Type at least 2 characters to search
No results found for ""
Courses
Lessons
navigate open
See all results →
Misingi ya Imani ya Kikristo

Misingi ya Imani ya Kikristo

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Misingi ya Imani ya Kikristo

Lead Writer: Stephen Gibson

Course Description

Kozi inatoa uelewa wa msingi wa mafundisho ya msingi katika kila kundi kubwa la Theolojia ya Kikristo, kama vile Mungu, Kristo, dhambi, wokovu, na mafundisho mengine makuu. Mwanafunzi ataelewa namna ya kuepuka makosa katika fundisho. Mwanafunzi anaandaliwa ili kufundisha mafundisho ya Kikristo kwa wengine

What You'll Learn

Kitabu cha Mungu
Sifa za Mungu
Utatu Mtakatifu
Wanadamu
Dhambi
Roho
Kristo
Wokovu
Masuala ya Wokovu
Roho Mtakatifu
Utakatifu wa Kikristo
Kanisa
Hatma ya Milele
Matukio ya Mwisho
Matamko ya Kale ya Imani

Course Objectives

(1) Kujifunza mafundisho ya msingi ya Imani ya Kikristo.

(2) Kutumia kwa usahihi Biblia kama chanzo cha mamlaka kwa ajili ya mafundisho.

(3) Kutambua makosa muhimu katika mafundisho.

(4) Kupata uelewa ambao utawasaidia watu kuwa na uhusiano wa kina na Mungu.

(5) Kupokea yaliyomo na muundo kwa ajili ya kuwafundisha wengine.

Introduction

Maelekezo kwa Viongozi wa Darasa

Tunakadiria kwamba somo litachukua dakika 90 au Zaidi. Inaweza kuwa nzuri zaidi kwa kundi kukutana mara mbili kwa ajili ya kila somo. Endapo kundi linakutana mara mbili, baadhi ya maelekezo yanaweza kutumiwa. Kwa mfano, hakutakuwa na jaribio katika mara zote mbili.

Kila mwanafunzi anahitaji kuwa na nakala ya kitabu hiki.

Notsi kwa ajili ya kiongozi wa darasa zimejumuishwa katika kozi yote pamoja na maelekezo kwa ajili ya sehemu mahususi za masomo. Zimewekwa katika mwandiko wa ulalo.

Mwanzoni mwa kipindi cha darasa, toa jaribio juu ya somo lililopita. Kila mwanafunzi anapaswa kuandika majibu kutoka katika kumbukumbu zake za kichwani pasipo kutumia msaada wowote. Endapo mwanafunzi atashindwa kufaulu jaribio, unaweza kumruhusu arudie tena wakati mwingine (Muda wa makadirio: dakika10). Majibu ya majaribio yanapatikana kwa ajili ya kupakua katika ShepherdsGlobal.org.

Baada ya jaribio, tumia orodha ya malengo kutoka katika somo lililopita kama maswali ya marudio. Uliza maswali kwa kila lengo na uruhusu wanafunzi kuelezea (muda wa makadirio: dakika 15).

Anza somo jipya kwa mwanafunzi kusoma kifungu cha andiko kilichotolewa. Waache wanafunzi wajadili kwa ufupi kuhusu kifungu kinasema nini kuhusiana mada ya somo (muda wa makadirio: dakika 10).

Pitia nyenzo za somo kwa kusoma na kuelezea kila sehemu. Washiriki wa darasa wanaweza kufundisha baadhi ya sehemu (muda wa makadirio: dakika 45).

Maandiko mengi yametumika katika kozi hii. Rejea za maandiko zilizotolewa katika mabano yenye maneno soma yanapaswa yasomwe darasani. Rejea nyingine za maandiko yanatoa msaada kwa maelezo katika andiko. Si lazima kuviangalia au kuvisoma vifungu hivyo darasani.

Maswali ya majadiliano na kazi za ndani ya darasa yameoneshwa kwa alama ►. Wakati mwingine maswali ya majadiliano yanatoa utangulizi wa sehemu; wakati mwingine wanarudia sehemu ambayo imeshasomwa. Kiongozi wa darasa anapaswa kuuliza maswali na kuwapa wanafunzi muda wa kujadili majibu. Sio muhimu sana kuelezea kikamilifu majibu kwa wakati mmoja, na hasa kama swali linatoa utangulizi wa sehemu.

Darasa linatakiwa kusoma “tamko la Imani” kwa pamoja mara mbili kila mwisho wa kila somo.

Mwishoni mwa kila somo, kila mwanafunzi atapewa kifungu cha maandiko kutoka katika orodha iliyotolewa. Kabla ya sehemu inayofuata, wanapswa kusoma kifungu cha andiko na kuandika kifungu cha maneno kuhusiana na ni nini kifungu cha maandiko kinasema kuhusiana na mada. Wanapaswa kuonesha kifungu hiki cha maneno kwa kiongozi wa darasa.

Angalau mara mbili wakati wa kozi, mwanafunzi anatakiwa kufundisha somo au sehemu ya somo kwa watu ambao hawako ndani ya kanisa. Mafundisho haya yanaweza kufanyika katika darasa kanisani, katika kundi la kujifunza Biblia, au Mazingira yeyote yale. Katika kila mwisho wa kipindi cha darasa, wakumbushe wanafunzi kuhusiana na zoezi, na wape wao nafasi ya kuripoti kama wamefanya mafunzo yeyote tangu darasa lililopita.

Mwishoni mwa kila darasa, wakumbushe wanafunzi kusoma nyenzo za somo linalofuata kabla ya kipindi kinachofuata (makadirio ya muda kwa ajili ya matangazo na mazoezi: dakika 10).

Wanafunzi wanapaswa kuhudhuria vipindi vya madarasa na kukamilisha mazoezi. Endapo mwanafunzi atakosa darasa, anapaswa ajaribu kusoma somo alilokosa, afanye jaribio, na kuandika zoezi. Fomu imetolewa mwishoni mwa kozi hii kwa ajili ya kunakili mazoezi yaliyokamilika.

Maelekezo kwa Ajili ya Wanafunzi

Unapaswa kusoma nyenzo kwa ajili ya kila somo kabla ya darasa kukutana, ili uweze kushiriki katika majadiliano ukiwa na uelewa mzuri.

Mwanzoni mwa kila kipindi cha darasa, kuwa tayari kufanya jaribio kuhusiana na somo lililopita. Soma au jifunze maswali ya jaribio yaliyotolewa.

Mara zote uwe na Biblia, nakala ngumu ya somo, na kalamu kwa ajili ya notsi zako za nyenzo.

Uwe tayari kuaangalia rejea ya maandiko, jibu maswali ya majadiliano, na shiriki kama ambavyo kiongozi wa darasa anaongoza.

Kila mwisho wa somo, utapewa vifungu vya maandiko. Kabla ya kipindi kijacho cha darasa, soma na andika kifungu cha maneno kuhusiana na kile ambacho kifungu kinasema kuhusiana na mada ya somo. Onesha kifungu cha maneno kwa kiongozi wa darasa.

Angalau mara tatu wakati wa kozi hii unapaswa kufundisha somo au sehemu ya somo kwa watu ambao hawako katika darasa. Mafundisho haya yanapaswa kufanyika katika darasa kanisani, katika kundi la kujifunza Biblia, au Mazingira yeyote yale. Ripoti kwa kiongozi wa darasa kila wakati unapomfundisha mwingine.

Ready to Start Learning?

Choose a lesson from the sidebar, or jump right in.

Start Lesson 1