Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Course Description
Kozi hii inatoa kanuni za kibiblia ambazo huongoza mbinu za uinjilisti. Inaelezea aina za uinjilisti na kutoa masomo ya kutumia kufundisha wapya waliobadilishwa.
Introduction
Maelezo Kuhusiana na somo
Kozi hili ni nyenzo ya kusaidia kanisa katika kutimiza utume wake.
Kozi hii inatilia mkazo kitovu cha kanisa la mahali, kioneshacho kwamba injili ndiyo utume wa kanisa, na kwamba asili ya injili inapaswa kuonesha sura ya kanisa.
Kwa kuelezea misingi ya injili, kunasahihisha baadhi ya makosa yanayotokana na mfumo wa kisasa ambao haumwelekezi mtenda dhambi kuokoka kiukweli na kuishi maisha ya Kikristo.
Mwanafunzi ataandaliwa kuikuza huduma yake.
mada nyingi katika somo hili zinaweza kufundishwa kama somo kamili kwa ajili ya vikundi mbalimbali. Kwa mfano, somo linaweza kutumika katika kufundisha njia ya kuwasilisha injili.
Katika kozi hii, wanafunzi watajifunza jinsi ya kuwafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu. Shepherds Global Classroom imetengeneza nyenzo ya kutumika kuwafanya watu kuwa wafuasi hususani kwa ajili ya waumini wapya. Kitabu hiki cha masomo cha jinsi ya kuwafanya watu kuwa wafuasi, kinachoitwa, Masomo ya Kukuza Uanafunzi, kinapatikana kwa kupakua kutoka shepherdsglobal.com. Kila somo katika masomo 26 ya Masomo ya Kukuza Uanafunzi, kumewekwa na kitabu cha mwongozo cha mwalimu pamoja na kurasa za wanafunzi.
Ufafanuzi na Maelekezo kwa Viongozi wa Madarasa
Mambo ya kukumbuka kwa ajili ya viongozi wa madarasa yamewekwa katika somo nzima ikiwa ni pamoja na maelekezo kwa ajili ya sehemu maalumu za masomo. Mambo hayo yameoneshwa kwa herufi mlazo.
Maswali ya kujadiliana na kazi za ndani za darasa zimeoneshwa kwa alama ►. Kwa ajili ya maswali ya kujadiliana, kiongozi wa darasa atapaswa kuuliza swali na aruhusu wanafunzi kujibu. Siyo lazima swali lijibiwe kwa usahihi sana wakati wa majadiliano. Mafundisho yaliyoko kwenye somo yatajibu swali hilo. Kama mwanafunzi yule yule huwa wa kwanza kujibu na wanafunzi wengine huwa kimya, kiongozi anaweza akaelekeza swali kwa mmoja wao: ”Emanueli, ni kwa jinsi gani utaweza kujibu swali hili?”
Kila somo linamalizikia na kazi za kufanya. Kazi za kufanya zinapaswa zimalizike na kuwakilishwa kabla ya muda wa kuanza somo linalofuata. Kama mwanafunzi hatakamilisha kazi ya kufanya, anaweza akaifanya kwa wakati mwingine. Hata hivyo, kiongozi atapaswa kuwahamasisha wanafunzi kutunza na kuendana na wakati ili waweze kujifunza zaidi kutoka darasani.
Wanafunzi wanatakiwa kukamisha kazi za kuandika za aina zote. Kwa kawaida kiongozi wa darasa atapaswa kukusanya kazi zote za kufanya zilizoandikwa mwanzoni mwa kipindi cha darasa (Kazi mbili za kufanya Somo la 6, Kazi ya kufanya ya 1, na Somo la 14, Kazi ya kufanya ya 1) hazitahitajika kukusanywa bali zitatolewa taarifa tu.)
Wanafunzi pia watapaswa watawasilisha Injili kwa watu wengi kwa kutumia vigezo walivyojifunza darasani. Kila baada ya kuwasilisha, wataandika mambo yanayohusu uzoefu wao na kushirikishana darasani ni kwa jinsi gani uwasilishwaji huo ulivyofanyika. Wataandaa mahubiri ya uinjilisti kwa ajili ya watu wazima na somo kwa ajili ya watoto wadogo. Kuna mitihani miwili katika kozi hii, baada ya somo la 5 na la 10. Wanafunzi watapaswa kuuandika mtihani huu kwa kutumia akili zao tu bila kunukuu kutoka katika maandiko yoyote au kwa kusemezana. Hakuna mwongozo wa majibu unaotolewa kwa mwalimu kwa sababu majibu yanapatikana kwa urahisi kutoka katika masomo ya kitabu hiki.
Somo la 13 linajumuisha pamoja na maelekezo ya jinsi ya kugawa vipeperushi vya injili. Wanafunzi watapaswa kujua ni mahali gani watapata vipeperushi kwa ajili ya kuvigawa. Ikiwezekana, vinaweza vikaletwa wakati wa kipindi cha darasani.
Kama mwanafunzi atahitaji kupata cheti cha kufuzu mafunzo kutoka Shepherd’s Global Classroom, atapaswa ahudhurie vipindi vyote vya darasa na amalize kufanya kazi zote zilizotolewa. Fomu imetolewa mwishoni mwa kozi hii kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi za kufanya zilizokamika.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.