William Wilberforce (1759-1833) alikua mbunge wa bunge la Uingereza. Yeye alikua mkristo na alipinga biashara ya utumwa, ajira ya watoto na unyanyasaji wa maskini. Ilimchukua miaka ishirini kupitisha sheria ambayo ilikomesha biasahara ya utumwa ya kuchukua mateka afrika na kupelekwa kuuzwa katika dola yote ya Uingereza. Mara nyingi alipata msongo wa mawazo kuona ya kwamba wengine hawajali kuhusiana na jambo hili. Mara alipopata wingi wa kura za wabunge kuunga mkono sheria, wapinzani walishawishi baadhi ya wabunge kutohudhuria kikao cha bunge kwa kuwapa ticketi za ukumbi wa burudani na sheria haikupitishwa. Sheria ya kumaliza biasheria ya utumwa ilipitishwa mwaka wa 1807, ingawa utumwa wenyewe haukufanywa haramu. Wilberforce aliendelea na harakati zake za kuhakikisha kuwa utumwa umekomeshwa katika dola ya Uingereza. Ilipofikia mwaka wa 1833 biashara ya utumwa ilikuwa imeisha sehemu nyingi za dola ya Uingereza. Wilberforce alifariki siku tatu baada ya kupokea habari nzuri kwamba sheria ya kuharamisha biashara ya utumwa ilikua ipitishwe.
Utangulizi
Kumekuweko na tofauti kubwa wa kimahusiano kati ya wakristo na serikali zao. Wakati fulani na mahali fulani katika historia ya Kanisa kulikuwa na kanisa la kitaifa ambalo lilikuwa na ushirika na serikali. Wakati mwingine na mahali pengine serikali iliharamisha kanisa na kulitesa. Kuna mataifa ambayo yanaruhusu uhuru wa kuabudu dini yeyote na serikali haidai kupendelea dini yeyote.
Uhusiano kati ya wakristo na serikali husababisha maswali mengi magumu. Wakati mwingine kanisa likiwa pahali hujenga uhusiano na serikali ambao hauwezi kupatikana sehemu nyingine duniani ambako serikali ni tofauti.
Hili somo halitajibu kila swala au kueleza mkristo atafanya nini katika mazingira ambayo atapitia bali tutatazama kanuni kutoka kwenye Bibilia kuhusu uhusiano wa mkristo na serikali.
► Mwanafunzi asome Warumi 13:1-7 kwa niaba ya kikundi. Ni sentensi gani kuhusu serikali unaona katika kifungu hiki?
Biblia inatueleza ya kwamba Mungu ndiye huziweka serikali za wanadamu. Mungu anataka serikali iwepo na mtu anayekataa kutii serikali ya wanadamu anamwasi Mungu (Warumi 13:2).
► Kusudi la serikali ni nini kulingana na mistari hii?
Kusudi moja la serikali ni kuadhibu tabia mbaya kwa kutekeleza sheria (Warumi 13:4). Mtawala anamtumikia Mungu na hutimiza kusudi la Mungu anapoadhibu wavunja sheria (Warumi 13:4).
► Mwanafunzi asome I Timotheo 2:1-2 kwa niaba ya kikundi.
Tunahitaji kuombea kwa wale watu ambao wako kwenye serikali ili tuishi maisha yaliyo na utilivu na amani. Inatueleza ya kwamba serikali ikifanya kazi kama vile inavyohitajika inalinda amani ya jamii.
Ushawishi wa Kikristo
► Yesu alituambia tuwe kama chumvi na mwanga (Mathayo 5:13-16). Alimaanisha nini?
Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini ya kwamba wakristo hawapaswi kupiga kura au kuwa na nyadhifa kwenye serikali kwa sababu serikali za dunia hazitawali kwa kufuata kanuni za ukiristo. Wengine wanaamini kuwa kanisa inapaswa lijitenge kutoka kwa jamii kwa sababu jamii imeharibka sana.
Nabii Yeremia aliwaandikia Wayahudi ambao walikua wanaishi uhamishoni kwenye jamii ya kipagani. Hawakwenda huko kwa hiari yao. Kama kulikuwa na waumini wa Mungu walikuwa na sababu za kujiepusha na ushiriki katika jamii, hakika Wayahudi hawa walifanya hivyo. Walikuwepo huko kinyume na mapenzi yao, dini ya jamii walimo ishi ilikuwa ya kipagani, serikali ilikuwa ya dhuluma na iliangamiza taifa lao, na wayahudi walikuwa wanasubiri siku ambayo watarudi kwao.
