Dale Carnegie alipata umaarufu kwa kitabu chake, Jinsi ya Kupata Marafiki na Kushawishi Watu. Aliamini kuwa watu wote wanastahili kuzingatiwa na kuheshimiwa kwa sababu wanathamani kama watu. Taasisi ya Dale Carnegie ilianzishwa kufundisha kanuni zake.
Kuna wakati Fulani taasisi ya Dale Carnegie ilifundisha masomo ya jioni kwa wafanyabiashara, wakifundishwa jinsi ya kuwa na urafiki na kujenga mahusiano na watu. Wanafunzi walipopewa mtihani, walishangazwa na swali moja. Swali ambalo halikutarajiwa lilikua hivi, “Je jina la mwanamke ambaye ambaye huwa anafanya usafi kwenye ukumbi unapotoka darasani anaitwa nani?” Wanafunzi mara nyingi walikuwa wakimpita wakitoka darasani kuelekea nyumbani lakini hawakulichukulia Kama ni jambo la muhimu sana kumjua, hata ingawa walikuwa wametoka kwenye darasa la mafunzo ya kuwa na urafiki na kujenga mahusiano. Walidhani kuwa watatumia ujuzi wao mpya kwa kujenga mahusiano na watu wa maana pekee yao.
Thamani ya Kikristo ya Ubinadamu
Binadamu wote ambao wanaweka Imani yao katika Kristo ni washirika wa mwili mmoja-Mwili wa Kristo: “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa waa huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28).
Injili ya Luka inatueleza mazungumzo wakati Yesu aliponukuu amri “…na jirani yako kama nafsi yako.” Mwanasheria akamuuliza swali, “Je jirani yangu ni nani?” (Luka 10:29). Hilo swali lilikua lenye umuhimu sana kwa sababu mwanasheria alidhani kuwa hakuwa na haja ya kumpenda kila mtu. Alifikiri kuwa amri ilimuhitaji kupenda watu wa kikundi fulani.
Watu wa tamaduni na mila zote wana maadili yanayofanana. Wanajua kwamba kuiba, kuua na dhuluma ni makosa. Hata hivyo hawafikirii kuwa kila mtu anastahili kutendewa haki. Labda hawaibi kutoka kwa rafiki, lakini wataiba kutoka kwa mgeni wasiyemjua. Labda wasimuue mtu wa taifa lao lakini wamuue mgeni. Labda wasidhulumu watu wa jamii yao, lakini wadhulumu watu wa kabila ambalo wanalidharau.
Wakristo wanaamini kuwa kila binadamu ameumbwa katika mfano wa Mungu na thamani yake haina kikomo.
Wakati wowote ambapo malaika walionekana mbele ya watu kama vila ambavyo imeandikwa katika maandiko, maneno yao ya utangulizi yalikuwa “usiogope,” kwa sababu uwepo wao ulikuwa wa kushangaza na kupita kiasi. Wakati mwingine watu walianguka chini kwa heshima mbele ya malaika kwa ajili ya kuabudu.[1] Lakini mwanadamu ni wa maana zaidi kuliko malaika (1 Wakorintho 6:3).
Unaweza kutana na mtu ambaye ni ombaomba wa tabaka la chini, hajasoma, asiye na akili sana, wa tabia mbaya na upungufu wa ujuzi, hana ushawishi, maumbile yanayo chukiza, utu usiopendeza lakini bado anafanya maamuzi ya matokeo ya milele. Kama amekombolewa na Mungu atakuwa kiumbe mkuu kuliko yeyote tuliyemuona duniani.[2] Kwa hivyo anastahili heshima.
► Mwanafunzi asome Wagalatia 3:28 kwa niaba ya kikundi.
Aya hii inataja namna tatu ambayo watu mara nyingi wanaainishwa- kikabila, tabaka la kijamii na jinsia. Tabaka la kijamii inajumuisha viwango vya uchumi. Tunaweza kuongeza sababu zingine kama vile umri, viwango vya masomo na ujuzi. Hakuna uainishaji wowote tuliotaja unaopaswa kuathiri thamni ya Mungu kwa mtu.
► Mtu mmoja anaweza kuwa na thamani zaidi kuliko watu wengine? Eleza.
