Mwezi wa Septemba 2018, tetemeko kubwa la ardhi chini ya kisiwa ilisababisha sunami (wimbi kubwa) kuelekea jiji la Palu, Indonesia. Mwanaume aliyekuwa juu ya jengo refu aliona wimbi likija. Kwa sauti kubwa akawaonya watu waliokuwa kwenye mitaa chini ya jengo, lakini wengi wao wakampuuza. Zaidi ya watu 4, 000 walifariki, na watu 10, 000 wakajeruhiwa.
Miaka kumi kabla (2008), serikali iliweka maboya 22 ya kuelea ambayo ilikuwa na teknolojia ya kielectroniki ili kuonya watu endapo sunami inakuja. Hata hivyo, baada ya miaka michache kupita maboya yale yaliharibika na hayakufanya kazi tena. Hakuna hata boya moja lililotoa tahadhari wakati wa sunami mwaka 2018.
Mawasiliano na Komanda wetu
► Ni nini ambacho huwekwa katika kila gari la jeshi?
Kila kifaru, gari, ndege n.k ina redio. Sio kwa ajili ya wanajeshi kusikiliza muziki jinsi wapendayo, lakini ni redio ya mawasiliano.
Mawasiliano ni ya muhimu ili kushinda vita. Wanajeshi akiwa vitani hawawezi kuona uwanja wote wa vita. Hawawezi kujua mahali ambapo rafiki zake wapo na mahali palipo na adui. Hawawezi kujua mwelekeo wanaopaswa kupiga risasi na hawatajua waelekee upande upi, bila mawasiliano kutoka kwa Komanda.
Kumekuwa na kesi nyingi, ambapo wanajeshi wameuliwa na wenzao katika mazoezi, wakati ambapo risasi imefyatuliwa pasipo maelekezo. Kumekuwa na wakati ambapo makombora na mabomu yameshambulia marafiki na sio maadui kwa sababu ya mawasiliano mabaya.
Katika vita vya kisasa ni bayana ya kwamba kila mmoja hujaribu kushambuli jumba la mawasiliano la maadui zake. Upande ambao utafanikiwa kuna uwezekano utashinda adui.
Tuko katika vita vya kiroho. Shetani hujaribu kutudanganya. Dunia inajaribu kutuvuta katika mitindo ya kimaisha. Watu wanao tuzunguka wakati mwingine wanatuzuia, wanatuvunja moyo sisi kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Sisi ni kama wanajeshi walio katika nchi katili, tukiwa tu na marafiki wachache na maadui wengi.
Mungu anapenda tushinde vita vya kiroho. Maombi ndio njia ya kuwasiliana na Komanda.
Hebu fikiria askari katika vita ambaye aliamua kupuuza amri za komado na kwenda mwenyewe. Huenda akafanya madhara badala ya wema; anaweza kushindwa kuwasaidia watu wanaomtegemea; na pengine anaweza kuuawa au kutekwa.
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa kila jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” (Waefeso 6:18).
Aya hii inakuja mwisho wa kifungu pale ambapo Paulo anaonyesha Wakristo silaha za kiroho kwa kilinganisha na silaha za kijeshi za wakati ule. Anasema adui zetu sio wa kimwili ni wa Kiroho.
Labda kama redio zingekuwapo wakati wa Paulo, angezitumia kuonyesha silaha nyingine katika vita vya Kiroho kwa jeshi la kiroho-maombi. Baada ya kueleza silaha Paulo akasema kwamba maombi yanatumiwa sambamba na silaha za Kiroho.
tunaposimama katika vita kinyume na roho chafu, lazima tuwe tunaomba, tudumu katika mawasiliano na Komanda wetu. Tumeitwa kuwa wenye ushujaa katika maombi, tuwe waangalifu na wavumilivu.
Mungu ameahidi kuongoza wale ambao watamsikiliza.
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri Yeye naye Atanyosha mapito yako” (Mithali 3:5-6).
“Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana” (Zaburi 37:23).
Mkristo hafanyi maamuzi sawa na jinsi ambavyo dunia hufanya. Watu wengine huongozwa na matakwa na tamaa zao. Wanasema, “Nitafanya kile ambacho ni kizuri kwangu.” Wanamaanisha kwamba lazima wazingatie mapenzi yao kuliko kuruhusu wengine wawaongoze. Wanafikiri uhuru unamaanisha ubinafsi. Mkristo ni tofauti kwa sababu anataka kumpendeza Mungu na kuwabariki wengine kwa maisha yake.
