Mau wa kiafrika alienda kumtazau mtoto wake mdogo aliyekuwa akicheza chini ya mti. Alishikwa na mshangao alipoona joka kubwa lenye sumu likininginia juu ya mti karibu na kichwa chake. Lile joka lilikusudia kumuuma yule mtoto. Mau alijua ya kwamba angejaribu kumuonya mtoto wake angeangalia juu badala ya kuondoka mahali pale upesi. Badala ya kumwelezea, alimuita, “mwanangu lala chini sakafuni sasa hivi.” Yule mvulana alichanganyikiwa, lakini kwa sababu alikuwa amefundishwa kutii, akafanya hivyo hivyo. Mau yake akasema tana “Tambaa pole pole huku ukija kwangu.” Mara nyingine tena yule mvulana akatii na akaokolewa kwenye hatari ya lile joka.
Kwa nini mtoto alitii hata kabla hajaelewa sababu ya ile amri? Aliheshimu mau yake kwa sababu alikuwa tayari amefundishwa kutii, na tayari alikuwa amewahi kurekebishwa wakati ambapo hakutii. Pia alimuamini mau yake kwa sababu alijua mau yake anampenda. Tunatakiwa kumtii Mungu kikamilifu sio kwa sababu tunaogopa adhabu yake bali kwa sababu tunajua anatupenda.
Motisha ya Upendo
► Nini kitatokea endapo mtu atampenda Mungu sana? Unaweza kuzingatia swali hili kwa kukamilisha sentensi ifuatayo: “Kama nitampenda Mungu sana nita…”
Mojawapo ya matokeo ya kumpenda Mungu sana imeelezwa kwenye kitabu cha Wafilipi 1:9-11:
Na hii ndio dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
Kifungu hiki cha Maandiko kinazungumza kuhusu mchakato endelevu katika maisha ya mwamini. Upendo wake uwe wa kuongezeka. Upendo wake kwa Mungu unakua, uwezo wake wa kupambanua yaliyo bora unafanywa kuwa bora na unapanuka. Wakati anapambanua kilicho bora, anayakita Maisha yake katika kuwa makini na kile kilicho bora zaidi. Lazima hii ifanyike ili mkristo awe mkamilifu pasipo dosari.
Kama ambavyo mtoto mchanga aliyezaliwa ana maisha ya kujifunza mbele yake, vivyo hivyo na sisi tunapofanywa upya katika maisha ya Kikristo, hatuwezi kuelewa kikamilifu ukweli unaotuelekeza katika maisha. Katika mistari iliyotangulia, Paulo anawandikia watu waliokuwa wakristo kwa muda sasa. Na bado Paulo anawaombea kwamba wampende Mungu zaidi na kwa kumpenda Mungu Zaidi wataelewa na kutii mapenzi ya Mungu.
Tunatarajia kubadilisha maisha kwa kadri Mungu anavyotupa ufunuo. Mungu anataka utii wetu kamili katika nyanja zote za maisha, sio tu katika mambo ya kiroho peke yake.
Tusipuuze na kudhani ya kwamba tunajua kila kitu ambacho tunahitaji kujua kuhusiana na jinsi tunavyopaswa kuishi. Tusidhani ya kwamba tumeshafanya mabadiliko yote yanayohitajika katika misha yetu.
Maeneo Ambayo Mkristo Anatakiwa Kubadilika
(1) Uangalifu Katika Ushawishi (Mithali 22:1; Mathayo 5:14-16)
Je kuna mambo ambayo unafanya na usingependa watu wengine wafanye? Je utasikitika ukiona mchungaji wako anafanya mambo ambayo wewe unafanya?
(2) Kiasi (Mithali 16:32, Mithali 25:28; Wagalatia 5:22-23)
Je wewe unatawala hisia na matamanio yako ili ufanye kile ambacho unapaswa kufanya au wakati mwingine unaruhusu hisia na tamaa zako kukuongoza kufanya kama yeye asiyeamini?
Je wewe hutunza mwili wako kama silaha madhubuti iliyowekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa vile mwili wako ni wa Mungu haupaswi kuharibiwa. Hautakiwi kutunza mwili wako isivyostahili.
(4) Uchaguzi wa Burudani (Wakolosai 3:17; 1 Wakorintho 6:12)
Je burudani yako husababisha majaribu ambayo hufanya wewe upapambane na majaribu kwa kukusababishia mawazo na nia mbaya? Kuwa makini sana na mambo ambayo yanawakilisha Dhambi lakini huvutia sana na kufurahisha.
