Ujenzi wa hekalu umeanza. Ni msingi tu ambao umeshajengwa, lakini hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa. Umati wa watu ulikusanyika kusherehekea. Watu wengi walikuwa wakipiga kelele kwa shangwe na kumtukuza Mungu. Lakini wakati wazee walipouona ule msingi, walitambua kwamba hekalu jipya halitakuwa zuri kabisa kuliko lile la mwanzo. Walilia kwa masikitiko kwamba lile hekalu kubwa walilokuwa wanalikumbuka lilikuwa limeondoka kabisa. Masikitiko na shangwe vilikuwa vimechangamana kutoa katika zile sauti za umati wa watu. Ilikuwa ni wakati wa mabadiliko makubwa, na watu walikuwa na hisia tofauti kuhusu vipengele tofauti kwa ajili ya mabadiliko (Ezra 3:10-13).
Dunia inabadilika kwa haraka. Teknolojia ya kisasa inakua kwa haraka. Bidhaa mpya zinatengenezwa. Watu wengi wanabadilishwa imani zao kuhusu maisha, dunia, na dini.
Mabadiliko yanaleta athari kwa mashirika. Mashirika ni lazima yabadilike ili kukidhi mahitaji kwa ajili ya mazingira yanayobadilika. Hayapaswi kubadili maadili yao au makusudi yao; lakini ni lazima wabadilishe malengo, mikakati na hatua zao.
Kiongozi lazima aongoze mabadiliko katika shirika lake. Ikiwa hajajiandaa kwa mabadiliko, atakuwa anajibu tu mabadiliko yanayotokea kutoka nje. Kiongozi hapaswi kutamani tu dunia ibadilike kwa namna itakayosaidia shirika lake. Hapasi kukubali kushuka kwa shirika kwa sababu ya mabadiliko yasiyodhibitiwa na yeye. Badala ya kulalamika kuhusu dunia inavyoendelea kubadilika, kiongozi anapaswa kubadilisha shirika ili kukidhi mahitaji ya dunia inayobadilika.
“Huwa inasemwa kwamba kuona mbele kwa ajili ya wakati ujao ni jukumu la kiongozi ambalo haliwezi kukabidhiwa au kukasimiwa kwa mtu mwingine. Linaweza likashirikishwa kwa watu wengine. Lakini ni jukumu la kiongozi kutengeneneza wakati leo ili kuhakikisha kwamba kuna kesho.”[1] Kiongozi anapaswa ahakikishe kwamba kuna mustakabali wa baadaye kwa ajili ya shirika kwa kuliandaa kukutana na siku zijazo. Kama kiongozi hataweza kufanya hivyo, hakuna mtu mwingine atakayeweza kufanya. Kama kiongozi anakuwa ni msimamizi au meneja tu wa hali za sasa, kazi halisi ya kiongozi haitafanyika.
► Je, kwa nini ni muhimu kwa kiongozi kuwa na wasiwasi kuhusu siku zijazo?
[2]Mabadiliko yanahitajika siyo tu kwa sababu ya mabadiliko ya nje, lakini kwa sababu ya maendeleo ya shirika. Ni dhahiri kwamba shirika linaloshindwa linapaswa libadilike, lakini hata kwa shirika lile linalofaulu vizuri, ni lazima liweze kubadilika ili kuweza kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu. Siyo kila badiliko ni kuendeleza, lakini pasipokuwepo na mabadiliko hakuna muendelezo au mafanikio.
Baadhi ya watu hujaribu kukwepa matatizo kwa kuepuka mabadiliko. Kwa watu hawa, kila wazo ni tatizo kwa sababu ni wazo kwa ajili ya mabadiliko. Kiongozi mzuri huyaona matatizo kwenye njia ya maendeleo.
► Je, ni kwa jinsi gani inawezekana kuliona tatizo kama nafasi iliyojitokeza?
Mtume alimwambia mfalme Hezekia kwamba hukumu itakuja, lakini siyo katika kipindi chake. Hezekia alijisikia kuhusika kidogo wakati aliposikia kwamba matokeo ya matendo yake yataleta athari kwa kizazi chote kijacho badala ya kutokea mara moja (2 Wafalme 20:16-19).
