Utangulizi
Jia hakuweza kumwona rafiki yake kijana Lee kwa wiki mbili. Alipoulizia kwa jirani yake, alipewa taarifa za kusikitisha kwamba mama yake na kijana Lee alifariki kutokana na ugonjwa wa muda mrefu. Lee alikuwa ameenda Taoyuan kuungana na familia yake.
Wakati Jia alipokutana na Lee wiki mbili baadaye, alielezea masikitiko yake kutokana na kifo cha mama yake. Lee alimshukuru sana yule dada kwa wema wake, lakini baadaye akaongea kwa uchungu, “Hii ndiyo maana mimi siwezi kumwamini Mungu wa Wakristo. Kama kuna Mungu, kwa nini aliruhusu mama yangu ateseke kiasi hicho? Mnasema Mungu wenu ni mwenye nguvu sana na mwenye upendo sana. Kama kweli alikuwa anampenda mama yangu, na kama kweli alikuwa na nguvu za kuweza kuzuia mama yangu asiteseke, kwa nini alimwacha ateseke kiasi hicho? Inawezekana kuna Mungu, lakini hana uwezo wa kutusaidia. Au inawezekana kuna Mungu, lakini hajali kuhusu mateso yetu. Au labda hakuna Mungu. Naamini tuko peke yetu katika ulimwengu huu.”
► Utamjibuje Lee?
.jpg)

