Ndugu Lawrence alikuwa Mtawa aliyeishi kwenye nyumba ya watawa katika miaka ya 1600. Akawa maarufu kwa kufanya kazi ya kawaida-kuchonga viazi, kuosha vyombo, nk.- kutokana na upendo wake kwa Mungu hakuacha uwepo wa Mungu ukae mbali naye. Wakati wote alimfanya Mungu kuwa katikati ya kila jambo maishani mwake, hata kazini.
The Practice of the Presence of God (Zoezi la uwepo wa Mungu) ni kitabu kidogo ambacho kimesomwa na mamilioni. Kinahusisha mahojiano na barua kutoka kwa ndugu Lawrence. Anaandika, “Utakaso wetu hauegemei kubadilisha kazi, lakini hufanya kile ambacho tunajifanyia kwa uzuri wetu kwa Mungu.”
► Kazi ni nini? Je kazi ni kuajiriwa tu? – kuajiriwa ili ufanye jambo.
Kazi huhusisha kuajiriwa, lakini pia inahusisha kujitunza sisi wenyewe na kutunza wengine, kutunza mali tuliyo nayo, kuzalisha, kufanya biashara kwa faida na kusaidia wengine bure.
► Ni vizuri Mkristo afanye kazi? Kwa nini?
Watu wengi hufikiri ingekuwa vizuri kuwa na pesa ili wasifanye kazi. Wanafikiri maisha yangependeza kama yangekuwa maisha ya kustarehe.
Mtazamo wa Biblia kwa kazi
Fikiri jinsi ambavyo Mungu aliumba ulimwengu hapo mwanzo. Iikuwa kamilifu. Yalikuwa mazingira kamilifu kwa watu wa kwanza ambao Mungu aliwaumba. Mungu alitoa kazi ya kwanza kwa watu. Mungu angeumba dunia iwape wanadamu mahitaji yote pasipo kazi, lakini Mungu alijua maisha bora kwa watu yatahusisha kazi.
Mungu alipanga kazi yetu iwe na uhusiano. Watu lazima wajifunze kushirikiana, kutegemeana, wawe wa kutumainiwa, tutumie nguvu kuwasaidia wengine walio wadhaifu, tukumbane na changamoto pamoja, tutatue kutoelewana, turekebishe makosa, tufundishwe na tufundishe wengine.
Mungu alitupa mamlaka na majukumu ya kuweza kutawala dunia, kuiweka chini ya uongozi na kuikuza kwa utukufu wake. Kazi hii imetuelekeza katika ukulima, ufugaji, uchimbaji wa migodi na uendelevu wa teknolojia.
Mungu alituumba sisi juu ya kila kiumbe maana tuko na kitu katika maumbile yake ndani mwetu. Zaburi 8:6-8 yasema
Umemtawaza juu ya kazi za mikono; umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ngombe wote pia; naam, na wanyama wa kondeni; ndege wa angani na samaki wa baharini; na kila kipitacho njia za baharini.
Kwa sababu ya dhambi ya kwanza dunia ilibadilika, na kazi kujumlisha ugumu na ukataji tamaa ambao haukuwa katika mpango wa kwanza wa Mungu. Hata hivyo, lazima tutambue Mungu ametuumba na tunahitaji kazi.
Kazi yetu ni sawa na kazi ya Mungu ya uumbaji. Kazi ya mwanadamu ni njia moja ya kutengeneza mazingira. Mapato sio kusudi tu la kufanya kazi. Watu wana majukumu ya kubadilisha mazingira. Wanajaribu kufanya bora nyumba zao. Wanajaribu kutupa mbali takataka. Mtu yeyote ambaye hatamani tena kufanya kazi amekata tamaa ya kubadilisha mazingira. Amekata tamaa ya kufanya kile ambacho kinamuanisha kuwa mwanadamu.
► Wewe hufikiria nini ukiona nyumba ambayo haijatunzwa?
Mwanadamu katika hali ya uumbaji, mpangilio, uzalishaji na kufanya kazi ni mojawapo ya sura ya Mungu ndani ya mwanadamu. Kwa hivyo kazi yote ni nzuri kwa mkristo. Kazi yote ni tendo la ibaada ikifanywa kwa kumtukuza Mungu (Wakolosai 3:17, 23). Yesu anasema Baba yake alifanya kazi kwa hivyo yeye pia anafanya kazi (Yohana 5:17).