Kiongozi mwaminifu hufikiri jinsi matendo yake yatakavyoweza kuleta athari kwa watu wake kwa kipindi cha baadaye. Baadhi ya matokeo ya maamuzi yanaweza yasijitokeze kwa miaka mingi, lakini kiongozi anapaswa kukumbuka kwamba anaitengeneza hatima ya baadaye kwa maamuzi yake.
Mabadiliko mazuri
Je, mabadiliko ni mazuri? Siyo siku zote. Kupungua kwa thamani au manufaa, uharibifu, na kuoza yote ni mabadiliko, lakini siyo mabadiliko yaliyo mazuri.
Usipende kufanya mabadiliko kwa ajili tu ya kuwa na mabadiliko. Mabadiliko ni lazima yafanyike kwa uangalifu mkubwa katika kufikia malengo.
Wakati kiongozi anapoanza kufanya mabadiliko, watu wengi kwenye shirika huwa wanajijua kwamba wanahitaji baadhi ya mabadiliko. Kwa kufanya mabadiliko yanayohitajika, kiongozi huongeza fursa ya kujiamini. Anapokuwa anafanya mabadiliko magumu hatua kwa hatua, kujiamini kwao kutaongezeka endapo mabadiliko hayo yataleta matokea mazuri.
Mabadiliko makubwa sana hutokea wakati shirika linapokuwa limebainisha maadili yake na kusudi, kisha kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye malengo na mikakati yake. Huu ni mchakato. Ikiwa mabadiliko yatafanyika kwa haraka sana, watu wengi hawataweza kushiriki kwenye mabadiliko hayo. Hayawezi yakafanywa na kiongozi peke yake kwa sababu maadili na kusudi ni lazima vishirikishwe kwa watu wengi walioko kwenye shirika.
Mashirika mengi huwa yanahitaji mabadiliko kwenye bajeti zao, ili kwamba fedha zao ziweze kutumika kwenye kitu ambacho ni cha umuhimu na kitakacholeta matokea bora zaidi. Mara nyingi matumizi hayaendani na vipaumbele vya shirika, Mabadiliko makubwa sana ya bajeti yatatokea endapo shirika nalo litabadilika kwa sababu bajeti huenda mahali ambapo vipaumbele vinajitokeza.
► Je, ni kwa nini matumizi huonyesha vipaumbele halisi?
[1]Ken Blanchard and Mark Miller, The Secret: What Great Leaders Know and Do (San Francisco: Berrett-Koehler Publishers, 2014), 51
[1]Ni kazi ya kiongozi kuelezea kwa ufasaha na usahihi ukweli unaohusiana na yeye mwenyewe na timu yake. Inapotokea kuwepo na tatizo la kutatua, hali inakuwa ni mbaya zaidi kuliko tunavyoweza kufikiria, mchakato wa kufanya marekebisho unachukua muda mrefu kuliko tunavyopanga, na gharama ni kubwa kuliko tunavyotegemea. Kiongozi anajaribu kulifanya tatizo kuwa dogo ili kuwafanya wafuasi wake waweze kujiamini, lakini hatimaye hilo linaweza kuleta madhara katika uaminifu wake.
Kiongozi anaweza akawakasirikia wale watu ambao wana mwitikio hasi wa mawazo yake, lakini anapaswa asikilize kwa umakini mkubwa mashaka yao na maonyo wanayotoa. Ni lazima achukue yale mambo ya ukweli kwa kumaanisha kabisa. Kama atafikiria kwamba wazo lake ni zuri sana kiasi kwamba litafanya kazi ingawaje atakuwa hajaweza kufikiria kuhusu mazingira yote yaliyopo, atakuwa anajikatisha tamaa yeye mwenyewe na watu wanaomwamini yeye. “Hauwezi kabisa kufanya mfululizo wa maamuzi mengi kabla kwanza hujakabiliana na kweli katili zilizopo.”[2]
Wakati wa kutengeneza mkakati, tafakari. “Ni kwa jinsi gani tuko nje ya muda katika kufikiri, utaratibu, mafunzo, na ustadi.