Mtu aliye na akili nyingi, masomo, ujuzi, nguvu za kimwili, uzoefu wa uongozi au fedha ana thamani zaidi kwakuweza kukamilisha majukumu fulani ya kazi. Hata hivyo ni makosa kuzingatia kuwa mtu ana thamani zaidi kama binadamu kwa sababu ya hizi sifa. Hizo sifa zina thamano ya vitendo, lakini asili ya muhimu ya ubinadamu iliyofanywa kwa mfano wa Mungu ina thamani isiyo na kikomo na ni ya milele.
[1]Mfano mmoja wah ii ni Ufunuo 22:8-9, “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.”
[2]1 Wakorintho 15 inaeleza mabidiliko ya ajabu ya miili ya Kikristo ambayo yatatokea wakati wa ufufuo.
Ubaguzi
Watu hufikiri kwamba watu wote wenye kikundi fulani cha kabila wana sifa ambazo ni sawa. Hizi sentensi mara nyingi hutolewa kwa kuangalia rangi ya Ngozi kama vile “Watu weupe wakati wote __________________” au “watu weusi wote _________.”
Wakati mwingine sentensi inahusu utaifa, kama vile Wahaiti au Wajerumani au Wajapani. Wakati fulani ni maalum zaidi, kama vile jina la kikabila au kabila fulani kwenye taifa.
Sentensi ambazo watu wanatoa kuhusu makundi ya watu wakati mwinginw ni za kusifu au pongeza, lakini mara nyingi ni za kushutumu au kukosoa. Sentensi hizo zaweza kusema kuwa kila mtu kwenye hicho kikundi anakosa au upungufu fulani.
Hapa kuna mfano wa sentensi za kukosoa ambazo watu husema kuhusiana na vikundi vya makabila au mataifa. Majina ya makundi mbalimbali yatawekwa kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
_________________ ni wavivu.
_________________ wanalewa mara kwa mara.
_________________ wataiba wakipata fursa.
_________________ wanapigana mara kwa mara.
_________________ hawamalizi kazi vizuri.
_________________ hawana akili za kutosha kufanya vizuri shuleni.
_________________ wanakasirika kwa haraka.
_________________ wandanganyifu.
Ni wazi kuwa tofauti za kikabila zipo, na hizi tofauti ni zaidi ya mwonekano wa kimwili. Kundi la kikabila linaweza kufaulu katika michezo fulani au kazi kwa sababu ya uwezo wa kimwili au akili.
Kundi la watu huwa na sifa fulani za kitamaduni. Utamaduni hufunza watu kujibu kwa njia fulani katika hali fulani. Kwa hivyo tunajifunza kutarajia vitendo fulani kutoka kwa watu wa tamaduni fulani.
Si vibaya kuona sifa za kimaumbile na kitamaduni za kikundi. Hata hivyo, ni makosa kuhukumu tabia ya mtu kwa sababu ya kabila lake au utamaduni. Mtu kutoka kwenye kikundi chochote cha kabila anaweza kuwa mcha Mungu, mwaminifu na mkarimu. Itakuwa ni makosa kumtendea kama ana tabia mbaya wakati haumjui mtu huyo kibinafsi.
Uzoefu wetu binafsi unathiri jinsi tunavyowaona watu wengine. Kama mtu anatendewa vibaya na watu wa kabila lingine, anaweza kuhisi kuwa watu wote kutoka hilo kabila wako na tabia hiyo. Hisia hiyo inaimarishwa kama mtu anatendewa vibaya mara kwa mara na mtu wa hiyo kabila au mambo mabaya yanafanyika wakati yeye ni mdogo.
Migogoro ya muda mrefu katika ya makabila mawili yanaweza kuzalisha vizazi vya watu ambao wana chuki dhidi ya kila mmoja.
Mtoto anaposikia wazazi wake na watu wengine wazima wakiongea kuhusu kuhusu kabila fulani, maoni yake kuhusu hilo kabila yanatengenezwa.
Mkristo anapaswa kuchunguza mtazamo wake kuhusu vikundi vya makabila. Na aombe Mungu amsaidie ili aweze kuonesha haki na upendo. Tukumbuke kuwa Mungu anajali kuhusu wengine kama vile anavyojali kuhusu sisi na hafurahii tunapowatendea wengine bila haki.
