Mwisho kabisa wa somo hili, mwanafunzi anatakiwa awe na uwezo wa:
(1) Kuelewa ni nini Biblia humaanisha inapozungumza kuhusu “dunia.”
(2) Kutambua maeneo ambayo dunia na maadili yake yameathiri Maisha yake.
(3) Kueleza ni kwa jinsi gani na ni kwanini namna ya kufikiri ya mkristo ni lazima iwe tofauti na mwenye dhambi.
(4) Kuelezea inamaanisha nini mkristo kuishi maisha ya uadilifu.
(5) Kuonyesha kwamba kweli ya kikristo lazima udhihilishwe katika kila Nyanja ya maisha.
Yohana Chrysostom, Mhubiri wa Uadilifu
Yohana Chrysostom (370’s),[1] alikuwa mchungaji mcha Mungu aliyejulikana kama “Mdomo wa dhahabu” kwa sababu ya mahubiri yake yenye nguvu na ya kukaririwa sana. Alipendwa na mwanadamu wa kawaida na akawa mhubiri mwenye sifa sana katika dola ya Rumi Mashariki. Alitekwa nyara mnamo 398 na akapelekwa katika mji mkuu wa Konstatinopo (kwa sasa Istanbul, Uturuki) alihudumu kama mchungaji na askofu wa kanisa la kitaifa lenye washirika 100,000.
Yohana alijulikana kwa msimamo wake thabiti. Alitumia ofisi yake kutumikia mahitaji ya mji wote, na sio tu matajiri. Alilisha maskini, akajenga hospitali, aliwasaidia wajane. Aliwaandau maaskofu katika Asia ndogo kwa sababu ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha na alihubiri na kukemea anasa na usherati. Aliwaonya matajiri wa Kostantinopo kwamba, kuhudhuria viwanja vya maonyesho machafu kutawaharibu. Alilinganisha mambo hayo na virusi hatari vya kufisha, Yohana alisema,
Ukimuona mwanamke asiye na adabu katika ukumbi wa michezo akiwa na kichwa ambacho hakijafunikwa na hisia za ushujaa, nguo zake zikiwa na rangi za dhahabu, huku akionyesa hisia zake za ngono na kuimba nyimbo zisizo na maadili, akionyesha viungo vyake akiimba na akiyatamka maneno yasio na adabu …utasema hamna kitu ambacho ni cha kawaida ya kibinadamu kimekutokea? …baada ya ukumbi kufungwa na kila mtu ameondoka, hizo picha zitakuwa bado katika nafsi yako, maneno yao, tabia zao, sura zao, kutembea kwao kukaa kwao-viungo vyao vikiwa wazi- na wewe utaenda nyumbani umefunikwa na vidonda elfu! Isitoshe hautakuwa peke yako pia yule kahaba atenda na pamoja wewe ijapokuwa sio kwa uwazi na kwa kuonekana… lakini kwa moyo wako na dhamili yako na ndani mwako atawasha tanuru ya Kibabeli ambako amani katika nyumba yako na usafi wa moyo wako na furaha ya ndoa yako itateketea.
Kwa matajiri Yohana aliwaonya,
Ni upumbavu na ukichaa wa wazi kuwa na hazina ya mavazi na huku ukiwaacha wanadamu walioumbwa kwa sura na Mfano wa Mungu wakiwa uchi huku wakitetemeka kwa baridi kiasi kwamba hawawezi kusimau wima… Wewe ni mkubwa na mnene, unafanya karamu za unywaji pombe mpaka usiku wa manane, na unalala katika kitanda laini na chenye joto. Na wala haujafikiria jinsi utakavyo toa hesabu ya jinsi ulivyotumia vibaya zawadi kutoka kwa Mungu… kwa maana fedha setu ni za Mungu ijapokuwa tumezitafuta. Ndiposa Mungu amekuruhusu uwe na vingi, na sio ya kutumia isisvyostahili… bali kuwagiwa wale ambao wana uhitaji.
Yohana Chrysostom alipewa adhabu ya kuhamishwa kuelekea katika fukwe za mashariki mwa Bahari Nyeusi lakini alikufa akiwa safarini (A.D. 407). Maneno yake ya mwisho yalikuwa “Utukufu uwe kwa Mungu kwa mambo yote. Amina.”
[1]Gerald L. Sittser. Water from a Deep Well. (Downers Grove: InterVarsity Press, 2007), 135
Mtazamo wa kimaandiko kuhusu ulimwengu.
