George Washington Carver alizaliwa katika utumwa Marekani miaka ya 1860. Baada ya utumwa kupigwa marufuku alitaka sana masomo. Elimu haikupatikana kwa urahisi kwa watoto wenye rangi nyeusi wakati huo lakini mwanamke mmoja mwenye moyo mkuu akamwambia, “ni lazima usome kwa kadri uwezayo halafu urudi kwa watu na kuwapa maarifa uliyojifunza.” George akaomba, “Bwana nionyeshe siri za ulimwengu,” na akasema Bwana akasema, “wewe ni kijana sana kujua siri za ulimwengu.” George baadae akaomba, “Basi Bwana, nionyeshe siri za karanga,” na anasema Bwana akaitikia. Karanga ilikuwa ni ya maana sana kwa sababu ililimwa na watu wengi maskini. George alijua ya kwamba kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na karanga itaongeza thamani ya karanga. George akagundua bidhaa 300 kutokana na karanga na bidhaa 100 kutokana na viazi vitamu. Akafundisha kilimo katika chuo cha Tuskegee kwa miaka 47 na akagundua njia zaidi za kilimo za kusaidia wakulima waboreshe ardhi yao na wapate mazao bora zaidi. George Washington Carver alikuwa Baraka kubwa kwa sababu ya imani yake ndani ya Kristo na uhakika aliokuwa nao katika uumbaji wa Mungu, ukitunzwa vizuri, unaweza kuleta manufaa mengi kwa wanadamu.
Ufafanuzi: Ekologia ni somo ambalo linaelezea jinsi ambavyo viumbe hai hutegemeana vyenyewe na pia na mazingira yao.
Mamlaka ya Mwanadamu juu ya asili
► Mwanafunzi asome Mwanzo 1:1 na 1:26-28 kwa niaba ya kikundi.
Majukumu ya mwanadamu kwa ulimwengu yamethibitishwa na ukweli ya kwamba Mungu aliumba ulimwengu kwa ajili ya utukufu wake (Zaburi 148) na akaweka wanadamu kama waangalizi. Kama watu walioumbwa katika sura na mfano wa Mungu tumeumbwa kutawala kama vile ambavyo Mungu angetawala; “atawale” kulingana na asili ya Mungu. Mzaburi anasema, “Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji la utukufu na heshima. Umemtawaza juu ya kazi ya mikono yako; umevitia vitu vyote chini ya miguu yake” (Zaburi 8:5-6). Wanadamu wana majukumu maalum katika dunia. Wao sio wanyama. Mungu aliwapa binadamu jukumu la utawala juu ya dunia na viumbe vyote vinavyoishi humo.
Mungu aliwaambia Adamu na Hawa waongezeke na wajaze nchi. Akawaambia waitiishe. Hali ya kuitawala nchi ingeendelezwa na watoto wao. Hali ya kuitiisha dunia inahusisha uvumbuzi, kujifunza kuishi mahali papya, kuvumbua na kutumia madini, kuwafuga wanyama, na kukuza teknologia.
Kila kitu kilikuwa kizuri wakati Mungu alipokiumba. Kazi ya mwanadamu ilikuwa ni kutunza bustani ya Eden (Mwanzo 2:15) ilikuwa kazi ya kufurahia na ya urafiki na mazingira. Baada ya dhambi kuingia, mazingira asili yaliharibiwa na laana, na kazi ya mwanadamu ikawa ngumu (Mwanzo 3:17-19). Dunia haina tena ukamilifu wa hapo mwanzo (Warumi 8:18-23), lakini bado inaonyesha utukufu wa Mungu katika muundo wake.
Baada ya gharika Mungu alisema kwamba mwanadamu wanaweza kula wanyama (Mwanzo 9:3). Mungu alimpa Musa sheriaambayo iliwakataza wanadamu kula wanyama wa aina fulani, lakini agano jipya linatuonesha ya kwamba sasa tumeruhusiwa kula yeyote ambae anayefaa kwa chakula (Marko 7:19, 1 Timotheo 4:4). Wanyama hawana haki yeyote ambayo inawaweka katika kiwango sawa na mwanadamu.