Lakini sikiza ujumbe wa Mungu aliompa nabii Yeremia kwa hawa watu:
Kautakieni amani mji ule ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yakemji huo ninyi mtapata amani (Yeremia 29:7)
Shalom, Neno la kiebrania kwa kawaida hutafsiriwa amani, haimaanishi tu amani yenyewe bali baraka ambazo zina ambatana na amani. Linarejelea baraka za Mungu. Hawa wanao mwabudu Mungu watapata baraka za Mungu wanapojaribu kuleta hizo baraka kwenye jamii yenye dhambi na ambayo haijui lolote kuhusu Mungu na inatesa pia watu wa Mungu.
Watu ambao wanamtumikia Mungu ni lazima washawishi jamii yao kwa kuheshimu mapenzi ya Mungu ndipo jamii yao iweze kubarikiwa. Hawapaswi tu kuhubiri injili bali pia kutumia kanuni za kimungu katika kila hali na kila uamuzi.
Serikali na jamii inapaswa iboreshwe na Neno la Mungu. Kutokana na ukweli wa Mungu uliofunuliwa yanapaswa kuja maadili (kanuni na matendo sahihi), kutoka kwenye maadili tunapaswa tupate siasa (serikali ya haki na uhuru), halafu uchumi (usimamizi wa rasilimali). Kwa hivyo mpangalio sahihi wa kweli hii, maadili, siasa halafu uchumi.
1. Ukweli kutoka kwa Maandiko ya Mungu
2. Maadili
3. Siasa
4. Uchumi
Tabia ya asili ya binadamu ni kugeuza utaratibu huo. Watu hufanya uchumi wao binafso au Fedha kuwa ni kipaumbele, halafu watamaanga mkono viongozi na sharia ambazo zitawapa kile wanachotaka hata kama itamaanisha ya kwamba watapoteza haki na uhuru. Basi baaada ya kufanya hivyo wataweza kutunga maadili kuendana na ile wanataka, kisha tena watabuni dini kuidhinisha tabia yao. Kwa hivyo utaratibu wa kawaida ni uchumi, halafu siasa, halafu maadili, halafu dini.
1. Uchumi
2. Siasa
3. Maadili
4. Dini
Dini kama hiyo imeumbwa na kanuni mbaya ambazo hazina ukweli.
Kanisa ni lazima lisimame kwenye msingi wa ukweli wa bibila, sio tu kwa kukataa dhambi katika jamii bali kwa kueleza na kuonyesha kwa vitendo vile jamii inavyohitaji kuwa. Kama wakristo hawawezi kueleza na kuonyesha kwa matendo jinsi jamii inavyohitaji kufanya, tutatarajia ya kwamba watu wasio fahamu ukweli wa kibiblia watashindwa kutuumia katika Maisha yao.
Wakristo wasiikosoe tu jamii lakini lazima wawe sehemu ya jamii. Wakristo wanapaswa kushiriki kikamilifu katika jamii zao na kuwa watetezi wa haki. Wakristo pia lazima wawe wenye maadili katika ushirikiano wao wote na hivyo ndivyo watakuwa sauti ya ushawishi kwa wengine kwa haki na kweli. Ni lazima washiriki kwenye serikali na mashirika ambayo yana ushawishi katika jamii alimradi wafanye hivyo bila kukiuka kanuni za kikristo. Kama wataruhusiwa, wapige kura na wawaunge mkono wagombeaji wa nyadhiva za ofisi za siasa ambao wana sifa za kikristo.
► Ni mfano upi wa shinikizo la kijamii kwa kanisa la kufanya uamuzi kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi badala ya kufanya uamuzi unaotegemea ukweli wa kimaandiko?
Wakristo na sheria za serikali ya wanadamu
Wakristo katika historia wametatizika kujua jinsi ya kufuata kanuni za kikristo wakati serikali yao inafuata kanuni tofauti. Wakati mwingine mzozo huwa mkali, na wakristo wanateseka kwa ajili ya msimamo wao wa Imani kwa sababu hawawezi kufanya vitu ambavyo serikali inawahitaji wafanye.
Biblia inatueleza tulipe ushuru ambao unahitajika na serikali (Warumi 13:7, Mathayo 22:21).
Biblia inatuambia tutii sheria za taifa letu (Tito:3:1). Hata hivyo, biblia pia inatuambia kuwa ni lazima tumtii Mungu wakati wowote ambapo amri za Mungu zinapingana na sheria za mwanadamu (Matendo ya mitume 5:29)
Serikali inaweza kuwataka watu wajiunge na jeshi kupigana vita kwa sababu isiyostahili. Serikali inaweza kutaka vifo vya watoto wachanga ili kupunguza idadi kubwa ya watu. Serikali inaweza kuwataka watu katika nchi washiriki katika utumwa wa kabila au makundi fulani ya kikabila.