Yohana 17 ni maombi ya Yesu kwa wanafundi wake muda mfupi kabla ya kusurubishwa. Yanaonesha kujali na upendo mkuu ambao Yesu alikuwa nao kwa wanafunzi wake. Alisema pia anawaombea wale ambao wataamini ujumbe wa mitume (mstari wa 20) kwa hivyo wakristo wa leo wamejumuishwa.
► Mwanafunzi asome Yohana 17:14-18 kwa niaba ya kikundi.
Yesu alimaanisha nini aliposema yeye sio wa ulimwengu? Tunajua yakwamba asili yake si ya hapa ulimwenguni, yeye ni mwana wa Mungu, aliyekuja duniani kutoka mbinguni. Ijapokuwa anaposema jambo hili kwamba yeye sio wa ulimwengu hauanishi ya kwamba ametoka mahali fulani tofauti katika ulimwengu huu. Akasema pia wanafunzi sio wa ulimwengu huu pia kama vile yeye asivyo wa ulimwengu huu. Yesu alikuwa anaongea kuhusu watu waliozaliwa katika dunia hii na wazazi ambao ni wanadamu na wakakua na kuwa wananchi katika nchi zao.
Kwa hivyo Yesu alimaanisha nini aliposema wanafunzi wake sio wa ulimwengu huu? Lazima tuelewe basi maadiko yanauanisha nini wakati yanaposema kuhusu ulimwengu.
► Mwanafunzi asome Waefeso 2:1-3 kwa niaba ya kikundi.
Mistari hii inatuonyesha kwamba kuishi kama ulimwengu unavyoishi ni sawa na kuzifuata njia za shetani. Tunaona pia ya kwamba watu wa ulimwengu hufuata tamaa zao mbaya na watapata adhabu kutoka kwa Mungu. Waaminio wamepokea maisha mapya na hawaishi tena kama ulimwengu.
► Mwanafunzi asome 1 Yohana 2:15-17 kwa niaba ya kikundi.
Ulimwengu unaonyeshwa hapa katika 1 Yohana kama mahali paovu. Sio pa kupendwa, wala yaliomo ndani yake si ya kupendwa. Tamaa na nia mbaya ni kawaida ya ulimwengu. Tamaa mbaya huitwa tamaa ya kidunia.
Shetani anaitwa mtawala wa ulimwengu huu (Yohana 16:11). Hii haimaanishi kwamba ulimwengu ni wake kihalali, yeye ni kiongozi wa uasi kwa Mungu na watu wa ulimwengu wanamfuata. Yeye alishahukumiwa tayari, na watu ambao wanaendelea kumfuata pia watahukumiwa.
Kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu (Yakobo 4:4).
Ulimwengu una mamillioni ya watu kimwili, walioanguka, waliotengwa na Mungu na kuunganishwa na kile ambacho wanashirikiana kwa pamoja.Kwanza wana mvuto na tamaa mbaya. Wanapenda mambo ya ulimwengu kuliko muumba wa Dunia. 1 Yohana 2:15-17 yasema, “Msiipende dunia… Kwa maana vyote vilivyo katika dunia—tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima—sio ya Baba bali ni ya dunia.”
Pili, tamaa yao mbaya huwaelekeza katika tabia mbaya; maisha ambayo yanalenga kujitosheleza wenyewe, kwa kutohurumia wengine na kuwanyima haki na rehema (Amosi 5:11-15; 21-24). Wanaenda katika njia zao wenyewe, wakidai wanachohitaji na wanajiamulia kilicho sawa na kisicho kwa ajili yao wenyewe. Japokuwa wana aina nyingi za dini, wote walio wa ulimwengu hujifanya (wenye elimu ya kibinadamu, hekima ya kibinadamu, Hamu ya kibinadamu, uzuri wa kibinadamu, nguvu za kibinadamu) kuwa kitovu cha ibada yao (Warumi 1:25). Hawaamini nguvu na uweza wa Mungu lakini wanaamini filosofia ya Maisha ambayo huhalalisha kile walichoona na kuamua kuwa ni haki wao kutenda. Hawatafuti kufahamu yaliyo haki na kuyatenda. Wanafanya kile ambacho wanataka halafu ndipo wanatafuta namna ya kueleza kwamba ni sawa.