Usifikiri kazi kama jambo ambalo halipendezi lakini inahitajika, kama vile kutumia dawa ukiwa mgonjwa. Kazi sio tu jambo la maana ili wewe uishi. Ni sehemu ya maumbile ya Mungu kwa wanadamu.
2 Wathesalonike 3:10 yasema, “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwa kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula.”
Tufanye nini kama kazi yetu itaonekana kau isiyo ya maana? Mahatma Gandhi alisema, “Kile ambacho unafanya kinaweza kuonekana sio cha muhimu, lakini ni muhimu sana ukifanye.” Fikiria mtu aliye ajiriwa kufagia sakafu. Ambayo inaonekana sio ya muhimu, lakini anafanya uamuzi mzuri. Wakati anaenda kazini kila siku, anaamua kufanya hiyo kazi kuliko kutumia muda wake kukaa bure, pasipo kuongeza thamani kwa yeyote. Anachagua kuwajibika kwake mwenyewe kuliko awe kupe kwa marafiki na familia. Anasaidia wale ambao wanamtegemea labda mke na watoto, kuliko kuwalazimisha wao wajitafutie msaada. Kwa kuzingatia haya yote inatusaidia kutambua ya kwamba kazi inaweza kuonekana sio ya muhimu, lakini ni muhimu sana kwa sababu alichagua kuifanya.
Je kuna watu ambao hawawezi fanya kazi kwa hakika? Hapana. Hata kama mtu huyu hawezi kuajiriwa kufanya kazi ya mshahara, anaweza fanya kitu kutimiza haja ya mwingine.
Mkristo lazima afanye kazi maana ana majukumu yake na ya wengine. Mtu hastahili kutarajia wengine akutane na mahitaji yake kama hataki kufanya kile ambacho anaweza.
Mwamini ana majukumu ya familia yake kwanza. “Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini” (1 Timotheo 5:8).
Mwamini ameamriwa na maandiko afanye kazi ili akutane na mahitaji ya wengine. “Mwibaji asiibe tena, bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia muhitaji” (Waefeso 4:28). Tambua tofauti kati ya anayeiba, na kuchukua kitu na yule ambaye anafanya kazi ili kwamba aweze kutoa. Mkristo sio mtu tu asiyeiba lakini afanyaye kazi ili atoe.
Unaweza pata kazi hata kama haujaajiriwa na mtu. Tafuta namna ya kuwa msaada kwa mtu ambaye anahitaji. Ni vizuri kuishi namna hiyo kuliko kutofanya kitu na kulalamika kuwa watu hawakusaidii.
Mwamini lazima afanye kazi ajisaidie na asaidie familia na pia wengine walio na mahitaji.
Njia za kawaida za Mungu kukutana na mahitaji yetu
► Utamwambije mtu ambaye husema hatafanya kazi kwa sababu anamtumainia Mungu akutane na mahitaji yake?
Fikiri ya kwamba msimu mmoja wa kiangazi unatembea katika bustani na upate nyanya, mahindi, maharagwe na mboga zimekua na zitakutosha kwa mda mrefu.
Hilo litakaa kama muujiza? Ilifanyika kwa maelfu ya watu wakati wa kiangazi kilichopita. Walitembea katika bustani zao na waka pata hayo yote yamefanyika na zaidi. Lakini hawakushangaa wala kushikwa na butwaa kwa sababu miezi kadhaa kabla, walikuwa wamelima mashamba yao na kupanda mbegu kwa miezi wakamwagia maji na wakapalilia. Kwa hivyo walipopata mimea ni ile tu walicho kutarajia.
Utaonaje, “Basi huo haukuwa muujiza kamwe.” Lakini Mungu alifanya mamilioni ya mbegu na mwanadamu hajafanya hata moja. Zaburi 104:14 yasema, “Huyameesha majani kwa makundi na maboga kwa matumizi ya mwanadamu ili atoe chakula katika nchi” Mungu huyafanya hayo lakini mwanadamu hutayarisha shamba kwa kupanda mbegu, na kunyunyuzia maji wakati unapo hitajika.
Watu wengi hufikiri tendo la Mungu sio la kawaida, pasipo kanuni za dunia za kawaida, kama vile wakati Yesu aliponya au wakati jua lilisimama. Kwa hivyo katika mtazamo huo kukua kwa mimea sio maajabu lakini ni la kawaida.
