Huduma Ya Uongozi
Huduma Ya Uongozi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 17: Mambo ya Binafsi: Fedha, Muda, na Mavazi.

19 min read

by Stephen Gibson


Utunzaji wa Fedha

Kanuni ya Uwajibikaji

► Mwanafunzi atapaswa kusoma Mathayo 25:14-30 kwa ajili ya kikundi. Je, aya hii inatueleza nini kuhusu utunzaji wa fedha?

Fedha ni rasilimali muhimu sana kwa ajili ya huduma. Viongozi wanapaswa wawe watunzaji wa fedha ili kupata matokeo bora zaidi. Tutawajibika mbele ya Mungu kwa ajili ya rasilimali anazotupa ili tuzitunze.

Kumbuka hadithi ya Msamaria aliyekuwa amemsaidia yule msafiri aliyekuwa amejeruhiwa na wanyang’anyi (Luka 10:30-35). Kusudi la hadithi hii lilikuwa ni kuelezea inamaanisha nini kuwapenda watu unapokutana nao. Hata hivyo, tunaweza kupata pointi nyingine hapa kwa kutazama baadhi ya vipengele kwa undani ingawaje pointi hii haikuwa imekusudiwa iwe muhimu na mwandishi.

Msamaria alikuwa na punda, na alikuwa fedha ya kulipa kwa ajili ya kumtunza yule mtu aliyekuwa amejeruhiwa. Je, kama angekuwa ametoza rasilimali zake ingekuwaje kabla ya kukutana na mtu aliyekuwa amejeruhiwa? Angekuwa hana uwezo wa kumsaidia. Wako watu wengi wanaosema kwamba wanaona huruma kwa mateso ya watu wengine na uhitaji wa uinjilisti, lakini hawazitunzi rasilimali zao ili kwamba waweze kuwajibika na mahitaji hayo. Kamwe hawana uwezo wa kusaidia watu wengine.

Fedha zinaweza kutumika kwa vitu vinavyotumika na kuisha, au zinaweza kutumika kwa vitu vyenye thamani ya kudumu katika ulimwengu huu na ule wa milele. Ni jambo la muhimu kwetu kutumia fedha kwa ajili ya mahitaji yetu; lakini kwa namna yeyote itakavyowezekana, tunahitajika kuwekeza kwa ajili ya baadaye.

Watu wengi hawafanyi uwekezaji kwa sababu wanafikiri hawana vinavyotosheleza. Lakini kama mtu atatunza na kuwekeza kidogo, viwango vidogo vya fedha kila mara, kwa hakika matokeo makubwa yangepatikana. Mkulima, haijalishi ni mtu maskini kiasi gani, anatambua kwamba ni lazima atunze kiasi cha kutosha cha fedha kwa ajili ya kuotesha tena msimu unaofuata. Tunapaswa tutafute njia ambazo tutatunza na kuwekeza rasilimali zetu.

► Je, ni njia zipi zilizopo za kuweza kutunza na kuwekeza viwango vidogo vya fedha?

Kanuni ya Imani.

Mtume Paulo alitoa ahadi kubwa sana kwa kanisa la Filipi. Walikuwa wamejitolea dhabihu kwa ajili ya kusaidia huduma. Aliwaahidi kwamba Mungu angewajaza kila kitu walichokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake (Wafilipi 4:19).

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba hawapaswi kuishi wakisumbukia maisha yao, bali wamwamini Mungu kutoa kwa ajili yao (Mathayo 6:25-34). Ufalme wa mbinguni ungekuwa ndiyo kipaumbele chao, hata kabla ya mahitaji yao ya msingi.

Imani haimaanishi kwamba hatuchukui majukumu ya kujitafutia au kujihudumia kwa ajili yetu wenyewe na watu wanaotutegemea. Tunapaswa kufanya kazi ili kuwa na uwezo wa kuhudumia mahitaji yetu (Waefeso 4:28). Kama mtu haitunzi familia yake, huyo mtu siyo mfano mzuri wa mtu aliyeokoka (1 Timotheo 5:8).

Mtu hapaswi kukaa kiuvivu bila kufanya kazi akitegemea Mungu amhudumie. Mungu amepanga kwamba tupate faida kutokana na kazi tunazofanya na tuzalishe kitu cha thamani.