Katika kukuza maono, jiulize swali hili, “Endapo ungekuwa umepata msaada wa aina zote na fedha ulizokuwa unazihitaji, utapenda kukamilisha nini? Kama utajikuta huna jibu, basi hauna maono.
► Jadiliana kuhusu aya iliyotangulia. Kwa nini swali hilo linaonyesha kama mtu alikuwa na maono? Kwa nini ni muhimu kuwa na jibu la swali hili?
“Ujasiri ni kile kinachowezesha kusimama na kuongea; ujasiri pia ni kile kinachowezesha kukaa chini na kusikiliza.”
- Winston Churchill
[2]Jim Collins, Good to Great: Why Some Companies Make the Leap... and Others Don’t (New York: Harper Business, 2001), 70
Kipingamizi cha Mabadiliko
Je, ni aina gani ya mambo ambayo watu huzungumzia wakati wanapokuwa wanapinga mabadiliko?
Watu wanaopinga mabadiliko ya huduma wanaweza wakawa wanasema mambo kama haya:
“Huu ni utaratibu ambao Mungu alishaubariki tangu wakati wa zamani; hatupaswi tufanye jambo lingine lolote tena.”
“Viongozi wa kiroho wa wakati wa zamani walitufundisha sisi kufanya hivi; huwezi ukasema walikuwa wanafanya kwa makosa.”
“Hatuhitaji taratibu nyingine nzuri zaidi; badala yake tunahitajika tuombe zaidi.”
“Mungu hahitaji kwamba sisi tufanikiwe; bali anatuhitaji tuwe waaminifu, kwa hiyo tunapaswa tuendeleze kile tunachokifanya.”
Watu ambao hawajajitolea kabisa katika kuwezesha maendeleo wanaweza kuwa na mambo kama haya ya kusema:
“Njia tuliyokuwa tunatumia inafanya kazi vizuri sana; kwa nini kuwepo na mabadiliko?”
“Sina muda wa kufanya kazi nyingine yeyote ya ziada.
Kuna sababu mbalimbali tofauti za kuzuia mabadiliko, na hatupaswi kudhania kwamba kila mtu atakuwa na sababu zinazofanana.
Watu hukataa mabadiliko wakati wanapokuwa:
Hawaelewi kusudi.
Hawakubaliani na utaratibu.
Wanapokuwa wanathamini sana kitu ambacho kinakusudiwa kutupwa au kuachwa.
Wanahofia kwamba matatizo mengine yanaweza yakajitokeza
Wako katika kipindi cha kufurahia.
Wanataka kubakia kwenye uwigo wa utendaji bora.
Wanazuia kuwajibika kwa ziada au kwa kujitoa dhabihu.
Wenye mihemuko au mafungamano ya kidini ya mapokeo ya kizamani.
Kuwaandaa watu kwa ajili ya Mabadiliko
Kiongozi mzuri huwapeleka watu wake kupita kwenye mabadiliko yenye matokeo bora zaidi na uharibifu mdogo sana kwa kadiri inavyowezekana. Ni kama vile unayetaka kukipeleka kikundi kwenda kwenye safari, fanya kwanza utafiti ili kwamba uweze kuwaelezea ni kitu gani wategemee katika safari hiyo. Unatakiwa uwe umejipanga.
Timu ya msingi ya shirika inahitajika iongozwe katika kupitia hatua za kugundua maadili na kusudi la shirika. Mahitimisho yote yanapaswa yawekwe kimaandishi.
Ushirikishwaji wa umiliki kwa ajili ya kusudi ni jambo muhimu; vinginevyo, itaonekana ni kama tu mtu binafsi anayehitaji msaada kwenye malengo yake. Malengo yaliyoshirikishwa yanaunganisha timu.
Kumbuka kudumisha muunganiko kwenye historia ya shirika. Usijifanye kana kwamba chochote kilichofanyika hapo nyuma kilikuwa hakina thamani. Onyesha ni kwa jinsi gani maendeleo ya baadaye yanavyoweza kujijenga juu ya kile ambacho kilishakamilishwa.