Ubaguzi katika Huduma
Hadithi ya agano la kale ya Yona inafundisha. Yona anatuonesha kwa nini alimtoroka Mungu:
Akamwomba Bwana, akasema, “Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndio sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshih; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa Rehema, nawe waghairi mabaya! Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi” (Yona 4:2-3).
Yona alikimbia kutoka kwa Mungu kwa sababu ya chuki yake kubwa sana kwa Waashuru na kwa sababu alijua kwamba Mungu alimwita kufanya kazi kati ya watu wa Ninawi ilimaanisha ya kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa Mungu angekuwa mwema kwao.
Biblia inafundisha kwamba wanadamu wote ni jamii moja - jamii ya wanadamu: “Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakat alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makaazi yao” (Matendo ya Mitume 17:26).
Mungu analitaka kanisa kufikia kila kabila duniani na injili (Matendo ya Mitume 1:8). Thamani ya roho ya mwanadamu ni sawa bila kujali kabila lake.
Kutoheshimu makundi ya Watu
Kwa sababu watu huwa wanakubali vipaumbele vya kidunia wao hutumia njia siziso sahihi za kutambua thamani ya watu. Jamii nyingi zinawagawanya baadhi ya watu kama wasio na umuhimu sana na huwachukulia kana kwamba wao ni chini ya binadamu.
Hapa chini ni orodha ya mifano ya namna ambazo jamii mbalimbali zimewatendea baadhi ya makundi ya watu bila heshima. Baadhi ya hivi vitendo ni ya kihistoria; na vingine bado vinatendwa.
Mifano halisi ya kutoshemu makundi ya watu:
Wazee hawana manufaa tena, kwa hivyo wanawachwa mahali pa pekee ili wafe.
Watu wanawamiliki watu kutoka makundi fulani ya kikabila kama watumwa na wanaweza kuwauza au kuwatendea vile wanavyotaka.
Matangazo ya biashara yanasema kuwa watu wa kabila fulani hawataajiriwa.
Wanawake wanachuliwa kuwa mali ya waume zao na watatendewa vile waume wao wapendavyo.
Watoto wasichana wanawachwa kufa kwa sababu familia walitaka mtoto wa kiume.
Serikali ya kitaifa inapeleka wanajeshi katika eneo fulani la inchi kuua kila mtu wa kabila fulani.
Watoto huachwa kwa sababu wana ulemavu wa kiakili au wa kimwili.
Taifa lina sheria zinazokataza mwanamke kuendesha gari au kupata elimu ya chuo kikuu.
Watu wanozungumza lugha ya kawaida ya kitaifa lakini sio lugha inayotumika kwenye shule hawaruhusiwi kujisemea katika afisi za serikali.
Watu wanaajiriwa kwa sababu kwa sababu wana majina ya kingereza badala ya majina ya kiafrika.
Wasichana wanawezwa kuuzwa utumwani au kwenye ukahaba na baba zao.
Watoto wanauawa kabla ya kuzaliwa kwa sababu mama hayuko tayari kupata Watoto.
Baadhi ya filosofia na dini zinaunga mkono unyanyasaji wa makundi ya watu.
Wanaugeuzi wasio mwamini Mungu hawaamini kuwa watu wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Wanaamini kwamba mwanadamu wa sasa wamekua kimaendeleo kwa kushindana na kuharibu makundi dhaifu na yasiyo na akili ya wanadamu. Waliamini kuwa “kuishi kwa walio na nguvu”- ndiyo kumetuzalisha. Kama hiyo ingekuwa ukweli basi ingekuwa vyema kwamba watu waendelee kuharibu aina dhaifu za binadamu. Lakini tunajua kuwa watu wote waliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa hivyo wako na uhusiano wa pekee na Mungu.
Mataifa mengi ya dunia yanaruhusu madaktari kuua Watoto kabla hawajazaliwa. Serikali zingine wamelazimisha mauji ya Watoto kwa sababu ya idadi kubwa ya watu. Katika mataifa mengi, wamama huomba madaktari kuua watoto kabla hawajazaliwa kwa sababu hawako katika hali nzuri ya kuweza kupata mtoto. Hii inapuuza thamani ya binadamu na haki za mtu ambaye hawezi kujisemea mwenyewe.
