Makocha wa timu za michezo wanaelewa kwamba kipaji tu hakitoshi. Wachezaji wa timu ni lazima wahamasishwe katika kuweza kufanya vizuri. Ni sehemu muhimu sana ya kocha kuongea na timu na kuwatia moyo ili waweze kutumia juhudi sana. Kundi la watazamaji huishangilia timu kwa sababu kutiwa moyo huisaidia timu katika kufanya vizuri. Endapo mchezaji wa timu alijifunza tu mambo ya ustadi wa mchezo na akawa anaifanya kazi yake kwa ajili ya kulipwa, jambo hilo halitatosha katika kupata ushindi.
Kanuni hii siyo kwamba inatumika tu kwa michezo, lakini kwa kila shirika. Ushindi wa shirika hutegemea msimamo wa watu wanaohusika. Msimamo wa kweli inamaanisha kwamba wanajitoa kwa uwezo wao na akili zao ili kuweza kulifanya shirika lifanikiwe.
Mtu aliyeunganishwa na kujitoa kwa shirika pia atajihusisha na shughuli za shirika hilo. Tunaita hii "ushiriki."
Hapa chini kuna hadithi fupi za jinsi mtu alivyoweza kufanya ziada ya alivyokuwa anategemewa kufanya kwenye shirika.
Ephraimu alifanya kazi kwenye biashara ya kuuza mbao kutoka kwenye yadi kubwa. Kazi yake ilikuwa ni kusaidia wateja kupakia mizigo katika magari yao. Aligundua kwamba kulikuwa na rundo la mbao kwenye yadi lililokuwa limeanguka. Baada ya kumaliza kumsaidia mteja wake, alikwenda kwenye lile rundo la mbao lililokuwa limeanguka na kulipanga tena mahali pake kwa upya, ingawaje tajiri yake hakuwa amemwambia au kumwagiza afanye hivyo. Kwa nini Ephraimu alifanya hivyo?
Mikaeli alikuwa anacheza mpira wa vikapu kwenye timu ya wachezaji wa kulipwa. Wakati wa mchezo alianza kwa kutaka kuurusha mpira wa kufunga lakini akawa hayuko kwenye nafasi nzuri. Kwa haraka akaurusha mpira kwa mchezaji mwingine ambaye alikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuweza kufunga. Kwa nini Mikaeli hakutaka kujaribu kufunga yeye mwenyewe?
Petro alifanya kazi kwenye kituo cha mafuta kwa ajili ya kuwajazia mafuta wateja. Ilipoonekana kwamba pana watu wengi, Petro kwa kweli alikimbia kwa haraka kwenda kwa mteja anayefuata ili kuokoa muda. Je, kwa nini Petro akimbie?
Siku ya Jumapili, Barnaba aligundua kwamba paa la kanisa lilikuwa limeharibiwa na mti uliokuwa umeanguka. Siku ya Jumatatu Barnaba alikwenda kununua vifaa vya kurekebisha akaja navyo pamoja na vifaa vyake vya ufundi na kurekebisha lile paa. Barnaba hakuwa mwenye kanisa na wala hakulipwa kuifanya kazi hii. Je, kwa nini Barnaba arekebishe paa?
Dorkasi alikuwa anafanya kazi kwenye duka la bidhaa na mboga kama Keshia. Siku moja mchana alipokuwa anaenda kwenye mapumziko, aliona kwamba kulikuwa na mafuta ya kupikia yaliyokuwa yamemwagikia chini na kusambaa mahali pale. Badala ya kuondoka aende kwenye mapumziko yake, alianza kufanya usafi kwenye ile sehemu ambayo mafuta yalikuwa yamemwagikia na kusambaa. Je, kwa nini Dorkasi aliacha kwenda mapumziko na akafanya usafi wa mafuta yaliyokuwa yamemwagika chini?
Nuhu alikuwa shemasi wa kanisa na mwalimu wa shule ya Jumapili. Siku moja Jumapili asubuhi aliwasili kanisani mapema sana na akakuta choo hakijafanyiwa usafi. Alikifanyia usafi kile choo kabla ya kusanyiko la kanisa halijaanza kuwasili. Je, ni kwa nini Nuhu alikifanyia choo usafi?
Kama mwenye biashara atajali tu kuhusu mafanikio yake, biashara hiyo haitaenda vizuri. Kama mchungaji wa kanisa anataka tu kanisa lake lifanikiwe, kanisa litakwama. Kama kocha atataka tu apate ushindi kutoka kwa timu yake, timu itashindwa.