Wanasaikolojia na washauri wa kidunia huwasaidia watu kutatua hukumu katika dhamira zao pasipo toba na msamaha wa Mungu. Wana filosofia wa kidunia hujaribu kueleza kusudi la kuishi ambalo halimshirikishi Mungu. Wanasayansi wa ulmwengu hujaribu kueleza chanzo cha kila kitu huku wakimkataa muumbaji. Wanasiasa na wafanyakazi za kijamii katika ulimwengu hujaribu kutafuta namna ya kuzuia maadhala ya kiasiria ambayo husababishwa na dhambi pasipo kuona dhambi kama chanzo cha shida zote. Wanamitindo wa mavazi wa duniani wanafanya bidii sana kutengeneza mavazi yenye kuleta hisia na yenye mvuto. Watumbuizaji wa kidunia hufanya vichekesho na mizaha ya dhambi, maadili na dini. Wachungaji wa kidunia wanamwamini mungu ambaye anavumilia Dhambi na ambaye anajali sana wewe kuwa tajiri na mwenye mali, mwenye furahana mwenye kujithamini.
Wakolosai 2:8 yatuonya tusindanganywe na kuibiwa na filosofia na uongo kwa mambo ya ulimwengu. Msanii tapeli huwaibia watu kwa kuuza wazo la uongo. Kwa kushawishi watu kwa maoni potovu, dunia huwaibia wanadamu ushirika wao na Mungu, faida zao za kiroho, na Mbingu.
Filosofia na kudhibiti motisha za kidunia huonekana katika mtindo wa maisha ya watu wa ulimwengu. Kuongea kwao, mitazamo, namna ya kuvaa, burudani, na tabia za kidunia huonyesha dhambi katika mioyo yao.
Wakristo hawawezi kufuata maadili ya jamii zao. Wakristo wanatakiwa kuwa tofauti na jamii zao.
Tamaduni kutengenezwa na kitu hiki ambacho Biblia huita ulimwengu. Vizazi vya watu mahali fulani hutengeneza tamaduni. Wao hupenda mambo mengi mazuri kama vile usalau, mafanikio na familia iliyo imara, lakini huyatafuta mambo hayo kwa kutumia filosofia za ulimwengu na hudhamiria kupata pasipo kunyenyekea kwenye neno la Mungu. Hiyo inamaanisha kwamba wakristo hawawezi kufuata kila kitu katika tamaduni zao. Biblia inaushawishi katika baadhi ya tamaduni kuliko zingine, lakini hakuna tamaduni ya taifa lolote ambalo ni la kikristo kikamilifu.
► Kulingana na kile kulichosoma hadi sasa, ina maanisha nini kwamba wanafunzi wa Yesu’ sio wa ulimwengu?
Wakristo hawafuati tamaa na matamanio ya dhambi. Zaidi ya yote wanataka kumpendeza Mungu. Mapenzi yao yamekuwa na yanazidi kubadilishwa (Wafilipi 1:9-11). Sheria ya Mungu imeandikwa mioyoni mwao (Yeremia 31:33). Amri za Mungu sio nzito kwa wakristo bali wanazifurahia (1 Yohana 5:1-3; Zaburi 19:7-11). Wakristo wana vipaumbele vya milele (Mathayo 6:33). Tabia zao huonyesha wanataka kushinda majaribu na kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi.
Watu wa dunia hufikiri wakristo ni wa ajabu kwa sababu hawavutiwi na vitu vya kidunia kama wao (1 Petro 4:4). Yesu alisema ulimwengu unawachukia watu ambao ni tofauti kiroho (Yohana 17:14). Ulimwengu una uhasau na wale ambao sio wake. Hawaelewi, wanakasirikia haki, na wanahukumiwa na dhambi zao. Ndio maana Yesu alisema “…ulimwenguni mnayo dhiki…” (Yohana 16:33). Mtume Paulo anasema, “Naam, na wote wapendao kuishi Maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” (2 Timotheo 3:12).
► Mwanafunzi asome 2 Wakorintho 6:14-18 kwa niaba ya kikundi.
Biblia huwaeleza wakristo wawe tofauti na dunia. Tofauti hii huanza na mtazamo wa mtu binafsi kama inavyoelezwa na Yesu katika mahubiri ya mlimani. Hapa anaelezea mtazamo wa mkristo kuwa ni mtazamo wa unyenyekevu, kuhuzunika kwa ajili ya dhambi, upole, haki, rehema, usafi wa moyo, amani na kukubali kuvumilia mateso. Mtazamo ulio wa tofauti matokeo yake ni tabia tofauti. Kwa mfano mkristo hawezi kushirikiana na kikundi ambacho kinafanya maovu. Mungu ameahidi kuwa Baba kwa wale wanaoamua kuwa tofauti na ulimwengu. Kumbuka tuliangalia kifungu cha Maandiko kinachosema rafiki wa ulimwengu ni adui wa Mungu (Yakobo 4:4).
