Kanisa la XYZ linajulikana kwa muda wanaoutumia katika ibada. Huduma zao zinafuata muundo huu:
Taratibu za Huduma ya Kanisa la XYZ
Utangulizi na matangazo
Muda wa ibada (nyimbo za sifa)
dakika 30
Sadaka/muziki maalumu/maombi
dakika 15
Mahubiri
dakika 30
Muda wa ibada (nyimbo za sifa)
dakika 15
Watu katika kanisa la XYZ wanapenda muziki. Wageni wanapongeza ibada yenye nguvu sana ingawa, Mchungaji Bill amekuwa na wasiwasi kuhusu matokeo ya muda mrefu ya huduma yake. Waongofu wapya hivi karibuni wanahamia kwenye makanisa mengine. Jambo baya zaidi, utafiti wa washirika wa muda mrefu uligundua kwamba kanisa “halitengenezi wanafunzi imara wa Yesu Kristo. Idadi, ndiyo; wanafunzi, hapana.”[1]
Bill anaamini kwamba sehemu ya tatizo ni uelewa wa kanisa kuhusu ibada. Katika Kanisa la XYZ, ibada inalingana na muziki tu. Mchungaji Bill anaanza kuuliza, “Je, ibada ya kweli inajumuisha zaidi ya muziki? Je, tunatenganisha Neno la Mungu na maombi kutoka kwenye ibada? Je, hii inapunguza matokeo ya mahubiri?”
► Tafadhali jibu wasiwasi wa Mchungaji Bill. Je, kuna tofauti kati ya ibada na mahubiri? Kanisa la XYZ linawezaje kuunganisha sehemu zote za ibada katika akili za waabudu?
[1]Hii imenukuliwa katika utafiti uliofanywa na moja ya makanisa makubwa zaidi Marekani. Waligundua kuwa wengi wa waongofu wapya hawajawahi kufikia hatua ya kuwa wanafunzi wa kweli.
Umuhimu wa Maandiko katika Ibada
Kama wainjilisti tunafundisha kwamba mafundisho na ibada zetu zinaongozwa na maandiko. Tunaamini kwamba Biblia inapaswa kuwa na nafasi kuu katika ibada yetu. Mungu huzungumza na watu wake katika usomaji wa Neno. Tangu nyakati za Agano la Kale, maandiko yamekuwa muhimu katika ibada.
Kwa kusikitisha, ingawa tunasema kwamba Biblia ndiyo mzizi wa ibada yetu, makanisa mengi yanajumuisha maandiko machache katika ibada zao. Inawezekana kuhudhuria ibada katika baadhi ya makanisa na kusikia si zaidi ya mistari michache ya maandiko. Hii ni mbali na mfano wa kibiblia wa ibada.
Kusoma Neno lilikuwa muhimu katika ibada za kibiblia.
► Soma Kutoka 24:1-12.
Katika Kutoka 24:7, Musa akakitwaa kitabu cha agano, na kukisoma masikioni mwa watu. Watu waliahidi kuzifuata amri za Mungu: “Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.” Kufuatia haya, Mungu aliandika muhtasari wa agano (Amri Kumi) kwenye mbao za mawe. Israil walikuwa watu wa Kitabu. Agano lililoandikwa lilikuwa kiini cha ibada ya Israeli.
Neno la Mungu lilikuwa katikati ya Hema na Hekalu. Sikukuu za kila mwaka zilikuwa matukio muhimu zaidi katika mwaka wa Kiyahudi. Katika Pasaka, Sikukuu ya Malimbuko, na Sikukuu ya Vibanda sehemu za Neno la Mungu zilisomwa hadharani. Kila baada ya miaka saba, taifa lilikusanyika ili kusikiliza sheria ikisomwa, na agano lilifanywa upya.[1]
Katika Agano Jipya, Paulo aliwaamuru Wakristo kusoma maandiko hadharani. Hii ilijumuisha Agano la Kale, barua za Paulo, na maandishi mengine yaliyoainishwa kama maandiko.[2] Alimwagiza mtumishi kijana kujishughulisha na usomaji wa hadhara wa maandiko, kuonya, na kufundisha (1 Timotheo 4:13). Neno la Mungu lilikuwa kiini katika ibada ya Agano Jipya.
Kuhubiri Neno lilikuwa muhimu katika ibada za kibiblia.
► Soma Nehemia 8:1-18.
Baada ya kurudi kutoka uhamishoni, Ezra aliwasomea watu Sheria. Watu wakakusanyika ili kusikiliza Ezra alipokuwa akisoma torati mbele ya wanaume na wanawake, na wale walioweza kuelewa; na masikio ya watu wote yakakisikiliza kitabu cha torati (Nehemia 8:3). Kwa kuitikia, watu walisema “Amina” na wakaanguka kifudifudi katika ibada. Ezra na wenzake waliposoma, walifafanua andiko hilo na kuwafanya wasikilizaji waelewe usomaji huo. Huu ni mfano wa kibiblia wa kuhubiri, kueleza, na kutumia Neno la Mungu kwa mahitaji ya watu. Mahubiri ya kweli ya kibiblia huchochea ibada katika mwitikio wa Neno.
Yesu alikuja kwenye sinagogi siku ya Sabato kama ilivyokuwa desturi yake na kusoma kitabu cha nabii Isaya. Alipomaliza, Yesu alihubiri mahubiri ambayo alionyesha kwamba amekuja kutimiza ahadi ya Isaya (Luka 4:16-29).
[3]Katika mahubiri yake siku ya Pentekoste, Petro alionyesha kwamba ahadi za Agano la Kale zilitimizwa katika huduma ya Yesu na ujio wa Roho Mtakatifu. Alimalizia maelezo yake ya maandiko kwa kuwaalika watu kutubu na kubatizwa (Matendo 2:14-41). Mahubiri ya Biblia yalitaka mwitikio kutoka kwa wasikilizaji. Mahubiri huzungumza na akili, lakini lazima pia yazungumze na moyo. Mahubiri lazima yahitaji mwitikio wa msikilizaji sawasawa na mapenzi yake. Yesu alipofungua maandiko njiani kuelekea Emau, mioyo ya wasikilizaji iliwaka ndani yao (Luka 24:32).
Kuhubiri kulikuwa muhimu katika kuenea kwa kanisa la kwanza. Katika Matendo ya Mitume, neno la Mungu linatajwa zaidi ya mara 20. Mitume walihubiri neno la Bwana; walisema neno la Mungu kwa ujasiri; walifundisha neno la Mungu. Na matokeo yake, watu wengi walipokea neno la Mungu; neno la Mungu likakua na kuongezeka; neno la Mungu likaenea; na mataifa wakalitukuza neno la Bwana. Neno la Mungu lilikuwa msingi wa ujumbe wa mitume.
Ingawa kuhubiri sio njia pekee ambayo maandiko huzungumza, ndiyo njia kuu ya kuleta Neno la Mungu kwa watu wa Mungu. Ili kutimiza kusudi hili, mchungaji hapaswi kusahau kamwe kwamba Neno la Mungu lazima liwe kiini. Mahubiri ya Biblia lazima yaanzie katika Neno la Mungu, yafafanue Neno la Mungu, na yatoe itikio la kibinafsi kwa Neno la Mungu.
Kuhubiri Neno lilikuwa muhimu katika historia ya kanisa.
Mahubiri yalikuwa muhimu katika ibada karne za mwanzo za kanisa. Katika karne ya pili, Justin Martyr aliandika kwamba Wakristo walikusanyika Jumapili ili kusoma Nyaraka na Manabii na kusikiliza zikifafanuliwa. Kufikia karne ya tatu, sehemu za kila sehemu kuu ya Biblia zilisomwa wakati wa ibada.
Katika kipindi cha karne za kati, kanisa Katoliki lilipunguza jukumu la kuhubiri, lakini Wanamatengenezo walirudisha kuhubiri katika nafasi kuu katika ibada. Lengo la kurudisha mahubiri halikuwa burudani, ajenda ya kibinafsi ya mhubiri, au mahitaji ya kitamaduni ya jamii. Kusudi la kuhubiri lilikuwa ufafanuzi makini wa Neno la Mungu; kufafanua maandiko kwa njia ambayo iliwagusa wasikilizaji na kutaka jibu la kubadilisha maisha.