Lakini katika kutaka muujiza pia tunapuuza njia za Mungu za kawaida za kufanya kazi. Kulikuwa na mamilioni ya watu walio tembea katika bustani zao leo na hawakupata kitu ambacho wengekula. Hawakushirikiana na njia ya Mungu ya kutokeza chakula. Njia ya kukuza chakula ni moja mfano ya kawaida kazi ya Mungu. Kwa mfano njia ya kawaida ya Mungu ya kutupatia ni mwanadamu kufanya kazi. Mithali 14:23 yatufundisha “Katika kazi yote kunayo faida…” pia Mithali 19:15 yatuonya kwamba “…nafsi yake mvivu itaona njaa.”
Kuna watu ambao wanatamani kama Mungu angewafanyia jambo lakini wana puuza nafasi za kufanyia kazi, kwa sababu nafasi hizo sio za kazi ambazo wangependa kufanya.
Na kama unapenda kufanya kazi na hupati mtu wa kukuajiri? Kuna kazi ambayo ungefanya kuwasaidia wengine, na kupitia hiyo baadhi ya mahitaji yako utakutana nayo. Kama hujaajiriwa una wakati. Kwa nini usiangalie hapo karibu na wewe na uone unaweza saidia aje mtu mwingine?
Utaonaje mtu ambaye hajaajiriwa na anatumia masaa yake yote kukaa na hafanyi chochote. Hakuna kitu kabisa cha maana cha yeye kufanya? Katika ujirani wake kuna watu ambao wanahitaji msaada. Kuna takataka ambazo zahitaji kuchukuliwa. Kuna shamba inahitaji kulimwa ili kuleta mazao. Kuna vitabu ambavyo angehitajika kusoma ili aongeze maarifa. Kuna mtu ambaye anaweza kumuombea. Mtu ambaye anakaa kitako na asifanye kitu ana mfanyakazi mmoja, yeye mwenyewe, na mfanyakazi haizalishi au akui. Yeye si mwajiri mzuri way eye mwenyewe, kwa hivyo hatapata nafasi ya kuwaaajiri wengine.
Kwa wakati mwingi na mahali watu hawaajiriwi na wengine. Wanazalisha jambo kwa kubadilisha na lingine, au wanatoa huduma kwa wengine. Hizi ndizo njia Mungu hutupatia.
Kanuni za Maandiko za kuajiri Wakristo
Kanuni ya uwajibikaji na uaminifu hutupa maadili ambayo Wakristo hutumia kazini.
► Mkristo atawezaje kutumia hizi kanuni kazini kwa muajiri wake?
Agano Jipya linatupatia mwelekeo ya wafanyakazi. Wakati ambapo vitabu katika Agano Jipya ziliandikwa wafanyakazi wengi walikuwa watumwa. Mwajiriwa leo anatofauti na mtumwa kiasi kwamba anaweza pata kazi mahali kwingine na aajiriwe. Uhuru huo unawezesha kukubali au kukataa masharti ya ajira. Lakini kama wamekubaliana kufanya kazi pamoja kwa ajili ya manufaa fulani, wanatakiwa na maandiko kuwa watenda kazi wazuri ilimradi tu wabaki na mwajiri wao.
Unaweza kuwa katika hali ambayo haikuruhusu kuchagua kazi utakayo fanya. Labda unalazimishwa kufanya kazi katika mazingira ya kugandamiza. Ni vizuri pia uwe na nia ya mkristo. Watu wengine hufanya kazi kwa upole na vibaya wanapolazimishwa kwa sababu wanataka kuonesha kwamba hawataki kufanya kazi. Mtu akifanya hivyo anaonyesha hana uhuru wa kufanya kazi. Ukitaka kufanya kazi kwa uhuru ni vizuri ufanye kwa furaha na ufanye kazi vizuri. Ukifanya kazi hivyo unafanya ukiwa huru, na hakuna mtu atakulazimisha kufanya hivyo.
Kama hakuna mtu amekuajiri, wewe unajisimamia. Je wewe umekuwa mwajiriwa wa aina gani kwako mwenyewe?
Waefeso 6:5-8 – Kanuni ya majukumu
► Mwanafunzi asome 6:6-8 kwa niaba ya kikundi. Jadili maana ya kifungu, kisha uangalie maana iliyoorodheshwa na ujumlishe kwa yako.
Baadhi ya mambo ya kufanya katika Waefeso 6:6-8:
1. Mfanyakazi anapaswa kumtii mwajiri wake, si tu anapotazamwa, bali wakati wote (…wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo…) Hiyo pia inamaanisha kwamba hapaswi kupuuza maelezo ambayo labda hayatachunguzwa.
