Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Warumi
Course Description
Kozi hii inafundisha theolojia ya wokovu na dhamira kama inavyoelezewa katika vitabu ya Warumi, kujadili masuala kadhaa ambayo yamekuwa ya kutatanisha katika kanisa.
Introduction
Maelezo ya Kozi
Barua ya Paulo kwa Waamini wa Kirumi inaelezea kuhusu umisheni na ujumbe wake. Alielezea kuhusu teolojia ya Injili kwa kusudu la kuelezea ni kwa nini kila mtu anaihitaji. Barua hii imekuwa na mgoso mkubwa kwa muda wote wa historia ya kanisa. Imani nyingi zenye kutatanisha zimekuwa na mizizi yake kutokea hapo. Kozi hii inachunguza Kitabu cha Warumi na kisha kayawezesha yatumike kwenye Maisha ya kuishi Kikristo.
Muundo wa Masomo
Masomo yameandaliwa kufundishwa kila moja kwenye kipindi kimoja, lakini muda unaohitajika kutumika kwa kila somo unaweza ukawa masaa mawili au hata zaidi. Kama vipindi vifupi vitahitajika, masomo yanaweza kugawanywa kwenye vifungu vidogo vidogo.
Maelekezo ya kiongozi wa darasa katika somo yako katika mwandiko wa kulala.
Darasa linapaswa kila mara kurejelea kwenye “muhtasari wa kitabu cha Warumi” ambao somo la 1 linafuatia baada yake. Darasa linaposoma kila kifungu, wakumbushe wanafunzi jinsi kifungu kinavyoendana na muktadha wa sehemu hiyo ya kitabu, na muktadha wa kitabu kizima.
Maswali ya Mapitio yametolewa kwa ajili ya kila somo. Kwenye kila mwanzo wa kipindi cha darasa, kiongozi wa darasa ni lazima aulize maswali ya mapitio ya somo lililopita na maswali machache kutoka katika masomo mengine yaliyopita. Hakikisha kwamba unasaidia katika kumwezesha kila mwanafunzi kushiriki katika kutoa majibu. Kama mtu ataonekana kuwa hayuko tayari kushiriki katika kujibu maswali, elekeza swali moja kwa moja kwake kwa kumtaja jina. Huu ni muda muafaka wa kusahihisha yale ambayo yalikuwa hayajaeleweka katika somo lililofundishwa. Maswali ya mapitio ndiyo hayo hayo yatakayotumika kwenye mtihani wa mwisho. Fanya mapitio na masahihisho ya majibu yako kwa kadiri itakavyowezekana. Viongozi wa madarasa wanaweza kuangalia majibu ya maswali haya kutoka kwenye jedwali la majibu katika shepherdsglobal.org.
Alama ya ► ni kiashirio cha maswali ya kujadiliana na mazoezi ya darasani.
Katika maswali ya kujadiliana, kiongozi wa darasa anapaswa kuuliza swali husika na kuruhusu wanafunzi kadhaa kutoa majibu kwa kifupi. Mara nyingine swali litakuwa linarejelea kwenye mambo yaliyokuwa yamefundishwa wakati huo huo. Wakati huo, wanafunzi wanapaswa kuwa na uwezo wa kutoa jibu sahihi. Ikiwa kuna mkanganyiko, kiongozi wa darasa anapaswa kuelezea habari kwa undani zaidi. Katika nyakati nyingine, wanaweza kuingiza mambo mengine mapya yanayoendana na somo hilo. Halafu, siyo lazima mwanafunzi aweze kujibu kwa usahihi kabisa, na siyo lazima aweze kufikia kwenye hitimisho. Swali linawaandaa tu wanafunzi katika kujifunza mambo mapya yanayohusiana na somo.
Siyo lazima kuangalia kila rejeo la Maandiko kutoka katika mabano. Marejeo yametolewa kwa ajili ya kuunga mkono taarifa zilizooanishwa.
Wakati mwingine, rejea itaonyesha wapi pa kupata nyenzo nyingine katika somo au sehemu nyingine ya kozi. Siyo lazima kwenda kuangalia jambo hilo linalohusiana na somo labda kuwepo na hitaji kwamba darasa linahitaji maelezo ya ziada kwa haraka wakati huo huo.
