Hernando Cortes sio mfano mzuri ambao tunaweza kuuiga katika tabia na makusudio. Hata hivyo tendo lake moja linaonesha kujikita kikamilifu kwa malengo yake. Katika majira ya baridi ya mwaka 1519, Hernando Cortes aliongoza msafara wa kijeshi wa kuiteka nchi ambayo sasa inaitwa Mexico. Serikali ya Uhispania ilifadhili misheni hiyo kwa kuwapa meli kumi na moja na wanaume mia saba. Baada ya miezi kadhaa katika bahari Cortes na wanaume wake walifika katika fukwe za Mexico. Changamoto iliyo fuata ilikuwa ni kuvuka miji hadi jiji kuu. Cortes alijua kwamba kutembea katika nchi kavu ilikuwa ngumu na hatari. Alitaka wanaume wake wajue ya kwamba kurudi nyuma isingewezekana kamwe kwa hivyo akachoma moto meli zote. Akafanya njia ya kurudi Uhispania kutowezekana na wakati huo huo akawapa wale wanaume hamasa kubwa ya kufaulu. Vivyo hivyo, kila mtu anayeingia katika ndoa lazima ajue ya kwamba hakuna kurudi nyuma.
Utangulizi
Ndoa ya kimaandiko ni nzuri sana.[1] Lakini wapendanao wakitaka kupata uzuri na kufurahia wema wake lazima wayachunguze maandiko jinsi yanavyosema kuhusu ndoa, na kufuata na kutii walichojifunza. Ndoa ambayo yatosheleza yahitaji kujitoa na bidiii kubwa.
Ili uweze kuielewa ndoa tunatakiwa kurudi mwanzo katika hadithi ya uumbaji. Habari ya uumbaji itatufundisha kuhusiana na ndoa.
► Je kuna mtu anaweza kutushirikisha kuhusiana na jinsi ambavo aliingia katika ndoa akitarajia faida bila kujua ya kwamba kujitoa ni kwa muhimu?
“Bwana Mungu aksema si vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwanzo 2:18).
Kama jins ambavyo Mungu ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu walivyo katika ushirika, Mungu alituumba sisi tuwe wa ushirika. Tuliumbwa tuwasiliane. Tuliumbwa kwa ajili ya urafiki wa karibu na ushirika. Mungu akasaema kuwa pekee sio nzuri!
Kila sehemu ya mwanzo inaonyesha kwamba Mungu aliipa heshima ndoa. Mungu alichukua ubavu kutoka kwa mwanaume na akamfanyia mwenzake mrembo, na “akaletwa kwa heshima kwa mwanaume kama kazi iliyo bora zaidi ya mwisho ya Muumbaji. Kila hatua na kiwango katika maelezo inakusudiwa kuinua hadhi ya ndoa.”[1] “Neno (“akamletea”) linaonesha kukabidhiwa kwake katika vifungo vya agano la ndoa, ambalo linaitwa agano la Mungu (Mithali 2:17).”[2]
Ndoa inapaswa kuwa ya umoja ulio na furaha.
Wakati Adamu aliposema, “Huyu sasa ni mfupa katika mifupa yangu…” (2:23) alikuwa anaonyesha heshima na furaha. Adamu hakusema “mwishowe, nimepata mtumwa! Nimepata mtu wa kunifulia, kunipikia chakula, kunikanda mgongo na kufanya kazi zanguza nyumbani!” Hapana, Adamu alisema “hatimaye nimepata anaye fanana na mimi!”
Ndoa inapaswa kuwa ya Umoja wa Usawa.
“BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (2:18).
Matthew Henry anatukumbusha sisi, “Mwanamke aliumbwa kutokana na ubavu wa Adamu; siyo kutoka kichwani amtawale, siyo kutoka miguuni, ili amkanyage, bali kutoka ubavuni mwake ili awe sawa na yeye, chini ya mkono wake kulindwa, na karibu na moyo wake kupendwa.”[3] Adam Clarke anasema, “Alipaswa kuwa mfano kamili wa mwanaume, bila kuwa duni wala bora zaidi, bali akiwa sawa naye katika mambo yote.
Ndoa inapaswa kuwa ya Muungano wa Agano.