Waheshimu wengine, kwa sababu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na wana hatima ya milele. Watu huwa na tabia ya kuonyesha utuwema. Lazima ujifunze kuonesha utu wema kwa namna ambayo watu watatambua. Kuwa mtu mwema hata kama watu unaowatendea wema hawastahili.
(6) Tabia Katika Biashara (Mithali 20:23)
Je wewe ni mwaminifu katika biashara zako? Je wewe hueleza vitu kama vilivyo au humfanya mtu afikirie kwamba jambo fulani si kweli?
(7) Kuwa Makini na Muda (Kutunza Muda) (Wagalatia 5:14)
Muda ni wa muhimu sana na tunapaswa kuutumia sana kwa ajili ya Mungu. Je wewe huthamini muda wako na wa wengine kwa kufuata ratiba kila panapo hitajika?
(8) Mavazi (1 Timotheo 2:9; 1 Petro 3:3-4)
Je mavazi yako yanaonyesha maadili?
Adabu – Je yanafunika mwili vizuri?
Unyenyekevu – siyo ya kuleta mvuto na umakini ambao hauitajiki kutokana na ulichovaa.
Ubadhilifu – kutonunua mavazi ya gharama ya juu kuliko unavyohitaji.
(9) Lugha (Wakolosai 4:6, Waefeso 4:29)
Je, maneno yako ni ya heshima kwa Mungu na wengine?. Maneno mengi ambayo dunia hutumia kama vifungu vya mshangao (vielezi au sauti za mshangao) hutokana na matusi au majina ya Mungu
Je wewe hutunza ahadi? Je, watu wanaweza kutarajia ufanye kile ambacho ulisema? Je huwa unasahau ahadi zako kama siyo rahisi?
Watu wengi hawatilii maanani umuhimu wao kubadilika au kujiboresha. Wanahisi kuwajibika tu katika amri zilizo wazi katika maandiko, pasipo kujua ya kwamba amri hizi hutumika sehemu nyingi za maisha ya kila siku.
Tunahitaji kufahamu ya kwamba kuwa bora kumeshikamanishwa na kuongezeka kwa upendo wetu kwa Mungu. Tunahitaji kutafakari kwa kumaanisha maandiko tuliyoanza nayo katika somo hili (Wafilipi 1:9-11). Kama upendo wetu unazidi kuongezeka, uwezo wetu wa kupambanua na kuchagua tabia sahihi utaongezeka.
Kushiriki kwa vikundi
► Ni mfano gani wa kubadilika ambao umeufanya katika maisha yako wakati ambapo Mungu alikuonyesha jambo fulani, mtazamo, nia, tabia au matendo ambayo siyo mazuri?
► Je, kuna kitu katika maisha yako ambacho unajua unapaswa kukibadilisha? Utakibadilisha?
► Je, unafanya jambo ambalo hauna uhakika kama linampendeza Mungu?
► Je, unakubali Mungu akuonyeshe katika maombi jambo lolote ambalo unastahili kulibadilisha?
Tujitoe kuomba wiki hii tukiwa na moyo ulio wazi ili Mungu atamaaonyeshe njia zake na badiliko lolote ambalo tunapaswa kulifanya katika maisha yetu. Je unajitoa kufanya hivyo? Juma lijalo nitakuuliza kama ulitekeleza.
Kanuni za Biblia za Kutekeleza Kibinafsi
► Je, meshawahi kutambua tofauti kati ya wakristo, na hasa katika mambo halisi ya kivitendo kwa yale ambayo wanafanya na yale ambayo hawafanyi? Kwa nini hizi tofauti zipo, na wakati wanatumia Biblia ile ile? Kwa sababu kunatofauti nyingi sana kwa wakristo, je yale tunayoyatenda ni muhimu? Kwanini?
Siyo wakristo wote wanakubaliana kwa pamoja juu ya undani wa jinsi ya kuziishi kanuni na maadili ya kibiblia. Lakini ni lazima kwa Mkristo kumaanisha na kuwa na uzito wa kuishi sawasawa na kile anachokiamini.
Tabia, maamuzi ya burudani na aina ya mavazi huonesha kitu kuhusiana na makusudio ya moyo.
Hapa kuna kanuni ambazo kila mkristo ni lazima azikumbuke anapojaribu kupambanua nini ambacho ni mtindo mzuri wa maisha.
Kanuni za Maamuzi Kuhusiana na Mtindo wa Maisha
(1) Lazima tutii amri amri zote za kibiblia kwa wakristo.