► Mwanafunzi asome Mathayo 5:13-16 kwa niaba ya kikundi.
Kuwa tofauti kwa ulimwengu hakumaanishi wakristo kujitenga na jamii na kuanzisha au kutengeneza jamii yao wenyewe. Yesu alisema haombi wanafunzi wake watolewe ulimwenguni (Yohana 17:15). Alisema pia wanafunzi wake ni taa na chumvi ya ulimwengu, hii inamaanisha kwamba lazima ulimwengu uwaone. Mkristo lazima ahusike katika mambo ya serikali na katika maeneo yake katika jamii ispokuwa wakati ambapo atatakiwa kufanya kile ambacho sio sawa.
Gerald Sittser anatuambia jinsi hii ilivyokuwa katika Ukristo wa kwanza:
Aristides, na Athenian wanafilosofia walio… ishi katika karne ya pili waliorodhesha mambo kadhaa ambayo yalionesha tofauti ya Wakristo na halaiki ya watu wengine. Wakristo, walisema, walikuwa na uaminifu, ukweli, kutosheka, heshima kwa wazazi, upendo kwa majirani, utamaawa, uvumilivu wanapokumbana na mateso na ukarimu kwa wageni. Waliwatunza wajane na yatima. Waliwatunza watumwa kwa wema usio na kipimo. “Watumwa wa kike na wa kiume… waliwashawishi kuwa Wakristo kwa upendo waliowaonyesha. Waliofanyika Wakristo, walikuwa ndugu pasipo ubaguzi.”[1]
[1]Gerald L. Sittser. Water from a Deep Well. (Downers Grove: InterVarsity Press, 2007), 54
Imani Halisi
Barua ya Yakobo inasisitiza kwamba Imani ya kweli ya Kikristo hudhihirishwa katika maisha. Yakobo anasema mtu anayesikia neno la Mungu na asilifanye anajidanganya (1:22). Watu wengine hufikiri ni wema kuliko wengine kwa sababu wanajua zaidi ukweli wa kikristo-hata kama hawatii-lakini hiyo siyo kweli.
Yakobo anasema watu wengine ni wa kidini, lakini dini yao haina manufaa. Mungu anapendezwa na dini ya mtu ambaye anakutana na mahitaji ya wengine na anajiweka safi, asichafuliwe na ulimwengu (1:27).
► Mwanafunzi asome Yakobo 2:14-26 kwa niaba ya kikundi.
Kuna watu husema kwa sababu wokovu hupatikana kwa imani na sio kwa matendo, hazijalishi tabia zetu. Wanafikiri kuna uwezekano wa mtu kupata wokovu hata kama nia yake, maisha yake ni kama ya wasioamini. Kifungu hiki cha maandiko katika barua ya Yakobo inaongea kuhusu watu kama hawa.
Yakobo anasema kuamini tu hakutoshi; hata mapepo wanaamini, lakini hawana ushirika na Mungu (aya 19). Mtu amwaminiye Mungu lakini hawezi kunyenyekea ni kama mtu asikiaye injili lakini wala hatubu.
Ni muhimu kueleza mstari wa 21 na 24. Inasema ya kwamba Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, na kwamba mtu anahesabiwa haki kwa matendo pamoja na imani. Maandiko haya ni kama yanakinzana na maandiko ambayo yanaweka mkazo kwamba mtu huokolewa kwa neema sio matendo (Waefeso 2:8-9, Wagalatia 2:16, Warumi 3:28). Yakobo hauanishi kwamba mtu huokolewa kwa imani na matendo lakini mtu huonyesha ameokoka kwa imani na matendo. Yeye haokolewi kwa matendo, lakini kama hataishi kama Mkristo, hana imani iletayo wokovu. Yakobo anasema imani ya mtu imekufa kama maisha yake hayaambatani na hiyo imani (Mstari 26).
Yakobo anasema kwamba haiwezekani mti uwe na aina mbili za matunda au kisima kiwe na aina mbili za maji, mtu hataweza kunena Baraka na laana kwa wakati mmoja (3:9-12). Tabia za mkristo kila wakati zitafanana na imani yake.
