Maisha Na Huduma Ya Yesu
Maisha Na Huduma Ya Yesu
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Maisha Na Huduma Ya Yesu

Author: Randall McElwain

Course Description

Kozi hii inasoma maisha ya Yesu kama mfano kwa huduma na uongozi katika karne ya 21.

Introduction

Kozi hi ni ya kujifunza maisha na huduma ya Yesu kama kielelezo cha kuigwa katika maisha na huduma kwa wakati wa sasa. Siyo tu utafiti wa kina wa Vitabu vya Injili. Badala yake, kozi hii inaangalia katika vipengele kadhaa vya huduma ya Yesu ili kupata mafunzo kwa ajili ya huduma za wakati wa sasa. Kama una matarajio ya kujifunza kwa undani maisha ya Yesu, ninapendekeza ujipatie mojawapo ya vitabu vilivyooredheshwa kwenye Vianzo Vilivyopendekezwa kwenye mwisho wa kitabu hiki.

Kama ni kujifunza katika kikundi, mnaweza kupeana nafasi ya kusoma mafundisho haya. Inabidi msimame kwa wakati fulani ili kupeana nafasi ya kufanya majadiliano ya darasa. Kama kiongozi wa darasa, unao wajibu wa kuhakikisha kwamba majadiliano hayayumbishwi kutoka kwenye mada inayojadiliwa. Itasaidia kuwa na kiwango cha muda kwa kila kipindi cha majadiliano.

Maswali yanayohusiana na mjadala na shughuli za ndani za darasa zimeonyeshwa kwa alama hii. ► Endapo utakutana na alama hii, uliza swali au maswali yanayofuata mbele yake na utoe nafasi kwa wanafunzi kutoa majibu. Tafadhali chukua mud ili kupata majibu yaliyo sahihi na yenye maana. Bila kufanya hivyo, wanafunzi wanaweza kuyaunganisha mafundisho haya ya huduma ya Yesu na huduma zao leo.

Aya nyingi za maandiko zimeorodheshwa kwenye kozi yote, kwenye mafundisho ya msingi na kwenye tanbihi. Aya ambazo itapaswa zisomwe kwa sauti zimeonyeshwa pia kwa alama ya ►. Wanafunzi wanapaswa wazisome hizi aya ndefu kabla ya darasa kuanza. Aya fupi zitasomwa darasani.

Sehemu zilizoonyeshwa “Angalia kwa kuzingatia” zinaelekeza kwenye mada maalumu zinazohusiana na somo linalojadiliwa.

Kila somo litahusisha kazi moja au mbili za kufanya. Kama mwanafunzi atahitaji kupata cheti cha kufuzu mafunzo kutoka Shepherds Global Classroom, atapaswa ahudhurie vipindi vyote vya darasa na amalize kufanya kazi zote zilizotolewa. Fomu imetolewa mwisho wa kozi hii kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi za kufanya zilizomalizika.

Kusudi mojawapo la kozi hii ni kuwaanda wanafunzi kuwa waalimu. Kiongozi wa darasa anapaswa kuwapa wanafunzi nafasi ya kuinua viwango vyao vya kufundisha. Kwa mfano, kiongozi wa darasa mara kwa mara atapaswa kumpa mwanafunzi nafasi ya kufundisha sehemu fupi ya somo katika darasa.

Ready to Start Learning?

Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.