Yesu akasema Mathayo 5:19,
Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
Hatuwezi kuchagua tu kile ambacho tunafikiri ni muhimu zaidi. Hakuna amri katika maandiko ambayo si ya umuhimu ili yapuuzwe
(2) Amri za Mungu ni za Manufaa Kwetu.
Kumbukumbu la Torati 10:12-13,
Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?
Zaburi 84:11,
Kwa kuwa Bwana Mungu ni jua na ngao: Bwana atatoa neema na utukufu: Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu.
Mungu hawezi kutuzuilia kile ambacho ni kizuri, au kutuamrisha kufanya kile ambacho ni hatari kwetu. Tusingekuwa sawa pasipo masharti yake. Kukataaa maelekezo yake ni kutilia shaka hekima na upendo wake. Tunadhibitisha kwamba tuna imani katika uzuri na hekima yake wakati ambapo tunatii maagizo na neno lake kuliko kufuata maoni ya watu.
(3) Uhuru wa mkristo sio uhuru wa kutomtii
Paulo anaandika haya kwa wakristo 1 Wakorintho 9:21:
Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
Tunakombolewa kutokana na mfumo wa –sheria ya Musa na matakwa ya Mungu ya kimaadili kwa njia ya kuhesabiwa haki, kwa maana tunaokolewa kwa neema sio kwa kutimiza sheria za Mungu. Pia tunaokolewa kutokana na hukumu ya sheria kwa sababu dhambi tulizozifanya zimesamehewa.
Hata hivyo hatujawekwa huru kutoka katika hitaji la kumtii Mungu au jukumu la kupenda “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo” (Wagalatia 5:13). Kama 1 Wakorintho 9:21 (hapo juu) inaonyesha, sisi tuko chini ya mamlaka ya Mungu. Mapenzi yake kwetu yananadhihirishwa katika Biblia.
Ufuasi wa sheria ni neno maalum linalotumika wakati watu wanazungumzia masuala yanayohusiana na kumtii Mungu. Ni muhimu sana kuelewa maana ya kweli ya neno hili. Ufuasi wa sheria ni imani isiyo sahihi kwamba mtu anaweza kuokolewa au kukua kiroho kwa kutimiza masharti fulani, badala ya kuokolewa kwa neema ya Mungu pekee. Hata hivyo, si ufuasi wa sheria kwa mtu kuelewa kwamba anapaswa kumtii Mungu katika mambo yote ya maisha kwa sababu anataka kumfurahisha Mungu.
“Mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki” (Warumi 6:18).
(4) Kama Tunampenda Mungu Tunataka Tujue Mapenzi yake sio Kuyapuuza.
1 Yohana 5:2-3 yasema
Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
Yeremia 31:33 yasema, “Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
Mtu anayempenda Mungu hatamaaliza kwanza, “Mungu atanihukumu kwa hili?” lakini ni “Mungu atapendezwa na lipi zaidi?” au “nini ni zuri zaidi la kufanya?” (Wafilipi 1:10; Tito 3:8).
(5) Maandiko yanatupea misingi ya kujifanyia kanuni katika maisha.
Maandiko hayatoa Kanuni za ujumla tu. Maandiko kadhaa yametolewa katika Zoezi la pili ambalo linampa mkristo msingi wa kuishi Maisha makini ya kikristo. baadhi ya Maandiko yanatoa maelekezo mahususi kwa ajili ya kuishi maisha ya kikristo.
(6) Kanuni kuhusiana maelezo ya maisha sio imani yetu ya msingi.
Wafarisayo walifanya makosa ya kuweka mkazo kwa vitu vidogo. Katika Mathayo 23:23 Yesu akawaambia
Ole wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
Andiko hili halimaanishi kwamba kuna yale ambayo si ya msingi, lakini linamaanisha mengine ni ya muhimu zaidi. Tunahitaji kuongea kuhusu yalio ya muhimu zaidi.
(7) Kuzingatia Kanuni Haitoshi Kuthibitisha Utii au Upendo Wako kwa Mungu.
Katika mazungumzo hayo Yesu anawaambia mafarisayo (Mst 25),
Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano na ndani yake vimejaa unyang’anyi, na kutokuwa na kiasi.
Mtu anaweza kuishi maisha ya kujidhibiti sana lakini bado hawampendi Mungu au pia wala hamtii Mungu kikamilifu. Kwa upande mwingine mtu anaweza kumpenda Mungu kwa moyo wake wote lakini asione umuhimu wa viwango vingine vya kanuni. Kwa hivyo haimaniishi kwamba mtu anayejidhibiti sio wa kiroho zaidi.
