Utangulizi
Katika Maonyesho ya Dunia ya Chicago mwaka 1893, Bunge la Dini mbalimbali liliruhusu uwakilishi wa wajumbe kutoka kila dini kubwa za dunia kutoa mada. Wanenaji kutoka kila dini walijaribu kuishawishi hadhira kwamba dini zao zilikuwa bora na za maana zaidi kuliko za wengine.
Mwakilishi wa mwisho kunena alikuwa Mchungaji Yusufu Cook, aliyekuwa akiwakilisha imani ya Kikristo. Kabla ya Cook kunena, msemaji wa dini ya Hindu akaushambulia Ukristo kama “dini iliyo mbaya kuliko dini nyingine zote” kwa sababu inawaita watu “watenda dhambi.”
Badala ya kushambulia dini nyingine yeyote, Yusufu Cook alianza kwa kumwelezea Bi. Macbeth kutoka kitabu cha Shakespeare. Alielezea jinsi Bi. Macbeth, kutokana na wivu na matamanio, alivyomshawishi mumewe kumwua mfalme Dankani wakati alipokwenda kumtembelea katika kasri lake.
Baada ya kitambo kidogo, Bi. Macbeth alipatwa na maumivu makali ya kujisikia mwenye hatia. Wakati wa mchana, alikuwa na tamaa ya makuu na mjasiri. Lakini usiku, Bi. Macbeth ataamka mara kadhaa kwenda kuosha mikono huku akilia, “Nina doa.” Je! Kwa kuosha mikono atatakasika?
Yusufu Cook alimwuliza mwakilishi wa kila dini, “Je! kuna chochote katika dini yenu kinachoweza kuondoa damu ya hatia iliyoko kwenye mikono ya Bi. Macbeth?” Hakuna hata mmoja aliyeongea. Hakuna dini yenye uwezo wa kuosha damu kutoka katika mikono ya Bi. Macbeth?” Hakuna aliyeongea. Hakuna dini yenye uwezo wa kuosha damu kutoka katika mikono ya Bi Macbeth. Kisha Mchungaji Cook akageukia kwenye hadhira na kuhitimisha, ‘Damu ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, inatutakasa kutokana na dhambi zetu!”
Katika somo hili, tutaona kwamba Ukristo uko tofauti na dini nyingine zote. Tofauti iliyopo kati ya injili na dini nyingine ni hii: tunaamini kwamba alikuja duniani katika sura ya kibinadamu ya Mwanae, Yesu, kutoa njia ya msamaha kwa ajili ya dhambi zetu na kuturejesha tena katika sura na mfano wake.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)