Imani inamaanisha kwamba tunajitambua hatuwezi kuishi bila ya uwepo wa baraka za Mungu. Nguvu zetu na fursa ya kufanya kazi hutoka kwa Mungu, na pia hutubariki kwa vitu ambavyo havitokani na kazi zetu, Kwa kuwa tunamtegemea Mungu, tunapaswa tuombe kama Yesu alivyotuelekeza. “Utupe mkate wetu wa kila siku.”

Tunapaswa tuwe wakarimu kwa watu wengine kwa sababu:

  • Tunajua kwamba Mungu huturuzuku.

  • Kazi yetu haizalishi vyote tulivyo navyo.

  • Hatustahili baraka za Mungu.

  • Tunaonyesha upendo wa Mungu kwa kutoa.

Hatuwezi tukawa kama mtoto mwenye ubinafsi anayechukua kipande kikubwa zaidi cha keki au kuficha peremende yake kwa sababu anajua kwamba hataweza kupata nyingine tena. Mungu anavyo vitu vingi, na hahitaji sisi tuwe wachoyo au watu wa siri, kana kwamba kamwe hatatupa tena zaidi.

Kiongozi wa huduma hasimamii tu fedha zake mwenyewe, bali na rasilimali za huduma. Mungu atatoa kwa huduma ambayo inafuata mapenzi yake. Hata hivyo, mapenzi yake siyo yale ambayo sisi wakati wote tunayaona ni dhahiri kwetu. Wakati mwingine watu wameweka fokasi yao kwenye kuimarisha taasisi, na wakipuuzia kupata mwelekeo ulio wazi kutoka kwa Mungu. Wakati mwingine watu wanajitahidi kufanya jambo jema, lakini hawafanyi katika njia ambayo Mungu anataka. Siyo wakati wote tunaweza kuwa na utambuzi kamili kwenye mambo haya, lakini ukosefu wa fedha kwa ajili a huduma unapaswa utuhamasishe sisi katika kuelewa vizuri na kwa mapana mapenzi ya Mungu

Kanuni ya Uaminifu

Kanuni ya imani inaelekeza kwenye kanuni ya uaminifu. Kamwe hatupaswi tufanye jambo ambalo litamchukiza Mungu, kwa sababu tunataka tumfurahishe yeye, na tunataka tubarikiwe na yeye.

Kama unamtegemea Mungu na kumwamini, utakataa fursa zinazojitokeza za kujinufaisha kwa kufanya mambo yasiyokuwa na uaminifu. Wakati fursa inapojitokeza, unapaswa utafakari swali hili, “Je, Mungu atatoa kwa njia hii?” Kama fursa iliyojitokeza ni ya kujinufaisha kwa njia isiyokuwa ya uaminifu, tunatambua kwamba hiyo siyo njia ambayo ya Mungu anaweza akaitoa. Mtu anayefanya jambo la uovu kwa ajili ya kujipatia faida hamwamini Mungu kwa ajili ya mahitaji yake.

Mtu aliyeko kwenye huduma kwa kawaida husimamia rasilimali ambazo siyo zake. Ni jambo la muhimu kwake kutofautisha kati ya fedha za huduma na fedha zake mwenyewe. Katika tamaduni kadhaa, watu hawaielewi kwa urahisi sheria hii. Hata hivyo, aidha iwe kwenye huduma, serikali, au biashara, mtu hapewi nafasi ya mamlaka hadi watu watakapomfikiria kwamba ana uwezo wa kuitambua tofauti hii. Kama mtu akitumia fedha ya shirika kama ni zake, anakiuka uaminifu (1 Wakorintho 4:2).

Kiongozi wa huduma anapaswa aanzishe sera ambazo zitaweka umakini wa uwajibikaji wa fedha za shirika. Hapaswi kukusanya na kuzitawala fedha yeye mwenyewe. Watu kadhaa mchanganyiko wanapaswa washirikishwe katika kuweka kumbukumbu za mapato na kupanga matumizi.

Kanuni ya Kusaidia Shirika

Mungu alipanga kwamba huduma zinapaswa zifadhiliwe au zisaidiwe kifedha. Hata hivyo, kiongozi wa huduma mara kwa mara anaweza akawa kwenye mazingira ambayo huduma yake haina ufadhili kamili wa kifedha.