Dini kama vile Uhindi na Ubudha zinaamini kuwa watu wanateseka kwa sababu ya matendeo yao mabaya katika maisha yao ya hapo awali. Wanaamini kuwa watu waliodhulumiwa wanastahili hadhi waliyo nayo. Wanaamini kuwa mtu akiweza kustahimili vyema mateso na dhuluma, anaweza kuwa na maisha mazuri wakati mwingine. Hizo dini zinatoa sababu ndogo kumsaidia mtu aliyedhulumiwa, kwa sababu ya kufikiri kwamba mtu anapitia mchakato unaohitajika.
Falsafa na dini potovu husababisha watu kuvumilia unyanyasaji wa kutisha wa tabaka za watu. Jamii zinakubali hali za ukosefu wa haki uliokithiri katika jamii kama kitu cha kawaida. Wakristo wako tofauti. Fundisho la ukristo la uumbaji maalum kwa sura na mfano wa Mungu hutoa msingi wa kutosha wa thamani ya binadamu.
► Ni aina gani ya kutoheshimu kundi la watu ni jambo la kawaida katika jamii yako?
Jirani Mwema
Kama ilivyo mifano mingi ya Yesu, hadithi ya Msamaria Mwema (Luka 10:29-37) iliwashangaza wasikilizaji wake. Alipowaambia namna ambavyo kuhani na mlawi walivyompita mtu aliyejeruhiwa bila kumsaidia hakuna mtu aliyeshangaaa. Makuhani na walawi walikuwa sehemu ya taasisi za kidini lakini watu walifikiri walikuwa wameharibiwa na fedha na madaraka.
Wasikilizaji walitarajia mtu wa tatu awe shujaa wa hadithi, lakini walishtuka na kukataa tamaa kwa sababu alikuwa Msamaria. Wasamaria walikuwa ni mchanganyiko wa kikabila, na walichanganyikiwa kidini. Wayahudi waliwadharau kwa sababu ya hizo sifa zote mbili.
Kumbuka, Mwanasheria Myahudi alikuwa amemuuliza Yesu swali, “je jirani yangu ni nani?” alikuwa anataka yesu afafanue watu ambao yeye angewapenda, akipunguza ili liwe kundi godola wale awapendao. Kama watu wengi wa dunia, alidhani kuwa wajibu wa kimaadili ulikuwa tu wa kikundi fulani cha watu waliochaguliwa, na kwamba hakukuwa na sababu ya kujali wengine.
Yesu alimjibu swali kwa kumuonyesha kwamba inatupasa tujali mtu yeyote tunayekutana naye. Mtu yeyoye tunayekutana naye ni jirani yetu. Lakini pia yesu alijibu swali ambalo hakuna mtu yeyote alikuwa ameuliza, “Nani jirani mwema?” Au “Mtu aina gani anaonyesha upendo kama huu?” Alionyesha kuwa mtu ambaye haheshimiwi na jamii anaweza kuwa mtu ambaye anampendeza Mungu kwa kuwa anaonyesha upendo ambao Mungu anataka kuona.
Mtume Yakobo analionya kanisa kuheshimu watu kwa viwango vya ulimwengu.
► Mwanafunzi asome Yakobo 2:1-9 kwa niaba ya kikundi. Umeona Makanisa yakifanya nini ambacho kina mahusiano na haya?
Watu ambao wanachukuliwa kuwa muhimu duniani sio watu ambao wanaheshimiwa mbele za Mungu. Watu wengi ambao wanampendeza Mungu hawaheshimiwi hapa duniani. Yesu alinena kuwa katika umilele hadhi za watu wengi zitabadilishwa (Mathayo 19:30).
Wakati ndugu wakristo wanapokuja pamoja, yule mtu maskini anapata hadhi ambayo asingeipata kule duniani, kwa sababu anaheshimiwa kama ndugu mkristo. Mtu tajiri anapoteza hadhi yake aliyonayo hapa duniani, kwa sababu fedha haimuweki juu ya wengine kanisani (Yakobo 1:9-10).
Utumwa
Utumwa ni hali ambayo mtu anamilikiwa kama mali ya mtu mwingine. Katika mataifa mengi ambayo yanakubali utumwa, mtumwa hana haki kama binadamu. Mmiliki anaweza kufanya lolote atakalo kwa mtumwa kana kwamba mtumwa ni mnyama au mashine. Matakwa binafsi ya mtumwa yako chini ya mapenzi ya mmiliki. Mume na mke wanaweza kutenganishwa na mmiliki, na Watoto wachukuliwe kutoka kwa wazazi wao.