Jukumu la mwanadamu kuwa mwangalizi wa raslimali
Japokuwa mwanadamu ana mamlaka juu ya uumbaji haimaanishi yeye ni ndio wa mwisho katika mamlaka. Mwanadamu anawajibika kwa Mungu. Dunia na vyote ni mali ya Mungu.
► Mwanafunzi asome Zaburi 24:1 and Zaburi 50:10-11 kwa niaba ya kikundi.
Nchi ni ya Mungu. Mungu aliumba dunia ili adhihilishe utukufu wake (Zaburi 19:1), na akutane na mahitaji ya mwanadamu (Mwanzo 1:29), na dunia iwe mahali pazuri pa kuishi. Anataka tuifurahie na pia tufurahie vilivyomo. Hatuwezi kuiabudu dunia kwa sababu ni mali na kazi ya mikono ya Mungu (Warumi 1:25). Pia dunia haipaswi kuharibiwa kutokana na mbaya.
Wakati mwingine watu hupata faida kutokana kwa ardhi na pia wakati huo huo wanaiharibu. Watu huchimba madini na wanaawacha ardhi ikiwa wazi na isiyoweza kutumika tena. Wakati mwingine watu hukata miti na huacha mchanga wazi na unabebwa na maji. Wakati mwingine watu huwawinda wanyama hadi wanaisha katika eneo husika. Watu huweka takataka kwenye mito hadi maji yanachafuka yasiweze kutumika tena.
Mungu aliiumba dunia ili izalishe. Ni makosa watu kutumia ardhi kwa njia ambayo inaiharibu. Matumizi mabaya ya ardhi hayaleti sifa na heshima kwa Mungu.
Mungu aliumba ulimwengu ili utumike kwa vizazi na vizazi kwa maelfu ya miaka. Lazima tufikirie kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kizazi kijacho. Mtu anayeharibu mazingira kwa faida ya haraka haonyeshi upendo kwa jirani na kizazi kijacho.
Ungependa kufikiria ya ya kwamba miaka ishirini ijayo mtu atawaibia watoto wako? Kwa hakika hapana. Na bado watu wanawaibia watoto wao kwa kuharibu mazingira ambayo watoto wao wataishi. Kama hauna watoto wako mwenyewe basi jali watoto wa wengine ambao watarithi hiyo ardhi baadae.
Watu wengi hujali sana ile ardhi wanayoimiliki lakini hawajali sana arhi ya umma. Wakristo lazima wawe kielelezo kwa kutunza mazingira, kwa sababu tunajua ni mali ya Mungu na pia tunawajali majirani na kizazi kijacho.
Wakati wengine watu hufikiri, “hii ardhi siyo yangu, kwa hivyo naweza kuacha takataka yangu hapa,” au “naweza kata miti yote hapa hata miche ile midogo.”
► Mwanafunzi asome Kumbukumbu la Torati 22:6 kwa niaba ya kikundi.
Katika sehemu ya dunia ambako kitabu cha kumbukumbu la Torati kiliandikiwa, kuna ndege ambao wangekamatwa kwa wepesi wakiwa kwenye viota vyao. Ikiwa watu watu watamchukua mama na mayai au Watoto hao ndege hawatendelea kuwepo. Mungu aliwaambia wawachilie wamama ili aina (spishi) hii isiharibiwe. Sheria zetu leo mahali tofauti tofauti tunakoishi mambo yanaweza kuwa tofauti, lakini andiko lasema ni vizuri tutunze rasilimali katika ya ardhi ya umma.
Kutambua Uzuri wa mazingira
Mungu alipoumba mimea, hakuumba tu mboga na matunda, aliumba maua na vitu vingine vya kupendeza, hii inamaanisha kuwa Mungu hajali tu jinsi ambavyo tunatumia ardhi lakini pia anajali uzuri wake (Luka 12:27). Mungu aliumba mazingira yawe ya kupendeza ili watu waishi ndani yake.
Milima, majangwa, mito, mahali tambalale na misitu yote yana uzuri wake asili. Wakati mwingine watu waliozaliwa mahali fulani hawaoni uzuri wa mahali walipo kwasababu ya kuzoea mazingira na pia ni ya kawaida kwao.
► Tafakali ya kwamba wewe ndiwe msanii, fikiri ya kwamba unatumia wakati mwingi kuchora michoro na kupaka rangi na kisha unampatia rafiki. Halafu, wakati mmoja umtembelee na kisha uikute ile zawadi yako chini na imeharibiwa kwa kukanyagwa. Utajisikiaje?