Kuielewa Ushiriki
Ili mtu aweze kuwa mshiriki inamaanisha kwamba atafanya vizuri kwa kadri inavyowezekana, na siyo tu kile kinachohitajika kifanyike. Atatumia uwezo wake wote na mawazo yake kwa ajili ya shirika. Hafungwi na ukomo wa kiwango cha muda uliopangwa na jukumu maalumu la kufanya. Siyo mikono yake tu, lakini pia kichwa chake na moyo wake vinahusika.
► Je, unafikiri kifungu kifuatacho kilichonukuliwa kinamaanisha nini?
Wakati Moyo, Akili, Mikono, na Mazoea vinaambatana, viwango vya juu vya uaminifu, imani, na tija vitapatikana.[1]
Wakati mwingine viongozi hudhania kwamba watu watafanya kazi vizuri wakati wakiwa chini ya mamlaka au kwa sababu wanalipwa mishahara. Ukweli ni kwamba watu watafanya kazi vizuri sana pale watakapojisikia kuwa na msimamo thabiti wa binafsi na shirika.
Shirika ambalo hutegemea watu wa kujitolea wanaweza kufanya kidogo sana bila ya watu ambao wana miadi ya kuwa wahusika. Watu hawawezi kutoa muda wao na rasilimali pasipo kushirikishana malengo ya shirika.
Watu wa shirika hawako katika kiwango kimoja cha ushiriki. Wanaweza kuwa katika viwango tofauti tofauti.
Kiongozi anawathamini watu walio na ushiriki wa juu na anawategemea. Kiongozi huenda asielewe kwa nini watu wengine hawajihusishi, lakini kazi yake ni kuinua kiwango chao cha ushiriki.
Kiongozi anatakiwa atumie muda wake wa kutosha katika kuinua kiwango cha miadi ya kushiriki ya watu wake. Hiyo ni mojawapo ya kazi muhimu sana ya kazi za kiongozi, na hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuifanya kazi hiyo vizuri kama atakavyoweza kuifanya yeye mwenyewe. Kiongozi aidha atakuwa anaongeza kiwango cha miadi ya ushiriki ya watu au anaweza akawa kizuizi chake.
Makanisa yana watu wenye pesa ambazo hawazitoi. Mashirika yana watu wenye muda, lakini hawapatikani. Biashara zina wafanyakazi wenye mawazo ambayo hawashirikishi.
Wakati mwingine wachungaji wanatafuta mtu kutoka nje ya kanisa kusaidia au kusaidia kifedha. Hata hivyo, wana watu ndani ya kanisa ambao wanaweza kusaidia na hawafanyi hivyo, na watu ndani ya kanisa ambao wanaweza kutoa na hawatoi. Shida ni kwamba watu hawawezi kushiriki. Watu wa kanisa hawahisi kwamba kanisa ni lao. Watu hawataweza kujihusisha na maono na kazi ya kanisa isipokuwa wakiwa na uhusiano na shirika na kiongozi.
Fikiria mfano wa familia. Wanafamilia husaidiana wenyewe kwa wenyewe katika njia mbalimbali bila ya kutegemea kupewa zawadi zozote maalumu kwa mambo wanayoyafanya. Je, kwa nini wafanye hivyo? Wanafanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya familia; wameunganishwa.
Kama watu wa shirika hawatoi na kufanya kile kinachohitajika kufanyika, hawajisikii kwamba wameunganishwa. Mtu anapokuwa ameunganishwa, malengo ya shirika ni malengo yake, mahitaji ya shirika ni mahitaji yake, na mafanikio ya shirika ni mafanikio yake.
Wakati mwingine viongozi hawatambui upungufu wa ushiriki. Wanafikiri kwamba watu wao wanahitaji mafunzo, lakini mafunzo siyo suluhisho kwa mtu ambaye hafanyi kile ambacho angeweza akakifanya. Tatizo ni kwamba hajaunganishwa.
Wakati mwingine viongozi hawatambui ukosefu wa ushiriki. Wanadhani kwamba watu wao wanahitaji mafunzo, lakini mafunzo si suluhisho kwa mtu ambaye hafanyi kile anachoweza. Shida ni kwamba hajashikamana.