Kwa kiongozi wa Kikristo, fedha haipaswi iwe ndiyo sababu iliyomfanya akubaliane na nafasi ya uongozi au sababu ya yeye kutumika kwa jitihada nzuri sana. Motisha kwa ajili ya huduma ni wajibu wa kumtii Mungu, matamanio ya kumpendezesha Mungu, na upendo kwa watu wanaohudumiwa (1 Petro 5:2, 1 Wakorintho 9:16, Yohana 21:15-17).

[1]Wakati Yesu alipowatuma wanafunzi wake alisema, “Mmepata bure, toeni bure” (Mathayo 10:8). Ni makosa kutoza gharama kwa huduma ya kiroho. Mojawapo ya karipio kali kabisa katika Biblia lilitolewa kwa mtu aliyekuwa anataka kutoa fedha kwa ajili ya kupata nguvu za kiroho ili aweze kuzitumia katika kupata faida (Matendo 8:18-23).

Huduma hazizalishi fedha kama ilivyo kwa aina nyingine za kazi, kwa sababu haizalishi kitu au haitoi huduma ya kuuza kwa ajili ya kupata fedha. Huduma inapatiwa msaada pale tu watu wengine walioko kwenye nafasi za mamlaka wanapoamua kwamba wanapaswa wapewe msaada.

Kiongozi wa huduma anaweza kuwatia moyo watu wa kufadhili kwa kuwasilisha thamani ya huduma, na uwajibikaji wake kwa ajili ya huduma husika. Kwa kawaida hawezi akawa anangojea msaada kabla ya kuanza kwa huduma. Taarifa za huduma yake zinapaswa zitolewe mara kwa mara, ziwe zenye ukweli, na zenye uaminifu kabisa.

Watu wengi huwa wafuasi au waungaji mkono wa huduma kwa sababu wanaona thamani ya huduma hiyo, si kwa sababu mhudumu anahitaji msaada. Kiongozi wa huduma hapaswi kujaribu kutafuta msaada kwa kuzungumzia mahitaji yake, bali kwa kuonyesha matokeo ya huduma na kueleza maono ya huduma yake. Pia ni muhimu kujenga mahusiano na watu anaowahudumia ili waone kujitolea kwake na kuthamini huduma anayowapa.

Baadhi ya watu watapenda kumpa kiongozi msaada binafsi badala ya kutoa kwenye shirika. Kiongozi anapaswa awe makini sana asiwe mtu wa kujijengea kupata msaada wake mwenyewe badala ya kulijenga shirika. Wajibu wake mkubwa uwe ni kulijenga shirika.

Kiongozi anapaswa aepukane na madeni. Kukopa fedha ni kutumia fedha kutoka kwenye wakati ujao. Deni huondoa na kuuweka mbali uhuru wa kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kwa wakati ujao. Kuwa na deni kunamaanisha kwamba unafanya maamuzi kuhusu mambo ya baadaye kabla hujafika pale. Deni ni kutumia rasilimali za baadaye wakati mahitaji ya baadaye hadi sasa bado hayajajulikana.

Kiongozi anapaswa aepukane na madeni binafsi, kwa sababu yatamwekea ukomo wa maamuzi ya huduma yake kwa siku za baadaye. Kiongozi anapaswa aepuke kuliongoza shirika kuingia kwenye madeni. Tumia tu fedha ambazo Mungu ameruhusu uzipate. Usikope, ukifikiria kwamba Mungu atatoa njia ya kulilipa hilo deni. Ikiwa Mungu atapenda kutoa kwa ajili ya hitaji maalumu, anaweza akafanya hivyo kabla hujakopa, badala ya kufanya baadaye. Kukopa kunaondoa mojawapo ya njia za kutambua au kufahamu mapenzi ya Mungu, kwa sababu inamaanisha kwamba huwezi ukangojea kuona ni nini Mungu alichokusudia kutoa.

Ruhusu baadhi ya wanafunzi washirikishane kuhusu ni kwa jinsi gani wanategemea kubadilisha makusudi au matendo yao kutokana na somo hili la kanuni kuhusu fedha.


[1]

“Kazi ya Mungu iliyofanyika sawasawa na mpango wa Mungu, kamwe haitakaa ikose kuruzukiwa na Mungu.”

- J. Hudson Taylor