Baadhi ya watu hutushauri tusikilize ndani yetu ili kupata majibu. Wana amini kwamba hisia na akili zatosha kwa kuwaongoza kufanya maamuzi. Wanahimiza vijana kupuuza tamaduni na mahusia ya wazee. Wanapuuza utamaawa wa dini. Aina hii ya ushauri ni maarufu sana katika burudani ya Hollywood ya kisasa. Wanaonyesha au kuelezea vijana wanaofanikiwa kutokana na kuasi amri na tamaduni na kufuata ndoto zao binafsi. Hawaonyeshi ukweli kwamba maamuzi hayo huelekeza kwenye huzuni na janga kuu.
Katika tamaduni zingine, uamuzi wa mtu binafsi hidhibitiwa na ukoo au kabila. Mtu binafsi haruhusiwi kuondoka mkoani kwake, kubadilisha kazi, kuendelea na masomo au kuoa kabla hajathibitishwa na kikundi. Jambo gumu kabida katika mazingira haya ni kubadilisha dini. Endapo mtu atakuwa Mkristo na anaongozwa na kanuni ambazo watu wake hawazielewi anaweza kuteswa na kuumia. Mkristo katika hali hiyo lazima aombe ili kupata hekima na maongozi ya kimungu.
Tunahitaji kuongozwa na Mungu wakati wote, na anatuongoza kwa njia ambazo wakati mwingine hatuzijui. Yeye hawezi kutusahau kamwe, hata wakati ambapo hatumfikirii. Lakini kuna wakati ambao tunapaswa kutafuta njia zake na kuelekezwa na yeye na tumuombe atusaidie kuona chaguzi jinsi zilivyo. Mungu angetaka kubadilisha mwelekeo wetu kwa njia ambayo hatutarajii.
► Ni nyakati zipi ambazo tunahitaji mwelekeo maalumu kutoka kwa Mungu?
Tunastahili kutafuta mwongozo kutoka kwa Mungu…
1. Wakati tunafanya maamuzi yatakayo badilisha maisha: Ndoa, kazi, elimu, majukumu ya Kanisa.
2. Wakati wa maamuzi mahususi: Nafasi ya kazi, mahali pa kuishi, manunuzi ya hali ya juu.
3. Wakati unapanga kufanya huduma:[1] Mwito wa mtu binafsi, wapi na utahudumia nani, jambo la kuhubiri na kufundisha.
4. Wakati tunaoshiriki katika maisha ya kanisa:[2] Jinsi ya kuabudu, nini ya kujifunza, utatoa nini, jinsi ya kuwa sehemu ya mwili wa Kristo duniani.
[1]Matendo Ya Mitume 16:6-9 yaeleza jinsi ambavyo ushauri spesheli ambao Roho mtakatifu alimpa Paulo na Sila katika safari yao ya misionari.
[2]Kanisa la kale walikuwa nyeti kwa Roho mtakatifu alipoelekeza ibada, kulinda Imani yao, walivyoongozwa kutatua shida, na pia kupa nguvu ujumbe wao. Ona Matendo Ya Mitume 15:28, Matendo Ya Mitume 5:3-5, na Matendo Ya Mitume 6:10.
Jinsi unavyo tambua vizuri uongozi wa Mungu
(1) Mkaribie Mungu kwa maombi. Kama muda mwingi wa maisha yako utatenganishwa na mawasiliano na Mungu, wewe unafuata akili zako na mawazo yako mwenyewe.
(2) Usitumaini akili yako kuliko kweli kweli iliyo katika maandiko. Kama vile maandiko yanavyosema hapo juu, “...Usitumainie akili zako mwenyewe” (Mithali 3:5).
(3) Wakati wote tii kile ambacho unajua ukweli kuwa ni mapenzi ya Mungu. Hiyo itaboresha mtazamo wako. Mtu ambaye hatii neno la Mungu maana yake hataki mapenzi ya Mungu kwa sababu Mungu anaeleza mapenzi yake katika maandiko. Ukitii tu sehemu ya neno la Mungu utachanganyikiwa sana-na mwangaza utabadilika kuwa giza (Luka 11:35).
Tunajua ya kwamba ni mapenzi ya Mungu sisi:
Kujitwika msalaba wetu kila siku na kumfuata Yesu (Luka 9:23).
Kufanya haki na Kusema ukweli kutoka moyoni (Zaburi 15:2).
