Katika hadithi ya kuigiza, Robinson Crusoe, Mwanaume aliyenusurika kwa kuogelea mpaka kisiwani meli ilipozama. Hapo alikuwa peke yake kwa miezi. Akajenga kibanda, akatengeneza mavazi, na akajifunza jinsi ya kutafuta chakula. Siku moja alipokuwa akitembea karibu na ufukwe wa bahari alishangaa kuona alama za nyayo za mtu kwenye mchanga. Hii ili maanisha kulikuwa na mtu mwingine pale. Hakujua kama mtu huyu alikuwa rafiki au adui. Hakujua chochote kuhusu tabia, lugha, tabaka au sababu ya mtu huyu kuwa hapo. Hakujua mtu huyu angebadilishaje maisha yake katika kisiwa hiki. Na kwa sababu uhusiano huathiri sana maisha ya mtu binafsi, Robinson alikuwa na tumaini na uoga kwa wakati mmoja alipoona hizo nyayo.
Umuhimu wa mahusiano katika kukua kiroho
Katika karne ya kwanza kanisa ilifanya kazi katika migogoro mbalimbali… Wayahudi na Watu wa Mataifa… madaraja katika jamii… tamaduni… jinsia… Mtume Paulo aka waambia “mkaribishane ninyi kwa ninyi…” (Warumi 15:7).
► Fikiri mtu akiwa peke yake kwenye kisiwa. Anaweza kuwa mvumilivu na yeyote? Anaweza kusamehe yeyote?
Huwezi kukua na kuonyesha subira ya mkristo pasipo kuwa na ushirika na wangine. Hauwezi kusamehe wengine au kusamehewa kama huna ushirikiano na wengine.
► Je ni mambo gani mengine ambayo ni sifa ya mkristo yanayo hitaji watu wengine?
Mambo haya hufanyika katika mahusiano na watu wengine. Tabia njema inaweza kukuzwa na kuonyeshwa katika mahusiano peke yake. Hii inamaanisha mahusiano yetu na watu yanaathiri ukuaji wetu wa kiroho.
Biblia inatupa mwelekeo katika mahusiano mbalimbali. Kuna maelekezo maalum kati ya mke na mume, wazazi kwa watoto, mwajiri na mwajiriwa, wachungaji na makanisa, wazee kwa miaka na walio vijana.
Kuna kanuni tatu katika maandiko ambayo zinahusishwa katika aina yoyote ya mahusiano ya mwanadamu: Kanuni ya amani, upendo na heshima.
Kanuni ya Amani
“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” (Waebrania 12:14).
Aya hii inaeleza umuhimu wa uhusiano kwa msisitizo. Utakatifu uko karibu na umeunganishwa na kutafuta amani na watu wote.
► Ni mambo gani tuyafanye ili tutafute amani na watu wote?
Kutafuta amani, angalau umpe kila mtu kile ambacho anastahili. Kwa wale wanaohitaji shukrani, heshima, au utiifu, ni lazima uwape. Kama hutawapa hauna hatia ya kusababisha mtafaruku. Ukikosa kutimiza majukumu yako, ahadi au kulipa wengine, wewe hautafuti amani. Unapotambua umeanguka kwa kutotimiza yale ambayo ilikubidi, inabidi uombe msamaha na utimize majukumu yako kadri uwezavyo.
Lakini kutafuta amani ni zaidi ya kutoa kile ambacho unadaiwa. Inahusisha kuonyesha upendo na utu wema ambao hudaiwi.
► Mwanafunzi asome Tito 3:2-3 kwa niaba ya kikundi.
Lazima tuwe na subira na msamaha, tukielewa kwamba wale ambao hawaja okolewa huwa na nia mbaya na mtazamo mbaya.
Ukitaka amani utatafuta urejesho mahali penye vurugu. Utakuwa tayari kusamehe. Hautakuwa mwepesi kupuuza ya kwamba amani inaweza kurejeshwa. Hautakubali kwa wepesi kutengana katika maisha.
