Abraham alifanya kazi katika duka. Siku moja alitambuwa ya kuwa hakumrejeshea mteja chenji halisi. Mteja alikua ameshaondoka. Aliishi maili kadhaa nje ya mji huko vijijini, na Abraham alijua ya kwamba hatamuona tena hivi karibuni. Hata ingawa fedha ilikuwa kidogo alikuwa na wasiwasi kuwa mteja huyo anaweza kuzihitaji. Alitaka pia kuhakikisha kuwa mwanamke asije akafikiri kwamba alikuwa amechukua fedha yake kwa makusudi. Duka lilipofungwa baada ya kazi, Abraham alitembea maili kadhaa kwa ajili ya kurudisha fedha kwa yule mteja. Kwa sababu ya uangalifu wake katika hiyo hali na hata nyakati zingine, marafiki zake walimuita “mwaminifu Abe.” Baadaye alikuwa mwanasheria na kisha akajihusisha na serikali. Uaminifu wake uliheshimiwa na hatimaye akahudumu kama Rais wa Marekani.
Asili Ya Mungu
Biblia inatueleza kuwa Mungu hawezi kusema uongo (Tito 1:2, Waebrania 6:18). Asili yake daima ni thabiti na haibadilki (Yakobo 1:17). Mungu hasemi tu ukweli inapo mletea faida. Hasemi uongo ili kupata matokeo mazuri. Tunaweza kuwa na Imani kuwa neno la mungu ni kweli kabisa na la kutegemewa. Ukweli wake unatupa Uhakika (Zaburi 40:11, Zaburi 91:4).
► Je, mahusiano yako na Mungu yataathiriwa vipi ikiwa humwamini kwa kusema ukweli nyakati zote?
Fikiria kuhusu vile ukweli ni wa muhimu katika uhusiano wetu na mungu. Mungu anatuita tujitoe kwake kabisa. Hatuwezi kufanya hivyo ikiwa hatumwamini kabisa.
Viwango vya Mungu vya Kweli
Mungu anataka tuseme ukweli kila wakati. Mtu anayesema uongo sio mwadilifu machoni pa Mungu (Mithali 12:17).
Wakati mwingine watu husema uongo kushinda kesi mahakamani. Watu walio na fedha wanaweza kumlipa hakimu kukubali uongo ili waweze kuchukua mali kutoka kwa wengine (Yakobo 2:6). Watu wenye mali huepuka hukumu na kuwafunga watu wasio na hatia kwa kulipa hongo ili kuanzisha uongo (Yakobo 5:1, 6).
Ni dhambi kushuhudia uongo, hata kama ukifiria sababu yako kuwa ni sawa. Biblia inashutumu mashidi wa uongo na hairuhusu ubaguzi (Kutoka 20:16, Mithali 6:16-19, Mithali 14:25, Mithali 19:5, 9). Watu wengi wanafikiri kuwa unaweza kusema uongo kama uongo utasaidia kuleta mema bila kusasabisha madhara. Lakini Biblia haijatupa chaguo hilo. Hatujaelezwa kwenye maandiko kwamba kuna wakati tunaweza kusema uwongo.
Wakristo wanapaswa kuongea ukweli bila kujali mazingira. Ukweli ni muhimu kwa uhusiano yetu.
Waefeso 4:15 inasema kwamba kusema ukweli ni muhimu kwa ukuaji hadi ukomavu wa kiroho.
Wakolosai 3:9 inasema kwamba kusema uongo ni sehemu ya maisha ya dhambi ambayo tumetoka.
Mungu atawahukumu wale wasemao uongo. Waongo Wamejumuishwa kwenye orodha ya watenda dhambi wabaya waliohukumiwa na sheria ya Mungu (1 Timotheo 1:10, Ufunuo 22:15). Wasema uongo wote watatupwa kwenye jehanamu ya moto (Ufunuo 21:8). Waongo hawataingia katika mji wa Mungu (Ufunuo 21:27).
Kutumia Ukweli Kwenye Biashara na Mahusiano
► Mwanafunzi asome Mithali 11:1 kwa niaba ya kikundi.