Katika Agano la Kale, Mungu aliweka sheria za kumiliki mtumwa kuwa finyu na akalinda haki fulani za watumwa. Kujali haki za watumwa haikuwa jambo la kawaida nyakati hizo. Katika Agano Jipya Mungu anasema kuwa yeye ndiye Bwana Mkuu wa watu wote, hapendelei mtu yeyote kwa sababu ya hadhi yake na Bwana wa watumwa ni sharti awe mwenye upendo (mkarimu) na mwenye haki (Waefeso 6:9). Kanuni ya kwamba mtumwa anapaswa kutendewa kwa kuzingatia kile anachostahili kila mwanadamu ilipelekea kukomeshwa kwa biashara ya watumwa katika mataifa mengi ambayo yanashiwishika na mandiko ya Biblia.
Utumwa bado upo sehemu nyingi duniani katika njia au namna tofauti. Kwa mfano, sehemu fulani watoto wanauzwa na wazazi ili kufanya kazi au kwa sababu za ngono. Wakati mwingine watoto wanapelekwa katika mahekalu ya kipegani ili kukombolewa kutoka kwa magonjwa na laana. Wakati mwingine wanawake wanalazimishwa kuwa makahaba kinyume cha mapenzi yao. Wakati mwingine watu wanaingizwa katika nchi nyingine kwa madhumuni ya kufanywa watumwa.
Ukandamizaji wa kiuchumi
Sehemu ambazo zinakosa uhuru wa kiuchumi, hali inaweza kufanana na utumwa. Watu hawana uhuru wa kuendesha au kufanya biashara zao. Kuna fursa ndogo kwa mtu kubadilisha kazi yake kwa kitu bora. Wanaume wengine hufanya kazi kwa ujira ambao hulisha familia zao kwa shida. Mara chache hununua chochote isipokuwa chakula cha msingi. Hawawezi kumudu huduma ya matibabu. Hata wafanye kazi namna gani hawataweza kuwa na nyumba nzuri za kuishi kwa sababu fedha walizo nazo hazitoshelezi mahitaji yao. Waajiri wao hawalipi zaidi kwa sababu wanaweza kupata wafanyakazi ambao wako tayari kulipwa mishara midogo.
Ukandamizaji wa kiuchumi ni swala ngumu na lenye changamoto na ambalo lawama sio tu ya waajiri pekee yao. Baadhi ya mataifa kuna wafanyakazi wengi ambao wanapatikana lakini kuna upungufu wa viwanda na biashara kubwa kubwa. Kama serikali ni nyenye ufisadi, inaweza kuzuia biashara za wiwango kubwa kuanza kwa kudai ushuru wa kiwango cha juu na hongo. Kama biashara nyingi zinaruhusiwa, mishara ya wanyakazi itakuwa ya kiwango cha juu kwa sababu wafanyakazi watakuwa na uhuru wa kuchagua pale ambapo wangependa kufanya kazi na watavutiwa kwenye biashara ambazo malipo ya mishahara na hali ya kazi ni nzuri. Kwa sababu biashara chache zinaruhusiwa na wafanyakazi wana chaguzi chache za kikazi, waajiri wanaweza kulipa wafanyakazi wao mishahara midogo. Wafanyakazi hawalipwi vya kutosha kutimiza mahitaji yao.
Madhumuni ya serikali ni kuwatumikia wanainchi kwa kuwalinda kutokana mashumbulizi na kulinda uhuru wao. Uhuru wa msingi wa binadamu ni: haki ya kuzungumza maoni yake, uhuru wa dini, kufanya kazi kwa faida, na kumiliki mali. Mtu ambaye haruhusiwi kufanya vitu hivi hatendewi vyema kama binadamu.
Wakati mwingine wakristo wakiwa mahali fulani hukubali hali ya ya unyanyasaji kama ni kitu cha kawaida na hawafanyi lolote kusaidia wale ambao wananyanyaswa kiuchumi.