Yesu akasema ni lazima uende kwa aliye kukosea na umweleze kile ambacho alifanya (Mathayo 18:15). Kama unaona hilo jambo ni ndogo na halihitaji kukutana, usiwaambie wengine au usiwe na uchungu kwa yule aliye tenda hilo jambo.
Wakati mwingine watu hupambana na kutosawamehe wakristo wenzao waliowakosea. Tunaweza kutarajia kunyanyaswa na watu, ambao hawaja okoka lakini ni vigumu kuelewa wakati mkristo mwingine amekutendea kosa.
Yesu akasema kwamba lazima tuwe tayari kusamehe sabini mara saba (Mathayo 18:21-22). Jambo ambalo hufanya watu kuacha kanisa na kuacha mambo ya kiroho ni uchungu na kuumizwa na wakristo wengine. Uchungu huja kabla ya mapungufu mengine ya kiroho.
Mtu anapokataa kusamehe, anaweka sehemu fulani katika maisha yake kukataa mamlaka ya Mungu, kwa maana Mungu anataka sisi tusamehe. (Soma Waefeso 4:32.) Eneo hilo hufanyika Sehemu ambayo shetani ataitumia kuathiri sehemu zingine katika maisha. Kama mtu atakataa kusamehe, hivi karibuni hataweza kushinda majaribu ambayo yanaonekana hayahusiani na hilo kabisa.
Msingi wa kila kosa la kibinafsi ni thamani yetu ya haki zetu binafsi. Kwa sababu tuna amini ya kwamba tuna haki ya kupata heshima fulani, na tunahudhika tusipoipata. Tunaamini tunastahili kilicho bora kuliko kile ambacho tumepata.
Kitu muhimu katika kusamehe wengine ni kuelewa ukombozi. Ukombozi una maanisha kununua tena. Kwa sababu Mungu ametukomboa sisi, sisi ni wake, haki zetu ni zake. Ni lazima tukabidhi haki zetu kwake kwa hiari. Unaweza kuomba, “Bwana najua ya kwamba haki zangu zote ni zako. Nataka uchukue usukani na unipe kile ambacho unaona kinanifaa na ni kizuri kwangu.” Halafu, watu wanapokufanyia mazuri, unaweza kumshukuru Mungu kwamba aliwezesha hiyo nafasi kwako. Mtu anapokufanyia mabaya, kumbuka ya kwamba Mungu ndiye mwenye usukani wa haki zako, na aliona utakua vizuri bila kuwa na haki hiyo wakati huo.
Kwa kusamehe wengine, unajitoa kwa Mungu na kufanya yeye akukuze jinsi apendavyo. Kanuni hii ya kuachilia haki zako kwa Mungu inatumika katika kila uhusiano wa mwanadamu. (Nukuu zingine za msamaha zinapatikana Wakolosai 3:13, Mathayo 6:15, na Warumi 12:19.)
Kanuni ya Upendo
Mtu ambaye hatudai chochote tunapaswa kumuonyesha upendo pia. Kwa sababu tulipokea neema, tuna deni kwa Mungu. Hatuwezi kumlipa. Yeye hana mahitaji, lakini ametuagiza tuwape wengine upendo tuliopokea ambao hatukustahili.
“Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana” (Warumi 13:8).
Upendo ni hakikisho ya kwamba mtu ni mkristo halisi.
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona (1 Yohana 4:20).
Kuna upendo maalumu kati ya Wakristo, na Yesu anachukulia kibinafsi matendo yako na nia yako kwa Wakristo wengine. Atasema siku ya hukumu, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mathayo 25:40).
Lakini upendo wa Wakristo haupaswi kuelekezwa kwa Wakristo wengine tu. Katika Mathayo 5:44-45 Yesu akasema,
Lakini mimi ninawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Watu wengine hupata ugumu kuwa wema kwa wale wanaowaudhi, lakini hakuna sababu ya kuwa katili. Hatuwezi kulipiza ubaya kwa ubaya. Ni vizuri tuwapende watu na tuwe wema hata kama hawastahili. Tukumbuke kwamba tulipokuwa watenda dhambi, hatukustahili upeno wa Mungu, lakini alitupenda (Tito 3:2-3).