Mstari huu unaongea kuhusu mizani ambazo hutumika kupima uzito wa kitu, kama vile matunda au mboga au nyama. Wakati mwingine watu wana mizani ambazo zimeundwa ili kutoa uzito usio sahihi ili mfanyabiashra aweze kupata fedha za ziada. Huu Mstari unatukumbusha kuwa Mungu anachukia vitendo vyote vya kutokuwa na uaminifu.
Ni makosa kwa mtu kuuza kitu huku akisema uongo kuhusu hali ya kitu au kuficha kasoro zake. Ni makosa kusema uongo unapoeleza mtu kiasi cha fedha ulichonunulia ili kukiuuza kwa bei ya juu.
Sio vyema kutia sahihi ya jina kwa kitu ambacho sio kweli ili kuepuka kulipa fedha. Sio vyema kwa mtu kumsaidia mwajiri wake kudanganya watu kwa faida.
► Je, ni aina gani mbalimbali za ukosefu wa uamanifu umewahi kuziona?
Biblia inasema kuwa watu waovu hukopa na hawalipi (Zaburi:21, Mithali 3:28). Baadhi ya watu hukopa na wanahisi kuwa hawana jukumu la kulipa deni lao. Biblia inasema kuwa lazima tuhakikishe kuwa hatukosi kuwapa wengine kile wanachotudai (Warumi 13:7-8).
Uaminifu inamaanisha kuwa unatimiza ahadi yako na kujitoa. Zaburi 15 inaeleza mtu aliye na uhusiano mzuri na Mungu. Sifa moja ni kuwa huyo mtu anatoa ahadi na kuitimiza hata ikiwa ni gharama kwake (Zaburi 15:4).
Ni kukosa uaminifu wakati mtu hafanyi kazi kama navyostahili kwa mtu aliyemwajiri (Waefeso 6:5-6).
Ni Makosa kwa mfanyakazi kumuibia mwajiri wake (Tito 2:9-10).
Ni makossa kutoa risiti za uongo kuonyesha kitu kina gharama ya juu kuliko ilivyokuwa. Ni makosa kwa mfanyakazi au wakala kusema uongo kuhusu bei ya kitu ili aweze kupata kiasi fulani cha fedha.
Ni makosa kwa mwajiri kuwanyima wafanyakazi mishara iliyoahadiwa (Yakobo 5:4).
Ni makossa kuchukua kitu ambacho mtu mwingine amekipoteza kwa bahati mbaya. Unapaswa kukirudisha kwa mmiliki kama inavyowezekana (Kumbukumbu la Torati 22:1).
Kama wewe ni meneja wa rasilimali za mtu mwingine (Kama vile mwajiri au huduma), ni makosa kutumia fedha au vitu vya kazi kwa sababu za kibinafsi kama haujapewa ruhusa.
Kielezo cha Changamoto za kitamaduni kwa Uaminifu
Katika baadhi ya jamii watu wanaishi chini ya uangalizi wa chifu. Watu ni waaminifu kwa chifu, na chifu anatarajia kuwasaidia kwa kila hitaji. Katika hizi jamii watu wengi hawana mali ya kibinafsi. Rasilimali muhimu kama vile ardhi ni mali ya jamii. Viongozi wanahitajika kusimamia rasilimali kwa faida ya kila mtu. Mtu anapokuwa na hitaji, anahisi kuwa ana haki kuchukuwa chochote atakacho kutoka kwenye rasilimali ya jamii.
Gerald alizaliwa Kijiji cha msituni. Familia yake na nyinginezo karibu nao walilima mazao ya chakula kwenye ardhi iliyokuwa mali ya Kijiji. Walipata rasilimali kwenye msitu. Hakuna yeyote aliyemiliki ardhi kibinafsi hata sehemu ambazo nyumba zilikuwa zimejengwa. Familia zilisaidiana kulipotokea shida. Chifu alikuwa kama baba kwa Kijiji. Watu walitarajia kuwa atatimiza mahitaji yao.