[1]Timothy J. Ralston, “Scripture in Worship” in Authentic Worship. Edited by Herbert Bateman. (Grand Rapids: Kregel, 2002), 201
“Baraka ya ufafanuzi wa kweli wa Biblia ni moyo uliowaka, si kichwa kilichojaa.”
- Warren Wiersbe
Kufanya Maandiko kuwa Kitovu cha Ibada
Ikiwa Neno la Mungu linapaswa kuwa kiini katika ibada yetu, je, tunawekaje kanuni hii katika vitendo? Hatua za kivitendo za kufanya maandiko kuwa muhimu katika ibada zetu ni pamoja na:
Maandiko Yanapaswa Kujumuishwa Katika Sehemu Zote za Ibada
Hatupaswi kusubiri hadi mahubiri ili kusikia maandiko katika ibada. Hakuna njia bora ya kuanza ibada kuliko kwa Neno la Mungu.
Chunguza namna mbili za ufunguzi wa ibada. Je ni mwaliko gani unafaa kuingia katika uwepo wa Mungu?
1. “Asante kwa kuja kanisani leo. Mvua ilifanya usafiri kuwa mgumu kwa baadhi yenu, lakini nina furaha mmekuja. Hebu tuelekeze mawazo yetu kwa Mungu na ibada. Je, unaweza kusimama tunapoimba, ‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu?’”
2. “‘Nalifurahia waliponiambia, na twende nyumbani kwa BWANA!’ Karibu katika nyumba ya Mungu! Katika Hekalu, Isaya alimwona Bwana juu na akiwa ameinuliwa. Alisikia malaika wakiimba ‘Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.’ Ungana nami katika sifa tunapoimba ‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu.’”
Kiongozi wa kwanza alitukumbusha ugumu wa safari; kiongozi wa pili alitukumbusha furaha ya ibada. Kiongozi wa kwanza alianza kwa maneno ya kawaida; kiongozi wa pili alianza na Neno la Mungu. Kiongozi wa kwanza alitangaza wimbo wa kawaida; kiongozi wa pili alitukumbusha kwamba malaika huimba wimbo huu kwa kumsifu Mungu. Ni kanisa gani litaimba kwa shauku zaidi?
Baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani, waumini walikusanyika katika makanisa yao siku ya Jumapili kwa ajili ya ibada kama kawaida. Linganisha ufunguzi wa ibada kutoka kwa makanisa haya mawili:
1. “Asante kwa kuungana nasi leo. Hii imekuwa wiki ya huzuni katika taifa letu. Wengi wetu tunahuzunika. Asante kwa kuja kuabudu hata katika wakati huu wa giza. Tutaanza kwa kuimba ‘Msalaba uliochakaa.’”
2. “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Katika nyakati hizi ngumu, hatupaswi kusahau kwamba yeye ndiye tumaini letu; Yeye ndiye kimbilio letu. Jiunge pamoja tunapokumbuka kwamba ‘Ngome Yenye Nguvu Ni Mungu Wetu, ngome isiyoshindwa kamwe.’”
Kiongozi wa kwanza aliwakumbusha waumini juu ya huzuni yao; kiongozi wa pili aliwakumbusha kuwa Mungu ndiye tumaini lao. Maandiko na utenzi kulingana na andiko hilo ulitoa msingi thabiti katika juma ambalo uthabiti wa watu ulikuwa ukijaribiwa.
Maandiko yanaweza kutumika katika sehemu nyingoi za Ibada:
Maneno ya ufunguzi wa Ibada
Mwaliko wa kutoa sadaka
Maneno ya wimbo
Maombi
Ibada yetu inapaswa kujazwa na Neno la Mungu. ibada ni majibu kuhusu ufunuo wa Mungu juu yake mwenyewe katika Neno lake. Maandiko yanapaswa kuwa msingi wa sehemu zote za ibada.
Usomaji wa Maandiko Unapaswa Kupokea Nafasi Kuu Katika Ibada
Je, umewahi kumsikia mchungaji akisema, “Tuna muda mfupi leo na nina mahubiri marefu, kwa hivyo nitaruka usomaji wa vifungu vya biblia?” Ni lipi lililo la maana zaidi, Neno la Mungu au maneno yetu? Ni lazima tutoe muda kwa maandiko katika ibada.
Kwa sababu usomaji wa maandiko ni ibada, tunapaswa kuzingatia jinsi tunavyosoma. Inapaswa kusomwa kwa uwazi na kwa usahihi. Msomaji (awe mchungaji au mtu wa kawaida) anapaswa kufanya mazoezi kabla ya ibada. Katika karne tatu za kwanza za kanisa, nafasi ya msomaji wa maandiko ilikuwa amana takatifu. Wasomaji waliweka vitabu walivyopangiwa nyumbani na kufanya mazoezi ya usomaji. Waliposoma katika ibada, walikuwa tayari kusoma kwa uwazi na kwa kueleza.[1]
Kumbuka, hili ni Neno la Mungu linalosomwa katika nyumba ya Mungu kwa watu wa Mungu kama tendo la ibada. Ikiwa nyimbo za ibada zinastahili mazoezi, Neno la Mungu linastahili mazoezi pia. Si jambo la kujivunia uwezo wetu; ni jambo la kuhakikisha kwamba Neno la Mungu linawasilishwa kwa wasikilizaji. Hili ni Neno la Mungu; ni muhimu!
Tunapaswa kufanya usomaji uwe na maana. Kutumia aina tofauti za usomaji kutafanya andiko kuwa safi katika masikio ya wasikilizaji.
(1) Wakati fulani andiko linaweza kusomwa na kiongozi huku waumini wakimsikiliza Mungu akisema. Aina hii ya usomaji inafaa kwa sehemu kubwa ya vitabu vya musa na vitabu vingi vya unabii.
(2) Wakati mwingine kiongozi na waumini wanaweza kubadilishana usomaji. Zaburi nyingi zinafaa kwa aina hii ya usomaji wa kuitikia.
► Soma Zaburi 136. Mpe kiongozi wa darasa kuanza kila mstari; darasa linapaswa kujibu kwa nusu ya pili ya kila mstari, “kwa maana fadhili zake ni za milele.”
Heri zinafaa kwa usomaji wa kuitikia (Mathayo 5:1-10):
Kiongozi: Heri walio maskini wa roho, Waumini: Maana ufalme wa mbinguni ni wao. kiongozi: Heri wenye huzuni, Waumini: Maana hao watafarijika.
(3) Maandiko mengine yanaweza kusomwa na waumini kwa umoja. Kama wimbo wa pamoja, kusoma maandiko kama mwili kunaonyesha umoja wa kanisa. Kanisa lote linaungana katika kunena Neno la Mungu. Maombi kama vile kwenye Zaburi 124 yanafaa kwa usomaji wa pamoja.
Simulizi ya Nehemia kuhusu kusomwa kwa sharia na Ezra kunaonyesha matokeo ya kuwa na maandiko kama kitovu katika ibada yetu.
► Soma Nehemia 8 tena ikiwa unataka kupitia upya simulizi hii.
Angalia maelezo ya usomaji.
Ezra akakifungua kitabu mbele ya macho ya watu wote. Kulikuwa na muunganisho wa kuona na Neno.
Alisimama juu ya watu wote. Msomaji angeweza kuonekana wazi na kusikika.
Alipoanza kusoma, watu wote wakasimama. Kulikuwa na mwitikio wa kimwili kwa Neno.
Alipokuwa akisoma, watu wote wakajibu, “Amina, Amina,” wakainua mikono yao, wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudia BWANA kifudifudi. Walionyesha utii wao kwa Neno la Mungu.
Walawi wakaisoma sheria ya Mungu kwa uwazi, wakatoa maana, hata watu wakaelewa usomaji huo. Walitoa umakini kwenye kuelewa Neno la Mungu. Hili ndilo lengo la mahubiri leo.
Watu walilia, waliposikia maneno ya sheria. Nehemia aliwaamuru wafurahi, “kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.” Neno la Mungu lilichochea toba na shangwe.
Ingawa si kila jambo la tukio hili maalum litarudiwa katika ibada zetu, simulizi hii inaonyesha nguvu ya Maandiko. Ni lazima tuweke Maandiko kuwa kitovu cha ibada zetu.
Kujipima
Je, waumini wako wanatambua umuhimu wa kusoma Biblia katika ibada? Eleza baadhi ya tabia na mwitikio ambao unauona unapotazama kuzunguka kanisa wakati wa usomaji wa maandiko.