2. Mfanyakazi atahifadhi ubora na uadilifu wa kazi kana kwamba anamfanyia Mungu. (“…mkitenda yampendezayo Mungu...”).
3. Mfanyakazi atabarikiwa na Mungu kwa uaminifu kazini (“…atapewa lilo hilo na Bwana...”).
Tito 2:9-10 – Kanuni ya kuwa wa ukweli
► Mwanafunzi asome Tito 2:9-10 kwa niaba ya kikundi. Jadili maana ya fungu, alafu uangalie orodha ilio hapa chini alafu ujumulishe.
Baadhi ya mambo ya kufanya katika Tito 2:9-10:
1. Mfanyi kazi lazima awe na heshima katika anapoelekezwa na mwajiri wake (“...wasiwe wenye kujibu...”). Matokeo ni yapi wakati mfanya kazi ana ongea pasipo heshima kumhusu mwajiri wake?
2. Mfanya kazi asimwibie mwajiri wake, ata kau anafikiri angepewa mshara mnono kidogo (“...wasiwe waibaji...”).
3. Kufanya kazi kwa uaminifu ni ushuhuda kwa injili; kutokuwa mwaminifu ni chukizo kwa injili (“...ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu...”).
► Ni nini baadhi ya mifano ya njia watu hukosa uaminifu kazini? Eleza jinsi ambavyo Mkristo anastahili kuwa tofauti.
Maandiko katika Tito na Waefeso yanasema kuhusu jinsi ambavyo mtu anastahili kufanya kazi anapoajiriwa. Kanuni sawasawa inafanya kazi kwa mtu ambaye ameajiriwa kurekebisha au kujenga kitu fulani. Lazima afanye kazi bora na ya kupendeza kama vile ambavyo angependa mwingine amfanyie kazi. Mtu anayetengeneza bidhaa za kuuza asifiche madhara kwa mnunuzi akifikiri ili kufanya mnunuzi anunue.
Kukuza ubora unaohitajika kuajiriwa
Ni ubora upi ambao mwajiri anataka mwajiriwa awe nao? Utafiti unaonyesha ya kwamba waajiri wanataka watu ambao wana nia nzuri kwa kazi. Wanataka watu wanaoweza kutumainiwa na wako tayari kujifunza. Watu huajiriwa kwa mtazamo wa nia zao kwa kazi zaidi ya mafunzo na talanta. Mungu pia anajali mtazamo wetu kwa kazi kama tulivyo ona katika maandiko tayari.
Kuza mbinu ambazo zitakufanya uwe mfanyakazi anaye thaminiwa. Uwe tayari kutumika, uwe mwaminifu, wa kutumainiwa na mwenye subira. Waajiriwa wengine hufikiri kile ambacho wana hitaji pekee. Mwajiri hakuajiri akusaidie, anakuajiri umsaidie. Lazima uwe mtu ambaye ana thamani kwa mwajiri wake.
Mtu anaweza sema, “Nitakuwa rafiki, wa msaada na mwaminifu kama nitalipwa kwa hiyo, “lakini mwajiri hataajiri mtu ambaye hana urafiki na amlipe awe rafiki. Mwajiri hataajiri mtu asiye aminika ili amlipe awe mwaminifu. Anatafuta kwa mtu mwenye urafiki, wa msaada na mwaminifu ili wamuajiri.
Kanisani mambo ni tofauti hatuwezi subiri mtu awe na urafiki kabla ya kumsaidia. Pia Mungu anakufikia na ana kubariki kabla hujafanya chochote kizuri. Lakini kwa manufaa yako mwenyewe unatakiwa kuanza kumuelekea kwa neema. Jifunze kujitoa na kutumika na tabasamu.
Kuza ubora wako. Jifunze mbinu kwa kufanya kazi na walio na mbinu hizo. Labda unaweza toa huduma kwa wengine. Au unaweza tengeneza bidhaa za kuuza au unaweza kuza mmea fulani. Zaidi ya yote kuwa na nia ya kusaidia wengine hata kama haileti faida kwako. Mungu atabariki huduma yako.
Ina maanisha nini kutumika? Kutumika ni kutumia uwezo wako, wakati, nguvu kwa manufaa ya mtu mwingine.