Jamyla aliishi katika kijiji kidogo ambapo hakukuwa na ajira. Aliwawacha Watoto wake watatu chini ya uangalizi wa bibi yao na akaenda mjini kufanya kazi kama msaidizi wa nyumbani katika nyumba ya mchungaji ambapo alikuwa analipwa 50$ kwa mwezi. Ilikuwa ni nadra sana kuwaona watoto wake. Watu wengi hawaoni kama ni jambo nzuri kwa mama kutengana na watoto kwa ajili ya kazi, lakini wakristo huajiri watu kama hawa walio katika hali ya Jamyla. Wanashanga kwa nini walipe zaidi ilihali kuna mtu ambaye yuko tayari kulipwa huo mshara mdogo. Kwa nni wawe na wasiwasi kuhusu yeye kutenganishwa na watoto ikiwa yeye alifanya uamuzi wa kuwaacha Watoto na kufanya kazi?
► Je, wakristo wana wajibu wa kuingilia kati katika hali ya Jamyla? Kwa namna gani?
Kitabu cha Amos mara kadha kinazungumzia kuhusu ukandamizaji wa kiuchumi. Katika Amosi 5:11-12 nabii anaongea kuhusu rushwa ambavyo inafanya hakimu apendelee yule mtu aliye na fedha na kufanya haki isipatikane kwa wale walio maskini. Katika Amosi 8:4-6 nabii Amosi aliwashutumu watu waliotumia vipimo vyenye uwongo kuwandanga masikini. Katika Amosis 4:1 alisema kuwa wanawake pia ni wenye hatia kama wataishi kwenye anasa ambazo waume zao walipata kwa njia ya kukandamiza maskini. Nabii alisema haki inapaswa kumwagika kama mto (Amosi 5:24), ikimaanisha kuwa ni lazima iwe tele na ipatikane kwa yeyote anayehitaji.
Thamani ya Mwanadamu na Majukumu ya Mamlaka
Ukweli Kwamba kila mtu ana uthamani usio na kikomo haimaanishi kwamba Kusiwe na muundo wa mamlaka miongoni mwa watu. Thamani sawa haimaanishi mamlaka sawa. Kwa mfano, ingawa kila mtu kwenye utatu ni Mungu kikamilifu, Mwana yupo chini ya Baba (Yohana 6:38). Mungu ameamuru mke awe mtiifu mumewe; hiyo haimaanishi kuwa yeye ni duni kuliko mume (Waefeso 5:22). Mungu amewaambia Watoto watii wazazi wao; hiyo haimaanishi kwamba hao ni wa chini kuliko wazazi isipokuwa tu katika makuzi (Waefeso 6:1).
Mungu ndiyo ameweka serikali (Warumi 13:1-5). Ameweka pia mamlaka kanisani (Waebrania 13:17).
Viongozi wote ni lazima wakumbuke kuwa hao ni watumishi (Mathayo 20:25-28). Kutumikia kwa kuongoza inamaanish kuongoza kwa faida ya wale ambao ni wafuasi. Kiongozi haongozi kwa sababu ya faida yake binafsi lakini anajitolea kibinafsi bila kuzingatia faida yeyote kwa ajili ya kuwatumikia wale ambao wanamfuata.
► Je unawezaje kueleza ukweli kwamba kimsingi baadhi ya watu watu ni mhimu zaidi kuliko wengine na kwa maana nyingine watu wote ni sawa mbele ya mungu?
Matumizi ya mafunzo haya katika Maisha ya kila siku ya wakristo
Hakikisha kuwa watu wote wanatedewa inavyostahili na familia ya kanisa.
Wazee na watu wenye umri wanakumbukwa na kusaidiwa kama inavyohitajika?
Watoto wanathaminiwa na kupewa mafunzo na kutiwa moyo kulingana na viwango vyao vya ukomavu?
Watu maskini wanakaribishwa na kufanywa kujisikia vizuri na uhuru katika kanisa lako?
Unaepuka kuwaheshimu na kuwatambua watu kanisani kwa sababu ya mali zao au hadhi katika jamii?
Je watu wote wa kabila zote wanakaribishwa kwenye ushirika na kushiriki katika maisha na huduma ya kanisa?
Kuna kundi lolote la kikabila ambalo linahitaji kufikiwa na injili ya Yesu Kristo?
Kuna watu wanaonyanyaswa katika Sehemu yako unayokaa na wanahitaji mtu wa kuwatetea?