Wakati Gerald alipokuwa kijana alipata kazi na kampuni iliyokuwa inakata miti kutoka kwenye msitu. Aliondoka kijijini kuenda kuishi karibu na sehemu ya kazi. Alilipwa mshahara kila mwezi. Kuna wakati ambao hakukuwa na chakula cha kutosha kwa sababu hakukuwa na mazoea ya kupanga bajeti ya mshahara wake. Alitarajia mwajiri wake ampe chakula na alishangaa wakati mwajiri alipomuambia kuwa ni jukumu lake kama mfanyakazi kununua kila kitu kutoka kwenye mshahara wake. Wakati dada yake na Gerald alipohitaji huduma za daktari na Gerald alimuomba mwaajiri fedha kwa ajili ya dada yake. Geraald alikasirika pale mwajiri aliposhindwa kuwa wa msaada kwake. Gerald alifikiri kuwa mwajiri wake angemsaidia katika shida zake, lakini mwajiri akasema mshara ndio jukumu lake la pekee kwa Gerald. Wakati Gerald alipoacha kazi, aliiba baadhi ya vifaa vya kazi ili avipeleke kwenye Kijiji, kwa sababu alihisi kuwa mwajiri hakumsaidia vya kutosha.
Gerald baadaye alihamia mjini na mke na mtoto wake na akapata kazi kwenye duka la kuuza vitu vya chakula. Gerald alimuoma mwajiri wake kulipa karo ya shule ya mtoto wake lakini mwajiri hakufanya hivyo. Wakati fulani Gerald hakuwa na fedha za kutosha za kununua kila kitu ambacho familia yake ilikuwa inahitaji. Kwa sababu alifanya kazi kwenye duka ambalo lilkuwa linauza chakula, alidhani kuwa anastahili kuruhusiwa kuchukuwa chakula kutoka kwenye duka kwa ajili ya familia yake. Alijua kwamba mwajiri wake hangekubali, kwa hivyo akachukua chakula kwa siri.
Kuna baadhi ya wafanyikazi hawaelewi mipaka ya ahadi ya waajiri. Wanadhani kuwa waajiri wanajukumu la mahitaji yao yote. Wanaomba misaada ya aina nyingi zaidi ya mishara ya kazi yao. Wasipopewa kile wanahitaji, wanaona kuwa wana haki kuiba kwa sababu wanahisi ana deni kwao kwa vitu wanavyohijitaji.
► Mwanfunzi asome Tito 2:9-14 kwa niaba ya kikundi.
Mistari hii inatueleza kuwa mfanyakazi hapaswi kuiba kutoka kwa mwajiri wake. Mstari wa 10 unasema kuwa mwaminifu kunafanya Mafundisho ya Kikristo yawe na maana sana. Mistari ya mbele inaeleza maisha ya mtu aliyebadilishwa kwa neema.
Kutegemewa
Uaminifu sio tu kuhusu fedha na kumiliki.
Carlos aliahidi rafiki wake kwamba atamkuta 8.00 asubuhi. Hata hivyo alilala kwa kuchelewa na ikamchukuwa muda kupata chakula cha asubuhi. Alichelewa zaidi ya saa moja. alimwambia rafiki yake kuwa dereva wake amechelewa kuja kumchukua. Rafiki yake hakushangazwa. Marafiki wa carlos walijua kuwa yeye sio mwaminifu kwa ahadi zake.
Carlos hakukuwa na uamninfu kwa njia mbili:
1. Hakuweka au kuwa muaminifu kwa ahadi zake.
2. Alisema uongo kuhusiana na sababu zilizomfanya achelewe.
Watu wanaweza kukuamini unaposema kuwa utafanya kazi au utakuwa sehemu fulani? Je unajiamini unaposema haya? Unapoahidi kitu, unaahidi kuwa utafanya kila uwezalo kutimiza? Ni makosa kuahidi kitu halafu ukose kufanya bidii kutimiza ahadi yako.
Unaposhindwa kutimiza ahadi, ni vyema kuomba msamaha. Usiseme uongo kuhusiana na sababu zilizofanya ushindwe kutimiza ahadi.
Ni makosa kulaumu wengine kwenye shirika au kampuni kwa sababu ya makosa yako. Watu ambao mnafanya kazi nao kwa karibu hawatakuamini wakijua ya kwamba utasema uongo kuhusu makosa yako.