Kwa wastani wa kila Jumapili, ni vifungu vingapi tofauti vya Maandiko husikilizwa na waumini wako? Je, waabudu wanajua kwa nini kila kifungu kimejumuishwa?
Mahubiri Ya Neno Yanapaswa Kuwa Kitovu Kikuu Katika Ibada Zetu
Kama vile mitindo ya muziki inavyobadilika katika kila kizazi, mitindo ya kuhubiri inabadilika ili kukidhi mahitaji ya kila kizazi. Maandiko hayafafanui mtindo mmoja wa muziki kama mtindo wa kibiblia wa muziki wa Ibada; Maandiko hayafafanui njia moja ya kuhubiri kama mtindo wa kibiblia wa kuhubiri.
Mtindo unaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi na kutoka utamaduni hadi utamaduni; maudhui lazima yasibadilike. maandiko hayafafanui mtindo wa muziki, lakini yanafafanua maudhui. Vivyo hivyo, mitindo ya kuhubiri inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, lakini maudhui lazima yasibadilike.
Mahubiri katika maandiko yanaonyesha kwamba kuhubiri Neno la Mungu ni jukumu kuu la mhubiri anayesimama mbele ya kanisa. Shabaha kuhusu Neno la Mungu lazima Ibaki kuwa kiini katika mahubiri ya kisasa. Kubadilisha teknolojia na mitindo ya kujifunza kunaweza kuathiri mtindo wa kuhubiri; maudhui lazima yabaki na mizizi katika maandiko.
Je, ni matokeo gani ya vitendo ya kuona mahubiri kama ibada? Hilo litaathirije namna yetu ya kuhubiri?
Kuhubiri kunahitaji Maandalizi Mazuri.
[3]Ikiwa kuhubiri ni ibada, tunawajibika kujiandaa kwa uangalifu. Ni lazima tutoe kilicho bora kwenye madhabahu ya Mungu. Daudi hangempa kitu kisichomgharimu; hatupaswi kuleta mahubiri ambayo hatujayatayarisha kama zawadi yetu kwa Mungu. Tunapaswa kuyaandaa kwa umakini mahubiri yetu kabla ya ibada (2 Samweli 24:24).
Kuhubiri kunahitaji Mwitikio kutoka kwa Waumini
Ikiwa kuhubiri ni ibada, Itahitaji mwitikio kutoka kwa waumini. Katika ibada tunamuona Mungu, Tunajiona sisi wenyewe, na tunaona uhitaji wa dunia yetu (Isaya 6:1-8; angalia somo la 1.). Mahubiri yetu yanapaswa kumfunua Mungu kwa msikilizaji, mahubiri yetu yanapaswa kumfanya msikilizaji kugeuka katika njia zake, na mahubiri yetu yanapaswa kuhamasisha kanisa kufikia ulimwengu uliopotea. Kuhubiri kama ibada kutaleta hatia kwa wenye dhambi na kutawatia moyo waumini katika uinjilisti.
Kuhubiri kunahitaji mwitikio kutoka kwa mhubiri.
Ikiwa kuhubiri ni ibada, tutatambua kwamba kuhubiri kunahitaji mwitikio kutoka kwetu. Tukijiandaa kuhubiri kama tendo la ibada ya Kujidhabihu, tutamwona Mungu; tutahukumiwa kwa maeneo ya uhitaji katika maisha yetu wenyewe; na tutaona mahitaji ya ulimwengu unaotuzunguka. Kwa kujibu, tutalia pamoja na Isaya, “Mimi hapa; nitume mimi." Mahubiri ya kweli yatambadilisha mhubiri. Hatupaswi kuleta ujumbe wa Mungu kwa waumini wetu hadi Mungu azungumze nasi kibinafsi na sisi tumeitikia.
Yesu hakuwakemea waandishi (wahubiri) wa siku zake kwa mahubiri mabaya; aliwakemea kwa kushindwa kuishi yale wanayohubiri. Walijua maandiko na jinsi ya kueleza maandiko, lakini hawakubadilishwa na maandiko. Yesu alisema, “Hunena lakini hawatendi” (Mathayo 23:3). Ikiwa kuhubiri ni ibada, sisi kama wachungaji tutabadilishwa na kweli tunazohubiri. Naye, Mungu atazungumza kupitia sisi ili kubadilisha mioyo na maisha ya watu tunaowahubiria.
Mhubiri lazima awezeshwe na Roho Mtakatifu.
Ikiwa kuhubiri ni ibada, mhubiri lazima awezeshwe na Roho Mtakatifu. Kama vile maeneo mengine yote ya ibada yanamtegemea Roho Mtakatifu kwa nguvu za kweli, mhubiri lazima awe ametiwa mafuta na Roho wa Mungu ili awe na ufanisi.
► Soma 2 wakorintho 3:3-18.
Tunajidhabihu katika maandalizi ya mahubiri; hata hivyo, baada ya maandalizi yetu kukamilika, nguvu katika kuhubiri huja kupitia Roho Mtakatifu. Bila nguvu za Roho Mtakatifu, tunaweza kuzungumza kwa akili, tunaweza kuvutia waumini, na tunaweza kuwa na maudhui mazuri, lakini hatutabadilisha maisha yao.
Kujipima
Je, mahubiri yako ni tendo la ibada kibiblia? Ikiwa mtu anakusikiliza ukihubiri mara kwa mara, je, atasikia ukweli wa kibiblia unaofaa?
[1]Keith Drury, The Wonder of Worship, (Fishers, IN: Wesleyan Publishing House, 2002), 35
“Kuhubiri, kama si ibada, ni unajisi…. Mahubiri ya kweli ni tendo la Mungu, na si utendaji tu wa mwanadamu.”
- Adapted from J.I. Packer
Hatari za Ibada: Kupotea Kwa Neno
Biblia imepoteza nafasi yake katika maisha ya kila siku ya watu wengi wanaojiita waumini. Cha kusikitisha ni kwamba pia imepoteza nafasi yake katika ibada ya kila wiki ya makanisa mengi. Ambapo kanisa la kwanza liliimba zaburi, baadhi ya makanisa leo huimba nyimbo zenye maudhui machache ya kibiblia au hayana kabisa. Ambapo kanisa la kwanza lilisoma vifungu virefu vya Maandiko, leo baadhi ya makanisa husoma vifungu vichache pekee kabla ya hotuba. Kwenye ibada nyingi, nyimbo na mahubiri yasiyotoa kipaumbele kikubwa kwa Neno la Mungu yamekuwa mbadala wa Nafasi ya Maandiko.
Baadhi ya viongozi katika vuguvugu la kisasa la kuabudu wanasisitiza kwamba usomaji wa hadhara wa maandiko haugusi tena mahitaji ya kisasa. Hivi majuzi mchungaji mmoja mashuhuri aliwaomba wafanyakazi wa kanisa lake kutathmini mahubiri yake. Walimwambia kwamba anatumia Biblia nyingi kupita kiasi! “Ni vizuri kwako kujenga mahubiri yako kwenye Biblia, lakini unapaswa haraka kuelekea kwenye jambo linalohusiana vinginevyo tutakoma kusikiliza.” Wafanyakazi hawa wa kanisa hawakufikiria kwamba Biblia ilikuwa muhimu kwa watu leo!
Kama viongozi wa ibada, lazima tudumishe umuhimu wa maandiko katika ibada. Katika ibada, tunazungumza na Mungu kupitia maombi na nyimbo za sifa. Katika ibada, tunamsikia Mungu akisema nasi kwa kusoma na kuhubiri Neno. Bila kujali mtindo wetu wa kuabudu, hatupaswi kamwe kupoteza umuhimu wa Neno la Mungu katika ibada.
► Pitia Nehemia 8. Tengeneza orodha ya kila kifungu cha maneno kinachoonyesha thamani ambayo watu waliweka katika usomaji wa Sheria. Linganisha hili na usomaji wa maandiko katika ibada yako leo. Jadili hatua moja ya vitendo ambayo inaweza kuongeza matokeo ya maandiko katika ibada yako.
Umuhimu Wa Maombi Katika Ibada
Katherini[1] ni Mkristo aliyejitolea. Hata alipokuwa shuleni, alijitenga na Mungu kila asubuhi. Kabla ya kifungua kinywa, alitumia wakati katika Biblia na Maombi.