Familia ya kikristo lazima ioneshe kwa vitendo thamani ya watu wote. Mke na mume wote lazima waheshimiwe. Mahitaji yao lazima yazingatiwe. Watoto wasipuuzwe au kuchukuliwa kama hawana maana. Watoto wanapaswa kuwa na nidhamu ipasavyo. Hauna haki ya kuwa mkatili kwa watoto wako au mke zaidi sana huna haki ya kumtendea jirani yako hivyo.
Tunapaswa kusaidia maskini katika njia inayoimarisha na kujenga utu wao. Usitoe hadharani ili kujipatia heshima huku ukiwadhalilisha maskini. Ukimpa maskini kwa njia ya haki ili kujipatia kile anachohitaji, heshima yake inalindwa na anaweza kufanya uchaguzi, na anaweza kufanya kazi kwa ajili ya faida. Msaada mzuri ni ule ambao utampa maskini nafsi ya kubadilisha hali yake.
Manabii wa Agano la Kale walisisitiza kwamba Mungu anataka watu wake wawawekwe huru wale waliodhulumiwa na kunyanyaswa (Isaya 58:6).
Agano Jipya linasisitiza ukweli kwamba Yesu alikuja kati ya maskini. Alizaliwa mahali ambapo wanyama walihifadhiwa. Wengi wa marafiki na wafuasi wake walikuwa watu wa kazi na watu maskini. Yesu alionyesha kujali watu ambao hawakuwa wa maana katika jamii yake: maskini, wenye ukoma, wajane, wageni, na watoto. Alisema alikuja kuwaletea maskini habari njema. Alisema kwamba injili itawaweka huru waliokandamizwa.
Tangu siku za kanisa la kale, Wakristo wamekuwa watendaji katika jamii zao, Wamewachukuwa Watoto waliowachwa majumbani kwao. Kuwakomboa watumwa na kusaidia wagonjwa. Wamekuwa na moyo wa kujalia watu ambao jamii yao iliwaona kuwa hawana thamani.
Yesu alisema kwamba tunapaswa tuombe kuwa ufalme wa Mungu uje na mapenzi yake yafanyike hapa duniani kama vile mbinguni (Mathayo 6:10). Tunajua kuwa dhuluma zote zitaisha wakati ufalme wa Mungu utakapokuja kikamilifu hapa duniani. Kwa sasa hivi tuombe Mungu aingilie kati hali ya watu ambao wananyanyaswa kila mahali.
Kushiriki kwa vikundi
Katika vikundi vingi, mada hii itazua mjadala mkubwa. Baadhi ya wanafunzi wanaweza kuwa na hisia nzito kuhusu yale ambayo wamepitia au wameona.
► Ni kwa vipi mtazamo wako kwa vikundi vingine vya makabila utabadilika ukikumbuka kwamba kila mtu ana thamani kwa Mungu?
► Ni kitu gani ungetemani kufanya tofauti kwa sababu ya yale umejifunza sasa hivi kuhusu thamani ya mwanadamu? Himiza wanafunzi kushirikisha ahadi zao wenyewe zaidi ya kuonyesha hasira kuhusu yale ambayo wengine wamefanya.
► Jinsi gani thamani ya mwanadamu inavyopaswa kuathiri huduma ya kanisa?
Maombi
Baba wa mbiguni,
Ahsante kwa kutufanya viumbe vya pekee katika sura na mfano wako. Nisaidie niheshimu watu wote. Nisaidie nitubie chuki zozote nilizonazo dhidi ya watu.
Naomba ya kuwa utaleta haki kwa wale ambao hapa duniani wanatendewa visivyo kwa msingi wa kabila, jinsia, umri au sifa nyingine.
Nisaidie niwatetee walioonewa na kufanya bidii kuifanya jamii yangu kuwa bora kwa wote. Saidia kanisa na kila mtu mtu mkristo binafsi aonyeshe upendo wako kwa ulimwengu kwa njia maalum.
Amina
Zoezi la somo la 11
(1) Andika kuhusu jukumu ambalo Mungu amelipa kanisa kubadilisha vile ambavyo litawatendea watu katika jamii yake?
Kanisa linapaswa kufanya nini?
Wakristo binafsi wanahitaji kufanya nini?
Wewe utafanya nini?
(2) Soma kumbukumbu la Torati 24:10-22. Orodhesha amri zinaonyesha thamani ya watu. Eleza nia ya kila amri.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.