Martin Luther alijibadilisha kuwa mtawa kwa sababu alidhani kwa kufanya hivyo anatumikia Mungu kwa njia iliyo bora zaidi. Nidhamu ya Maisha ya watawa ilijumuuisha utaratibu makini kwenye mpangalio wa chakula, kufunga, kuvaa mavazi ya kawaida, uchache wa mali na useja. Adhma ya Martin ya kuutoa sadaka mwili wake kwa mungu ilimfanya pia auadhibu mwili wake kwa kuuchapa viboko. Baada ya Martin kuelewa ya kwamba injili ya wokovu kwa neema kupitia njia ya Imani, alitambua ya kwamba asingeweza kupata neema kwa kutesa mwili wake. Alibadilisha msimamo wake kuhusu viapo ya kitawa kuwa hazima msingi kwenye Biblia. Baadaye alimuoa Katherina ambaye alikuwa mtawa wa kike na wakabarikiwa kuwa na Watoto sita kwenye ndoa yao.
Utangulizi: Kuchanganyikiwa huko Korintho
Baadhi ya watu huko Korintho hawakuamini kuwa wakristo watafufuka: Walifikiria ya kwamba mwili wa binadamu utaharibiwa baada ya kifo na ni roho tu ya wakristo ndiyo itaenda mbiguni.
Wengine walisema, “Kwa vile mwili utakufa na utaharibiwa, haijalishi tunafanya nini na mwili sasa hivi. kuutumia mwili kwa vitendo vya dhambi haijalishi, kwa sababu mwisho mwili hauna thamani yoyote.”
Wengine waliopinga ufufuo walisema, “Mwili utatupwa kwa sababu tamaa zake ni mbaya. Mbiguni hatutakuwa na tamaa za kimwili. Kwa sababu tamaa za kimwili ni mbaya, hatuhitaji kuzifuata sasa hivi. Kwa hivyo tusile chakula kizuri, tuzivae mavazi mazuri na hata tusishughulike na kukutana kimwili katika ndoa. Tunafanye lolote tuwezalo tuutiishe mwili mpaka wakati tunauacha.”
Hizi zote ni dhana potofu. Yote msingi wake ni makosa. Katika I Korintho 15, Paulo anaeleza kwa nini fundisho la ufufuo wa Kristo ni la muhimu.
Ingawa ni vyema sisi tuweze kuongea zaidi kuhusu maisha ya kiroho kuliko maisha ya kimwili, miili yetu huathiri masuala ya kiroho. Mungu alituumba siyo tu kama viumbe wa kiroho bali wenye roho iliyo ndani ya mwili pia. Sisi siyo tu wanyama wa kawaida, lakini pia siyo viumbe tu vya kiroho ambavyo vinakaa kwenye mwili kwa muda.
Kujiweka Wakfu kwa Mungu
► Mwanafunzi asome 1 Wakorintho 6:19-20 kwa niaba ya kikundi.
Mistari hii inatueleza kwamba miili yetu ni mali ya Mungu kwa sababu ametukomboa. Miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu na hivyo isitumike kufanya dhambi.
Bibilia inatueleza kwamba mwili wa nyama lazima ukabidhiwe kikamilifu kwa Mungu.
► Mwanafunzi asome Warumi 12:1 kwa niaba ya kikundi.
Huu mstari unatueleza ya kwamba miili zetu lazima iwe mitakatifu kwa sababu ni mali ya mungu. Ibada ambayo mungu anataka kutoka kwetu ni kutii kikamilifu.
Hatuwezi kumtumikia Mungu kwa uthabiti kama bado hatuna uwezo wa kudhibiti tamaa zetu za mwili. Tabia yeyote ya dhambi ni kama uraibu (mazoea ya tabia mbaya).
Fikiri kuhusu mnyama aliye na mabwana au waajiri wawili. Mwajiri mmmoja anatoa amri, lakini mnyama hawezi kutii kwa sababu mwajiri ule mwingine amefunga mnyama kwenye mnyororo. Mwajiri mwenye mnyororo anaweza kuvuta mnyama popote atakapo. Mnyama anaweza kuwa na upendo zaidi kwa yule mwajiri mwingine, lakini hawezi kumtii. Hivyo ndivyo mazoea ya tabia mbaya yalivyo. Mtu angependa kumtumikia Mungu lakini mazoea ya tabia mbaya ni kama nyororo ambao inakuwa ni vigumu kuushinda/kuukataa.