Lakini kwa kuwa sasa yeye ni mama wa watoto wanne, maombi na usomaji wa Biblia unazidi kuwa mgumu. Mtoto mmoja ni mtoto mchanga na humwamsha Katherini wakati wa usiku. Katherini hujikuta kwamba mara nyingi anapata shida kuamka kitandani asubuhi kabla watoto hawajaamka. usiku, anakuwa amechoka sana hivyo hawezi kuzingatia maombi na kusoma Biblia.
Katherine ana furaha Jumapili inapofika. Kila Jumapili, yeye hutiwa nguvu kiroho wakati wa ibada, lakini katikati ya wiki huvunjika moyo. Anahisi kwamba maisha yake ya ibada yamekuwa kushindwa kabisa.
► Tafadhali mpe Katherine ushauri wa vitendo kwa maisha yake ya ibada.
Tulianza somo hili kwa kujifunza Maandiko katika ibada. Tutaendelea na somo la maombi katika ibada. Katika Maandiko, Mungu anazungumza nasi; katika maombi, tunamjibu Mungu. Maandiko na maombi yanapaswa kujaza ibada yetu.
Maombi ya Hadhara na ya Kibinafsi katika Ibada ya Biblia
Tumeona kwamba kitabu cha Zaburi kilikuwa kitabu cha nyimbo za ibada ya Kiyahudi. Pia kilikuwa “kitabu cha maombi” kwa ajili ya ibada ya Kiyahudi. Zaburi zilihusisha maombi ya ibada ya hadharani na maombi ya faragha. Maombi ya hadharani na ya faraghani ilikuwa muhimu kwa ibada ya Kiyahudi.
Nyumbani, wayahudi waaminifu waliomba mara tatu kwa siku (Danieli 6:10).[2] . Zaburi nyingi ni maombi ya faragha. Haya yanaweza kutambuliwa kwa matumizi ya mimi badala ya sisi katika maombi. Mifano ya zaburi za maombi ya faragha ni pamoja na:
Zaburi 18 – wimbo wa shukrani
Zaburi 32 – Maombi ya furaha kwa ajili ya msamaha[3]
Zaburi 38 – Maombi ya Toba
Zaburi 41 – Maombi ya Rehema
Zburi 51 – Maombi ya Toba
Zaburi 88 – Maombolezo wakati wa mateso
Zaburi 116 – Wimbo wa shukrani kwa utunzaji wa Mungu
Hekaluni, waabudu wa Kiyahudi waliungana pamoja katika maombi ya hadhara. Wakati wa kuwekwa wakfu kwa Hekalu, Sulemani aliongoza maombi ya kitaifa kwa ajili ya kibali cha Mungu kwa watu (2 Mambo ya Nyakati 6). Isaya alileta ujumbe wa Mungu kwa Yuda; “Kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote” (Isaya 56:7). Baada ya Uhamisho, ibada ya sinagogi ilikazia usomaji wa Sheria na maombi. Ibada katika sinagogi zilianza kwa mfululizo wa maombi.
Utaratibu wa maombi wa Kiebrania uliendelea katika kanisa la kwanza. Wakristo wa karne ya kwanza waliomba mara tatu kwa siku nyumbani. Wakristo walipokutana pamoja kwa ajili ya ibada, walisali kama mwili mmoja. Sala ya Bwana ilikuwa sehemu ya kila ibada. Maombi mengine yalitolewa katika kila ibada.
Maombi Katika Ibada Leo
Ikiwa maombi yalikuwa muhimu katika ibada ya kibiblia, maombi yanapaswa kuwa muhimu katika ibada yetu leo. Maombi ya hadhara na ya faragha ni muhimu.
[4]Maombi ya faragha hutuunganisha na Mzabibu na hutoa lishe kwa maisha yetu ya kiroho. Ukosefu wa maombi ya kibinafsi unaweza kuelezea ukosefu wa nguvu za kiroho katika makanisa mengi. Ikiwa Yesu alihitaji nyakati za maombi ya faragha wakati wa huduma yake hapa duniani, je, ni kwa kiasi gani tunategemea maombi ili kupata lishe ya kiroho na nguvu katika huduma.
Maombi ya hadhara ni kipengele muhimu cha ibada. Makanisa mengine hayazingatii sana maombi. Mchungaji mmoja alitetea ukosefu wa maombi ya hadharani katika kanisa lake kwa kusema, “Huwezi kuwavutia watu macho yao yakiwa yamefumbwa.”[5] Aliamini kuwa kufurahisha watazamaji ni muhimu zaidi kuliko kumpendeza Mungu.
Maombi ya ushirika husahihisha wazo potofu kwamba Ukristo unanihusu mimi tu na uhusiano wangu na Mungu; sisi ni sehemu ya mwili wa Kristo. Tunaposikia mahitaji ya maombi na kujiunga katika maombi ya pamoja, tunatambua ugonjwa wa Mkristo mwenzetu, maumivu ya kihisia, na hali za maisha. Maombi ya pamoja yanatukumbusha kwamba washirika wa kanisa ni mwili mmoja. Maombi ya ushirika hutukumbusha kwamba Mungu anajali kanisa kama mwili wake.
Kama vile maandiko yanavyopaswa kutumika katika ibada yote, maombi yanapaswa kutolewa katika ibada nzima. Kuanzia maombi ya ufunguzi ambayo yanakaribisha uwepo wa Mungu katika ibada, hadi wakati uliolengwa wa maombi kwa ajili ya mahitaji ya watu, hadi maombi ya kufunga ya baraka ambapo washirika wanakuwa wakioondoka kuhudumia ulimwenguni, maombi yanapaswa kuzingatia ibada yetu.
[1]Habari ya Katherini imenukuliwa kutoka kwenye kitabu cha Keith Drury, The Wonder of Worship, (Fishers, IN: Wesleyan Publishing House, 2002), 17.
[2]Kufuatisha desturi ya Danieli ilikuwa kawaida kwa wayahudi waaminifu.
[3]Yawezekana Zaburi hii iliandikwa mara tu baada ya toba ya Daudi katika Zaburi ya 51.
“Wakristo wengi zaidi wanaamini katika ibada za kibinafsi kuliko kuwa nazo.”
- Keith Drury
[5]Imenukuliwa kwa Keith Drury, The Wonder of Worship, (Fishers, IN: Wesleyan Publishing House, 2002), 28.
Kufanya Maombi Kuwa Kitovu Cha Ibada
Je, ni baadhi ya njia zipi za kivitendo ambazo tunaweza kufanya maombi kuwa sehemu ya maana zaidi katika ibada ya hadharani? Hapa kuna mapendekezo sita ya kivitendo.
Hakuna aliye tayari kuwaongoza wengine katika ibada hadi aanze kuabudu. Hakuna aliye tayari kuongoza Maombi ya hadhara mpaka awe ameomba kwanza faraghani. Ni pale tu tunapokuza maisha ya maombi ya faragha ndipo tunapowezeshwa kuongoza katika maombi ya hadhara. Kama kiongozi wa ibada, jitolee kuwa na nidhamu ya maombi ya faragha ya kila siku.
Jifunze Jinsi ya Kuomba
Wanafunzi wa Yesu waliuliza, “Tufundishe sisi kusali” (Luka 11:1). Ili kujibu, Yesu alifundisha sala ya kielelezo inayoitwa Sala ya Bwana. Sala unaweza kujifunza.
Kwa kiwango fulani, maombi ni ya asili kwa kila mtoto wa Mungu; hata hivyo, unaweza kujifunza sala. Mtoto mdogo anajifunza kuzungumza bila kuchukua masomo ya kuzungumza. Hata hivyo, mtoto anapokua, hujifunza zaidi kuhusu lugha, msamiati, na usemi unaofaa. Vivyo hivyo, kwa kawaida Mkristo mchanga hutamani kuzungumza na Mungu, lakini kadiri tunavyokomaa katika imani, uelewaji wetu na uthamini wetu wa sala huimarishwa.