Dhana ya Uadilifu
Katika Warumi 2:21-24, Paulo aliongea na Wayahudi waliofikiri wao walikuwa ni bora zaidi kuliko watu wa mataifa kwa sababu walikuwa na maandiko, hata kama hawakuyatii. Akawauliza “wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, waiba mwenyewe?” Akasema, “wewe ujisifuye katika torat, wamvunjia Mungu heshimakwa kuiasi torati.” Ukweli kwamba walijiinua wenyewe kama watu wa dini lakini hawakuwa na tabia nzuri na hii ilifanya mataifa kumtukana Mungu na Maandiko.
Neno uadilifu linatokana na asili ya neno kuunganisha. Kuunganisha humaanisha kulifanya jambo kuwa na mwendelezo au mshikamano unaolingana katika mfumo mzima. Kwa mfano, mtu mwaminifu ataonyesha uaminifu katika mwenendo wake wote na maneno yake. Mtu anayesema yeye ni mwaminifu lakini anatenda kwa udanganyifu, huyu hana uadililifu.
Neno uadilifu linaweza kutumika kwa tabia ya mtu. Katika lugha zingine linatumika kueleza mambo mengine kama vile muundo wa jengo.
► Unafikiri inamaanisha nini muundo wajengo kuwa na uadilifu?
Ni muhimu jengo kusimau. Ni lazima liweze kuhimili uzito wake lenyewe na uzito wa mambo yeyote ambayo hufanyika ndani yake. Ikiporomoka, watu na mali zitamaamia na thamani la jengo itapotea. Uadilifu wa jengo humaanisha ya kwamba kanuni za majengo thabiti lazima zitumike katika ujenzi wote.
Ni vizuri pia jengo lisimame kwa mda mrefu. Mtu ambaye hujenga nyumba hutumaini ya kwamba itasimau Imara kwa muda wote wa Maisha yake. Majengo ya serikali au kampuni hugharimu sana kwa sababu linatarajiwa kusimau kwa vizazi vingi.
Kama jengo litaanza kuegama au kuporomoka ni kwa sababu halina uadilifu. Wakati mwingine jengo huharibiwa na tetemeko la ardhi, ijapokuwa litakuwa limesimama lakini sio salama. Halina uadilifu.
Kabla jengo kuanza ni muhimu kuna ramani ya mchoro uliyo na maelezo. Maelezo ya muhimu ni kwa jinsi gani jengo hilo litakuwa na nguvu na uwezo wa kusimau. Sehemu zote za jengo hilo ni lazima kuunganishwa na kushikamanishwa kwa pamoja.
Ni ya muhimu kwa mjenzi kufuata mchoro anapojenga. Akipunguza gharau kwa kuacha sehemu muhimu za muundo, jengo hilo halitakuwa salau.
► Inamaanisha nini mtu kuwa mwadilifu?
Yesu anatumia mfano wa majengo yenye uadilifu. Anasema mtu anayesikia na kumtii Mungu ni kama mtu ambaye anajenga nyumba yake juu ya mwamba. Hiyo nyumba husimau wakati wa dhoruba. Mtu asiyemtii Mungu ni kama mtu anayejenga nyumba juu ya mchanga. Haitoshi kusikia tu na kujua ukweli.
► Mwanafunzi asome Yakobo 1:22-25 kwa niaba ya kikundi.
Yakobo anasema mtu anajidanganya kama atasikia neno la Mungu na asilitende. anarejelea mtu anayefikiria ni mzuri kwa sababu anajua ukweli katika Biblia japokuwa hafuati wala kuishi kwa huo ukweli. Mtu huyu hana uadilifu.
Yakobo anasema kwamba tunaposoma neno la Mungu tusiwe kama Yule mtu ambaye hujiangalia tu kwenye kioo lakini habadiliki kutokana na kile ambacho anaona. Kweli ya Mungu hubadilisha. Tunapo angalia neno la Mungu tunaona makosa yetu, na tunastahili kumruhusu Roho wa Mungu Abadilishe mienendo na tabia ili zifanane na kweli ya Mungu.
Uadilifu huonyeshwa katika mtindo wa maisha. Mtu hatakiwi kutosheka anapotambua kwamba nia au tabia fulani haiendani na kweli ya Mungu.
Jaribio la Tunda
Yesu alisema kutakuwepo na manabii wengi wa uongo. Hawa ni watu ambao wanataka vyeo vya kidini au wafanye Huduma kama biashara, lakini hawana tabia za Kikristo. Alisema tutawatambua kwa matunda yao (Mathayo 7:15-18). Tunda sio mafanikio. Tunda ni hali ya kawaida ya kuelezea tabia za mti. Tunda la mtu ni maisha yake yakidhihirisha utu wake wa ndani. Endapo mtu hatazaa tunda la Roho (Wagalatia 5:22-23; 1 Wakorintho 13), au anaishi maisha ya dhambi, ana tabia za dhambi na yeye sio kiongozi wa kweli wa kiroho (1 Wakorintho 6:9-10; 2 Wakorintho 11:13-15).