Kiongozi mwaminifu hawapatii watu wazo lake kwa kuwaambia mambo ambayo si ya kweli. Steven Covey aliandika kuwa “Uongozi ni kupata matokeo kwa njia inayohusisha uamininifu.”[1]
[1]Stephen M. R. Covey. The Speed of Trust: The One Thing That Changes Everything. (New York: Free Press, 2006).
Sababu ya Uhusiano
Watu wengi wanaamini kuwa ni makossa kusema uongo kwa marafiki au watu unaowafahamu lakini sio makosa kusema uongo kwa makundi mengine ya watu. Baadhi ya watu huiba fedha au mali nyingine kutoka kwa waajiri wao kwa sababu wanafikiri kwamba wanastahili kulibwa zaidi. Wengine wanawaibia watu matajiri hasa matajiri walio wageni. Watu wengine wanawafanyia vitendo visivyo haki watu kutoka makundi tofauti ya kikabila au tabaka la kijamii.
Yesu alisema tuwapende jirani yetu kama vile tunajipenda sisi wenyewe. Kumbuka swali ambalo mwanasheria alimuuliza Yesu? “Je, jirani yangu ni nani?” (Luka 10:29). Mwanasheria alitaka Yesu abainishe vikundi vya watu ambao wangependwa. Yesu alitoa hadithi ya” Msamaria Mwema.” Hadithi hiyo inahusu watu wawili kutoka makabila tofauti waliokutakana kwa mara ya kwanza. Hawakuwa na uhusiano hapo awali, na kulikuwa na mzozo kati ya makabila hayo mawaili. Msamaria alimsaidia mwanaume aliyekuwa na hitaji hata ingawa hakulazimishwa na uhusiano wowote. Jambo moja Yesu alifanya kwenye hadithi ni kuwa mtu yeyote asitengwe kutoka kwenye upendo wetu.
Hatutakiwi kuamua ni nani anastahili uaminifu wetu. Hatupaswi tuwe waaminifu tu na wale wachache tunaowachagua. Hata tukijua ya kwamba mtu hataadhirika na ukosefu wa uaminifu wetu, tunataka tumfurahishe Mungu kwa kuwa waaminifu (Matendo ya Mitume 24:16, pia Wafilipi 1:10, 2 Wakorintho 5:9).
Wewe ungependa uwe mtu wa aina gani? Mungu angependa uwe mtu wa aina gani?
Mtu anaweza asistahili heshima yako, lakini Mungu anataka uwe mtu wa heshima. Mtu anaweza kuwa hastahili uaminifu wako, lakini Mungu anataka uwe mtu wa uaminifu. Mtu anaweza kuwa hastahili upendo wako, lakini Mungu alikupenda wakati haukustahili, na anataka uwe mtu wa upendo.
► Mwanafunzi asome 1 Petro 2:21-23 na 3: 8-12 kwa niaba ya kikundi.
Usiruhusu tabia au sifa ya wengine kuamua tabia au sifa yako. Mtu anaweza sema uongo kwako, lakini wewe usiwe mwenye kusema uongo. Mtu anaweza kukuibia, lakini hiyo isilkufanye uwe mwizi. Mtu anaweza kuwa mwenye kiburi kwako, lakini wewe uwe mtu wa heshima.
Vielelezo kutoka katika Maisha
Vielelezo katika sehemu hii ni visa halisi, lakini majina na maelezo yamebadilishwa. Ni baadhi ya mifano ya kuiba, kusema uongo au zote mbili.
Kwa kiongozi wa darasa: Hakikisha wanafunzi wanaelewa kile kilichofanyika katika kila kielelezo. Waulize wanafunzi kueleza kwa nini kitendo katika kielelezo ni kosa.
1. George alifanya kazi kwenye kiwanda. Mara kwa mara alichukua vifaa vya kusafishia nyumbani, vyombo au zana na vitu vingine vidogo kwa sababu alijua kuwa kiwanda kitanunua vitu hivyo.
2. Amani alikuwa dereva wa lori la mizigo wa kampuni kubwa. Wakati alipokuwa anaendesha gari la kampuni angeona ishara kando ya barabara iliyosema “Tunanuna mafuta ya diesel.” Kuna wakati mwingine angesimamisha gari na kuwauzia mafuta kidogo kutoka kwenye lori, akijua kwamba kampuni isingejua kuwa mafuta kiasi kidogo yalikuwa yametolewa.