“Kwa hivyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (2:24). Ndoa zilizo simama imara hazitegemei hisia za mapenzi au mahaba, (hisia za mapenzi huja na huondoka) au raha (ijapokuwa ndoa iliyo na afya huleta furaha), au kutosheka kwa mtu (ingawa ndoa zenye nguvu zinztosheleza). Faida zilizozopo katika ndoa hazisababishi ndoa kuwa imara; bali zinatokana na ndoa Imara. Ndoa hujengwa katika msingi wa maagano ya mwanaume na mwanamke mmoja kila mmoja akijitolea kwa kipekee kwa mwenzake Maisha yao yote.
Ndoa inapaswa kuwa ya uwazi, kuaminiana, na uhusiano wa kukubaliana – “nao walikuwa uchi wote wawili, Adam na mkewe, wala hawakuona haya” (2:25). Kwa sababu dhambi ilikuwa bado haijaharibu hali ya kutokuwa na hatia ya wanandoa wa kwanza, basi ndoa yao bila hukumu, bila aibu wala uwoga. Agano jipya linatueleza, “Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi…” (Waebrania 13:4).
Ndoa iliyo imara haiwezi kupatikana mahali ambapo hapana usalama, kutoaminiana, kushuku mwenzako, au uwoga; mahali ambapo wanandoa hawana uhakika wa kujitoa kwa kila mmoja wao kwa kwenye ndoa. Ndoa iliyo imara yahitaji nadhiri, “Hadi kifo kitakapotutenganisha!”
Talaka au kutengana hakukubaliki ispokuwa tu kwa kutokuwa na uaminifu na unyanyasaji. Hata wakati haya yamefanyika kumbuka kwamba Mungu anaweza komboa.
Upendo wa Agano ni wa kujitoa, heshima na wa kupendeza hata wakati uhusiano ni mgumu (1 Wakorintho 13). Kujitoa kuliko dhaifu husababisha kutengana kihisia, kutengana na majaribu.
Mume anayeishi kulingana na upendo wa agano hawezi kukata tamaa kwa mke wake hata wakati ambapo mke wake hana heshima, hajiotoi, au mgonjwa. Mke ataishi kulingana na upendo wa agano anapochagua kumheshimu na kumtii mume wake kwa sababu ya Kristo hata wakati mume wake hampendi.
Upendo wake husababisha kupata heshima toka kwake. Na heshima yake husababisha kupata upendo kutoka kwake na wanazidi kukua!
► Kuna shida gani wakati ambapo watu wataoana na kutarajia kwamba watabadilisha maamuzi yao baadaye kama hawatafurahia ndoa? Kuna tofauti gani wakati ambapo wana ndoa wamejitoa na kuamini ya kwamba ndoa yao ni ya milele?
Ndoa ya Kibiblia ni mahali pa uumbaji: Uzazi
“Tazama wana ndio urithi wa Bwana uzao wa tumbo ni thawabu” (Zaburi 127:3).
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, na kwa upande mwingine watoto ni zawadi kwa Mungu kutoka kwa wazazi. “Au je kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu, mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana” (Malaki 2:15).
Wengine hupendelea maisha pasipo watoto, lakini maandiko yanasema kwamba Mungu anapendezwa na wazazi walio na watoto wacha Mungu.
Ni muhimu tujue ya kwamba sio tu kuongeza kizazi ndicho ambacho Mungu anataka lakini watoto wacha Mungu. Wazazi wameitwa na Mungu kuwafundisha watoto wao kumfuata Kristo.
Ndoa yaKibiblia ni ya Kristo.
Katika Waefeso 5:30-32, Roho mtakatifu anatoa maana na umuhimu wa ndani wa ndoa, ambao umefichika hadi kuja kwake Kristo. Ndoa ni picha ya ulimwengu —picha inayoonyesha—uhusiano uliopo kati ya Yesu Kristo na kanisa.
