiwaruhusu wanafunzi kumkosoa kupita kiasi mwanafunzi anayetoa taarifa.

(2) Muda wa Marudio Drasani (Muda Unaokadiriwa: Dakika 5-10)

Kiongozi wa darasa anatakiwa kuuliza maswali ya rejea kwa ajili ya somo lililopita, kisha maswali machache ya rejea kutoka katika masomo ambayo yameshasomwa tayari. Kusudi la hii ni kumsaidia mwanafunzi kuwa na kumbukumbu ya muda mrefu na kurekebisha kutoelewa kwa namna yeyote ambako wanaweza kuwa nako. Maswali ya rejea yanawasaidia kukumbuka taarifa za muhimu zaidi. Mwezeshaji anaweza kulifanya somo kuwa lenye ufanisi kwa kutumia maswali ya rejea. Maswali ya rejea yanapatikana mwishoni mwa kozi hii.

(3) Kukutana kwa Mara ya Kwanza

Mtu mmoja asome kifungu cha maneno chenye kichwa “Kukutana kwa Mara ya Kwanza.” Hili linatakiwa lifanyike pasipo kuchangia lolote wala majadiliano. Habari mara nyingi hazina hitimisho ili kutengeneza hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusiana na kundi linalosomwa. Katika hali chache, ushuhuda mwishoni mwa somo ni kuhusiana na mtu yule yule ambaye ametajwa katika Kukutana kwa Mara ya Kwanza.

(4) Kujifunza Andiko – Sehemu ya 1 (Muda Unaokadiriwa: Dakika 15)

Someni kifungu kilichoelekezwa kwa Pamoja kwa sauti. Wanafunzi kadhaa wanaweza kupokezana kusoma mistari. Kisha muwe na dakika chache za ukimya kwa ajili ya wanafunzi kuandika kifungu cha maneno cha ufupisho na kuorodhesha maelezo (maelekezo mahususi yanapatikana katika kila somo). Baada ya kuandika, waache wanafunzi kadhaa wasome kile walichokiandika ili kwamba kila mmoja ajifunze kutoka kwa mwingine.

(5) Kujifunza Kundi la Dini ((Muda Unaokadiriwa: Dakika 40)

Jifunze taarifa zilizotolewa kuhusiana na kundi la dini. Kiongozi au mtu mwingine katika kundi anaweza kusoma na kuelezea nyenzo kwa kundi. Wanafunzi tofauti wanaweza kusoma na kuelezea nukuu katika mstari wa pambizo.

Maswali ya Majadiliano na mazoezi ya ndani ya darasa yameoneshwa kwa alama ►. Kiongozi wa darasa anatakiwa kuuliza swali na kuwapa wanafunzi muda wa kujibu. Kadhaa yatakuwepo katika kila somo.

Maandishi Yaliyokolezwa na yenye mwandiko uliolala yanapinga au yanakanusha mafundisho na desturi zisizo sahihi za kundi la kidini. Baada ya kusoma ukweli kuhusiana na kundi la dini, rudi nyuma na kusoma tena maelezo na andiko lililotolewa.

(6) Tumia Kijitabu cha Mkononi cha Fundisho (Muda Unaokadiriwa: Dakika 20)

Kijitabu cha Mkononi cha Fundisho ni sehemu ya nyenzo katika kozi hii ambayo imeandikwa baada ya masomo. Kwa wakati huu katika somo, tazama mada katika Kijitabu cha Mkononi cha Fundisho zilizoorodheshwa chini ya sehemu hii. Wanafunzi wasome maandiko pamoja na kuhakikisha wameelewa namna ambavyo mistari inathibitisha dondoo. Kila mwanafunzi anapaswa aoneshe kwamba anaweza kuthibitisha dondoo kutoka katika maandiko. Baadhi ya dondoo zinatumika katika masomo kadhaa. Sio lazima kurudia kitendo kile kile katika dondoo ile ile endapo mwanafunzi anajifunza vizuri.

(7) Uinjilisti (Muda Unaokadiriwa: Dakika 10)

Sehemu hii inatoa baadhi ya mambo ya kivitendo ya kukumbuka wakati tunaongea kuhusiana na kundi mahususi la dini. Katika baadhi ya masomo sehemu hii imeunganishwa pamoja na sehemu “Tumia Kijitabu cha Mkononi cha Fundisho

(8) Ushuhuda

Mtu mmoja asome sehemu ya nyenzo yenye kichwa “Ushuhuda.” Shuhuda ni matukio halisi, ingawaje wakati mwingine majina yamebadilishwa.