Vitabu kuhusu maombi vinaweza kuongeza uelewa wako wa maombi. Vitabu vichache kuhusu maombi ambavyo vinaweza kumnufaisha kila Mkristo ni:
Power Through Prayer (Nguvu kupitia Maombi) E.M. Bounds
With Christ in the School of Prayer (Pamoja na Kristo katika Shule ya Maombi) by Andrew Murray
Mighty Prevailing Prayer (Maombi yenye Nguvu Inayotawala) by Wesley Duewel
Omba Maneno ya Maandiko
Hakuna mahali pazuri pa kujifunza maombi kuliko katika maandiko. Shule ya kwanza ya maombi ni Biblia. Zaburi na maombi mengine ya kibiblia yanatufundisha kuomba kwa ufanisi. Kupitia historia ya kanisa, Wakristo wakuu wamejaza maombi yao na maandiko. Baadhi ya maombi makubwa katika Biblia ni pamoja na:
Maombi ya Kutukuza. Kutoka 15:1-18, 1 Samweli 2:1-10, 1 Mambo ya Nyakati 29:11-20, Luka 1:46-55, Luka 1:68-79, 1Timotheo 6:15-16, na Ufunuo 4:8 -5:14.
Mombi ya Kuungama. Ezra 9:5-15, Zaburi 51, na Danieli 9:4-19.
Maombi ya Kuombea wengine. Mwanzo 18:23-33, Kutoka 32:11-14, Waefeso 1:15-23, na Wafilipi 1:9-11.
Zingatia Kuhusu Ushirika na Mungu
Mara nyingi, maombi yetu yanajikita tu kwenye kuomba vitu kutoka kwa Mungu. Watu wengine humpa Mungu orodha ya mahitaji yao ya maombi, wanamshukuru kwa kujibu maombi ya jana, na kusema “Amina.” Maombi ya kweli lazima yawe zaidi ya orodha ya kupeleka mahitaji; maombi ni ushirika na Mungu.
Sala ya Bwana hutoa kielelezo cha maombi (Mathayo 6:9-13). Sala ya Bwana ilijumuisha:
Kutukuza: “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.”
Utii: “Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”
Ombi: “Utupe leo riziki yetu.”
Kuungama: “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.”
Maombi ya Mwongozo: "Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu."
Sifa: “Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.”
Wengi wa wakristo wanafuata mfano wa sehemu nne ambao unajumuisha kila moja ya vipengele katika maombi ya mfano wa Yesu: kutukuza, ungamo, kushukuru na Dua.
Kutukuza
Maombi hayapaswi kamwe kuacha kutukuza na kusifu. Kwa kuanza na sifa, tunahakikisha kwamba maombi yetu siyo tu orodha ya maombi ya msaada. Zaburi hutoa mfano wa maombi ambayo msingi wake ni sifa. Hata zaburi za maombolezo zinajumuisha sifa. Ikiwa maombi ni ibada ya kweli, itajumuisha kusifu na kumwabudu Mungu.
Kuungama
Isaya 6 inaonyesha kwamba tunapomwona Mungu (kutukuza), tutajiona wenyewe. Tunapojiona katika nuru ya usafi kamili wa Mungu, tunaelewa hitaji letu la kuungama. Hakuna Mkristo, hata awe amekomaa kiasi gani, hata awe ametembea na Mungu kwa kiasi gani, hapaswi kufikia mahali ambapo atasema, “Sina haja ya kutubu. Ukamilifu wangu ni wa hakika." Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Msalipo, semeni … utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye.” (Luka 11:4). Ibada ya kweli inahusisha kuungama.
Shukrani
Kutukuza humsifu Mungu kwa jinsi alivyo; shukrani inamsifu Mungu kwa kile anachofanya katika ulimwengu wetu. Shukrani inatambua kwamba kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu (Yakobo 1:17). Katika kushukuru, tunamshukuru Mungu kwa yale ambayo ametutendea katika maisha yetu. Hadithi ya wakoma 10 inaonyesha umuhimu wa kushukuru (Luka 17:12-19).
Dua
Katika Sala ya Bwana, Yesu alionyesha kwamba Mungu anathamini maombi ya watoto wake. Mungu si kama mtawala wa kidunia ambaye ana shughuli nyingi sana kiasi kwamba atahangaishwa na mahitaji ya raia wa kawaida. Badala yake, Mungu ndiye Baba mkamilifu ambaye hufurahia kuwapa watoto wake zawadi nzuri. Katika Sala ya Bwana, tunatiwa moyo kuomba kwa ajili ya mahitaji ya kawaida (“tupe mkate wetu wa kila siku”) na kwa ajili ya mwongozo wa kiroho (“usitutie majaribuni”).
Katika Sala ya Bwana, tunajifunza kuwasilisha mapenzi yetu kwa Mungu tunapoomba. Tukiwa kama watoto wenye imani, tunajifunza kwamba mapenzi yake ni makamilifu; "hapana" yake ni kwa faida yetu. Maombi sio zana ya kichawi ya kumlazimisha Mungu kufanya mapenzi yetu. Maombi ni nidhamu ya kiroho ambayo hutuletea utii kwa furaha kwa mapenzi ya Mungu.
Sawazisha Vipaumbele Vyako na vya Mungu.
Mara nyingi maombi huonyesha lililo muhimu zaidi kwetu. Ni nini kinachochochea maombi yetu ya dhati, mahitaji ya kimwili au mahitaji ya kiroho?
Katika maombi yake kwa ajili ya Wakristo wa Thesalonike, Paulo alisema, “twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu; jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake…” (2 Wathesalonike 1:11-12) Dhumuni kuu la Paulo lilikuwa kwamba Mungu angetimiza kusudi lake katika maisha yao. Wakristo hawa walikuwa wakiteswa, lakini maombi ya Paulo haikuwa ili Mungu awaokoe kutokana na mateso. Badala yake, aliomba kwamba jina la Bwana Yesu litukuzwe ndani yao.
Kama vile maombi yetu yanavyoonyesha vipaumbele vyetu, shukrani zetu zinaonyesha vipaumbele vyetu. Ikiwa shukrani zetu ni kwa ajili ya baraka za kimwili, baraka za kimwili zinaweza kuwa kile tunachothamini zaidi. Ikiwa sehemu kubwa ya shukrani zetu ni kwa ajili ya msaada wa Mungu katika maisha yetu ya kiroho, kukua kiroho ndiko tunakothamini zaidi.
Katika maombi yake kwa ajili ya Wathesalonike, Paulo alitoa shukrani kwa Mungu kwa sababu imani yao ilikuwa ikiongezeka sana, na upendo wao kati yao ulikuwa ukiongezeka (2 Wathesalonike 1:3). Shukrani zake kuu zaidi hazikuwa kwa baraka za muda; shukrani zake kuu zaidi zilikuwa kwa ukuaji wao wa kiroho. Ni nini kinakupa sababu kuu ya shukrani, baraka za kifedha au ushahidi wa ukuaji wa kiroho katika maisha yako?
Zungumza na Mungu, si kwa waumini.
Kupitia maandiko, Mungu anazungumza na waumini. Katika maombi, waumini huzungumza na Mungu. Muda wa maombi ya hadhara sio fursa kwa kiongozi kuwaambia watu (kupitia maombi) anachotaka kuwaambia! Maombi huzungumza na Mungu.
Yesu aliwaambia wanafunzi wake jinsi ya kusali katika roho ya ibada ya kweli:
Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba (Mathayo 6:5-8).
Maombi ya kweli hayajaribu kumvutia Mungu au watu; yanazungumza kwa urahisi na uwazi kwa Baba yetu wa mbinguni.
► Utafanya nini ili kukua katika maisha yako ya kibinafsi ya maombi? Je, utafanyaje maombi kuwa sehemu ya maana zaidi katika ibada ya hadhara ndani ya kanisa lako?
“Jambo kuu katika maisha ya Kikristo ni uzoefu wa kila siku wa ibada na kumwabudu Mungu kama kitovu cha maisha yetu binafsi.”
- Dennis Kinlaw
Sadaka Kama Mwitikio wa Neno la Mungu
Maombi ni mwitikio wa asili kwa Neno la Mungu. Kwa sababu hii, tunapaswa kufuata usomaji wa maandiko na mahubiri na kufanya maombi. Katika maombi, tunaitikia kweli ambayo tumepokea kutoka kwa Neno la Mungu; tunajitoa kwa utii.
Sadaka pia ni mwitikio kwa Neno la Mungu. Katika Agano la Kale, dhabihu (sadaka) ilikuwa mwitikio wa anayeabudu kwa Sheria (Neno la Mungu). Katika Agano Jipya, sadaka inaashiria kujisalimisha kwa Mungu wa maisha yetu yote.