Mtume Petero anasema waumini hawastahili kuongozwa na tamaa za awali za kale bai wanapswa wawe watakatifu kwa vyote wanavyovifanya (1 Petro 1:14-15).
Tunda nzuri halimaanishi kwamba mtu huyo anaelewa vizuri kabisa jinsi ya kutumia kanuni zote za Kikristo katika tabia zake. Sisi sote tuko katika mchakato wa Kujifunza neno la Mungu. Mtoto akiwa anafanya kazi bustanini, kimakosa anaweza kung’oa mimea isiyostahili. Mungu hawezi kutuhukumu kwa makosa tusiyoyajua. Japokuwa, neema haituruhusu kutoomba msamaha kwa makosa tuliyoyafanya. Mtume Yohana anatuambia mtu husafishwa “anapotembea katika mwanga” kuishi sawasawa na ukweli (1 Yohana 1:7).
Uadilifu katika uongozi
Viongozi hufanya maamuzi ambayo wengine sio lazima kuyafanya. Wajibu na nafasi ya kiongozi hutengeneza fursa nyingi za majaribu. Uamuzi wa kiongozi ni wa muhimu kwa sababu unaathiri wengi.
Kiongozi katika huduma lazima akumbuke kwamba yeye, akiufuata mfano wa Yesu, ameitwa kumtumikia Mungu na Watu. Lengo lake lisiwe kuwa maarufu ambaye anasifiwa na kutumikiwa na wengine.
Kama kusanyiko lina watu wengi ambao hawaabudu Mungu katika kweli hubadilisha ibaada kuwa ni kuigiza. Watu hawa huheshimu vipawa kuliko kuwa na mtazamo wa kiroho. Wanapenda ibaada iongozwe kwa watumbuizaji lakini sio viongozi wa kweli wa kiroho. Wanatumbuizwa kimwili. Wako radhi kuwalipa wanamuziki ambao hawajaokoka gharau kubwa ambao wako tayari kupiga muziki katika kumbi za burudani na ambao hawajakidhi vigezo vya kushiriki katika ibaada. Mchungaji lazima alinde ibaada ya kanisa ili kuvutia na kuhudumia Waabudu wa kweli.[1]
► Kama mtu atahudhuria ibaada jumapili asubuhi na awaone wanamuziki walewale ambao aliwaona katika kumbi za burudani jumamosi usiku atafikirije kuhusu kanisa?
Kiongozi anaweza jaribiwa kujitoa katika sheria za kawaida za uadilifu. Baadhi ya wachungaji wengine wana mahusiano mabaya na wanaume au wanawake kanisani kama vile viongozi wa kidunia wanavyofanya. Makanisa mengine huvumilia tabia mbaya kwa wachungaji kwa sababu ya hadhi zao.
Mchungaji anaweza kujaribiwa kuamini kwamba kanisa ni lake. Endapo atafikiria hivi, ataweka watu katika nyadhifa za uongozi kwa sababu wananyenyekea chini yake, na sio kwa sababu wako tayari kufanya kazi nzuri. Aina hii ya mchungaji hupendelea ndugu zake na pia huchagua atakayerithi kanisa baada yake. Yeye hufunika dhambi na makosa ya wale wanao muunga mkono kanisani. Yeye hutumia fedha na mali za Kanisa kama zake binafsi.
Ushahidi wa Kanisa
Kanisa linaweza kuharibika endapo likikosa viwango vya uadilifu. Wakati Kanisa linashiriki katika tamaa za kidunia, wanakubali viongozi walio kama wa kidunia. Wanavumilia dhambi kwa viongozi wao wa dini. Hata Wakristo wa ukweli wanaweza kufuata viongozi waovu kwa sababu hawaelewi umuhimu wa uadilifu na tunda jema. Wakati haya yanafanyika, watu wa kidunia huongoza kanisa na kanisa linapoteza ushuhuda.