(9) Kujifunza Andiko – Sehemu ya 2 (Muda Unaokadiriwa: Dakika 20)

Mwishoni mwa kipindi cha kujifunza, soma tena kifungu cha Andiko kilichotolewa. Subiri kwa dakika chache ili kila mwanafunzi aandike kifungu cha maneno kinachoelezea ujumbe ambao kifungu kinatoa kwa ajili ya mshirika wa kundi la dini linalofundishwa. Waruhusu wanafunzi wachache washirikishe kile walichokiandika.

(10) Zoezi

Kila wakati hitimisha muda wa somo kwa kuwakumbusha wanafunzi kutengeneza ratiba ya fursa ya kuwasilisha injili. Wanafunzi wanatakiwa kuwa na mazungumzo na washirika wa dini ambazo zinasomwa, kama inawezekana. Wanatakiwa kujaribu kuwasilisha injili na kweli nyingine za kikristo. Kama haiwezekani kwa wao kuwapata washirika wa kundi la dini mahususi, wanapaswa kumtafuta mtu mwingine ambaye yuko tayari kusikiliza maudhui au mada ya injili. Wanapaswa kuelezea imni ya msingi ya dini, kisha watoe mwitikio wa kibiblia. Wanatakiwa kujiandaa ili kuliamdia darasa kuhusiana na mazungumzo yao.

Kila mwanafunzi anatakiwa kutoa taarifa ya mazungumzo kuhusiana na dini 10 wakati wote wa kozi hii. Ripoti ya maandishi ya kila mazungumzo inatakiwa kuelezea sifa za dini husika ambazo ni muhimu kwa mwinjilisti kuzifahamu. Katika ripoti, mwanafunzi ataelezea kile ambacho alikiwasilisha katika mazungumzo, na ni kwa namna gani mtu mwingine aliitikia. Ripoti ya kila mazungumzo inatakiwa kuwa na urefu wa kurasa mbili. Mwalimu anatakiwa kuelezea zoezi hili mara kadhaa wakati wa masomo machache ya kwanza. Ripoti nzuri zilizoandikwa na wanafunzi zinatakiwa kuoneshwa katika kundi kama mifano.

Mazungumzo 10 na mazoezi ya kuandika ni mazoezi ya msingi kwa kozi hii. Fomu itatolewa karibu na mwisho wa kitabu hiki kwa ajili ya mwalimu kutumia ili kutunza rekodi.

(11) Vyanzo Vinavyopendekezwa

Endapo mwanafunzi anataka kujifunza zaidi kuhusiana na kundi lolote la dini anapaswa aangalie Vyanzo Vinavyopendekezwa karibu na mwisho wa kitabu ili kuona vyanzo vinavyopatikana.


Shepherds Global Classroom ipo kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo kwa kutoa mtaala kwa ajili ya kuwaendeleza viongozi wa Kikristo duniani kote. Tunalenga kuongeza programu za mafunzo ya asili kwa kuweka chombo cha mtaala wa kozi 20 mikononi mwa viongozi wa kiroho wanaotoa mafunzo katika kila nchi duniani.

Kitabu hiki kinapatikana bure kwa njia ya kupakua kutoka katika https://www.shepherdsglobal.org/courses

Mwandishi Mkuu: Dr. Stephen K. Gibson

Hakimiliki © 2023 Shepherds Global Classroom

Ilitafsiriwa kutoka Toleo la Tatu la Kiingereza.

Haki zote zimehifadhiwa.

Nyenzo za wahusika wengine zilizotumika ni hakimiliki ya wamiliki husika ambazo zimeshirikishwa na kutumika humu chini ya leseni mbalimbali.

Tafsiri ya Maandiko “yaliyonukuliwa” kutoka chapisho la Kiingereza kwa ajili ya chapisho hili la Kiswahili yanatoka katika Biblia Takatifu ya Kiswahili, “Swahili Union Version Bible” (SUVB®).” Yametumika kwa kibali. Haki zote zimehifadhiwa.

Taarifa kuhusu vibali:

Kitabu hiki kinaweza kuchapishwa na kutawanywa bure kikiwa kimechapishwa na katika mifumo ya kidigitali chini ya miongozo ifuatayo: (1) Maudhui yaliyoko kwenye kitabu hiki hayawezi kubadilishwa kwa namna yeyote ile; (2) Nakala zinazopatikana haziwezi kuuzwa kwa ajili ya kupata faida; (3) Taasisi za elimu zina uhuru wa kutumia na kukinakili kitabu hiki, hata kama wanalipisha ada za masomo ya ziada; na (4) Kitabu hiki hakiwezi kufanyiwa tafsiri pasipokuwepo na kibali na usimamizi wa Shepherds Global Classroom.

Ready to Start Learning?

Choose a lesson to begin your journey through this course.