Mazoea ya tabia mbaya na aina nyingine za dhambi uharibu mwili na akili. Kwa sababu mili zetu ni mali ya Mungu una imewekwa wakfu kumtumikia, itakuwa ni vibaya tukiiharibu. Mhustari tuliosoma kwenye kitabu cha Warumi unatueleza tutoe miili yetu kama sadaka kwa Mungu lakini hatuwezi fanya hivyo kama hatuwezi kujidhibiti wenyewe.
► Mwanafunzi asome 1 Wakorintho 9:24-27 kwa niaba kikundi.
Mwili wako ni Mtumishi wako, unapaswa kuudhibiti. Ni Mtumishi mzuri sana. Endapo utakosa udhibiti, unakuwa bwana wako, na mwili ni bwana asiye mzuri kabisa (mkorofi). Paulo alisema kwamba alikataa kuruhusu tamaa za mwili kumtawala (1 Wakorintho 6:12).
► Mwanafunzi asome Warumi 6:13 kwa niaba ya kikundi.
Mwili ni kama seti ya zana ambazo unamiliki. Zana ziko chini ya mamlaka yako. Hauzitumii tena kwa kutenda dhambi lakini kwa ajili yaMungu.
Tamaa za Asili
Kuna baadhi ya watu ambao wanafikiria kwamba hatuwezi kuepuka dhambi kwa sababu ya tamaa zetu za asili. Ni kweli kwamba tumezaliwa na asili ya dhambi ambayo inatufanya tutende dhambi. Asili hiyo inajuumuisha sio tu tamaa za kimwili lakini pia tamaa za akili na utashi unaoegemea kwenye dhambi. Mtu ambaye hajazaliwa upya na Roho wa Mungu hana uwezo wa kujizuia kufanya Dhambi, ingawa anaweza fanikiwa kwa kiwango fulani kujizuia baadhi ya dhambi. Mwenye dhambi ambaye hajapokea neema ya mungu anaweza asiamini kwamba anaweza kuishi maisha ya ushindi.
Tamaa za asili siyo ndiyo tatizo. Ni Mungu ndiye aliyeumba tamaa hizi za asili. Adam alikua na tamaa za asili na hakua mwenye dhambi mpaka alipofanya uchaguzi wa kutomtii Mungu. Hizi tamaa ni sehemu ya vile ambavyo Mungu alikusudia mwanadamu awe. Tamaa zenyewe siyo dhambi, lakini zinafanya uwezekano wa majaribu kufanyika.
► Mifano ya tamaa za asili ni nini?
Chati ifuatayo haijaweka kila kitu, lakini inatupa mifano ya tamaa za asili, baadhi ya kawaida na matumizi bora ya hizi tamaa na baadhi ya njia ambazo hizi tamaa zinaweza kufanya majaribu yafanyike.
Tukizitazama tutaona ya kwamba tamaa za asili sio lazima ziwe ni kama tamaa za mwili. Ni asili kwa sababu zinatoka katika asili ya mwanadamu, ingawa zote sio tamaa za kimwili.
Makundi ya Tamaa za asili
Mfano wa utumiaji bora wa tamaa za asili
Uwezekano wa dhambi
Kujihifadhi
Kuchukua tahadhari za usalama
Uwoga
Kukubalika mbele ya wengine
Kuvaa kwa ungalifu, kuonyesha heshima
Kiburi, wivu
Kuridhika kimwili
Kula chakula, kulala, na kuwa na tendo la ndoa kwenye ndoa
Kujifurahisha kwa dhambi
Kufurahia kijamii
Kuwa na ushirika na wengine
Usengenjaji, uzushi
Faraja ya kimwili
Kupendelea utulivu na amani
Uvivu, tamaa ya mali
Uthabiti wa kifedha
Kuweka akiba na kufanya uwekezaji
Ufisadi, udanganyifu
► Kuna tamaa yeyote ya asili ambayo unaweza kutii daima?