► Je, kwa nini ni jambo muhimu kubakia ukiwa umeunganishwa kwenye historia ya shirika?
Kiongozi kijana ni lazima aonyeshe kwamba anathamini mafanikio ya wakati uliopita, Ni lazima athamini ushirika ambao shirika limeshirikisha. Hapaswi kuthamini tu maendeleo na ufanisi.
Anzisha njia ya kuweka “alama.” Kama ilivyo kwa mchezo wa burudani (mfano mpira au riadha), timu inahitaji kujua jinsi gani ya kupata “alama” na jinsi gani ni “kucheza faulo.” Ubao wa kurekodia alama ni muhimu kwa ajili ya kufanya tathmini, kufanya maamuzi, kufanya marekebisho, kutengeneza ushindi.
[1]Kumbuka kwamba uaminifu binafsi wa kiongozi ni muhimu ni jambo la msingi kwa ajili ya watu kukubaliana na maono. Watu huwa hawashawishiki na mpango hadi pale wanapokuwa wamemwamini kiongozi. Dumisha uaminifu wao kwa kutenda kwa uadilifu. Kamwe usitake kuwadanganya, na kamwe usiwazuie kupata taarifa au habari ambazo zingeweza kuwa kishawishi cha maamuzi yao.
Kiongozi anahitaji aina mbili za uaminifu kutoka kwa watu wake. Anahitaji waamini tabia yake. Anahitaji pia waamini uwezo wake wa kitaaluma. Wanalazimika kuamini kuwa siyo tu kwamba ana tabia nzuri, lakini pia ana uwezo kuongoza vyema. Kuna watu wazuri sana lakini hawawezi kuongoza, na kuna watu wenye sifa kubwa za ujuzi na uwezo ambao tabia zao haziwezi zikaaminika.
Watu wanahitaji kujua kwamba kiongozi wao anajali kuhusu mambo ambayo wao wanajali. Wakitokea kufikiri kwamba kiongozi siyo mtu wa kujali, watajitahidi kuchukua hatua za kujilinda wenyewe kwa njia ya kuzuia mabadiliko kwa kuficha maoni na matendo yao.
Mabadiliko mengi ya kudumu hayapaswi kufanywa kwenye wakati wa kukabiliana na dharura. Kwenye wakati a dharura, chukua muda wa kufanya tathmini ya hali halisi ilivyo. Kuna tishio gani la kweli lililopo? Fikiria kile ambacho kwa uhalisia kiko hatarini kudhurika na kisichokuwa hatarini. Fikiria ni mwitikio upi wa haraka unaweza kuzuia hatari bila kuandika sera za kudumu. Ni msaada gani unaoweza kupatikana? Liweke shirika kwenye hali ya utulivu.
Watu hukosa kujiamini wanapokabiliana na mabadiliko.
Wasaidie wajisikie kuwa wameandaliwa
Watu hujihisi wako peke yao hata kama kila mtu anapitia katikati ya mabadiliko sawa. Wanaweza wakaamua kulinda maslahi yao wenyewe na kufanya mipango ya siri.
Wasaidie wafanye kazi kwa pamoja, na kushirikishana mawazo ili wasijisikie kwamba wako peke yao.
Watu hufikiria kwanza kuhusu kile ambacho wanaweza wakakipoteza.
Waache wajadiliane kuhusu kile ambacho wanaweza wakakipoteza. Usijifanye kwamba hasara ya kupoteza ni kidogo au siyo halisi.
Watu huwa katika mashaka kwamba mabadiliko yanafanyika kwa haraka kuliko wanavyoweza kuyamili.
Watayarishe kwa mafunzo na msaada. Panga mabadiliko ili yasitokee kuwa ni ya ghafla sana.
Watu tofauti watakuwa kwenye viwango tofauti vya utayari wa mabadiliko.
Usiwe na haraka ya kuwahukumu watu ambao wanahitaji uhakikishe tofauti.