Kanuni ya Heshima
► Kama nitakupa bure noti ya dola mia moja ambayo ni chafu na imeraruka, utaichukuwa? Utaikataa kwa sababu ni chafu na imeraruka?
Utaikubali kwa sababu ina thamani ambayo haitegemei hali yake.
Kila mtu anastahili heshima kwa sababu mwanadamu ameumbwa katika sura na Mfano wa Mungu (Mwanzo 1:17). Sura ya Mungu inampa mtu thamani ambayo ni ya asili.
Hata kama mtu hana elimu, ujuzi, ufundi na kingine chochote ambacho kingemfanya afanikiwe au wa maana katika viwango vya kawaida, ana thamani kwa sababu ni mtu katika sura na Mfano wa Mungu.
Asili ya mtu na thamani yake inabaki vile vile hata kama amejishusha hadhi katika njia zingine na maamuzi ya kipuuzi. Labda aliacha shule, akaharibu afya yake, akaiga tabia mbaya, lakini ana thamani kama mwanadamu aliye na nafsi ya kuishi na sura ya Mungu.
Kwa sababu ya thamani ya Mfano na sura ya MUngu kwa mwanadamu, heshima lazima idumishwe katikati ya wanadamu. Adabu ni kiwango cha chini.
Ghiliba na udanganyifu ni makosa, kwa sababu kila mtu hufanya maamuzi yakiwa na matokeo ya milele na ni lazima ajue kiini hasa cha maamuzi. Kumsababisha mtu kufanya kitu kizuri kwa makusudio mabaya sio ufanisi, kwa sababu bado hajafanya maamuzi mazuri.
Kadri iwezekanavyo ni vizuri tuwape watu heshima hata kama tabia zao ni mbaya. Hata katika kurekebisha na kuadhibu makosa (kwa wale walio na mamlaka sahihi ya kufanya hivyo) yanafanywa kukiwa na ufahamu ya kwamba tunashughulika na viumbe visivyoweza kufa ambavyo vina kitu cha asili cha Mungu.
Kushiriki kwa vikundi
Ni vizuri kuwe na mifano mingi katika kuelezea kanuni hizi.
► Shiriki na uulize mifano ya wakati ambapo mtu alifanya bidii kutafuta amani.
► Shiriki na uaombe watu wajitoe ili kusamehe walio wakosea.
► Uliza ni katika wakati gani mtu anapaswa kuonyeshwa upendo zaidi hata kama hastahili.
► Eleza inamaanisha nini kumpa mtu heshima hata wakati tabia zake ni mbaya.
Kanuni za Kimaandiko kuhusiana na Mazungumzo
► Kuna msemo wa kale unao sema, “kalamu ina nguvu kuliko upanga.” Inamaanisha nini?
Kuna nguvu katika wazo, katika ushawishi na katika mawasiliano. Unaweza kutimiza mengi kwa kutia watu moyo kuliko kuwalazimisha. Wazo—fikra—yaweza kusambaa na kushawishi watu wengi.
Biblia inazungumza kuhusu nguvu za maneno kufanya mazuri au mabaya (Yakobo 3). Mpango wa ukombozi unahitimishwa na nguvu zilizopo katika injili, iliyo kabidhiwa kwa wajumbe ambao ni wanadamu.
Tunawezaje kutumia maneno kutimiza mazuri na kuzuia mabaya? Biblia inatupatia kanuni.
(1) Usizungumze sana.
“Upumbavu huongeza maneno…” (Mhubiri 10:14).
“Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili” (Mithali 10:19).
Kwa hivyo usizungumze sana. Azungumzae zaidi hayapimi maneno yake au ya wengine. Anayasema mambo ambayo hayamaanishi kabisa, na anadhani kuwa watu wengine wanafanya vivyo hivyo. Hutoa maoni pasipo hekima. Haustahili kutoa maoni kwa kitu ambacho haukijui; sio kila maoni yana umuhimu unaofanana.
(2) Usizungumze kabla ya kufikiria.
Usikubali hisia zako kukufanya utoe matamshi ambayo utayajutia.
“Hayo mnajua ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika” (Yakobo 1:19).
“Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; bali mwenye hekima huizuia na kuituliza” (Mithali 29:11).
“Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu” (Mithali 14:29).
(3) Usihukumu hali katika mtazamo wa kwanza.
“Yeye ajibuye kabla hajasikia ni upumbavu na aibu kwake” (Mithali 18:13).
“Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; lakini jirani yake huja na kumchunguza” (Mithali 18:17).
Michafuko mengi hutokana na kutoelewa. Subira na kwa kuchunguza huleta suluhu. Kama mtu aliye na haki inayojulikana akisema jambo ambalo haliko sawa kwako usiwe mwepesi wa kuhukumu.
“Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake” (Mithali 26:17).
(4) Kuwa mwangalifu wa mzaha.
Kwa sababu ya kile ambacho maneno yanaweza kusababisha, mazaha usio zuilika ni silaha mikononi mwa mwendawazimu.
“Kama mtu mwenye wazimu atupaye miyenge, na mishale, na mauti; ndivyo alivo amdanganyaye mwenzake, na kusema, je! Sikufanya mzaha tu?” (Mithali 26:18-19).
Usufanye watu wafanye makosa kwa sababu ya kuamini mzaha wako. Usiwaambie kwamba unamaanisha wakati haumaanishi-hawatakuamini tena. Usifanye mzaha kwa kasoro ambazo watu hawawezi kujizuia. Usifanye mzaha kwa mapungufu ya mwingine. Usifanye mzaha ambao utafanya dhambi kuwa kitu kidogo.
► Ni matumizi gani mengine mabaya ya mzaha?
(5) Usiseme kwa asiye faa.
“Mwenye kitango akisingizia ufunuo wa siri bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo” (Mithali 11:13).
“Moto hufa kwa kukosa kuni; na bila mchongezi fitina hukoma” (Mithali 26:20).
Kuna mambo lazima yasemwe, lakini inawezekana sio wewe unayestahili kuyasema. Hauwezi kuyasema kwa niaba ya wale walio na mamlaka ya kuyasema.
Usieneze maneno ya makosa ya watu wengine.
Watu hawatakuamini kwa taarifa zao za kibinafsi, kama watafikiri utawaambia wengine.
“Ujitetee na mwenzako peke yake; bali usifunue siri ya mtu mwingine” (Mithali 25:9).
Mpumbavu hueleza tatizo kwa watu wasio sahihi badala ya kufuata utaratibu katika Mathayo 18:15-17.
(6) Kuwa mwangalifu Unapokosoa.
Kuna wakati unaofaa na njia sahihi ya kukosoa.
“lawama ya wazi ni heri kuliko upendo uliositirika. Jeraha utiwazo na rafiki ni amini…” (Mithali 27:5-6a).
Hakikisha ya kwamba kukosoa kwako kuna lenga kujenga sio kubomoa. Lazima uonyshe unajali na unataka kusaidia. Kawaida uhusiano bora ni muhimu kabla ya msaada wako wa kukosoa.
(7) Usidanganye.
“Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake” (Wakolosai 3:9).
Udanganyifu huambatana na maisha ya dhambi, sio maisha ya Kikristo.
“Midomo ya uongo ni chukizo kwa Bwana; bali watendao uaminifu ndio furaha yake” (Mithali 12:22).
(8) Weka maneno yako safi.
“...Wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru” (Waefeso 5:4).
Usieleze kuhusu kashfa zilizopita au za sasa isipokuwa tu kwa wakati unaofaa kushughulikia hali fulani. Usiseme utani ambao lazima uuseme kwa siri. Watu mara kwa mara hutumia maneno ya kingono au maneno za sehemu za siri katika mshangao wao, lakini hiyo haifai kwa mkristo. Haifai kutumia maneno yanayo mwelekea Mungu au Yesu kama mshangao wakati wa shida, kama sio kumuita Mungu kwa usaidizi.
(9) Usigawanye watu kwa maneno yako.
“Mtu mshupavu huondokesha fitina na mchongezi huwafarakanisha rafiki” (Mithali 16:28).
“Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, vitu saba vilivyo chukizo kwake… [ya saba] Naye apandaye mbegu ya fitina kati ya ndugu...” (Mithali 6:16, 19).