Sadaka ni sehemu ya ibada. Mtunga-zaburi aliwahamasiha waabudu kuleta sadaka, na kuingia katika nyua zake (Zaburi 96:8). Mwandishi wa Waebrania aliunganisha ibada na kutoa; “lakini msisahahu kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu” (Waebrania 13:16). Paulo aliwaambia Wafilipi kwamba zawadi yao kwake ilikuwa ni sadaka yenye harufu nzuri, dhabihu inayokubalika na kumpendeza Mungu (Wafilipi 4:18).
Theolojia Ya Utoaji Ibadani
Waenda kanisani wengi huona kuwa sadaka kama njia ya kulipa bili za kanisa. Hii inafanya sadaka kuwa shughuli ya kifedha badala ya tendo la kiroho la ibada. Uwakili wa Kikristo unapaswa kueleweka kama sehemu ya ibada. Kila moja ya kanuni zifuatazo inapaswa kuwa sehemu ya theolojia yetu ya utoaji.
Utoaji ibadani huchochewa na neema, sio woga
Utoaji kama kitendo cha ibada huchochewa na shukrani kwa Neema ya Mungu. Paulo aliwasihi Wakorintho kutoa msaada kwa wakristo wenye uhitaji huko Yerusalemu. Hakuwatishia, “Ni lazima utoe kwasababu ipo siku utahitaji msaada.” Badala yake, Alihitimisha msisitizo wake na sifa, “Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake” (2 Wakorintho 9:15). Utoaji wao ungechochewa sana na shukrani kwa kipawa cha Mungu chenye neema. Ikiwa sadaka ni ibada ya kweli, hutoka kwenye moyo wa utayari.
Utoaji ibadani huchochewa na upendo, sio thawabu
Ibada ya kweli huchochewa na upendo kwa Mungu, sio tamaa ya kupata thawabu. Kipawa cha fedha ni ishara ya zawadi yetu sisi wenyewe kwa Mungu. Paulo aliwasifu Wakristo wa Makedonia kwa sababu “walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu” (2 Wakorintho 8:5). Karama zao zilikuwa ishara ya upendo wao kwa Mungu na kwa mitume walioleta injili katika eneo lao.
Kama vile muziki au shughuli nyingine yoyote ya ibada inaweza kufanywa kwa sababu zisizofaa, utoaji unaweza kuchochewa na tamaa ya kupata thawabu badala ya kumpenda Mungu. Wainjilisti wengine huahidi kwamba Mungu atalipa zawadi za pesa kwa baraka za kifedha. Kwa kupindisha maandiko kutoka katika muktadha wake wa kibiblia, wanaahidi thawabu mara mia kwa zawadi kwa Mungu. Utoaji huo hauwezi kuwa tendo la ibada ya upendo, bali utakuwa kama kununua tikiti ya bahati nasibu ambayo mtoaji anatarajia kushinda! Hakuna mahali popote ambapo Biblia husifu utoaji wa namna hii.
Badala yake, Biblia inapongeza utoaji wa Maria. Alipomtia Yesu mafuta, hakukuwa na thawabu yoyote mbele yake. Alimwaga akiba yake bila kufikiria kurudi. Hata wanafunzi walikasirika kwa sababu ya uharibifu wake. Ni Yesu pekee aliyeona na kusifu zawadi yake, zawadi ambayo ilichochewa na upendo pekee (Mathayo 26:6-13).
Utoaji ibadani hauchochewi tu na upendo kwa Mungu, bali upendo kwa wengine. Yohana aliwakumbusha wasomaji wake kwamba upendo wa kweli ni zaidi ya maneno; ni vitendo. Upendo wa Wafilipi kwa Paulo ulionekana katika utoaji wao. Upendo wa muumini kwa wengine unaonekana katika kutoa.
Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli (1 Yohana 3:17-18).
Utoaji wa ibadani huchochewa na ukarimu, sio ubakhili.
Paulo alitoa changamoto kwa kanisa la Korintho kwa kutoa kwa ukarimu aliposema, “Mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu.” Ukarimu wao ulikuwa udhihirisho wa shukrani zao kwa Mungu. “ maana utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu” (2 Wakorintho 9:11-12). Ili kutoa iwe ibada ya kweli, ni lazima kuwe na ukarimu.
Utoaji wa ibadani huchochewa na unyenyekevu, sio kiburi.
► Soma Mathayo 6:1-4.
Katika Mahubiri ya Mlimani, Yesu alionya kuhusu nia mbaya za kutoa. Wengine hutoa ili kupokea sifa kutoka kwa wengine; malipo yao ni sifa. " Wamekwisha kupata thawabu yao." Wengine hutoa kwa utulivu, huku wakijisifu kwa unyenyekevu wao; malipo yao ni kujitosheleza. Yesu akasema, “hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume.” Usijipongeze kwa ukarimu wako. Badala yake, mruhusu Baba yenu aliye mbinguni awaone na kuwapa thawabu kama apendavyo.
Hadithi ya Kutoa kwa Furaha
Yohana Wesley alikuwa amemaliza kununua picha za kupamba chumba chake wakati mjakazi alipokuja kwenye mlango wake. Ilikuwa siku ya baridi na aligundua kuwa alikuwa amevaa gauni jepesi tu. Aliingiza mkono mfukoni ili kumpa pesa ya kununua koti, na akakuta amebakiza pesa kidogo. Alilia, “Nimepamba kuta zangu kwa pesa ambazo zingeweza kumkinga kiumbe huyu maskini kutokana na baridi!”
Yohana alianza kupunguza matumizi yake ili apate pesa za kuwapa maskini. Katika jarida lake, alirekodi kwamba mwaka mmoja mapato yake yalikuwa milioni 5, na gharama zake za maisha milioni 4, hivyo alikuwa na milioni 1 kwa ajili alitoa. Mwaka uliofuata, mapato yake yaliongezeka maradufu, lakini bado aliishi kwa shilling milioni 4 na alitoa milioni 6. Katika mwaka wa tatu, mapato yake yalipanda hadi milioni 15; tena aliishi kwa milkoni 4, akitoa milioni 11 kwa wahitaji. Mwaka wa nne, alitengeneza milioni 20, akaishi tena kwa milioni 4, na akatoa milioni 16 kwa masikini.
Yohana alihubiri kwamba Wakristo hawapaswi kutoa zaka tu, bali watoe ziada. Aliamini kwamba kwa kuongeza mapato, utoaji wetu unapaswa kuongezeka. Alifanya mazoezi haya katika maisha yake yote. Hata mapato yake yalipoongezeka hadi mamilioni ya pesa, aliishi kwa urahisi na kutoa pesa za ziada. Mwaka mmoja mapato yake yalikuwa zaidi ya milioni 50; alitoa zote isipokuwa milioni 5.[1] Alisema kuwa hakuwahi kuweka zaidi ya milioni 20. Alitoa zaidi ya milioni 100 alizopata katika maisha yake.[2]
Hoja ya hadithi hii sio amri ya kisheria ya umaskini! Jambo kuu ni kumtii Mungu kwa furaha na kwa hiari. Mungu hawapi kila mtu mapato sawa na Yohana; Mungu halazimishi kila mtu kutoa kwa kiwango sawa na Yohana. Kipimo sio, "Je, mimi natoa kama mtu mwingine?" kipimo ni, “Je, ninamtii Mungu kwa furaha?” Mungu anatutaka tuabudu kwa kutoa dhabihu.
Mazoezi Ya Kutoa
Kwasababu utoaji ni kitendo cha ibada, sadaka zinapaswa kukusanywa kwa njia ambayo inahamasisha roho ya ibada. Zingatia mawazo ya kivitendo yafuatayo.
Mkazo kuhusu sadaka unapaswa kuwa ni Ibada, na sio mahitaji.
Labda sababu ambayo Wakristo wengi wanaona sadaka kimsingi ni njia ya kulipa gharama za kanisa ni kwamba msisitizo katika utoaji ni kulipa gharama! Hii inakuwa mbaya zaidi wakati shida ya kifedha inapotufanya kusema, "Kanisa litafungwa" au "Hatuwezi kutuma mmishonari" ikiwa sadaka za ukarimu hazijatolewa. Wakati mwingine mchungaji huomba msamaha kwa ajili ya kuomba sadaka; "ningependa tusiwe tunahitaji kuomba sadaka kwenu." Badala yake, sadaka inapaswa kuwa kielelezo cha shukrani yenye furaha.