Watu huwa na tabia ya kurudi katika njia zao za awali ikiwa mabadiliko hayatekelezwi na kudumishwa kwa uthabiti
“Kama lengo kuu la nahodha wa meli lingekuwa ni kuiweka meli ikae bandarini, angeiweka bandarini milele.”
- Thomas Aquinas
[2]Jedwali hili la taarifa limefanyiwa marekebisho kutoka kwa Ken Blanchard and Phil Hodges, The Servant Leader (Nashville, TN: Thomas Nelson, 2003), 66-67.
Utekelezaji wa Mabadiliko
Wajibu wa kiongozi ni kufafanua na kuelezea baadhi ya maadili, na kisha kufanya kazi ili kuona vikifanyiwa kazi kwenye shirika lote. Kiongozi hawezi akafanya haya pasipokuwepo na kujihusisha yeye mwenyewe kwenye mfumo wote wa uongozi wa shirika.[1]
Kazi ya kiongozi siyo kusimamaia undani wa kinachofanyika kwenye shirika. Ikiwa atafanya hivyo: (1) Atazuia kukua kwa viongozi wengine ambao wanategemewa wamsaidie yeye. (2) Ataweka ukomo wa kazi za shirika hadi kwenye kiwango cha yeye mwenyewe kuwa ndiye peke yake wa kusimamia.
Hata hivyo, hawezi kubadilisha shirika bila ya: (1) Kujua kwamba ni kwa jinsi gani kila kitu kinafanya kazi. (2) Kuelezea jinsi ya kuyatumia maadili kwenye kila sehemu ya kushughulika au utendaji.
Hii inamaanisha kwamba ni lazima awe na ufahamu wa kila kazi inayofanywa na kila idara, asaidie katika kufanya mabadiliko maalumu yanayohitajika, na kufundisha na kuwapandisha vyeo viongozi wote watakaosimamia vizuri maadili ya shirika kwenye idara zao za kazi.
…Kiongozi hufanya usimamizi ili kwamba yale yanayoaminika kwenye shirika yasiyokuwa na shaka yaweze kuheshimiwa, yadumishwe, yawasilishwe, na yawekwe kwenye utendaji wa pamoja.[2]
Haitoshi kwa kiongozi wa juu kabisa aendelee kuwa akifundisha tu maadili. Hata iwe ni kuwaelezea kwa matendo yake mwenyewe haitoshi. Ni lazima ahakikishe kwamba yanatekelezwa yote kwenye shirika lote. Ni lazima awatafute watu walioko kwenye shirika ambao kwa uhalisia wanaamini katika maadili hayo na wanao uwezo wa kumsaidia kuyatekeleza.
Matumizi ya shirika yanaonyesha vipaumbele vyake. Kusudi linalodaiwa lipo haliwi kusudi kamili hadi pale ambapo bajeti inaendana na kusudi hilo. Hiyo ina maana kwamba mabadiliko makubwa ya shirika siku zote yanamaanisha kuwa ni mabadiliko ya bajeti. “Viongozi wenye ufanisi mkubwa huweka uangalizi binafsi wa hali ya juu kwenye bajeti kwa sababu hapo ndipo makusudi halisi ya utendaji wa shirika yanajidhihirisha.”[3]
► Je, utawekaje kwenye muhtasari kuhusiana na kile ambacho kifungu hiki kinafundisha kuhusu wajibu wa kiongozi?
[1]Albert Mohler, The Conviction to Lead: 25 Principles for Leadership that Matters (Bloomington: Bethany House Publishers, 2012), 118
Shirika litakuwa malengo madogo ya muda mfupi; lakini b aada baada ya kusudi na maono kuwekwa wazi, kiongozi atapaswa kuweka lengo kubwa ambalo lina mvuto na uhamasishaji kwenye shirika.
Lengo kubwa linapaswa liwekwe baada ya shirika kuwa limepitia kwenye mchakato wote wa kutafuta maadili na makusudi yaliyoelezwa katika somo la 11, “Huduma yenye Lengo.”