[1]Ken Blanchard and Phil Hodges, The Servant Leader: Transforming Your Heart, Head, Hands, and Habits (Nashville: Thomas Nelson, 2003), 15
Ishara za Ukosefu wa Wameunganishwa kwenye Shirika.
Viongozi wanapata ugumu wa kuwapata washiriki wa kuchukua majukumu
Wanachama wanajisikika kutohusika katika maamuzi mbalimbali.
Wanachama huondoka kwa haraka wanapoona kwamba kuna matatizo.
Wanachama wanakosoa shirika lao wenyewe mbele ya watu wa nje.
Wanachama hawajali kuhusu mafanikio ya shirika.
Wanachama wanalitofautisha shirika na wao wenyewe.
Mwanachama anayejisikia kwamba hajaunganishwa hulizungumzia shirika kana kwamba ni kitu tofauti kilichotenganishwa na wanachama wake. Huzungumzia mambo ambayo shirika linapaswa kufanya. Hutumia neno wao badala ya neno sisi.
[1]Viongozi walioko kwenye shirika ambalo haliko kwenye uungwanishwaji mzuri linatoa mwanya wa nafasi ya kujitenga kati yao wenyewe na wanachama wa shirika.
Viongozi katika shirika ambalo halijashikamana vyema huweka umbali kati yao na watu wa shirika hilo. Viongozi wanakuwa ni tatizo watu kuweza kuwaona au kuwafikia, hata kwa ajili ya mawasiliano tu. Viongozi huzifanya kazi zao zionekane kwamba ni za ajabu ambazo watu hawawezi wakazielewa. Ni watu ambao hawataki kusikia mapendekezo ya watu wengine au malalamiko.
Wakati shirika liko katika hali kama hii, mapenzi ya kiongozi ndiyo hali pekee inayotambuliwa; ukweli mwingine wote hupuzwa huku watu wakijaribu kuendelea kwa kuficha makosa yao. Watu huogopa taarifa na ukweli wanapokosa kujihisi wameunganishwa na uongozi.
Makabila madogo na makundi ya urafiki wa karibu yanaweza kuibuka katika shirika lisilo na muunganiko. Makundi haya huundwa na watu wanaolindana dhidi ya mabadiliko na dhidi ya uongozi. Watu wanapohisi hatari ndani ya shirika, wanazingatia matatizo yao binafsi badala ya changamoto za shirika. Wanapokabiliana na ushindani wa kindani, hushindwa kuzingatia mafanikio chanya na ya kujitolea.
Wakati mwingine vikao vya shirika huonyesha kwamba wanachama hawajaunganishwa. Watu huacha kuhudhuria vikao:
Kama watakuwa wanafikiri kwamba vikao hivyo havina umuhimu katika utendaji wao.
Kama hawafikirii kwamba ushiriki wao utaleta utofauti.
Kama hawatashirikishana malengo ya viongozi wao na hawatataka kuwa watu wanaohusika.
Baadhi ya mashirika hupoteza nguvu kazi ya vijana wanaoinukia ambao wangeweza kuwa viongozi kwa sababu wanaona hawawezi kuwa sehemu ya utawala ambao tayari ulishawekwa. Viongozi hushikilia nafasi zao kwa kuwa na watu wenye ushawishi na hawatoi fursa mbalimbali kwa watu ambao hawajaunganishwa. Vijana wenye uwezo wanaweza wakaondoka wakaenda kujiunga na mashirika mengine ambayo yanatoa fursa kwao.
Makanisa mengine yanaweza yakaigiza mbinu na mipango yako, lakini kwa kawaida hawaondoki kwenye shirika ikiwa wanahisi kuna kushikamana.
Hii inamaanisha kwamba makali yako pekee ya ushindani ni uhusiano uliopo kati yako na watu wako…Kitu kimoja ambacho ushindani wako kamwe hauwezi kuiba kutoka kwako ni uhusiano wako ulio nao na watu wako…[2]
“Roho ya husuda inaweza ikaharibu; kamwe haiwezi ikajenga.”