Wakati mwingine masuala yanahusu ibada. Wakristo wanaweza kuteswa wasipo abudu miungu ya familia au makabila yao. Wakristo wanaweza kuteswa wakati dini fulani tofauti inapendelewa na serikali.
Kuna mataifa ambayo yana sheria ambayo inaharamisha uinjilisti na mafunzo ya Bibilia. Wakristo wanateswa wanaposhiriki katika kuhubiri injili. Mataifa mengine yanaadhibu wazazi wanaofundisha watoto kuhusu Mungu.
Tuna mifano kwenye Bibilia ya watu wa Imani ambao walikataa kutii amri kutoka kwa watawala waliokuwa na sheria zisokuwa na haki. Daniel aliendelea na maombi yake hata ingawa maombi yalikuwa yameharamishwa. Marafiki watatu wa Daniel walikataa kuabudu sanamu ya mfalme. Wakunga wayahudi hawakumtii Farao alipowaamuru waue watoto Wayahudi.
Katika historia, wakristo wamehubiri injili hata kama kufanya hivyo kulikua kumeharamishwa. Kwa kutotii sheria, wameweza kuchukua Biblia na kuzivusha mipaka ya kitaifa. Wakristo wameweza kukusanyika na kuabudu kisiri. Wakristo pia bila kutumia vurugu wameweza kuzuia zahanati za kutoa mimba. Wakristo wamesaidia watumwa kutoroka.
Wakristo wengi wanapendelea kuishi Maisha yao kwa amani bila ya kukabiliana na maamuzi tatanishi kama hiyo. Hata hivyo, kama mkristo atakabiliwa na tatizo la kimaadili ni lazima afanye kile ambacho ni sawa hata kama kinahitaji kuhatarisha maisha. Kama ana fursa ya kuzuia dhuluma au kushiriki injili, anafanya uamuzi mzito anapoamua kuchukua hatua au kutotenda.
► Unaweza kueleza shida ya kisheria inayoweza kutokea kwa mkristo katika nchi yako?
Rushwa
Mchungaji alikua anasafiri katika nchi ya kigeni. Alikuwa na hati sahihi, lakini mara nyingi alisimamishwa na askari ambao walimtaka awape kitu kidogo. Kama hawezi kuwapa fedha watamchelewesha safari yake na watamuweka kwenye hali ya shida.
► Mchungaji atafanya nini katika hali hii?
Hongo/rushwa ni fedha inayolipwa kwa mtu aliye na mamlaka kumshawishi aruhusu kitu fulani. Ni makossa kumuhonga mtu kufanya kitu ambacho yeye hakupaswa kufanya. Kwa mfano kama jengo au gari halihitimizi viwango vilivyowekwa, ni kosa kumuhonga mkaguzi kutia sahihi ya ubora kwa kitu ambacho sio kweli. Ni makosa pia kumuhonga hakimu au askari kutoa hukumu isio ya haki.
Wakati mwingine wale ambao wako kwenye mamlaka wanadai hongo ili kufanya ile wanalopaswa kufanya. Katika hali hiyo, mtu ambaye analipa hongo hamlipi yule anayedai hongo kufanya jambo mbaya. Ni makosa kwa afisa kudai hongo (Luka 3:4), lakini mtu anayelipa wakati mwingine hana chaguo. Kwa mfano kupata kibali cha kitu ambacho unaruhusiwa kupata au kupata uhuru wa mtu ambaye hana hatia. Wakati mwingine hongo ni kama wizi wa kutumia mabavu. Wizi wa kutumia mabavu ni makosa lakini hatuwalaumu mwathirika.
Mtazamo wa maandiko unatuonyesha ya kuwa Mungu anawashutumu wale ambao wanachukua hongo ingawa inawahurumia wale ambao wamelazimishwa kulipa (Kutoka 18:21, Kutoka 23:8; Kumbukumba la Torati 10:17, Kumbukumba la Torati 16:19, Kumbukumba la Torati 27:25). Wakristo hawastahili kulipa hongo kwa urahisi, lakini hawana hatia wanapolazimishwa kulipa na maafisa wafisadi.
► Ni mfano upi wa hongo au rushwa ya makosa?
Huduma za kijeshi
Wakristo wengi wanaamini ya kwamba ni makosa kutumikia kama askari jeshi wa nchi yao. Wanajenga imani yao juu ya sentensi fulani za kimaandiko. Yesu alisema tugeuze shavu lingine mtu anapotupiga shavu moja (Matayo 5:39). Yesu alisema watumishi wake wasipigane, maana ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36). Mtume Paulo alisema silaha zetu sio za kimwili (2 Wakorintho 10:4). Hawa wakristo wanaamini ya kwamba fujo yeyote dhibi ya watu wengine ni makosa. Wengi wa hawa kristo wanaishi kwenye inchi ambazo serikali hairuhusu uhuru na wakristo katika haya mataifa wamenyanyaswa.