Lengo kubwa linaweza kuwa ni jambo ambalo litachukua miaka kadhaa kulifikia. Litapaswa liwe kubwa sana na lenye changamoto kwamba litahitaji timu ya utendaji ya ngazi ya juu, nguvu, na mkakati.
Lengo kubwa litapaswa liwe rahisi kwa ajili ya kila mtu kulielewa. Itabidi liandikwe na lipewe msisitizo. Siyo tu jambo linalohusiana na ndoto, bali ni mategemeo halisi.
Lengo kubwa linatakiwa liunganishe shirika. Halipaswi liingizwe kwa ghafla na viongozi. Linatakiwe lifanyike baada ya majadiliano mengi ili kwamba watu watakaowajibika waone ni lengo lililo muafaka.
Wakati lengo litakapofikiwa, haliendelei tena kutumikia kusudi lake. Lengo jipya ni lazima liwekwe. Viongozi wanapaswa kujiandaa kuongoza kwenye uwekaji wa lengo jipya.
Kutumia Kasi
Kasi ni nguvu inayosonga mbele kutokana na nguvu ya awali au iliyopita. Tunapokuwa tunazungumzia kuhusu kasi kwa ajili ya shirika, inamaanisha kwamba watu wako tayari kuendelea kubadilika na kusonga mbele kwa ajili ya mafanikio yanayoonekana ya hivi karibuni
Kama kiongozi, zingatia ni kasi gani shirika inayo kutokana na mafanikio yaliyopatikana kabla wewe hujaja hapo. Je, ni kwa jinsi unaweza kuutumia kasi hio na kuuongeza?
Fikiria jinsi ya kuyageuza mafanikio ya wakati huu yawe kwenye kasi. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuyatumia mafanikio ya sasa kuwatia moyo watu kuingia kwenye juhudi nyingine?
Kamwe usidhanie kwamba kasi itajidumisha yenyewe: uongoze na uupe mafanikio mapya. Kwa makusudi kabisa panga na ratibu nyakati za kuongoza, kutia moyo, na kuutumia kasi. Sherehekea na tangaza mafanikio, ukiwa mkarimu kwa kutoa sifa.
Ni mambo gani ya kutia motisha yaliyoko kwa watu wako? Je, ni nini kinachowapa hisia ya kuwa na kasi?
Ruhusu baadhi ya wanafunzi washirikishane kuhusu ni kwa jinsi gani wanategemea kubadilisha makusudi au matendo yao kutokana na somo hili.
Muhtasari wa Taarifa Tano.
1. Mashirika ni lazima yabadili malengo yao, mikakati, na matendo ili kukidhi mahitaji ya dunia inayobadilika.
2. Kiongozi ni lazima ahakikishe kwamba hatima ya shirika ipo kwa kuliandaa liendane na mahitaji ya baadaye.
3. Watu hawako tayari kushawishiwa na mpango hadi wawe wamemwamini kiongozi.
4. Kiongozi mzuri huwapeleka watu wake kupita kwenye mabadiliko yenye matokeo bora zaidi na uharibifu mdogo sana kwa kadiri inavyowezekana.
5. Lengo kubwa sahihi linahamasisha, linachochea, na linaunganisha shirika.
Kazi za kufanya Somo la 12
1. Andika aya inayotoa muhtasari wa dhana ya kubadilisha maisha kutoka katika somo hili. Elezea kwa nini ni muhimu. Je, ni jambo gani zuri linaloweza kufanywa? Je, ni madhara gani yanayoweza kujitokeza kwa kutojua?
2. Elezea ni kwa jinsi gani unavyoweza kutumia kanuni zilizoko katika somo hili kwenye maisha yako mwenyewe. Je, ni kwa jinsi gani somo hili linabadilisha makusudi yako? Je, ni kwa jinsi gani umejipanga kubadilisha matendo yako?
3. Fanya kukariri Taarifa Tano kwa Muhtasari zilizoko katika somo la 12. Kuwa tayari kuziandika bila ya kunakili kutoka katika kumbukumbu za ufahamu wako mwanzoni mwa kipindi kinachofuata cha darasa.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.