- Margaret Thatcher
[2]Ken Blanchard, Thad Lacinak, and Chuck Tompkins, Whale Done: The Power of Positive Relationships (New York: Free Press, 2002), 58
Mifano kutoka katika Maandiko
Wakati kijana Rehoboamu alipokuwa mfalme, wazee walimshauri kuwahudumia watu. “Ukikubali kuwa mtumishi wa watu na kuwatumikia, watakuwa watumishi wako” (1 Wafalme 12:7). Walisema kwamba anapaswa kuunganika na watu kwa kuonyesha kwamba anajali kuhusu mahitaji yao. Kisha, watu wangeona kwamba ufalme huo uko kwa ajili yao, na wangekuwa waaminifu kwake. Wataweza kushirikishana malengo, matatizo, mahitaji, na kazi za ufalme.
Rehoboamu alifikiri kwamba nafasi yake ilikuwa ya kutosha. Alifikiri kuwa mamlaka yake ilimaanisha kwamba hakupaswi kuomba ushiriki. Alisema atatawala kwa ukali bila kujali watu.
Watu wengi walijitenga na Rehoboamu. Walisema, “Hatuna sehemu yeyote katika mfalme huyu; tutajitunza sisi wenyewe na wakaenda zao wakamwacha akae peke yake (1 Wafalme 12:16). Watu ambao hawajisikii kuunganishwa kwenye huduma za shirika hujali kushughulika na mahitaji yao peke yake na siyo mahitaji ya shirika. Hata kama watakuwa wamebakia bila kuondoka, watakuwa wanafanya kazi kwa malengo yao wenyewe.
Jibu la Rehoboamu lilikuwa ni kujaribu kutumia mamlaka. Yeye hakujaribu kuelewa mahitaji ya watu wake. Alimtuma mtoza ushuru, lakini hilo halikufanikiwa. Alipanga kutuma jeshi, lakini Mungu alimzuia. Kamwe, ufalme haukutokea tena kuwa na umoja.
Jeroboam alikuwa ni mwasi aliyejaribu kuwafanya watu wasiwe waaminifu kwa Sulemani. Hakufanikiwa na akakimbilia Misri ili kuepuka kuuawa. Baada ya Sulemani kufa, Jeroboam alirejea tena Israeli kuona kama kulikuwa na nafasi ya kuchukua madaraka. Aliongoza kundi la watu kutoka katika makabila kuzungumza na mfalme mpya, Rehoboamu.
Jeroboam kwa upumbavu wake akawaambia watu kwamba atawatendea kwa ukali sana, akidhania kwamba hawakuwa na chaguo lingine bali kumtii yeye tu (1 Wafalme 12:13-14). Watu walishikwa na hasira, na Jeroboam alikuwa na uwezo wa kutenganisha makabila kumi. Jeroboam aliwaongoza watu katika ibada ya sanamu ili wasije wakarejea tena Yerusalemu kwa ajili ya ibada (1 Wafalme 12:26-28).
Katika hali hii, nani alikuwa kiongozi mzuri, na nani alikuwa mbaya? Wote walikuwa wabaya. Upumbavu wa Rehoboamu ulimpa nafasi kiongozi mwenye hila na tabia mbaya.
Yeroboamu alikuwa tayari kufanya chochote ili kupata nguvu kwake, ikiwa ni pamoja na kuwatoa watu kwenye ibada ya Mungu. Viongozi wengi wa huduma bado wanatumia kutoridhika kwa watu kujenga ushawishi wao; mara nyingi hutumia udanganyifu, kuhamasisha minong’ono na usaliti, na kufundisha fundisho la uongo.
Jinsi ya Kujenga Muunganiko.
Muunganiko hufanyika vizuri zaidi kwa kutumia watu binafsi kuliko kwa watu wengi kwa pamoja au umati au kupitia programu mbalimbali. Kiongozi anayetaka kujenga mwunganiko wake binafsi na watu wake anapaswa aanze na kanuni rahisi au nyepesi za urafiki. Atapaswa kuwasifu ubora wao. Atatakiwa afanye mazungumzo nao kuhusu mambo ambayo hayahusiani na masuala ya kazi. Atapaswa aonyeshe moyo wa upendo kwa familia zao na hali zao binafsi walizo nazo. Atapaswa awatendee vyema watu wake na aonyeshe kwamba anawathamini.
Kamwe usiandike jambo lolote kwa mtu yeyote, hata kwa njia ya barua binafsi, kama hutakuwa unataka ichapishwe au inukuliwe. Huwezi ukajua ni nani atakayeweza kuja kuiona. Kumbuka kwamba wakati unapokuwa unaongea na watu kuna uwezekano mkubwa maneno yako yakanukuliwa na watu wengine. Usiseme mambo ambayo yatakuletea fedheha au aibu kuyaelezea kwa watu wengine baadaye au kwa wakati mwingine.