3. Tamaara aliaminiwa kunua mtambo wa kompyuta kwa ajili ya ofisi ambapo alikuwa anafanya kazi. Alimpa hongo muuzaji kwenye duka ili aandike risiti inaonyesha bei ya juu ili aweze kuchukua baadhi ya fedha.
4. Kwenye bustani katika jiji kubwa, mwanamume mmoja anauza balbu za mwanga ambazo hazifanyi kazi au kuisha nguvu. Wanunuzi wanajua kwamba hazifanyi kazi. Wanazinunua ili kuzipeleka ofisini ambako wataiba balbu nzuri na kuzibadilisha na hizi za zamani.
5. Alex alikuwa mkuu wa shule. Siku mmoja baba mzazi wa mwanfunzi alikuja kwake na akitaka kijana wake apewe daraja nzuri kwenye masomo ya algebra. Alipmatia Alex fedha. Alex aliamuru mwalimu wa algebra ampe mwanafunzi alama nzuri.
6. Angelo alikuwa profesa kwenye chuo kikuu. Mshahara wake ulikuwa mdogo. Aliwaambia wanafunzi katika darasa lake kuwa mtihani utakuwa mgumu na kuwa hakuna mwanafunzi atakayefanya vizuri katika mtihani bila hao kunua kutoka kwake ukurasa wenye majibu.
7. Samson alikuwa mkuu wa shule ya serikali. Siku moja Yakobo, anayefanya kazi na shirika la kimishonari akamuuliza kama shirika la kimishonari lingekodi vyumba kwenye jengo la shule. Samson akatoa bei, na Yakobo akaleta fedha kila mwisho wa mwezi. Samson aliweka hizo fedha kwa siri bila kutoa ripoti ya mapato.
8. Yakobo alifanya kazi na shirika la kimishonari ambalo lilihitaji kukodi nafasi za madarasa. Yakobo alienda kwa Rafiki yake Samson, mkuu wa shule. Wakukubaliana bei ya kukodi madarasa, halafu Yakobo akaenda kwenye shirika lake akataja bei ya juu. Kila mwezi Yakobo alimletea Samson fedha lakini alibaki na fedha za ziada.
9. Masanja alifanya kazi na huduma fulani ambayo ilihitaji jengo jipya. Hilo shirika lilimpa Masanja jukumu la kutafuta kampuni ya ujenzi kwa ajili ya kazi ya ujenzi. Masanja aliongea na kampuni mbalimbali za ujenzi. Badala ya kuchagua kampuni ambayo ingewapa bei iliyo bora zaidi, yeye alichagua ile kampuni ambayo iliahidi kumpa baadhi ya fedha ambazo wangepata kutoka kwa shirika.
10. Alisante alihitaji kulitafutia gari lake leseni. Lakini alijua ya kuwa gari lake lisingefikia viwango vya ukaguzi kwa sababu baadhi ya taa zilikuwa hazifanyi kazi. Alilipeleka gari kwenye idara ya ukaguzi na akaona foleni ndefu ya watu ambao walikuwa wameleta magari yao yakaguliwe, Mtu moja karibu na lango akamwambia kuwa, kwa kiwango fulani cha fedha ataweza kumsaidia apate leseni kwa haraka bila ukaguzi wa gari. Alisante alilipa fedha na muda sio mrefu akapata leseni na kaondoka kwenda nyumbani.
11. Simoni alikuja kuchukua gari lake kutoka eneo la kuegesha magari. Mhudumu wa maegesho alimwambia bei ya kugesha. Simon alimpa mhudumu fedha kidogo kuliko ada ya kawaida lakini akamuruhusu kutunza tiketi ya kuegesha ambayo angeweza kumpatia mteja mwingine ili aweze kuitumia na mhudumu angebaki na fedha ambazo amelipwa na Simoni.
12. Anna hakujianda vya kutosha kwa ajili ya mtihani. Alipokuja darasani alikaa karibu na mwanafunsi aliyekuwa mwanafunzi bora ili aweze kunakili majibu ya mtihani kutoka kwa rafiki yake.