Usijaribu kujifanya kuwa bora kwa kumfanya mtu mwingine aonekane duni. Usifanye vurugu kati ya wengine. Usiharibu huduma ya mwingine kwa fitina.
Kabla ya kuongea jiulize “ni ya ukweli?” pia “kwa nini niseme? “
Hitimisho
Mkristo awe tayari kuomba msamaha anapotambua ana makosa aliyoyafanya kupitia maneno yake. Awe tayari kurekebisha yale aliyo yasema ambayo sio sawa.
Maneno ya kuudhi kutoka kwa wengine haimaanishi wewe ulipize kwa maneno ya kuudhi pia.
Kuna makosa katika misemo yako ambayo unaweza kuyarekebisha pole pole. Kwa mfano, unaweza jifunza kuwaza hilo jambo kabla hujalisema. Kuna makosa megine ambayo huonyesha shida ya moyo, kama vile kutaka kuumiza mtu kwa maneno. Kama unajihukumu kwa shida kama hiyo ya matamshi, unapaswa kumuomba Mungu akusamehe na asafishe moyo wako kutokana na mazoea hayo.
Maneno yako huonyesha yaliyo moyoni mwako. Usiharibu ushuhuda wako kwa kuyanena yale ambayo sio sawa kwa maisha ya Mkristo.
Maneno yako yanaweza kubariki walio karibu nawe. Huduma nyingi huhusisha mawasiliano. Maana ya maneno yako huwa ya maana zaidi unapozingatia na kufuata kanuni za Biblia.
Kushiriki kwa vikundi
► Watu wengi huona makosa ya wengine katika maneno lakini sio yao wenyewe. Kiongozi lazima awe mfano wakati ambapo yeye mwenyewe ameshindwa kuwa mfano mzuri kwa kushindwa kufuata kanuni za Biblia au aeleze mojawapo ya udhaifu wake.
► Omba washiriki wachague kanuni ambazo ni wadhaifu kwazo na wamwamini Mungu atawasaidia.
Maombi
Baba wa mbinguni,
Nisaidie niishi kulingana na kanuni za kimaandiko za amani, upendo, na heshima kwa mahusiano yangu yote.
Nataka nisamehe walionikosea mimi. Nisaidie kutafuta urejesho kwa wale ambao tumekuwa na kutoelewana.
Nisaidie kuheshimu kila mtu kama kiumbe katika sura na mfano wako. Nisaidie kukumbuka matokeo ambayo mazungumzo yangu yanaweza kuwa nayo, na niwajibike kwa maneno yangu. Nataka maneno yangu yatimize mazuri sio mabaya.
Nataka ushuhuda wangu kwako uheshimiwe.
Asante kwa nafasi ya kueleza kushiriki ukweli wako.
Amina.
Zoezi la somo la 4
(1) Soma Yakobo 3. Ona uwezo mkubwa wa mazungumzo ulioelezwa hapa. Katika mstari 13-18 ona jinsi ambavyo usemi wake unavyotiririka kiasili kutoka katika hali ya kiroho ya mtu. Soma Waefeso 4:25-32. Andika aya ya ombi kutokana na andiko hili.
(2) Soma Waefeso 5:22–6:9. Orodhesha na ueleze mambo mahususi ya tabia katika mahusiano mbali mbali. Andika na ueleze jinsi ambavyo maelekezo haya yanahusiana na kanuni ya upendo, amani, na heshima kama tulivo jadili.
(3) Chukua matatu kati ya maswali yafuatayo. Andika aya huku ukijibu kila mmoja wapo:
Ni mambo gani hasa Mungu ametuitia kuyafanya katika hali ya kutafuta amani katika mahusiano yetu?
Kwa nini kusamehe wengine ni muhimu ili kudumisha wokovu?
Inamaanisha nini mtu kumpa Mungu haki zake?
Ni msukumo upi tulio nao wa upendo ambao tunastahili kuwapa wengine wasio stahili?
Ni kwa namna gani mtu kuumbwa katika sura ya Mungu inathiri uhusiano wetu na wengine?
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.