Kanuni Za Kikristo
Kanuni Za Kikristo
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Kanuni Za Kikristo

Lead Writer: Stephen Gibson

Course Description

Hii ni kozi ya theolojia ya kimfumo, inayoelezea mafundisho ya Kikristo kuhusu Biblia, Mungu, Mwanadamu, Kristo, Wokovu, Roho Mtakatifu, Kanisa, na Vitu vya Mwisho.

Introduction

Maelezo ya Kozi

Kozi hii inatoa ufahamu wa kanuni za msingi katika kila kimoja cha vitengo vikuu vya theolojia ya Kikristo, kama vile Mungu, Kristo, dhambi, wokovu, na kanuni zingine kuu. Mwanafunzi atajifunza jinsi ya kuepuka makosa katika kanuni. Mwanafunzi ataandaliwa kuwafundisha wengine kanuni za Kikristo.

Maelekezo kwa ajili ya Viongozi wa Darasa

Maelekezo haya yanaeleza jinsi darasa linavyoweza kufundishwa kwa kiwango cha juu zaidi cha ubora. Kiongozi wa darasa lazima azingatie kiwango hiki kwa ajili ya wanafunzi wanaopokea cheti kutoka kwa Shepherds Global Classroom au washirika wake. Kwa aina zingine za vikundi ambavyo haviwezi kutimiza viwango hivi, mwalimu anaweza kurekebisha viwango kulingana na uwezo wa kikundi husika na kutoa cheti tofauti.

Tunakadiria kuwa somo moja litachukua dakika 90 au zaidi. Inaweza kuwa bora kwa kikundi kukutana mara mbili kwa kila somo. Ikiwa kikundi kitakutana mara mbili, baadhi ya maelekezo lazima yarekebishwe. Kwa mfano, hakutakuwa na mtihani katika mikutano yote miwili.

Kila mwanafunzi anahitaji nakala ya kitabu hiki.

Vidokezo kwa ajili ya viongozi wa darasa vimejumuishwa katika kozi yote pamoja na maelekezo ya sehemu mahususi za masomo. Vimeandikwa kwa mwandiko wa mlazo.

Mwanzoni mwa kipindi cha darasa, peana mtihani wa somo la awali. Kila mwanafunzi lazima ayaandike majibu kutoka kwenye kumbukumbu yake bila msaada wowote. Ikiwa mwanafunzi hataweza kupita mtihani, unaweza kumruhusu ajaribu tena wakati mwingine (muda uliokadiriwa: dakika 10). Majibu ya mtihani yanaweza kupakuliwa kutoka kwenye ShepherdsGlobal.org.

Baada ya mtihani, tumia orodha ya malengo ya somo la awali kama maswali ya mapitio. Uliza swali kwa kila lengo na uwaruhusu wanafunzi waeleze (muda uliokadiriwa: dakika 15).

Anza somo jipya kwa kumwomba mwanafunzi asome kifungu kilichotolewa. Wape wanafunzi nafasi wajadili kwa ufupi kile ambacho kifungu hicho kinasema kuhusu mada ya somo (muda uliokadiriwa: dakika 10).

Pitia maudhui ya somo kwa kusoma na kufafanua kila sehemu. Washiriki wa darasa wanaweza kufundisha baadhi ya sehemu (muda uliokadiriwa: dakika 45).

Maandiko mengi yametumiwa katika kozi hii. Marejeo ya Maandiko yaliyotolewa kwenye mabano yenye neno soma yanapaswa kusomwa kwa sauti darasani. Marejeo mengine ya maandiko yanatumika tu kuunga mkono kauli zilizo katika maudhui. Si lazima kila mara kuangalia au kusoma vifungu hivyo darasani.

Maswali ya majadiliano na mazoezi ya darasani yanaonyeshwa kwa vishale. Wakati mwingine maswali ya majadiliano hutanguliza sehemu; wakati mwingine yanapitia sehemu iliyoangaziwa awali. Kiongozi wa darasa anapaswa kuuliza swali na kuwapa wanafunzi muda wa kujadili jibu. Si lazima kueleza kikamilifu jibu wakati huo, hasa ikiwa swali linatanguliza sehemu.

Darasa linapaswa kusoma “Kauli ya Imani” pamoja mara mbili mwishoni mwa kila somo.

Mwishoni mwa kila somo, kila mwanafunzi anapaswa kupewa kifungu cha maandiko kutoka kwenye orodha iliyotolewa. Kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa, wanapaswa kusoma kifungu hicho na kuandika aya moja kuhusu kile ambacho kifungu hicho kinasema kuhusu mada husika. Wanapaswa kumwonyesha kiongozi wa darasa aya hiyo katika kipindi kitakachofuata.

Angalau mara tatu wakati wa kozi hii, mwanafunzi anapaswa kuwafundisha watu wasioshiriki katika darasa lake somo moja nzima au sehemu ya somo. Hili linaweza kufanywa katika darasa kanisani, kikundi cha kujifunza Biblia nyumbani, au katika mazingira mengine. Mwishoni mwa kila kipindi cha darasa, wakumbushe wanafunzi kuhusu zoezi hili, na uwape nafasi ya kutoa ripoti ikiwa wamefundisha chochote tangu kipindi cha mwisho cha darasa.

Mwishoni mwa darasa, wakumbushe wanafunzi kusoma maudhui ya somo linalofuata kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa (muda uliokadiriwa wa matangazo na mazoezi: dakika 10).

Ikiwa mwanafunzi anataka kupata cheti kutoka kwa Shepherds Global Classroom au mmoja wa washirika wake, anapaswa kuhudhuria vipindi vya darasa na kukamilisha mazoezi. Mwanafunzi akikosa darasa, anapaswa kusoma somo alilokosa, afanye mtihani na afanye zoezi la kuandika. Fomu itatolewa mwishoni mwa kozi kwa ajili ya kurekodi mazoezi yaliyokamilishwa.

Maelekezo kwa Wanafunzi

Unapaswa kusoma maudhui ya kila somo kabla ya darasa kukutana, ili uweze kushiriki katika majadiliano ukiwa na uelewa bora zaidi.

Mwanzoni mwa kila kipindi cha darasa, jitayarishe kufanya mtihani wa somo la awali. Chunguza maswali ya mtihani yaliyotolewa.

Njoo siku zote na Biblia, nakala iliyochapishwa ya somo husika, na kalamu ya wino kwa ajili ya kuongeza vidokezo vyako mwenyewe kwenye maudhui.

Kuwa tayari kutafuta marejeo ya maandiko, kujibu maswali ya majadiliano, na kushiriki jinsi kiongozi wa darasa anavyoelekeza.

Mwishoni mwa kila somo, utapewa kifungu cha maandiko. Kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa, soma kifungu na uandike aya kuhusu kile ambacho kifungu hicho kinasema kuhusu mada ya somo. Mwonyeshe kiongozi wa darasa aya hiyo.

Angalau mara tatu wakati wa kozi hii unapaswa kuwafundisha watu wasioshiriki katika darasa lako somo moja nzima au sehemu ya somo. Mafundisho haya yanaweza kutekelezwa katika darasa kanisani, kikundi cha kujifunza Biblia nyumbani, au katika mazingira mengine. Toa ripoti kwa kiongozi wa darasa kila wakati unapomfundisha mtu.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.