Petro anawaonya viongozi waongo wa kiroho ambao wanalifanya Kanisa biashara (2 Petro 2:3). Kanisa likipata umaarufu katika dunia, watu wa kidunia wanapendezwa na kutaka kupata nafasi za uongozi katika hilo kanisa. Wanajifunza mfumo wa ibaada na wanakuwa viongozi wa dini pasipo kuokoka. Kanisa lisilokuwa na mafundisho mazuri haitawatambua.[2]
Yesu anatumia mfano wa chumvi kueleza nini hufanyika wakati kanisa linapopoteza utofauti wake (Mathayo 5:13). Chumvi ikipoteza ladha haina maana ni kama tu mchanga.
Kanisa likiwa kama ulimwengu, kanisa haliwezi kuubadilisha ulimwengu.
Ulimwengu unalidhihaki kanisa pale ambapo kanisa linafuata mtindo wa dunia na halifuati kweli ya maandiko.
[2]2 Petro 2 na kitabu cha Yuda vimeandikwa kwa mada ya viongozi wa kiroho wa uongo.
Kumuwakilisha Mungu
Theolojia ni mfumo wa imani yetu Wakristo, ikijumlisha mafundisho kumhusu Mungu, mwanadamu, dhambi, Kristo na wokovu. Imani yetu kumhusu Mungu ni msingi wa imani zingine zote.
Mungu anapoanza kujidhihirisha, kusudi la kwanza la ufunuo wake ni kuonyesha yeye ni Mungu wa aina gani. Kimsingi Mungu anajieleza kama mtakatifu. Neno la kiebrania la utakatifu (kadosh) limetumika zaidi ya mara 600 katika Agano la Kale. Kwa mfano, Isaya mara kwa mara anamtaja Mungu kama “Mtakatifu wa Israeli”. Utakatifu wa Mungu ndio uliokuwa kusudi la kumuabudu (Zaburi 99:3, 5). Watu wa Mungu hawakumuabudu kwa sababu ya nguvu zake pekee, lakini kwa sababu ya utakatifu wake.
Mungu pia anajidhihirisha kama upendo. Andiko katika agano la kale ambalo laonekana kwa wingi ni wakati Mungu anajidhihirisha kwa Musa na wana wa israeli Kutoka 34:6-7. Hapo Mungu anajidhihirisha kama, “…Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira mwingi wa upendo na ni mwaminifu, huwapenda maelfu na husamehe uasi na dhambi. Japokuwa hataacha dhambi bila kuadhibiwa…” Ni vizuri kuweka utakatifu na upendo wa Mungu pamoja. Neno ambalo hutumika kueleza utakatifu na upendo wa Mungu pamoja ni “upendo - mtakatifu”. Kwa sababu Mungu ni mtakatifu, anatutaka kuwa na utakatifu ndani yetu; kwa sababu Mungu ni upendo ametengeneza njia ya sisi kuwa watakatifu, kama yeye alivyo mtakatifu.
Utakatifu wa Mungu unaonyesha ya kwamba watu hawastahili kumwabudu na kumtumikia kabla kwanza ya kubadilishwa na kufanywa wapya kwa neema. Nabii Isaya aliona kwamba kuna kitu ambacho alikuwa nacho kilichofanana na wenye dhambi aliokuwa anawahubiria – alikuwa na moyo ambao haukuwa safi (Isaya 6:5). “Midomo michafu” iliwakilisha maneno na matendo machafu yaliyotokana na moyo usiosafishwa. Huku kutosafiwa kulimfanya Isaya kutofaa kuwa katika uwepo wa Mungu. Isaya hakubishana na kujifanya kuwa wa kukubalika na pia Mungu hakuidhinisha. Mungu aliitikia ungamo la nabii kwa neema; sio neema ya kuvumilia bali neema ya kutakasa na ya kubadilisha (Isaya 6:6-7).
Mungu wa Israeli alikuwa tofauti na miungu mingine ya uongo na alihitaji ibaada ya tofauti. Katika Zaburi 24 mfalme Daudi anauliza swali “ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?” (mstari 3). Alikuwa anauliza “nani aubaye Mungu humkubali kama mwabudu?” halafu akatoa jibu, “Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe” (aya 4). Sio kila mtu atakubaliwa kumwabudu Mungu. Mwabudu sio tu mtuyule ambaye anaweza kuinua mikono na kupata hisia. Mwenye dhambi hakidhi vigezo.[1]
Mungu alisema utakatifu wake ndio msingi muhimu na unaohitajika kwamba wanomuabudu wawe watakatifu. “Iweni watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:44-45, 19:2, 20:26, 21:8). Mungu hakuwa kama miungu ya mashariki au miungu ya ugiriki ya kisasa au ya dini za kirumi. Simulizi kuhusiana na miungu hawa ilielezwa kuwa ni miungu fisadi, wadanganyifu na wakatili. Miungu hawa walikuwa na udhaifu wote wa kibinadamu. Kama kivuli kwenye ukuta, walikuwa ni uzidisho wa upotovu wa sura ya mwanadamu. Miungu hawa hawakuhitaji kiwango cha maadili au viwango vya mienendo, na waliokuwa wanawaabudu walikuwa wenye dhambi na wakatili.