Paulo anaanza kwa kuwahimiza wakristo “wajazwe na Roho mtakatifu” (Waefeso 5:18). Ni katika muktadha huo anatoa maagizo yafuatayo kuhusu ndoa:
Mke aliyejazwa na Rohoataonesha utii kwa mume wake (“kichwa” chake), “katika Bwana,” kama ambavyo wakristo wanamtii Yesu (Waefeso 5:24, 32; ona pia 1 Petro 3:1), na hivyo kuonyesha heshima kwa Yesu na mumewe.
Ni muhimu kila mke awe na “Bwana” katika akili yake anapotii. Ni kwake na kwa ajili yake ndio ananyenyekea na si kwa ajili ya mumewe tu. Macho yake yapo kwa yesu asiye na dhambi. Mke aliye tayari kumtii mume wake ni tendo la kumwabudu Yesu.
Kutii kimaandiko, kama upendo, hakulazimishwi. Kutii kimaandiko ni zawadi ambayo wake huwatolea waume kwa sababu ya kumcha Kristo (Waefeso 5:33). Kutii kwa “kila kitu” (isipokuwa kile kinachotishia afya yake au kuhatarisha uhusiano wake na Yesu), ni tendo la kumwabudu Yesu.
Utii wa mke kwa mumewe ni tendo la heshima (mstari 33) kwake, kama sehemu ya maisha yaliyojaa Roho (5:18-21). Heshima hii itokayo kwa roho ya upole na wema ni ya thamani sana mbele za mungu (1 Petero 3:4).
Mume aliyejazwa na Roho. Atapenda mke wake kama vile Yesu alivyolipenda kanisa (Waefeso 5:25). Mume anastahili kumpenda mke kama vile aupendavyo mwili wake (Mstari 28-29). Lazima adhihirishe maisha yaliojazwa Roho na kujitoa kama vile Yesu alivyodhihilisha kwa kanisa “alipojitoa mwenyewe kwa ajili yake.” Hili ni tendo la “unyenyekevu” (Waefeso 5:21). Mtoa maoni mmoja aliiweka namna hii:
Kama yeye (Yesu) alivyojitoa kuteseka msalabani ili kuliokoa kanisa, vivyo tunastahili kujitoa wenyewe na kuchukua mateso na majaribio, ili kukuza furaha ya mke. Ni jukumu la mume kujukumika kwa mahitaji ya mke; ajinyime mapumziko kama inawezekana na kumshugulikia anapougua; kumlinda dhidi ya hatari; kumtetea akiwa katika hatari; kumvumilia wakati amekasirika; kushikamana naye hata wakati ambapo hamtaki; kuomba naye wakati yupo katika shida ya kiroho; na awe tayari kufa kwa ajili yake. Mbona hii isiwe hivyo? Kama meli imeharibika na wanazama majini na kuna kipande kimoja tu cha mbao ambacho juu ya hicho tu ndio kuna usalama, Je, haipasi yeye kumpa nafasi ya kwanza kuokolewa bila kujali hatari zinazomkabili mwenyewe? Lakini kuna zaidi… mume anastahili kuhisi ya kwamba ni jukumu lake kubwa kuona ya kwamba mke wake ameokoka. Anahitajika kumtimizia mahitaji yake yote atakayohitaji kiroho… na awe mfano; kumshauri anapohitaji ushauri; kufanya njia ya wokovu kwake iwe rahisi iwezekanavyo. Endapo mume ana Roho na moyo wa kujitoa kama Kristo, ataona kwamba hakuna gharama kubwa ya kulipa endapo ataweza kukuza wokovu wa familia yake.[4]
Mume anatakiwa kutafuta usafi wa kiroho wa mke wake kama vile Kristo ambavyo humsafisha bibi harusi wake ambaye ni kanisa, “…ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno …(na) apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Waefeso 5:26-27).
Nyakati za kale wake wa kifalme walioshwa mwili na mafuta ya urembo ya thamani kubwa- “miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake” (angalia Esta 2:12 na kuendelea). Kwa njia hii bikira aliandaliwa kwa mumewe.
Katika mtazamo wa kiroho, mume anastahili kujitoa kwa kila njia inayohitajika kwa ajili ya kunawiri kwa mke wake – uaminifu, upendo usio na masharti, maelewano, maombi, ushauri, mafundisho na utu wema.