Kuheshimu viongozi waaminifu wa Kiroho (1 Wathesalonike 5:12-13).
Kufurahi kila wakati (1 Wathesalonike 5:16).
Kuomba bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17).
Kushukuru katika hali zote (1 Wathesalonike 5:18).
Kutomhuzunisha Roho (1 Wathesalonike 5:19).
Kutopuuza unabii (1 Wathesalonike 5:20).
Kujaribu mambo yote (1 Wathesalonike 5:21).
Kushika sana kilicho kizuri (1 Wathesalonike 5:21).
Kukimbia maovu (1 Wathesalonike 5:22).
Kutakaswa kweli kweli (1 Wathesalonike 5:23).
Na kuna amri zingine ambazo zimefupishwa kwa neno moja: Upendo! (Warumi 13:8-10). Tunapofanya yale ambayo tunajua ni mapenzi ya Mungu, mengi ya maamuzi ya maisha yasiyo na uzito yatafanya kazi tu.
(4) Kuwa na subira. Itakubidi usubiri kwa muda wakati Mungu anafungua milango na kuandaa Mazingira kwa ajili yako. Usifanye maamuzi kwa haraka kwa sababu ya kukosa subira. “Ukae kimya mbele za Bwana nawe umngojee kwa saburi” (Zaburi 37:7). Usifanye kitu unachojua ni kibaya kwa sababu ya dharura.
(5) Sikiliza ushauri mzuri “Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita na kwa wingi wa washauri huja wokovu” (Mithali 24:6). Wakati Mungu anakutaka kufanya uamuzi mkubwa, ataonyesha hilo kwa watu wengine katika maisha yako. Kama kuna watu wa Mungu, watu wazima ambao wanampenda Mungu na wanakupenda, usiwe mwepesi wa kufanya kitu ambacho watafikiri ni makosa.
Kushiriki kwa vikundi
► Shiriki mfano wa jambo ambao unajua aliongozwa na Mungu. Mungu alikueleza kwa namna gani kwamba ni maamuzi sahihi?
► Itakuwa vyema pia ukishirikisha mfano wa maamuzi mabaya. Ulikosa kufuata mmojawapo ya kanuni nne ya jinsi ya kuongozwa na mungu?
Ruhusu wendine washiriki pia.
► Labda kuna mmoja ambaye anajaribu kufanya uamuzi ambaye angetaka kushirikisha.
Makosa ya kuepuka unapotafuta Uongozi wa Mungu
Hadithi inasimuliwa kwamba mhubiri mmoja aliyeitwa Charles Stalker alikuwa akiomba asubuhi moja wakati Mungu alipomwambia, “nataka uende China.” Stalker alishangaa kwa sababu hakuwa na fedha za nauli wala mtu aliyemfahamu huko uchina. Msukumo ndani yake ulikuwa mkubwa kiasi ya kwamba alibeba vitu vyake na akaelekea kwenye stesheni mahali ambapo safari ya namna hiyo ilikuwa ianzie. Hapo mtu ambaye hawakufahamiana akaja na kumuuliza, “wewe ni Charles Stalker?” naye akaendelea akasema, “nilitumwa hapa na tiketi yako ya kwenda China.”
► Je ni namna hii ambayo tunatarajia Mungu atuonyeshe mapenzi yake? Je kutakuwa na shida kwa mtu atakaye mtarajia Mungu aoneshe mapenzi yake kwa namna hii?
Watu wengine hungoja miujiza na ufunuo ili wajue mapenzi ya Mungu katika kila hatua wanayoichukua katika maisha. Wanapuuza kufikiri na mazingira, kwasababu wanafikiri mapenzi ya Mungu yanaweza kuwa kinyume na mawazo yote na mazingira.
Ni makosa kusititiza kwamba Mungu lazima afanye muujiza kwa maamuzi yetu kwa sababu mara kwa mara hataonyesha mapenzi yake kwa njia hizo. Endapo mtu atapuuza kufikiria na mazingira anaweza kufikiri anapata maongozi kutoka kwa Mungu na kumbe anafuata hisia zake.
Wakati ambapo jambo au kitu kimekubaliwa au kukataliwa na maandiko, tunajua mapenzi ya Mungu. Lakini, kuna maamuzi mengi ambayo tuna njia mbadala ambazo hazijakubaliwa wala kukataliwa na Mungu. Mtu atajuaje mahali atakapoishi, atafanya kazi aina gani, na atatumia fedha kwa njia gani?