Hakuna tamaa yeyote ya asili inaruhusiwa kutuongoza bila kujiuliza maswali. Hakuna tamaa ya asili ambayo utafuatwa daima na kwa usalama kwa sababu tamaa haiweki ukomo wa yale yanayofaa kwako. Kwa mfano, hamu ya njaa haitofautishi kati ya chakula chako na cha mtu mwingine au uwezo wa mtu kununua chakula.
Kuna wakati ambapo kudhihirisha kihalali hisia hata kama ni nzuri ni lazima uzuiliwe. Sio kwa sababu mtu anahisi njaa ina maana kuwa anaweza chukua chakula cha mwenzake. Nikawaida kutamani kupumzika lakini wakati mwingine utafanya kazi hata ukiwa umechoka. Ni kawaida kwetu kuepuka hatari, lakini lazima mtu akabiliane na ushawishi wa kutaka kuepuka hatari anapotakiwa kuwajibika ili kumuokoa mwingine.
Hamu za kawaida zinaweza kuharibiwa na kufanywa kukosa mwelekeo hadi kuchukua mtindo ambao si wa kibinadamu na si wa asili. Hiyo ndiyo sababu watu hufanya mambo potovu na ya jeuri. Hamu ya asili huharibiwa na kukosa mwelekeo kwa sababu ya mafundisho potovu, kukuzwa kwa mtindo mbaya wa mawazo, kuwa katika mazingira ya dhambi, au matendo maovu ya mtu binafsi.
Kila muumini anatarajia kupata majaribu kwa sababu ya tamaa au hamu ya asili. Neema haiondoi tamaa za asili, lakini inampa mtu nguvu ya kudhibiti matendo yake na kuelekeza hamu yake kwenye mambo mazuri.
Hamu ya kawaida hufanya nidhamu ya kiroho kuwa ya muhimu ili upate ushindi wa kiroho. Neema haikuweki huru kutokana na hitaji la kutii maelekezo ya maandiko, kuhudhuria ibaada, kuutiisha mwili, maombi na kujifunza Biblia. Muumini anaye maanisha kupata ushindi wa kiroho anaweza akajiwekea mipaka ili alinde maeneo yake ya udhaifu.
Majaribu yataonekana ya kuvutia, lakini moyo ukiwa umethibitishwa katika mapenzi ya Mungu, mtu anaweza kataaa majaribu kutoka moyoni mwake (1 Yohana 5:3). Hataona kama amepoteza kile ambacho kingemfanya awe na furaha. Kwa imani atajua ya kwamba Mungu hawezi kuzuia kile ambacho hakina madhara, hata kama haoni madhara ya kile kitu ambacho kimekatazwa (Kumbukumbu La Torati 6:24). Kwa imani anajua kwamba hakuna kitu ambacho ni kinyume na mapenzi ya Mungu kitamtosheleza, kwa sababu utoshelevu wake unapatikana ndani ya Mungu (Zaburi 16:2, Zaburi 84:11).
Lishe Bora na Mazoezi
► Maandiko yasema nini kuhusu chakula?
Hakuna katazo mahususi katika Biblia kuhusiana na chakula. Katazo la kutokutumia baadhi ya vyakula katika Agano la Kale hayakuhitajika kwa Wakristo wa Agano Jipya (1 Timotheo 4:4, Marko 7:19). Kulikuwa suala la chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, lakini hiyo haikuwa kwa sababu chakula chenyewe kilikuwa kibaya, lakini ni kwa sababu watu walikula kile chakula kama sehemu ya kuiabudu sanamu (1 Wakorintho 8).
Lishe ni muhimu kwa afya ya mwili na nguvu. Kwa sababu sisi ni watumishi wa Mungu ni vizuri tuwe na afya njema. Tusijaribu kuharibu miili yetu au kuyafupisha maisha yetu kwa sababu ya lishe mbaya. Watu wengi hawana chaguzi nyingi za lishe, kwa sababu ni lazima wale kile ambacho kinapatikana na wanaweza kumudu, lakini ni vizuri wafanaye mamuzi mazuri kwa kadri iwezekanavyo. Pia ni vizuri wawafundishe watoto wao kuhusu kuchagua lishe bora.