Wakristo wengine wanaamini ya kwamba ni lazima tuwe tayari kuilinda nchi yetu kama askari jeshi. Maandiko yanasema Mungu ndiye aliyeweka serikali na serikali inaweza kutumia silaha au zana kuwaadhibu wakosaji (Warumi 13:4). Inaonekana wazi kuwa Mungu alipanga mwanaume kuilinda familia, na kwa hivyo ni jambo la asili kuwa wanaume wanahitaji kuwa na muongozo fulani wa kulinda familia kutokana na mashambulizi kwa kuwa kwenye mfumo wa jeshi. Wakati askari alipomuuliza Yohana mbatizaji namna ya kutubu, Yohana alimwambia kuwa asikubali kupokea hongo au kufanya unyanyasaji wa kibinafsi lakini hakumwambia atoke kwenye jeshi (Luka 3:14). Yesu aliposema geuza shavu la pili, hakumaanisha ya kwamba hatuwezi kujilinda kutokana na mashambulizi, bali tusilipize kisasi sisi wenyewe kwa sababu ya vitendo vya kukera, kama vile kupigwa kofi usoni. Alisema watumishi wake hawapigani kuanzisha ufalme wa kidunia kwa niaba yake, kwa sababu hataanzisha ufalme kwa namna hiyo. Kama serikali ni jambo la Mungu, na kama serikali inastahili kulinda watu wake, hivyo basi ni vyema wakristo kuhudumia serikali yao kwa kuisaidia kutimiza malengo yake.
Kwa karne nyingi za historia ya kanisa, wakristo wengi katika mataifa mengi wamehudumu kwenye jeshi, hata kwenye mapambano, kwa sababu waliaamini kuwa ni lazima wafanye sehemu yao ya kulinda taifa lao kutoka kwa mashumbulizi mabaya.
Wakristo duniani kote hawana mafikiano kwa jambo la huduma za kijeshi. Ni vyema mtu atafakari kwa maombi maandiko na kutumia fikira zake binafsi, halafu afuate msimamo wa Imani yake kwa uaminifu.
► Makanisa katika inchi yako wanalijibu vipi hili swala la huduma jeshini?
Kushiriki kwa vikundi
Wakrsito wengi wana maoni mazito kuhusiana na haya mambo. Ni muhimu kuelewa kuwa wakristo katika wakati na sehemu tofauti hawajafikia makubaliano kuhusiana na haya masuala. Ni lazima tuepuke kupeana hukumu kuhusu motisha ya wengine kwa sababu ya moani yao.
► Tunapaswa kutathmini vipi uhusiano wa kawaida kati ya serikali na makanisa katika nchi yetu? Je, kuna kitu kinahitajika kubadilika?
Maombi
Baba aliye mbiguni,
Ahsante kwa kubuni serikali kutoa ulinzi na uhuru. Nisaidie niwe mwaminifu kwako licha ya mapungufu ya serikali za wanadamu.
Nisaidie nitimize majukumu yanguya kulinda wengine na kushawishi jumuia yangu.
Tunatarajia kuja kwa ufalme wako kwa ukamilifu.
Amina
Zoezi la somo la 12
(1) Biblia ina hadithi nyingi za Mungu akifanya kazi kupitia maafisa wa serikali kukamilisha kusudi lake katika Maisha ya watu wake. Mithali 21:1 yasema, “roho ya mfalme iko kwenye mikono ya Mungu, kama vile mito ya maji: yeye anabadilisha anapotaka.” Chagua moja ya hizi hadithi ukazisome:
Mwanzo 41:14-49, Mwanzo 42:1-3, Mwanzo 45:4-7
Esta 4, 7-8
Nehemia 1-2
Andika kuhusu uchunguzi wako:
Ni kitu gani kilihitajika kufanyika katika Maisha ya watu wa Mungu?
Jinsi gani Mungu alitumia watawala wasiomcha kutimiza kususdi lake?
Jinsi gani Mungu alitumia mtu anayemcha kutimiza kusudi lake?
(2) Chagua moja ya mada hizi:
Ushawishi wa kikristo
Wakristo na sheria za binadamu
Rushwa
Huduma ya kijeshi
Angalia maandiko yanayopatikana katika somo hili kuhusiana na mada yako. Andika ukurasa mmoja ukielezea kile unachofikiri ni mbinu ya kimaandiko kwa mada hii.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.