► Bila ufunuo maalumu, mtu atajuaje mapenzi ya Mungu kwa maamuzi ambayo hayajaelekezwa haswa kwa maandiko?
Watu wengine kwa sababu ya kuamini ya kwamba maelekezo ya Mungu lazima yawe na miujiza pasipo kufikiria na kuzingatia mazingira, wanapata njia ambazo sio za kimantiki na hufikiri Mungu atatumia hizo njia kuwapa mwelekeo. Wanaweza kumwambia Mungu awape hakikisho fulani ili kuthibitisha atafanya jambo fulani na kwamba huo ni mwongozo wake. Au wanaweza fungua Biblia kurasa yoyote na kutumia mstari fulani kusuluhisha jambo fulani.
Mashauri zaidi ya kufanya maamuzi mazuri
John Wesley anazungumza mambo mahususi ya jinsi ya kujua mapenzi ya Mungu. Alisema kwamba tunajua mapenzi ya jumla ya Mungu, kama yalivyo katika Biblia ni kwamba tuwe watakatifu na tutimize yale mazuri. Kwa hivyo ili kufanya uamuzi fulani ni lazima tuzingatie ni uchaguzi upi utafanya tuwe watakatifu na tukamilishe yalio bora zaidi.
Tunajifunza katika uzoefu ambapo tunatofautisha ni hali gani ni ya msaada kiroho na ipi hatari. Hali zingine ni hatari kiroho kwa wote, na zingine ni hatari kwa wachache na sio wote. Kwa kadiri iwezekanavyo tujiweke katika hali ambazo zitatukuza kiroho na tuepuke zile ambayo zitatuelekeza majaribuni (1 Wakorintho 10:12-13).
Kwa fikira na uzoefu, na kwa mashauri kutoka kwa wengine, tunaweza kupambanua ni uamuzi upi utaturuhusu kukamilisha mengi mazuri.
Sio kila Mungu wakati atajionyesha kwa miujiza. Anatarajia sisi tuweze kutumia kanuni za kimaandiko huku tukifikiri na kuangalia kwa maakini mazingira. Roho mtakatifu atatuongoza hata wakati mwingine pasipo hata sisi kufahamu. Kwa maamuzi mengi tusitarajie ufunuo lakini tuombe hekima na uelewa.
Watu ambao hudai mwongozo maalumu kutoka kwa Mungu, wakati mwingine hawawezi kuwasikiliza watu (Mithali 12:15). Wanaweza kukasirika wakati watu wanapowauliza maswali kuhusu uamuzi wao. Wanaonyesha kiburi na usumbufu badala ya unyenyekevu.
► Mwanafunzi asome 1 Petro 5:5-6 kwa niaba ya kikundi.
Isipokuwa katika hali chache, ni vizuri mtu asiseme Mungu amemwambia hasa la kufanya. Mtu akisema hivyo, ni vigumu kwa mtu yeyote kumpamahusia na ushauri. Itakuwa afadhali aseme anajaribu kufanya uamuzi wa busara na kwa msaada wa Mungu.
Kando na kanuni za Wesley alizotoa, unapopeana maoni yako zingatia
1. Je iko sambamba na amri zilizo wazi za kimaandiko? Mungu hataki ukose kutii Neno lake.
2. Je iko sambamba na vipaumbele katika maandiko? Biblia inaonyesha mambo ambayo ni muhimu kwa Mungu. Je maamuzi yako yanazingatia hayo?
3. Je inaambatana na mtazamo halisi wa mazingira? Unatakiwa kuona jinsi ambavyo Mungu amekuwa akikuandaa katika Mazingira hayo na uamuzi huo.
4. Linaleta maana? Wakati mwingine Mungu atakuelekeza kufanya jambo ambalo ni kama halina maana, lakini atafanya mapenzi yake kuwa wazi. Usikatae kamwe sababu kama njia ya kukusaidia kutambua mapenzi ya Mungu.
5. Je ni tabia ya kikristo? Usifikiri kuwa jambo kila hali si ya kawaida sana kiasi kwamba unaweza kufanya jambo ambalo halitampendeza Mungu.
6. Inaambatana na kuwapenda wengine kama unavyojipenda? Nia ya ubinafsi itaharibu kupambanua kwako.
7. Je itakuwa na ushawishi mzuri? Na wengine wakifanya jinsi ambavyo unafanya? Je, itakuwa vizuri kweli?
8. Je imethibitishwa na washauri wa kimungu? Sisi wote twajua jinsi ya kutafuta mafiki ambao watakubaliana nasi lakini watu ambao ni wa kiroho watasemaje kulingana na maamuzi yako?