Wakati wa kutoa sadaka, mkazo unapaswa kuwa ibada. Utoaji wa sadaka unaweza kutambulishwa kwa andiko linalowakumbusha waabudu kusudi la kutoa sadaka. Maandiko kama vile 2 Wakorintho 8:9 na 9:7, Kutoka 25:2, Matendo 20:35, na hata Yohana 3:16 yanaelekeza kwenye motisha ya kweli ya kutoa.
Sadaka inapaswa kuwa sehemu ya Ibada yenyewe
Katika tamaduni zingine, ni jambo la kawaida kuhimiza watu kutoa sadaka zao mbali na ibada yenyewe. Ingawa hii inaweza kuchochewa na tamaa ya kuepuka maonyesho au kuokoa muda katika ibada, inapelekea kutenganisha sadaka na ibada. Kuchukua sadaka kama sehemu ya ibada huwasaidia waabudu kuelewa utaoji kama tendo la ibada.
Kwa kuwa sadaka ni mwitikio wetu kwa Mungu, unaweza kufikiria kuchukua sadaka baada ya mahubiri kuliko kabla ya mahubiri. Hii inaonyesha, “Tunamtolea Mungu kwa kuitikia Neno lake.”
Wazazi wanapaswa kuwaanzishia watoto wao tendo la kutoa ibadani.
Kama vile tunavyowafundisha watoto wetu kuimba, kusali, na kusikiliza maandiko yanayosomwa na kuhubiriwa, tunapaswa kuwafundisha watoto wetu kutoa kwa furaha. Watoto wetu wanapojifunza kwamba kutoa ni tendo la kusifu la shangwe, wao pia wanakuwa waabudu.
Muziki wakati wa sadaka unapaswa kuwa ibada.
Ikiwa sadaka ni ibada, muziki wakati wa sadaka unapaswa kuwa ibada. Muziki huu unaweza kuwa wa kutumia vyombo vya muziki au sauti; unaweza kuongozwa na muimbaji binafsi au kanisa zima; unaweza kuwa wa utulivu na wa kutafakari au furaha na shangwe; bila kujali mtindo, unapaswa kuwa sehemu ya ibada. Wale wanaohudumu wakati wa sadaka wanapaswa kuomba mwongozo wa Roho kama vile kiongozi wa ibada anavyoomba mwongozo wa Roho. Hakuna sehemu ya ibada inayopaswa kuchukuliwa kirahisi.
Sadaka inapaswa kuambatana na maombi ya kujitolea.
Kwa kuwa sadaka ni zawadi kwa Mungu, sadaka inapaswa kuambatana na maombi ya kujitakasa. Hilo huwakumbusha waabudu kusudi la kutoa na hutoa uthibitisho unaoonekana wa kutoa kama ibada.
Viongozi wa kanisa wanapaswa kuwa mawakili wazuri wa karama za watu.
Katika sadaka, waabudu wanakabidhi zawadi zao kwa uwakili wa viongozi wa kanisa. Viongozi wa kanisa lazima wawe watunzaji wazuri wa zawadi hizo. Hesabu kwa waumini kuhusu matumizi ya fedha huonyesha kwamba sadaka zinatumika kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hii inachochea utoaji na kupunguza jaribu la kukosa uaminifu kwa uongozi wa kanisa. Katika ulimwengu ambao viongozi wa Kikristo wanatazamwa kwa shaka, tunapaswa kufanya kila linalowezekana kuonyesha kwamba sisi wenyewe hatuna hatia.
Sadaka ni zaidi ya njia ya kulipa bili; ni ibada. Kupitia Neno lake, Mungu anajifunua kwa waabudu. Tunaitika kwa kutoa zawadi za sadaka kutoka kwenye mioyo yenye furaha. Hii ndiyo ibada ya kweli.
Kujipima
Je, watu katika kanisa lako wanahisi kwamba wanaabudu wanapotoa sadaka, au wanalipa tu gharama za kanisa? Ni hatua gani zinazofaa unazoweza kuchukua ili kufanya sadaka iwe tendo la ibada?
[1]Kwa kulinganisha na hali ya leo, hii ni sawa na kupata Tsh 538,577,934 na kuitoa yote isipokuwa Tsh 13,464,448. Inakadiriwa Wesley alipata na kutoa kiasi cha Tsh 8,078,669,010 kwa thamani ya fedha za leo katika Maisha yake yote.
► Jadili jinsi mnavyoadhimisha ibada ya ushirika katika kanisa lako. Je, unaadhimisha Meza ya Bwana mara ngapi? Unapofanya ushirika, je, ni sehemu muhimu ya ibada?
Kama vile Mungu anavyofunuliwa katika Neno lililoandikwa (usomaji wa maandiko) na katika neno linalonenwa (kuhubiriwa kwa Neno lake), anafunuliwa katika neno lililoonyeshwa la Meza ya Bwana.[1] Meza ya Bwana ni ukumbusho wa kifo cha upatanisho cha Yesu na sherehe ya ufufuo wake. Karamu ya Mwisho ilihusiana na Pasaka, lakini pia ilizindua agano jipya.
► Soma Mathayo 26:17-30 na 1 Wakorintho 11:17-34.
Marejeleo ya Agano Jipya kuhusu Meza ya Bwana yanajumuisha maelezo katika injili na maagizo ya Paulo kwa kanisa la Korintho.
Maswali matatu mara nyingi huulizwa kuhusiana na kuadhimisha Meza ya Bwana.
Je, ni mara ngapi Meza ya Bwana inapaswa kuadhimishwa?
Je, ni kwa jinsi gani Meza ya Bwana inapaswa kuadhimishwa?
Nini maana ya Meza ya Bwana
Kuadhimisha Meza ya Bwana ni sehemu yenye maana katika ibada.[3] Paulo aliandika kwa kanisa huko korintho, akionyesha hilo katika Meza ya Bwana.
1. Tunatazama nyuma kwenye kifo cha Kristo ("unatangaza kifo cha Bwana").
2. Tunatazamia kurudi kwa Kristo ("mpaka atakapokuja").
Tunapoadhimisha Meza ya Bwana, tunakumbuka dhabihu yake, na tunatazamia kurudi kwake kwa ahadi. Vifaa vinawakilisha mwili na damu ya Kristo na vinatukumbusha ushiriki wetu katika kifo cha Bwana. “Kikombe cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, je, si ushirika wa mwili wa Kristo?” (1 Wakorintho 10:16) Meza ya Bwana ni ishara yenye nguvu ya kuendelea kuwepo kwa Bwana aliyesulubiwa na kufufuka.
Je, Meza ya Bwana Inapaswa Kuadhimishwa Mara ngapi?
Maandiko wala historia ya kanisa haitoi jibu la uhakika kwa swali hili. Katika kanisa la kwanza, inaonekana kwamba Meza ya Bwana ilichukuliwa kila Jumapili. Leo, baadhi ya makanisa husherehekea Ushirika kila juma wakati wengine huiadhimisha mara moja au mbili tu kwa mwaka.
Maadamu Meza ya Bwana ni sehemu takatifu ya ibada, kuadhimisha mara kwa mara hakupunguzi maana ya Meza ya Bwana kama vile usomaji wa Biblia wa kila juma hakupunguzi umuhimu wa maandiko katika ibada.
Je, ni kwa jinsi gani Meza ya Bwana inapaswa kuadhimishwa?
Paulo aliwaonya Wakorintho kuhusu kula na kunywa “isivyostahili” (1 Wakorintho 11:27 ).[4] Hatua kadhaa zinazofaa zaweza kutusaidia kuadhimisha Meza ya Bwana kwa njia inayostahili umuhimu wake kwa wakristo.
Ushirika Mtakatifu unapaswa kuwa sehemu kuu ya ibada, sio nyongeza.