Kuna jamii nyingi ambazo watu hutupa takataka zao chini. Wanang’arisha viwanja vya maeneo ya kwao lakini wanatupa takataka mahali popote. Mitaa ya jirani zao imejaa takataka.
► Ni kitu gani hawa watu wanahitaji kufahamu?
Lazima tutunze maeneo ambayo sisi hushiriki kwa pamoja, kwa ajili yetu na ya wengine pia.
► Kanisa lifanye nini ili kubadilisha walio karibu nalo?
Matumizi ya Wanyama
Wanyama ni tofauti na wanadanu. Hawajaumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Na hawana umilele (Mhubiri 3:21) na hawana haki za wanadamu.
Mungu aliwapa wanadamu ruhusa ya kula wanyama, ambayo humaanisha mwanadamu anaweza kuwinda wanyama kwa chakula na pia awafuge wanyama nyumbani kwa sababu ya chakula.
Katika historia pana ya mwanadamu pia imekuwa kawaida kwa mwanadamu kufuga wanyama ili awafurahie au pia wamfanyie kazi.
► Je Mungu hujali jinsi ambavyo tunatunza wanyama wetu?
► Mwanafunzi asome Mithali 12:10 kwa niaba ya kikundi.
Kifungu hiki kinatueleza kuhusu tabia ya mtu mwadilifu ya kwamba hutunza Wanyama wake kwa njia iliyo bora. Ukatili ni tabia ya watu waovu.
Mtu ambaye anamiliki mnyama lazima ahakikishe kwamba yule mnyama anapata chakula, maji na mahali pa kulala. Kuna kitu abacho si sawa kwa mtu ambaye hatunzi na hajali mahitaji ya wanyama.
Kumbuka wanyama wote ni wa Mungu (Zaburi 50:10-11). Wote wameumbwa na Mungu. Aliwaumba katika maumbile tofauti. Angewafanya wachache kwa ajili ya chakula na kazi, lakini aliwafanya wengi maelfu ya aina na jamii za wanyama pamoja na wadudu na wale ambao hawaonekani kwa macho pia. Maajabu na uwezo wa Mungu unaonekana katika uumbaji wa aina tofauti za wanyama na wadudu.
Wanyama wengine wanauwezo wa kuonyesha shukrani na unyenyekevu kwa wanaowatunza. Wanapenda kutunzwa na wanadamu na wanajifunza kujibu. Wana ya kutosha kujinza mambo mengi. Ni dhahili ya kwamba Mungu aliwafanya ili waweze kwa njia moja amab nyingine wawasiliane na mwanadamu. Mungu aliwapa wanyama heshima maalumu kwa wanadamu (Mwanzo 9:2).
Mungu aliwaumba wanyama na maarifa na hali ya kuwasiliana na watu. Kuwanyanyasa wanyama ni kutoheshimu mpango wa Mungu. Zaidi ya hayo ni vibaya sana kwa mtu kufurahia kuumiza wanyama na kuwasababishia uchungu.
Maandiko yanatumia sana kielelezo cha mchungaji. Daudi alikuwa mchungaji kabla hajakuwa mfalme wa Israeli. Daudi aliandika Zaburi 23 akilinganisha Mungu na mchungaji mwema, Daudi aligundua ya kwamba Mungu huwatunza watu wake vile ambavyo mchungaji huwatunza kondoo wake. Katika Agano Jipya, watumishi wa Mungu hulinganishwa na wachungaji (1 Petro 5:2 na kwingine). Kulinganishwa huku kusingeleta maana kama Mungu asingetaka tuwatunze wanyama.
Mafunzo ya Daudi kuwalea wanyama ni sehemu ya mafunzo ya kuwatunza watu. Katika njia hio pia, Mungu ametuamini kutunza ardhi na wanyama na kwa njia hiyo tunaandaliwa tuweze kuwatunza wenzetu.
Umuhimu wa kijani
Kijani kibichi ni rangi ambayo inaonekana sana katika mazingira yetu ispokuwa tu mahali ambapo hakuna maji au udongo mzuri. Ni rangi ambayo huyapa macho yetu utulivu.