Wakati mume anamtendea mkewe upendo wa aina hii, atalipwa furaha. Paulo anasema, “ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe” (Waefeso 5:28). Waume wapendao wake zao kwa hii njia ya kujitola watalipwa zaidi na Mungu, na zaidi ya hayo kwa heshima, upendo na uaminifu kutoka kwa mke wake.
► Ni mambo gani haswa ambayo mume anastahili kufanya ili ampe usaidizi wa kiroho mkewe?
[4]Albert Barnes, Commentary on Ephesians, (Sura ya tano)
Jinsi ambavyo wanandoa wanaweza kuboresha ndoa yao
(1) Ni lazima wafurahie mpango wa Mungu wa asili na watambue majukumu yao maalum kwenye ndoa.
Waume lazima wakumbuke kwamba wake zao ni zawadi kutoka kwa Mungu na “mwenza mkamilifu,” na kutoa maisha yao kwa sababu ya usalama wao na kiroho, kihisia na uzima wa mwili. Ni lazima achague kuwa na shukurani na kumpenda hata wakati ambao ni kana kwamba hastahili, akijua ya kwamba ni Mungu pekee anaweza kubadilisha kile ambacho lazima kibadilishwe ndani mwake. Mungu ataheshimu uaminifu wake na imani.
Mke ni lazima aheshimu chaguo la Mungu la mume wake kama kichwa chake kwa kumwonyesha heshima kwa kila njia iwezekanayo na aheshimu uongozi wake. Lazima achague kutii na kuheshimu hata wakati ambapo amefanya makosa na hastahili kuonyeshwa unyenyekevu, huku akiomba ya kwamba Mungu kubadilisha kile ambacho kinahitaji kubadilishwa ndani yake. Mungu ataheshimu utiifu wake na imani.
(2) Wanandoa lazima wakuze uhusiano wa kweli wa kiroho na kimwili.
Lazima wazingatie kujuana kila mmoja na mwingine bila uoga, ukosoaji, kulinganisha na wengine, unyanyasaji, tamaa, kujiridhisha binafsi au kumdhalilisha mwingine. Ni lazima waishi kwa uwazi na uadilifu mbele za Mungu na mbele ya kila mmoja.
(3) Wanandoa lazima watumie mfano wa neema ya Mungu wanapopungukiwa.
Adamu na Hawa walipoanguka katika dhambi walipata aibu na majuto, Mungu alifunua uwezo wake wa kuwakomboa katika udhaifu wao. Mungu alimtoa mnyama ili kufanya mavazi kwa ajili ya Adamu na Hawa ili kufunika uchi wao (Mwanzo 3:21). Tendo hili la upendo lilikuwa ni picha ya neema na ahadi ya Mungu ya ukombozi kupitia Kristo Yesu. Kuvalishwa na Mungu kupitia Kristo Yesu kuliwawezesha na kunatuwezesha sisi kusamehewa na kurejeshwa. Kupitia Kristo wanandoa wanaweza kurudi kwenye urafiki usio na haya baada ya kufanya dhambi.
Yesu Mfano wa Heshima kwa Wanawake
Wanawake walichukuliwa kuwa duni wakilinganishwa na wanaume katika karne ya kwanza katika ulimwengu wa Kirumi na katika dini ya Kiyahudi. Pia mtazamo huo huo unaonekana katika tamaduni za kisasa duniani, pia katika jamii na katika nyumba. Wanawake hawaheshimiwi na wanatumika kama vyombo vya starehe, na wanadhulumiwa. Lakini heshima kuu kwa wanawake kutoka kwa Yesu inapaswa kutumika kama mfano wa kuigwa.
Kwa Yesu wanawake wana hadhi na heshima sawasawa na wanaume. Yesu akasema, “...yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke” (Mathayo 19:4; Mwanzo 1:27). Wanawake wameumbwa katika sura na mfano wa Mungu kama vile wanaume, wanajitambua, wana uhuru wao, wana motisha wa maisha na wanawajibika kwa matendo yao.
Yesu aliwatambua wanawake Kama wanadamu wengine. Wafuasi wa Yesu walikuwa katika jinsia mbili, wakiume na wakike. Wale wa kike Yesu huwaona kama watu halisi, sio tu kama vyombo vinavyotumika kwa tamaa za wanaume. Anawaona kama watu ambao alikuja duniani kwa sababu yao.