Wakati wa kawaida wa Meza ya Bwana ni baada ya mahubiri. Katika hali hii, mahubiri yanapaswa kutuongoza kuelewa kwa kina Zaidi kuhusu Meza ya Bwana. Hii inaweza kufanywa kupitia mahubiri yanayolenga moja kwa moja Meza ya Bwana, au kupitia mahubiri kuhusu mada inayohusiana (ukombozi, upatanisho, neema, ufuasi). Kwa makanisa yanayoadhimisha Meza ya Bwana mara kwa mara, haifai kulenga mada ya kila ibada kwenye Ushirika. Hata hivyo, inapaswa kuwepo uhusiano wa wazi kati ya maadhimisho ya Ushirika na ibada iliyotangulia.
Ushirika Mtakatifu ni tukio kuu na la furaha.
Ushirika ni wakati wa kujichunguza na kusherehekea neema ya Mungu kwa furaha. Maadhimisho haya yanaakisiwa katika ukumbusho kwamba Meza ya Bwana huliwa kwa kukumbuka kifo cha Bwana. Furaha ya maadhimisho hayo inaonekana katika ahadi ya kurudi kwa Bwana.
Wakati fulani, kusherehekea ufufuo na kutazamia kurudi kwa Kristo kunaweza kuwa mkazo mkuu katika Ushirika. Wakati mwingine, sherehe kuu ya kifo cha Yesu na umuhimu wa kujichunguza mwenyewe kunaweza kuwa mkazo mkuu. Vipengele vyote viwili ni sehemu ya maadhimisho haya.
Tunafurahi katika Ushirika Mtakatifu kwa sababu Meza ya Bwana inawezekana kwa neema ya Mungu. Katika Meza ya Bwana, tunakumbushwa kwamba neema pekee hutoa wokovu wetu. Tunatambua maadhimisho ya Ushirika kwa sababu tunakumbuka kwamba kushiriki kwetu katika Meza ya Bwana kunawakilisha kujitolea binafsi kuikimbia dhambi. Katika Meza ya Bwana, kila mwabudu lazima ajichunguze mwenyewe.
Ushirika unapaswa kuonyesha umoja wa kanisa.
Inasikitisha kwamba Ushirika, agizo ambalo lilikusudiwa kuakisi umoja wa kanisa, wakati mwingine imekuwa sababu ya mgawanyiko. Tofauti za jinsi Meza ya Bwana inavyotolewa (vikombe vya mtu binafsi, kikombe cha kawaida, kuchovya mkate ndani ya kikombe) na tofauti za nani anaweza kushiriki (wote wanaojiita waumini, wale tu ambao wamebatizwa, washiriki wa kanisa la mahali pekee) zimeongoza kuleta mgawanyiko kati ya makanisa.
Paulo alikumbusha kanisa la Korintho kwamba waliposhiriki mkate mmoja, lazima wawe mwili mmoja. “Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja” (1 Wakorintho 10:17).
Tunapaswa kukumbuka kwamba katika Ibada ya Ushirika, kuabudu ni ya msingi huku taratibu zikiwa za pili. Ni lazima kanisa lidumishe taratibu ambazo ni aminifu kwa injili na 1 Wakorintho. Hata hivyo, bila kujali njia ambayo Meza ya Bwana inaandaliwa, haipaswi kuleta mgawanyiko. Katika Meza ya Bwana, tunasherehekea umoja wa kanisa.
[1]Franklin M. Segler and Randall Bradley, Christian Worship: Its Theology and Practice (Nashville: B&H Publishing, 2006), 178
“Meza ya Bwana ni miadi ya Bwana na watu wake. Wale wanaoshika miadi hii pamoja na Kristo wanaweza kutarajia kwa uhakika kwamba watakuja kukutana naye.”
[4]Katika KJV “kunywa isivyostahili” wakati mwingine inatafsiriwa kurejelea mtu asiye stahili meza ya Bwana. Walakini, katika “kwa namna isiyostahili” inaonekana kuwa ni tafsiri bora. Hakuna mtu anayestahili dhabihu ya Yesu. Tatizo la kusahihisha katika Korinto ilikuwa sio kutokustahili mwabuduji, lakini kutokuheshimu, namna isivyostahili ilikuwa ni njia isiyostahili ambayo walikuwa wakishiriki mlo huu mtakatifu.
Hitimisho: Ushawishi Mkubwa wa Ibada
Je, ibada ni muhimu? Hapa kuna ushuhuda kutoka 1945 unaoonyesha kile kinachoweza kutokea wakati mtu wa kawaida anaabudu kwa njia ya maombi.
Wakati wa Vita vya pili ya Dunia, mwanafunzi wa Kijapani-mmarekani aliyekuwa wa Imani ya kibbudha na kubadilika kuwa mkristo, katika Chuo Kikuu cha Baylor alikua chombo cha uamsho. Reiji Hoshizaki alifanya kazi kama mlinzi wa nyumba ili kulipa ada ya shule. Wakati alipokuwa akisafisha madarasa, alianza kuomba kando ya kila dawati.
Siku moja, baada ya wiki kadhaa za maombi, Reiji alikuwa ameketi darasani alipovamiwa na mzigo kwa ajili ya wanafunzi wenzake hivyo alipiga magoti na kuanza kulia na kuomba. Wanafunzi waliuliza, "Reiji ana shida gani?" Hakuna kibaya kilichokuwa kimemtokea Reiji; kiti chake kimekuwa madhabahu yake.
Kupitia maombezi ya Reiji, uamsho ulienea katika Chuo Kikuu cha Baylor na kisha kwenda jimbo la Texas. Makumi ya wainjilisti wanafunzi waliondoka chuo cha Baylor kwenda kuchukua uamsho katika kusini-magharibi mwa Marekani. Maombi ni sehemu muhimu ya ibada. Tunapoabudu, ulimwengu wetu unabadilishwa na nguvu za Mungu.
(1) Tunaweza kufanya Maandiko kuwa kitovu cha ibada kwa kuingiza Maandiko katika sehemu zote za ibada yetu.
(2) Kwa kuwa maandiko ni muhimu katika ibada, tunapaswa kuhakikisha kwamba yanasomwa kwa ufasaha, kwa uwazi, na kwa njia mbalimbali ambazo zitafanya usomaji kuwa safi.
(3) Kwa kuwa Mahubiri ni sehemu ya ibada:
Kuhubiri kunahitaji maandalizi mazuri.
Kuhubiri kunahitaji mwitikio kutoka kwa waumini.
Kuhubiri kunahitaji mwitikio kutoka kwa mhubiri.
Mhubiri lazima awezeshwe na Roho Mtakatifu.
(4) Njia za vitendo za kufanya maombi kuwa sehemu ya maana katika ibada ya pamoja:
Sitawisha maisha yako ya maombi ya kibinafsi.
Jifunze jinsi ya kuomba.
Omba maneno ya maandiko.
Zingatia kuimarisha ushirika na Mungu.
Sawazisha vipaumbele vyako na vya Mungu.
Zungumza na Mungu, si kwa waumini.
(5) Kwa kuwa sadaka ni sehemu ya ibada:
Utoaji unapaswa kuchochewa na neema, si na hofu.
Kutoa kunapaswa kuchochewa na upendo, si thawabu.
Kutoa kunapaswa kuwa kwa ukarimu, sio ubahili.
Utoaji unapaswa kuchochewa na unyenyekevu, sio kiburi.
Jinsi tunavyokusanya sadaka inapaswa kuchangia roho ya ibada.
(6) Meza ya Bwana
Inatazama nyuma kwenye kifo cha Kristo.
Inatazamia kurudi kwa Kristo.
Inapaswa kuzingatiwa kwa njia inayofaa.
Inapaswa kuzingatiwa kwa njia ya heshima na ya furaha.
Inapaswa kuzingatiwa kwa namna inayoakisi umoja wa kanisa.
Somo la 7 Mazoezi
(1) Katika Somo la 6, ulichagua nyimbo zinazohusiana na mada tano tofauti. Kwa kila moja ya mada hizi tano, tafuta marejeo 3-4 ya maandiko yanayozungumzia mada hiyo. Orodha zako zitatumika katika somo la baadaye unapopanga ibada.
3-4 mistari kuhusu asili ya Mungu
3-4 mistari kuhusu Yesu na kifo chake na kufufuka kwake
3-4 mistari Roho Mtakatifu na kanisa
3-4 mistari inayowaita watu kujitolea, maisha matakatifu
3-4 mistari kuhusu uinjilisti na umisheni
(2) Mwanzoni mwa somo linalofuata, utafanya mtihani kulingana na somo hili. Jifunze maswali ya mtihani kwa uangalifu katika maandalizi.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.