Malengo ya Somo
Mwishoni mwa somo hili, mwanafunzi anapaswa:
(1) Kufahamu tarehe sahihi na mazingira ya kihistoria ya Nyaraka za Kichungaji.
(2) Kuorodhesha mada kuu na kusudi la Nyaraka za Kichungaji.
(3) Kuibua sifa za kibiblia kwa viongozi wa Kanisa.
(4) Kupata heshima ya ndani kwa majukumu ya kichungaji kwenye maeneo kama vile mafundisho ya kimaelekezo, taasisi ya kanisa, na uongozi wa Roho Mtakatifu.
(5) Kupewa changamoto kuishi maisha ya uaminifu kwa wito wa Mungu.
(6) kufupisha kanuni za kiutendaji kwa huduma ya Kikristo kutoka kwenye nyaraka za kichungaji.
(7) Kuhusianisha ujumbe wa vitabu hivi katika uhitaji wa ulimwengu wa leo.