Kama au haufanyi kazi ya kuajiriwa, huduma inahitaji uweke kando baadhi ya haki zako na faida. Kwa mfano kama unafanya kazi kwa wengine hautaweza kulala kama utakavyo asubuhi, Na huwezi tumia masaa ya kazi kufanya kile ambacho wewe unataka. Itabidi kuweka pembeni mambo kashaa ya maisha yako kwa sababu ya kazi ambayo umeajiriwa. Ajira huathiri hata jinsi ya kuvaa na jinsi unavyo shiriki na watu wengine.
Kuwa tayari kuhudumu kuna faida nyingi:
1. Inatengeneza uhusiano ambapo mahitaji yako hutimizwa. Mara kwa mara hiii hufanyika kwa njia isiyotarajiwa, sio tu katika hali ya kusaidia watu ukitarajia watafanya kitu kwako.
2. Inakupa hadhi katika kanisa, mwili wa Kristo.
3. Itakufanya uwe mtu ambaye mtu atatamani kukuajiri.
Na kama utakuwa na mtazamo mpya-kutafuta njia ya kuhudumia wengine? Yesu akasema, “Ni heri kutoa kuliko kupokea” (Matendo ya Mitume 20:35). Je unaamini hakika hilo? Unaishi kama unavyo amini?
Wafilipi 2:4 inatufundisha kanuni ya kiroho: hatupaswi kuzingatia tu mahitaji yetu wenyewe, lakini tunapaswa kuzingatia mahitaji ya wengine. Pia kuna kanuni ya vitendo. Kumbuka, wale ambao wanaajiri watu kawaida hawafanyi hivo kusaidia watu walioajiriwa. Wanaajiri watu ambao wanaweza kutana na hitaji walio nalo. Kwa hiyo ikiwa mtu anaweza kufikiria tu kile anachotaka mtu amfanyie, huenda hafai kuajiriwa.
Mambo hufanyika wakati watu wana nia ya kufanya kazi. Faida itaonekana kama muujiza kama umefanyika usipo tarajiwa, lakini Mungu ana njia ya kwaida ya kufanya faida hii katika maisha yako.
Ni kupoteza muda unapotarajia, wazia, au pia kuomba Mungu afanye muujiza kama hauko radhi kufanya kazi ili upokee msaada kwa njia ambayo Mungu anapenda.
Kushiriki kwa vikundi
► Mtu anaweza shiriki tukio jinsi ambavyo kazi nzuri kwa mwajiri ilitoa nafasi kwa injili.
► Mtu anaweza shiriki tukio jinsi ambavyo kumsaidia mtu katika maeneo ya jirani ilikuwa ni onyesho zuri kwamba Wakristo hujali.
► Kikundi washiriki pamoja kuhusu nafasi zilizopo kwa mtu ambaye hajaajiriwa.
Maombi
Baba wa mbinguni,
Aasnte kwa nafasi ya kufanya kazi kwa ubunifu. Nisaidie nione nafasi ya kusaidia wengine. Kutana na mahitaji yangu ninapofanya kazi ili nishughulikie haja zangu na za wengine.
Nibariki mimi na rasilimali ili niweze kusaidia familia, nitoe kanisani, na nisaidie wengine kwa mahitaji yao.
Nisaidie niwe mwaminifu na wa kutumainiwa kwa majukumu yangu yote. Niandae kwa nafasi kubwa na majukumu kau hayo ni mapenzi yako. Asante kwa kuwa mwaminifu kila wakati kwangu.
Amina
Zoezi la somo la 3
(1) Soma vifungu vifuatavyo katika Mithali:
Mithali 6:6-11
Mithali 10:4-5
Mithali 12:11, 24, 27
Mithali 13:4, 11
Mithali 14:23
Mithali 18:9
Mithali 20:13
Mithali 22:29
Mithali 24:30-34
Mithali 26:13-16
Andika kurasa ya mambo ya kufanya kuhusu kazi na uzembe kutokana na aya hizo.
(2) Fanya kazi na mwenzako na muandae uwasilishaji katika mada zinazo orodheshwa hapa chini. (Kiongozi wa darasa atapatia kila kikundi mada ya kuwasilisha.) Shiriki uwasilishaji mwanzo wa darasa lijalo.
Kazi na sura ya Mungu katika mwanadamu.
Kazi na majukumu kwa mtu binafsi na wengine.
Jinsi ambavyo waajiriwa wakristo wanapaswa kufanya kazi.(Wasilisho hili lizingatie Waefeso 6:5-8 na Tito 2:9-10.)
Jinsi ambavyo Mungu kawaida huhitimiza mahitaji ya watu
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.