Kiongozi wa darasa anaweza kumwuliza mwanafunzi atoe maelezo kuhusiana na nukuu zilizoko kwenye michoro ya maboksi yanayoenda sambasamba pembezoni mwa masomo.
Masomo mengi yanayo michoro ya maboksi yenye picha na nukuu za kihistoria kuhusiana na Rumi. Rejea hiyo haihusiani na somo. Si lazima kujumuisha rejea ya kihistoria katika uwasilishaji wa somo.
Kwenye mwanzo wa kila kipindi cha darasa, kiongozi wa darasa anapaswa kukusanya kazi za kufanya zilizoandikwa kutokana na kipindi kilichopita na kuongoza kikundi katika kujadili yale waliyoandika.
Kazi za kufanya kwa Wanafunzi
Hili ni darasa la kujifunza Biblia. Wanafunzi watapaswa waweke Biblia zao wazi kwa ajili ya kuangalia kutoka hapo ile sura wanayojifunza.
Chati imewekwa kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za kazi za kufanya zilizokamilika. Chati hii imechapishwa nyuma ya kitabu cha kozi hii.
Kwenye wiki za mwendelezo wa kozi hii, mwanafunzi`atapaswa aandae mahubiri matatu ya kuhubiri au masomo yanayohusiana na sura yeyote kutoka katika kitabu cha Warumi na kuyawakilisha kwenye makundi mengine yasiyokuwa ya darasa moja. Baada ya kila uwasilishwaji, mwanafunzi atapaswa kuwauliza baadhi ya wasikilizaji wake wamweleze ni kwa jinsi gani anaweza kuboresha uwasilishaji wake. Atapaswa amkabidhi kiongozi wa darasa nakala ya maelezo yake aliyowasilisha, maelezo ya kikundi na tukio wakati alipokuwa akiongea, na mipango yake ya kuboresha zaidi.
Mwanafunzi atapaswa kuandaa angalau majadiliano na waamini wawili kutoka katika makanisa ambayo yana mafundisho ya imani tofauti na aliyo nayo yeye. Atapaswa awatake wamweleze ni kwa nini wanashikamana na mafundisho ya imani waliyo nayo. Atapaswa awafafanulie kuhusu sura zinazotokana na Kitabu cha Warumi zinazohusika na mada yao. Atapaswa aandike maelezo yanayotokana na majadiliano hayo na ayakabihi kwa kiongozi wa darasa. Itakuwa ni jambo jema sana kama kazi hii ya kufanya itakamilika baada ya kuwa wamejifunza somo la 9.
Kila somo lina kazi za kufanya kwa kuandika, Isipokuwa somo la 12. Kila mojawapo katika haya yatapaswa yakamilike kabla ya kipindi kingine kinachofuata kuanza. Kazi za Matendo zitapaswa ziwakilishwe kwa kiongozi wa darasa wakati kipindi cha darasa kinapoanza. Kiongozi wa darasa atapaswa aongoze majadiliano mafupi kuhusiana na kazi za matendo za kufanya za kuandika zilizowakilishwa kwake na wanafunzi.
Kwenye mwisho wa kozi kuna kufanya mtihani wa mwisho. Kila mwanafunzi atapaswa akamilishe kufanya mtihani peke yake bila ya kupewa msaada au kuangalia kumbukumbu zozote zilizoandikwa. Orodha ya maswali imeandikwa karibu na mwisho wa kitabu cha kozi hii. Wakati wa kufanyika kwa mtihani wa mwisho unaweza ukawa kwenye kipindi kingine cha darasa kitakachofuata au ukapangwa kufanyika katika wakati mwingine ulio muafaka. Ili kufupisha muda unaohitajika kufanya mtihani, kiongozi wa darasa anaweza kuchagua maswali 20 ya kufanya. Katika kuandika majibu ya maswali 20 kunaweza kuhitajika muda wa saa moja kwa baadhi ya wanafunzi. Wanafunzi hawapaswi wajue ni maswali gani yatakayotumika kwa ajili ya mtihani, na watapaswa wajifunze maswali ya marejeo ya masomo yote.
Wanafunzi wanapaswa wawepo kwenye kila kipindi cha darasa. Kama mwanafunzi atakosekana katika kipindi, atapaswa ajifunze kile kilichokuwa kimefundishwa, afanye marejeo na kiongozi wa darasa, na aandike kazi ya kufanya yaliyotolewa.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.