Watu wengi ambao wana fedha za kutumia kunua chakula hutumia kwa kununua chakula kingi sio kwa sababu ni lishe lakini kwa sababu ya ladha wanazozipenda. Pia kuna jaribu la kutumia fedha nyingi kwa kununua chakula ambacho hakina umuhimu mwilini. Watu wengine huona ni vigumu kununua kitabu cha huduma chenye mafundisho, lakini wanatumia fedha kiasi hicho kwa biskuti na soda.
Mazoezi ya mwili ni ya muhimu kwa mtu ambaye anataka kuishi maisha mazuri. Mtu yeyote hatakiwi kuruhusu ukosefu wa mazoezi kumsababishia ukosefu wa nguvu au kupata uzito uliozidi ambao unaweza kumzuia mtu kufanya yaliyo mazuri kwa Mungu. Kama ajira ya mtu inahitaji nguvu za mwili hahitaji mazoezi ya ziada; vinginevyo, anapaswa kuweka mwili wake ili uwe katika hali nzuri.
Mkristo anapaswa kufikiria lishe bora na mazoezi kwa maana yeye ni wa Mungu. Japokuwa maelekezo mahususi kuhusiana na lishe na mazoezi hayapo katika Biblia. Watu lazima watafute njia na kanuni za kujitoa kwa Mungu katika hali zinazo wakabili. Lazima tuepuke kuhukumu na kukosoa wengine. Mambo haya yasifanywe sheria ya maisha ya Kiroho ispokuwa kama kipo kikundi maalum cha watu ambao wameamua kufuata hiyo njia.
► Mwanafunzi asome Warumi 14:4 kwa niaba ya kikundi.
Ni lazima kila mmoja wetu kuzingatia kanuni za maandiko katika njia fulani, lakini tusiwahukumu wanaozitumia njia nyingine, wakati ambapo matumizi mahususi hayapo katika maandiko.
Uponyaji wa mwili wa ki-muujiza
► Mwanafunzi asome Warumi 8:18-23 kwa niaba ya kikundi.
Ugonjwa ni matokeo ya laana ambayo ilikuja kwenye uumbaji wote kwa sababu ya dhambi ya mtu wa kwanza. Mpango wa Mungu wa ukombozi utarejesha hali ya kwanza ya uumbaji na kumaliza mateso yote. Hata hivyo aya hizi zinasema urejesho hautafanyika kwa pamoja na mara moja. Japokuwa tumeokolewa tayari, miili yetu itaendelea kuzeeka na kuugua magonjwa hadi mpango wa Mungu wa ukombozi ukamilike.
Tayari Mungu hufanya miujiza katika dunia hii. Miujiza nyingi ya uponyaji imerekodiwa katika Biblia. Mungu ameahidi kuponya kupitia maombi ya imani itakayo fanywa na kanisa (Yakobo 5:14-15). Sio lazima mgonjwa awe na imani yake mwenyewe ili apate uponyaji; kanisa laweza kuwa na imani kwa niaba yake. Kwa hivyo mgonjwa asilaumiwe kwa kukosa imani.[1]
Hatutarajii kwamba mtu mwenye imani hatapata ugonjwa. Mungu aliruhusu Ayubu ateseke mwili wake kwa muda japokuwa Ayubu alikuwa mwaminifu kwa Mungu (Ayubu 2:8).
Paulo anasema Mungu aliruhusu mwiba katika mwili yake ili kumfanya anyenyekee na amtegemee Mungu. Paulo aliomba mara tatu kwa ajili ya uponyaji lakini mwishowe aligundua ya kkwamba Mungu alitaka kumpa ustahimilivu na sio uponyaji (2 Wakorintho 12:7-9). Inaonekana kwamba kuna uwezekano mwiba katika mwili wake ulikuwa ni kuugua kwa mwili wake japokuwa hatuna uhakika kwa hilo.