Wakati mapenzi ya Mungu yanapokuwa sio ya kawaida, atafanya uelewe bila mashaka yoyote. Malaika, maono, au kichaka kiwakacho moto kiliwapa watu wa zamani uhakika ya kwamba ni Mungu. Mungu anaweza pia kukupa hakikisho la ndani ya moyo ambalo halina mashaka. Lakini wakati hakuna ujumbe wazi kutoka kwa Mungu ni vizuri ufuate kanuni zinazo tumainiwa ili ufanye uamuzi mzuri. Usitarajie kupata ufunuo maalum kwa kila jambo. Endapo utatumia utashi waho vizuri katika maombi na unyoofu na kuwa na vipaumbele sahihi, Mungu atakuwa mwaminifu kuongoza maamuzi wako.
Katika Warumi 12:1-2 Paulo aliandika,
Basi ndugu zangu, nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu yakumpendeza Mungu, ndiyo ibaada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Aya hii inaonyesha hali ya mtu ya Kiroho inavyo athirika katika maamuzi. Ili kupata mapenzi ya Mungu, lazima mtu ajitoe kikamilifu kwa Mungu. Maamuzi ya Mkristo ni tofauti na maamuzi ya dunia, kwa sababu hajafuatisha namna ya dunia hii lakini amefanywa upya nia yake. Anafanya maamuzi kwa nia mpya.
Nia ni kiungo cha maana sana katika kutambua Uongozi wa Mungu. Mtu atafutaye mapenzi ya Mungu ili tu aamue nini afanye au asifanye hakika atachanganyikiwa. Kama mtu atatafuta mapenzi ya Mungu kulingana na maandiko na pia kwa kufikiri, na kwa moyo wake wote ameamua kufanya, hakika hatakosa mapenzi ya Mungu.
Kushiriki kwa vikundi
► Jadili baadhi ya matumizi ya kanuni za Wesley's. Mifano mingine inaweza kuwa ni kuchagua marafiki ambao wewe utatumia muda wako pamoja nao, kuchagua ajira, kuamua mwenzi wa ndoa. Chagua, “ni hali ipi ambayo itanisaidia kuendelea kuwa mtakatifu na kutimiza yaliyo mazuri zaidi?”
► Watu wengine huonekana kwamba hawawezi kudumisha Ukristo wao wanapokuwa na watu fulani, au mahali fulani. Fikiria mifano.
► Uwezekano wa mjadala zaidi ni:
Jukumu la motisha katika kufanya uamuzi.
Kosa la kungojea ishara.
Hatari iliyopo kwa kutegemea hisia sana.
Maombi
Baba wa mbinguni,
Asante kwa kunipangia mambo mazuri. Najua ya kwamba unaongoza hatua zangu zaidi ya nionavyo.
Nisaidie kukukaribia kwa maombi. Nisaidie kuwa makini na kweli ambayo unanionyesha.
Nataka niwe mtakatifu na nifanikishe mengi iwezekanavyo kwa utukufu wako.
Fanya nia yangu iwe safi ili kwamba isinielekeze mbali na mapenzi yako. Niongoze kwa kuwatumia washauri wenye hekima ambao umeweka maishani mwangu.
Nataka nikuamini katika kila uamuzi wangu. Nataka nikufuate kwa moyo wote na kwa kukutii.
Asante kwa kunitakia mema.
Amina.
Zoezi la Somo la 5
(1) Soma Mithali 3:1-12. Andika kuhusu vipaumbele, nia, mtazamo na tabia ambazo zimeelezwa hapa. Eleza jinsi ambavyo wewe binafsi unaweza kukuza tabia hizi. (Majibu yote yaandikwe karika kurasa 1-2.)
(2) Chunguza Yakobo 4:13-17. Tambua ukuu wa Mungu dhidi ya hali. Ni uovu upi - usiopendeza ambao unaoneshwa katika mstari wa 16. Andika aya ikieleza kile ambacho Andiko hili linatufundisha nini kuhusu kupanga kwa ajili ya maisha ya baadaye?.
(3) Andika aya mbili ukieleza uhusiano uliopo katika maombi na kufanya maamuzi. Jibu maswali yafuatayo
Ni kwa namna gani maombi yanaathiri maamuzi yetu?
Makosa gani uyazuie ambayo yanahusiana na maombi na kufanya maamuzi?
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.