(8) Imani yetu katika shuhuda za wengine haitegemei mambo madogo madogo ya mitindo ya Maisha yao.
Katika Warumi 14:10 Paulo anawauliza Wakristo
Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
Mstari huu unatoka katika kifungu ambacho kinajadili mitazamo tofauti tofauti ya wakristo katika maisha. Kuna maoni tofauti kuhusiana na kile ambacho wakristo wanapaswa na hawapaswi kufanya.
Muumini mwingine anaweza asikubaliane na tafsiri ya kifungu ulani cha maandiko, au asione ubaya wa kitu ambacho kimekataliwa. Inawezekana kuwa Mungu anafanya kazi ndani yake katika maeneomengine, au Mungu amemuweka mahali penye utamaduni tofauti. Hii haimaanishi kwamba Mtu huyo si mkristo wa ukweli.
► Unafikiri nini kuhusu sentensi hii? “Mungu atamuonyesha ukweli kila mtu kuhusiana na jinsi atakavyoishi; kwa hivyo, wakristo wote watakuwa na matendo sawa.”
Wakristo hawajakubaliana kabisa katika matendo mbali mbali katika maisha. Watu wanaompenda Mungu na wanaoishi katika maisha yanayompendeza Mungu hawakubaliani katika kila kiyu kuhusiana na tabia, Matendo na mafundisho. Ni vibaya sisi kusema wengine sio wakristo kwa sababu wanatafsiri na kutekeleza maaandiko tofauti na sisi. Tunaweza kuwakubali wao kama wakristo kamili japokuwa tunafikiri mawazo yao sio sawa. Kazi ya Roho Mtakatifu sio kufanya watu wote waishi maisha na tabia zinazo fanana.
Ni lazima pia sisi tuwe tayari kijifunza kutokana na mitazamo ya wakristo wengine. Kiburi hutufanya sisi tufikiri kwamba sisi au kanisa letu lina tafsiri sahihi ya maandiko. Mtu mnyenyekevu, anayefundishika, roho ya kukubali, hukuza umoja wa wakikristo na kuujenga mwili wa Kristo.
(9) Hali ya kuwa na mawazo tofauti haimruhusu yeyote kuishi maisha ya kutojali.
“Na kila mtu adhibitike katika akili zake mwenyewe” (Warumi 14:5b).
“Lakini aliye na shaka kama akila amehukumiwa kuwa ana hatia kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilo toka katika imani ni dhambi” (Warumi 14:23).
Kuna shida pale ambapo mtu anakiuka dhamiri yake. Mtu akiamua kufanya kitu ambacho anafikiri ni kibaya, yeye amefanya dhambi. Kuna Baraka wakati mtu anatembea katika nuru ambayo Mungu amempa (1 Yohana 1:7).
Kushiriki kwa vikundi
Hakutakuwa na ugumu katika kuanza kujadili juu ya mada hii. Wanafunzi wengine watapendelea kwamba makanisa yanahitaji sheria na mwongozo wa tabia. Wengine watasititiza kuvumilia tofauti.
Jaribu kuzingatia kanuni tisa ambazo tumezijadili hapo awali.
► Ni Kanuni gani kati ya hizo kanuni unafikiri watu watasahau?
► Ni Kanuni gani kati ya hizo kanuni wewe unaweza kusahau?
Nisaidie kupambanua yale ambayo yanakupendeza sana ili niishi maisha yasiyo na mawaa.
Nisaidie nione tabia na nia ambayo nahitaji kuibadilisha, ili nipate tabia na nia inayokutukuza wewe.
Nataka nizae matunda kwa ajili utukufu wako Mungu.
Amina
Zoezi la somo la 2
(1) Soma 1 Wakorintho 13. Hii sura inaeleza kuhusu mtu ambaye ana upendo ambao anapaswa kuwa nao kwa wengine. Acha Mungu akuonyeshe jinsi ambavyo angependa kukubadilisha na kufanya maisha yako yawe ya kuendelea sana katika upendo. Orodhesha mabadiliko ambayo ungependa Mungu akuwezeshe kuyafanya katika maisha yako.
(2) Soma maandiko yafuatayo ambayo yanatupatia misingi ya tabia za mkristo:
1 Wakorintho 6:19-20
1 Wakorintho 10:31
1 Wakorintho 11:14-15
1 Timotheo 2:9-10
1 Petro 3:3-4
Zaburi 19:14
Zaburi 101:3
Andika maana ya kimsingi katika kila andiko. Eleza mtindo wa maisha ambao unaamini utaishi kwa sababu ya maandiko hayo.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.