Paulo aliteseka alipokuwa anahubiri injili kwa Wagalatia (Wagalatia 4:13-15). Inaonesha Paulo alikuwa na shida katika macho yake, kwa sababu anawambia Wagalatia kwamba walimpenda kiasi ya kwamba wangejitolea kumpa macho yao. Hatujui kama Paulo aliponywa badaye, lakini hakuponywa mara moja. Ni wazi ya kwamba Paulo hakuundisha kwamba ni lazima kila mwamini awe huru kutoka magonjwa, na Wagalatia hawakufikiri kwamba ugonjwa wake unahitilafiana na injili aliyo hubiri.
► Mwanafunzi asome Wafilipi 2:25-30 kwa niaba ya kikundi.
Epafrodito alikuwa mgonjwa na katika hatari ya kifo. Alikuwa mgonjwa kwa sababu alifanya kazi sana kumsaidia Paulo. Paulo anasema kwamba Epafrodito anastahili heshima kwa sababu alihatarisha maisha yake kwa ajili ya kazi ya Kristo.
Mfano wa Ayubu, Paulo na Epafrodito inatuonesha kwamba hatuwezi walaumu watu kwa kukosa imani wakiwa wagonjwa. Tusichukulie ya kwamba wanadhibiwa kwa sababu ya dhambi zao. Ni Mungu pekee anayejua kama kuna sababu ya kiroho inayosababisha mateso. Baadhi wa Wakristo mashuhuri katika historia, watu wa imani kubwa waliugua kwa muda mrefu.
Biblia haizuii matumizi ya dawa na kutembelea madaktari. Hata kama tunaomba afya njema na uponyaji siyo vibaya kutumia msaada uliyo karibu.
Ni makosa kutafuta uponyaji kutoka kwa watu wanaodai kutumia nguvu za uchawi au tumia roho ambazo hazitoki kwa Mungu. Hatumtumikii shetani na hatuwezi kutafuta faida kutoka kwake. Uaminfu wetu ni kwa Mungu na tunapaswa kuridhika na baraka zake. Akichagua kutoponya tunastahili kuomba neema zake na nguvu zake na tubaki kuwa waaminifu.
[1]Yesu aliponya aliyepooza kwa sababu ya imani ya marafiki wake (Marko 2:5).
Dawa hatari
Watu wengine hutumia vitu ambayo inafanaya miili yao kuchangamka na vina matokeo mabaya.
Dawa za kulevya huharibu mwili, mawazo, na husababisha uraibu na ni kinyume cha sheria Sehemu nyingi duniani.
Isipokuwa kwa kiwango kidogo, pombe huathiri mtazamo wa binadamu na husababisha yeye kufanya na kutenda katika hali ambayo asingefanya kama asingekuwa ameathirika. Pombe inauraibu. Kwa viwango vikubwa inazorotesha afya. Inatumika zaidi katika Sehemu za burudani za kidunia zisizofaa. Biblia haijakataza pombe waziwazi lakini makanisa mengi hukataa kwa sababu inaathiri tabia, maamuzi, na inauraibu na mara kwa mara husababisha na tabia mbaya. Wakristo wengi wana wasiwasi kwamba mtu akitumia pombe kwa uangalifu huku akizuia hatari zake, anaweza kuwadhuru wengine vibaya hasa vijana.
► Mwanafunzi asome Mithali 20:1 na Mithali 31:4-5 kwa niaba ya darasa.
Tumbaku, ikivutwa au ikitafunwa mara kwa mara ina uraibu na inafupisha maisha kwa asilimia fulani. Anayetumia yuko katika hatari kubwa ya kupata saratani.
Biblia haijakataza mihadarati, pombe au tumbaku moja kwa moja. Japokuwa, watu wengi wanaoelewa madhara yake wanaamimi ya kwamba mkristo hapaswi kutumia. Hiyo haijawahi kuwa sawa hivyo kila mahali, katika nyakati kabla watu hawajajua madhara kamili ya dutu (sabstance) hizi.