James Borland, na John Piper na Wayne Grudem, wanatupa mfano ulio wazi wa jinsi Yesu alivyo wachukulia wanawake na jinsi alivyo waheshimu kama inavyoelezwa katika vitabu vinne vya injili:
(1) Yesu mara kwa mara aliwahutubia wanawake hadharani.
Haikuwa kawaida wakati wa Yesu mwanaume kuongea moja kwa moja na mwanamke hadharani (Yohana 4:27). Wanafunzi walishangaa kuona Yesu akiongea na mwanamke Msamaria kwenye kisima cha Yakobo pale Sikari (Yohana 4:7-26). Yesu aliongea kwa uhuru na mwanamke aliyefumaniwa akizini (Yohana 8:10-11). Luka anasema Yesu aliongea hadharani na mjane wa Naini (Luka 7:12-13), na mwanamke aliyetokwa na damu miaka kumi na miwili (Luka 8:48; Mathayo 9:22; Marko 5:34), na Yule mwanamke aliyemuita katika halaiki (Luka 11:27-28). Yesu aliongea na mwanamke aliyekuwa amejipinda mgongo kwa miaka kumi na minane (Luka 13:12) na kikundi cha wanawake waliokuwa wakilekea Golgotha alikosurubiwa (Luka 23:27-31).
(2) Yesu alionyesha heshima na hadhi ya juu kwa wanawake kwa namna alivyoongea wakati alipokuwa akiongea nao.
Aliongea kwa kujali na kwa kutafakari. Mathayo, Marko, na Luka wanarekodi kuwa Yesu alimuongelesha mwanamke aliyetokwa na damu kama “binti” na pia alimwita mwanamke aliyejipinda mgongo “binti wa Ibrahimu” (Luka 13:16). Kwa kuwaita “binti za Ibrahimu” Yesu anawaweka katika kiwango cha kiroho sawa na “wana wa kiume wa Ibrahimu.”
(3) Yesu anaonyesha asili na thamani ya wanawake kwa kufanya wao kuwajibika kibinafsi kwa dhambi zao.
Hii inaweza kuonekana kwa jinsi alivyokabiliana na mwanamke msamaria kisimani (Yohana 4:16-18), kwa mwanamke aliyezini (8:10-11), na mwanamke mwenye dhambi aliyetawadha miguu yake Yesu (Luka 7:44-50). Dhambi zao hazikupuuzwa lakini zilikabiliwa. Matendo yake yalionyesha kwamba kila mwanamke alikuwa na uhuru wa kibinafsi na uwajibikaji kwa maamuzi yake, na ni lazima kila mmoja kibinafsi akabiliane na dhambi, toba, na msamaha.
Jinsi ambavyo Yesu aliwathamini wamawake kunapaswa kuongoza kanisa la sasa.
Nafasi bora ya kibiblia ya wanawake katika huduma na nyumbani inajadiliwa sana katika kanisa la sasa, kama inavyostahili, japokuwa thamani na usawa wa mwanamke kuwa ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu sio jambo la kutilia shaka. Yesu aliendeleza kuonyesha thamani na hadhi ya wanawake kama watu. Aliwatuma kama wajumbe wake wa kwanza kutangaza habari njema za kufufuka kwake (Yohana 20:17). Alithamini ushirika wao, maombi, huduma kwa wakristo, msaada wao wa kifedha, ushuhuda wao na kushikiki kwao katika injili. Yesu aliwaheshimu wanawake, akawafundisha, akawahudumia huku akiwawaza.
Heshima kwa wanawake katika agano jipya.
Mfano wa Yesu akiheshimu wanawake unaonekana katika maisha ya Roho Mtakatifu. Katika siku ya penteconte, Roho Mtakatifu alimwagwa juu ya wote “wana wenu na binti zenu,” na Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; “watumishi wangu wanaume na wanawake” (Matendo 2:17). Roho Mtakatifu hakuonyesha ubaguzi.