Wengi ambao wanaishi katika miji hujisikia vizuri wanapotoka mijini na kwenda katika maeneo yenye kijani cha asili.
Miji mingi haina mimea. Mchanga wake umefunikwa kwa rami au simenti. Mahali pengine wameanza kutengeneza bustani na mahali penye kijani katika miji. Watu kila mahali lazima wafanye bidii kupanda miti na mimea iweze kukua. Wanapaswa kuhifadhi ukijani kwa ajili ya watu kufurahia na hasa kwa watoto kucheza. Familia pia zaweza kuwa na nafasi zenye kijani katika viwanja na nyumba zao kwa kupanda mimea.
Tofauti ya Ikolojia ya mkristo.
Mwanzo wa somo hili kuna maelezo kuhusu ikolojia.
► Kwa nini mkristo atunze ikologia?
Watu wengine hufikiria tunaweza kuokoa dunia kwa kuzuia uchafuzi wa hewa. Sisi wanadamu hatuwezi kuiokoa, japokuwa tunapaswa kufanya sehemu yetu kuihifadhi kwa kadri tuwezavyo. Wakristo wanajua ya kwamba hatuwezi kuitunza kimamilifu dunia inanyoharibika. Mungu hatimaye ataifanya upya dunia (Ufunuo wa Yohana 21:1). Kwa hivyo tunajua ya kwamba hatuwezi kuiokoa dunia.
Wengine hufikiri wanadamu siyo wa muhimu zaidi kuliko viumbe vingine, na ni lazima tuheshimu wanyama kwa sababu haki zao ni sawa na zetu. Wakristo wanajua Mungu alimpa mwanadamu uwezo na mamlaka ya kutawala dunia. Tunajua kwamba mwanadamu ni tofauti na mnyama kwa sababu tumeumbwa katika sura na mfano wa Mungu na tuna roho ya milele. Kwa hiyo, wanyama hawana haki zinazolingana na haki za binadamu.
Wakristo wanaitunza dunia Kwa sababu
1. Ni mali ya Mungu.
2. Wanadamu amepewa wajibu wa kuitunza dunia.
3. Tunajali kizazi kijacho cha wanadamu.
► Nini ambacho ni cha kawaida ambacho kinaonesha ya kwamba wanadamu hawana hali ya kuelewa ikolojia ya mkristo?
►Kama inawezekana kuwa mjadala wa darasa zima: Pata mtu wa karibu akafunge macho yake na aeleze kile anachokiona kila wakati anapotoka kwenye uwanja wa kanisa? Mazingira hapo nje ya kanisa yako namna gani? Kuna takataka? Panaonekana kana kwamba watu wanapajali? Nani anastahili kushugulikia mahali hapo? Eleza jinsi ambavyo washirika kanisani wanaweza kushugulikia hilo jambo. Kwa nini tushugulikie eneo hilo? Utunzaji wao unaweza kuwa na ushawishi gani kwa wengine? Wanafunzi wafikirie hivyo kwa maeneo yao pale nyumbani.
Kushiriki kwa vikundi
► Unapaswa kubadilisha tabia gani?
► Kanisa lako litaleta tofauti gani katika maeneo yake katika mafunzo na kuwa mfano?
► Je jamii yako itabadilishaje mazingira kama watu katika jamii yote wangeshirikiana?
Maombi
Baba wa mbinguni,
Asante Kwa kuumba dunia inayopendeza na rasilimali. Asante kwa kutuamini na kutupa jukumu la kutunza dunia uliyoiumba.
Tusaidie tuishi kwa shukurani kwa ajili ya uumbaji wako wa kupendeza. Tusaidie kufanya kazi pamoja ili tulinde dunia na raslimali na uzuri wake.
Amina
Zoezi la somo la 8
(1) Andika ukurasa mmoja ukieleza mpango wako wa kubadilisha tabia yako kupitia ukweli ambao tumesoma katika somo hili.
(2) Andika ukurasa ukieleza mazoea au tabia mbaya katika jamii yako. Kisha endelea kueleza jinsi ungemfafanulia mtu kwa nini mbinu hizo zinapaswa kuwa tofauti. Weka msingi wa mjadala wako katika maandiko na mtazamo wa Biblia.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.