Hatari iliyo kuu ya dutu hizi ni uraibu. Uraibu huongoza maisha ya Mwanadamu. Hutumia rasilimali zake. Inaathiri mtazamo wake na maamuzi na hufanya yeye kuona ni vizuri. Yeye hufanya maamuzi ambayo yanaumiza familia yake na kazi. Uraibu huo unadai uaminifu unaofanana na wa dini, na unaopingana na uaminifu kwa Mungu.
Usafi na Mwonekano
Mkristo anapaswa kuwa na tabia za usafi wa kimwili ambazo ni nzuri angalau kama desturi za kawaida katika utamaduni wake. Hapaswi kuwa na sifa mbaya ya mwili kuwa na harufu mbaya, nywele ambazo haijashughulikiwa au nguo ambazo ni chafu au zilizo katika hali mabaya. Mtu aliye katika umaskini anaweza kupata ugumu kuwa katika mwonekano mzuri lakini afanye bidii kwa kadri awezavyo.
Lazima usikilize rafiki zako wanapokukosoa kuhusiana na mwonekano wako na usafi. Wazazi lazima wafundishe watoto wao tabia nzuri.
Wakristo hawapaswi kufuatisa namna ya ulimwengu huu kwa kutumia mavazi au mapambo ili kujionyesha kuwa wao ni bora kuliko wengine. Hata hivyo kuonekana kuwa asiyejali kunaweza kuonyesha ya kwamba mtu hana heshima kwa wale ambao anakutana nao. Kwa mfano kama haujali kuvaa kwako unapoenda kwenye kikao inaweza kumaanisha hauheshimu kikao wala watu waliopo katika kile kikao. Wakristo wanapaswa kuonyesha heshima kwa Mungu na kwa wengine kwa mwonekano wao mzuri.
Watu ambao hawana vipaumbele katika maisha ya kiroho na ya milele wanatumia miili yao na mavazi yao ili wapate kutambuliwa. Mwanaume angependa kuonyesha misuli yake. Mwanamke angependa kuonyesha urembo wake wa mwili kwa wanaume. Mkristo hastahili kuonyesha maringo na kupata mtazamo mbaya kupitia mavazi yake.
Kushiriki kwa vikundi
Watie moyo wanafunzi kufikiri jinsi ambavyo kujitoa kwa Mungu kunatakiwa kuleta mabadiliko katika maisha.
►Je, tabia zako zinaoneshaje ya kwamba mwili wako ni mali ya Mungu?
Epuka mijadala mirefu yeyote ambayo inalenga kuweka sheria za lishe au vikwazo sawa kama matakwa kwa wakristo.
► Utamwelezaje mtu juu ya kwa nini hutumii vitu fulani?
Maombi
Baba wa mbinguni,
Asante kwa mpango mzuri uliotupa sisi wa kuishi kwanza duniani na baadaye mbinguni.
Nisaidie niishi maisha makamilifu ya kujitoa kwako nikijua ya kwamba uliniumba na ukanikomboa mimi.
Nisaidie niishi kwa huru kutoka kwa chochote ambacho kinaweza kuzuia huduma yangu kwako na kukuabudu wewe.
Asante kwa heshima nzuri kwamba niwe hekalu la Roho Mtakatifu. Nataka kuishi kwa namna inayokuheshimu.
Amina
Zoezi la somo la 13
(1) Andika jibu kwa kila swali lifuatalo katika kitabu chako binafsi (Hii sio ya kumpa kiongozi wa darasa.)
Je umejitoa kwa Mungu kikamilifu? Hii ina maanisha nini kwako?
Ni tamaa gani za asili ambazo mara nyingi hukuongoza kwenye majaribu maishani mwako?
Maandiko gani mawili au matatu ambayo itakubidi uyakariri ili yakusaidie kuyashinda majaribu haya?
Mabadiliko gani ambayo Mungu amesema na wewe ubadilishe katika somo hili?
(2) Soma 1 Wakorintho 15. Kwanza gawa vifungu katika sehemu ndogo ndogo ukieleza ujumbe katika kila sehemu hizo. Andika mstari katika kila fungu. Ni hatua gani ya kuchukua ukizingatia somo hili?
Print Course
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.