Katika Warumi 16, Paulo anamthibitisha mwanamke aitwae Fibi kama “mtumishi wa kanisani” (mstari wa 1), Pirisila na Aquila kama “watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu” (mstari wa 3-4), Mariamu ni mojawapo ya “aliyejitaabisha sana” (mstari wa 6), Junia kama mmoja “ambao ni maarufu miongoni mwa mitume” (mstari wa 7), na wanawake wengine pia.
Katika 1 Wathesalonike Paulo anathibitisha kwamba ni Mungu aliyewapa upole na upendo anapoandika, “Bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe” (1 Wathesalonike 2:7). Katika Waefeso anawaamrisha wanaume kuwapenda wake zao, “kama Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa kwa sababu yake,” na “kama miili yao wenyewe” (Waefeso 5:25, 28). Petro anawasihi wanaume “kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima…” (1 Petro 3:7).
Ni wazi kwamba wanawake waliheshimiwa na wanaume walifundishwa kukaa kwa heshima na wao katika kanisa la kwanza. Ni wakati wa kila kiongozi wa kanisa popote kusimama na kuwatetea wanawake ili waheshimiwe na desturi za kuwafanya wanawake duni zikemewe. Ni wakati wetu sasa kuthamini wanawake kama watu maalumu walioumbwa na Mungu katika sura yake. Mafundisho yoyote ya majukumu ya wanaume na wanawake kanisani au nyumbani lazima yaanze katika misingi hii la sivyo mafunzo yetu yatakuwa njia na chanzo cha unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Hitimisho
Ndoa ni uumbaji wa Mungu na sio wa mwanadamu, kwa hivyo ni lazima twende kwa Mungu kwa ushauri na maelekezo sio katika dunia wala tamaduni zetu. Ni yeye pekee awezaye kufanya ndoa zetu kuwa imara, dhabiti na za furaha. Lakini hatutaweza kuwa mwanandoa ambao tunastahili kuwa pasipo Roho Mtakatifu!
Kushiriki kwa vikundi
► Eleza kanuni ambazo Kanisa lazima lifundishe ili kufanya ndoa kuwa thabiti. Ni kipi hasawa ambacho kinakosekana katika maeneo yako?
► Je tamaduni yako humchukulia vipi mwanamke akilinganishwa na mwanaume?
► Je ni jinsi gani makanisa katika nchi yako huwachukulia wanawake tofauti kwa kulinganisha na wanaume? Je kuna tofauti kati ya kanisa na tamaduni?
► Ukizingatia mfano wa Yesu ni desturi zipi lazima zibadilishwe?
Maombi
Baba wa mbinguni,
Asante kwa zawadi ya ndoa. Tusaidie tujitoe kwa mambo ambayo ni ya muhimu na ambayo yatafanya sisi kufanya ndoa iwe kama ulivyokusudia.
Tusaidie tuoneshe upendo kama ule ambao unaoneshwa na Kristo kwa Kanisa.
Tusaidie twende zaidi ya tamaduni zetu kwa kuheshimiana kila mmoja na mwingine.
Asante kwa Roho mtakatifu ambae anafanya uhusiano uwe na furaha wenye nguvu na wa kuwezekana.
Amina
Zoezi la somo la 6
(1) Eleza kwa kuandika tofauti iliopo kati ya wanaume na wanawake katika tamaduni yako. Je tofauti hizi zinawezaje kubadilishwa kwa uangalifu tukitumia ukweli ulio katika neno la Mungu?
(2) Chagua kanuni mbili ambazo zimekuwa mpya kwako katika somo hili. Andika aya moja ukizieleza kwa maneno yako mwenyewe.
(3) Andaa taarifa ya kuwasilisha kati ya mojawapo ya mada ambazo zimeorodheshwa (kiongozi wa darasa atampa kila mwanafunzi mada ya kuzingatia.) shiriki utafiti wako katika somo litakalofuata.
Mpango wa Mungu wa muungano katika ndoa.
Kusudi la kimaandiko katika ndoa.
Njia za kuboresha ndoa.
Mtazamo wa Biblia kuhusu wanawake
Majukumu katika ndoa kama vile ambavyo Mungu ameelekeza na umuhimu wa kujazwa na Roho Mtakatifu ili kutimiza majukumu haya.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.