13. Kajiala aliendesha trekta iliyokuwa ikivuta majembe ya kulima kwenye shamba kubwa la serikali. Alitaka kumaliza kazi mapema. Aliinua jembe ili lisiwe chini sana na kumfanya aendeshe trekta kwa haraka. Shamba lilionekana kuwa tayari, lakini halikuweza kukuza mimea mizuri kwa sababu halikulimwa vizuri.
14. Mchungaji Amos alitumwa na misheni ya kanisa kuwa mchungaji wa kanisa. Misheni ilimtumia mshahara kila mwezi. Kwa sababu mchungaji Amos alitaka kanisa limlipe pia, aliwambia washirika wa kanisa hilo kuwa misheni haimpi msaada wowowte.
15. Mwizi alikuja kwa nyumba ya Abihudi na akaiba fedha. Alipowaeleza rafiki zake kuhusu yaliyotendeka, alisema mwizi aliiba vitu vingine ingawa huo haukuwa ukweli. Rafiki zake walimuhurumia kwa kumpa fedha kununua vitu ambavyo walidhani vilikuwa vimeibiwa.
16. Chalamila alikua chifu wa Kijiji kidogo. Alikuwa kiongozi katika kanisa la Kijiji. Watu wake walikuwa wa kale, wasio na elimu na maskini ingawa Kijiji kilikuwa kilikuwa na ardhi kubwa. Wafanyabiashara kutoka mjini walitaka kununua ardhi kwa ajili ya miradi ya ukulima. Chalamila aliuza ardhi yote ya Kijiji na akatumia fedha kujijengea nyumba huko mjini.
17. Kila mwaka Kanisa la Fairfield Community huchagua mama mmoja kumtuza kama “mama wa mwaka.” Walimchagua Sara, sio kwa sababu alikuwa na sifa nzuri kama mama, lakini ni kwa sababu walijua atachangia fedha kwa kanisa. Baada ya kutuzwa, Sara alichangia fedha kanisani kwa ajili ya kununua milango mipya kwa ajili ya mali ya kanisa. Mwaka uliofuata kanisa liliamua kumteua tena Sara kama mama wa Mwaka hata ingawa alikuwa amehamia jiji lingine.
18. Hango alikuwa dereva katika huduma fulani. Kila jioni alichukuwa gari la kazi na kuliegesha sehemu yenye ulinzi. Wakati mwingine kabla ya kuegesha gari alikuwa analitumia kubeba abiria na mizigo kama wateja wake wakibinafsi.
Janga la kitaifa la Ukosefu wa Uaminifu
Hii hadithi ni ya kubuni lakini inaeleza kile kinachofanyika sehemu nyingi.
Wakristo katika jiji la Borol walitambua kuwa kulikuwa na jamii kubwa ya watu katika eneo jirani ambao walikuwa wanaishi kwa umaskini. Watu wa hilo eneo walikuwa wa kabila liitwalo Ibanese. Kwa vizazi watu wa Ibanese waliishi maisha ya kale sana katika nyumba zao bila kufikiwa na huduma za afya au masomo. Wengi hawakuwa na chakula cha kutosha na baadhi yao walikuwa na njaa.
Wakristo wa Borol walianza kutoa fedha kusaidia Waibanese. Walituma wawakilishi wao kwa makanisa kwenye maeneo mengine kuomba michango.
Wakristo wa Borol walianza kupeleka msaada wa chakula kwa Ibanese kutumia lori za mizigo. Walianza kutegemea viongozi wa kanisa la Ibanese kusambaza chakula.
Viongozi wa Ibanese walianzisha masoko ya kuuza chakula kwa watu wao. Watu wenye fedha pekee ndio walikua na uwezo wa kununua. Kwa hivyo hakuna chakula chochote kiliweza kuwafikia watu ambao walikua na njaa. Viongozi wa kanisa na marafiki zao walichukua faida. Baadhi ya chakula kilipelekwa kwenye maeneo mengine kuuzwa ambako mapato yalikuwa ya juu.
Wakristo wa Borol walisisitiza kuwa chakula lazima kipewe bure kwa wale ambao walikihitaji sana. Viongozi wa kanisa pale Ibanese walitengeneza bajeti ya kusambaza ambayo ilijumuisha kukodi lori la mizigo na madereva na kulipa watu wa kusaidia. Walipanga bei kuwa juu kuliko kawaida na kuchukua fedha za ziada. Wakristo wa Borol walipohitaji ripoti za matumizi, waibanese walitoa ripoti za uongo.