Mungu wa Israeli sio sura ya mwanadamu iliyo inuliwa. Siyo wa kufikirika, bali amejidhihirisha mwenyewe kwa wanadamu. Yeye ni wa tofauti, na ni kwa sababu hiyo wanaomwabudu lazima wawe tofauti.
Viwango vya Mungu vimerudiwa katika agano jipya: “Bali kama yeye aliyewaita ni Mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:15-16). Mazungumzo ni neno ambalo linaonyesha nia, tabia, mienendo-katika kila nyanja ya maisha. Mungu haitaji tu wanaomwabudu wawe watakatifu kwa muda au waitwe “watakatifu” wakati wao si watakatifu. Anawahitaji wanaomwabudu waishi maisha matakatifu.
Mtazamo wetu na tabia zetu zinaonesha namna tunavyofikiri kumhusu Mungu na ushirika tulio nao na yeye. Mtume Paulo alisema kwamba wayahudi ambao walijivunia kuwa na sheria za Mungu hawakumuheshimu Mungu kwa kuzivunja. Kwa sababu ya tabia zao, watu walisema mambo mabaya kumhusu Mungu wao (Warumi 2:23-24).
Unamuwakilisha Mungu wa aina gani? Watu wanafikiri nini kumhusu Mungu wako? Kama unataka watu wajue Mungu wako ni mtakatifu na pia anasamehe na ni wa neema wanahitaji kukuona wewe ukiwa hivyo.
Makanisa yanahitaji wachungaji wao wafundishe kwa utaratibu mzuri mafundisho sahihi yenye uzima. Mchungaji asipuuze mafundisho ya msingi. Kila kizazi na wakristo wapya wanahitaji kusikia hayo. Hata wakristo waliokomaa wakumbushwe. Mahubiri ya mchungaji sio tu yawe na hisia na yale yanayofanya watu wasisimke. Ni lazima amuelezee Mungu na pia aelezee jinsi maisha ya Wakristo yanavyopaswa kuambatana na maandiko katika kila Nyanja.
Kanisa lazima libadilishe jamii na utamaduni, lakini hii itafanyika tu wakati ambapo dhana za kibiblia kumhusu Mungu itatekelezwa katika kila Nyanja ya Maisha yetu.
[1]Kwa uchunguzi kamilifu wa ibada halisi, tazau Shepherds Global Classroom somo Utangulizi wa Ibada ya Kikristo, inapatikana kwa https://www.shepherdsglobal.org/courses
Kushiriki kwa vikundi
► Katika somo hili, ni mambo gani ni mapya kwako? Ni kwa namna gani kubadilisha mtazamo wako katika maisha ya kikristo?
► Jambo gani ambalo unafikiri linapuuzwa sana katika makanisa katika utamaduni wako? Utaeleza vipi jambo hili kwa mtu unayemjua?
Maombi
Baba wa mbinguni,
Nataka kukuheshimu kwa maisha ambayo yaambatana na tabia zako. Nataka nikuwakilishe wewe katika dunia ambayo haijanyenyekea kwako.
Fanya maisha yangu daima yalingane kweli yako. Nisaidie kukubali kubadilisha jambo lolote ambalo sio sehemu ya maisha ya mkristo
Asante kwa kunipa roho wako anitiaye nguvu na neema ibadilishayo.
Amina
Zoezi la somo la 1
(1) Andika aya moja kuhusu mtazamo wa dunia ambao umeathiri tabia yako na fikra zako hivi karibuni. Tafuta maandiko mawili ambayo yanaongea kuhusu jambo hili na uyaandike. Andika aya moja kuhusu namna ambavyo unaweza kuanza kuishi kwa kutii maandiko hayo.
(2) Soma Tito 2:11-14. Andaa taarifa fupi kuhusu maadili ya mkristo kutokana na andiko hilo. Tumia andiko hilo kueleza kwa nini kweli za Kibiblia zinatakiwa kutendewa kazi katika kila Nyanja ya Maisha. Shirikisha taarifa hii mwanzoni wa darasa lijalo.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.