Kila wakati wakristo wa Borol walipogundua vitendo vya kukosa uaminifu, walikata tamaa na kushushwa moyo. Walipojaribu kutafuta tafuta viongozi wengine kutoka kwa jamii ya Ibanese kuwasaidia lakini walikabiliana na shida hiyo hiyo. Wakristo wengi wa Borol waliaacha kutoa. Wengine waliendelea kutoa. Muda sio mrefu wachungaji wachache wa Ibanese walikuwa na magari na nyumba nzuri kwa sababu ya msaada kutoka Borol. Wachungaji wengine wakaanza kuwaonea wivu na wakatamani mahusiano na watoaji wa Borol. Wale ambao walikuwa na njaa maeneo ya mbali hawakupata msaada wowote.
Kielelezo Cha Kuhitimisha
Warren Buffet alikuwa mkurugenzi mtendaji kwenye kampuni iitwayo Berkshire Hathaway. Alitaka kunua kampuni iitwayo McLane Distribution ambayo ilikuwa inamilikiwa na Walmart. Bei ya kununuliwa ilikuwa dollar bilioni 23. Kwa kawaida ununuzi huu ulihitaji miezi ya ukaguzi ndiyo mnunuzi aweze kuangalia na kukagua kila kitu. Buffet alikutana na viongozi wa Walmart na wakawa na makubaliano kwenye kikao kimoja. Hakutuma mtu kuhakikisha kuwa mali zilikuwa sawa. Baadaye alisema, “Tulijua kuwa kila kitu kilikuwa sawa kwa vile Walmart walisema itakuwa na ikawa.” Huu Mpango mkubwa wa kibiashara ulimalizika kwa haraka kwa sababu viongozi waliaminiana.[1]
Sasa jaribu kufikiri kuhusu viongozi tuliowaangazia kwenye kielelezo cha awali. Hakuna mmoja wao ambaye anaweza kufanya maafikiano kama haya, kwa sababu sio wakuaminiwa. Kila kitu lazima kikaguliwa ni hiyo inachukuwa muda mrefu sana na gharama kubwa.
[1]Stephen M. R. Covey. The Speed of Trust: The One Thing That Changes Everything. (New York: Free Press, 2006), 15
Kushiriki kwa vikundi
► Ni baadhi ya mazoea gani ya kukosa uaminifu ambayo ni vigumu kwa watu kuepuka katika utamaduni na mila ya kwako?
► Ni Mazoea gani unapswa kubadilisha?
Maombi
Baba wa mbiguni,
Tunakusifu kwa kuwa Mungu wa uadilifu na ukweli. Tunakushukuru kwa kuwa wakati wote wewe ni mwenye ukwelli kwenye shughuli zako na sisi.
Tusaidie tufuate viwango vya uamnifu ambao unavyo kwa ajili yetu.Tusaidie tutumie katika Maisha yetu ya kila siku kanuni za uaminifu kwa kila tusemalo na kufanya.
Ahsante kwa kuwa kuwa Baba yetu ambaye hutoa na kutuongoza. Tunataka tukuamini kuwa utatutunza.
Amina
Zoezi la somo la 10
(1) Andika aya kuhusu kila moja ya yafuatayo:
Eleza uhusiano kati ya sifa ya Mungu (ukweli) na viwango vya Mungu kwetu (uaminifu). Eleza kwa nini Mungu anahitaji sisi tuwe waaminifu kwa yale tunayosema na katika shughuli zetu zote.
Kwa ufupi eleza kile ambacho Biblia inasema kuhusu uaminifu. Tumia angalau maandiko matatu kwa mafupisho yako.
Eleza angalau njia nne ambazo uaminifu au udanganyifu huathiri uhusiano wetu na wengine.
(2) Jiandae kufanya uwasilishaji wa kibiblia kuhusu uaminifu ambao unaweza kushiriki na kikundi kutoka utamaduni au mila yako.Toa msingi wa kibiblia kwa msimamo wa Mungu una kisha uonyeshe matumizi wenye mifano mahususi.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.