Viongozi wengine wanataka wawavutie watu wao ili watu hao wapende kuwafuata. Lakini, katika kujenga mwunganiko wa aina mbalimbali, ni muhimu zaidi kuwa na hisia zinazotokana na watu wako, kuliko wewe kutaka kuwavutia wao. Kuna msemo wa kale unaosema, “Hawajali unajua mambo kwa kiasi gani mpaka watakapojua ni kiasi gani unachojali.”
Viongozi wengi ni wadhaifu katika ustadi au uwezo wao wa kusikiliza kwa sababu wanafikiria kwamba tayari wanajua hali ilivyo, wanajua ni nini kinachohitajika kifanyike, na wako tayari kuwashawishi watu wengine. Watu hawawezi kushiriki lolote kama mawazo yao hayathaminiki. Kwa kushindwa kusikiliza na kutambua vyema mawazo yao wanayotoa, kiongozi anashindwa kuwathamini watu wake, kwa hiyo hawatoi kilicho bora.
Wakati mwingine watu walioko katika shirika wanakuwa na hisia kali. Wanasema kwa hasira au kwa kuchanganyikiwa. Kiongozi anaweza akafanya kosa la kujaribu kuwapa watu maelekezo wakati wakiwa wanajihisi tu haja ya kuelezea hisia zao
Stephen M. R. Covey anatoa maelezo kwamba:
Kwa ujumla, kwa kiwango kile ambacho mtu anafanya mawasiliano akiwa na mihemuko mikubwa, yeye anakuwa bado hajajihisi kwamba haeleweki.
Kwa kawaida mtu hawezi kuomba ushauri wako hadi pale atakapojihisi kwamba ataeleweka. Kutoa ushauri mapema sana kwa kawaida kutaibua mihemuko zaidi – au – kutasababisha kwa urahisi tu mtu apuuzie kile unachosema.[1]
Wakati ujao ukiwa katika hali kama hiyo, jaribu kufanya hivi: badala ya kujaribu kubadilisha ufahamu wa watu wenye mihemuko, wasikilize. Onyesha kwamba unaelewa kwa kuthibitisha hisia zao (“Unajisikia kuchanganyikiwa kwa sababu…”) hata kama hukubaliani na maoni yao. Utaona wataanza kutulia na, hatimaye, kuanza kukusikiliza kwa sababu wanafikiri unawaelewa. Hadi hapo watakapofikiri kwamba unaelewa, hawaoni kama maoni yako yanafaa kuzingatiwa.
Ongoza kwa kuuliza maswali—sio kudanganya, bali kuelewa na kuchochea kufikiri. Ikiwa watu ambao wangeweza kusaidia hawasaidii, maswali yatawasaidia kujihusisha. Ikiwa wanashiriki maadili yako, unaweza kuwapata ili kukusaidia kutimiza malengo.
“Je, ni kitu gani unachofikiri kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi?”
“Je, unadhani tunapaswa tujaribu kufanya nini?”
“Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi zaidi kwenye ______?”
Kwa jinsi watakavyokuwa wanakusaidia kwa mawazo, watapenda pia kutoa na msaada kwa kazi iliyopo. Watu huwa hawapendi kutoa msaada kama uthamani wao hautambuliwi.
Kama utafikiri kwamba wazo la mtu alilotoa ni zuri, atakufikiria kwamba wewe una hekima. Kiongozi anapaswa awe na namna ya kukaribisha malalamiko na taarifa zozote zilizo hasi. Watu hawatakuwa na mawasiliano hadi wamejihisi kwamba wako salama. Endapo watakuwa na fikra kwamba wataadhibiwa kwa ajili ya kutokubaliana katika jambo lolote, hawatataka kutoa maoni yao.
Ushiriki unasaidiwa na desturi ya kuwa na mikutano kabla ya mkutano mkubwa. Kabla ya kufanya mkutano na kila mtu ili kupendekeza mabadiliko, ongea na watu binafsi na vikundi vidogo ili kupata maoni yao na kuelezea mpango wako. Waulize wanavyofikiria na wasikilize kwa makini. Jibu pingamizi zao ili kwamba pingamizi hizo zisijitokeze katika mkutano mkuu. Mara tu watu wanapokuwa katika mkutano mkuu, hawapaswi kushangazwa na maamuzi ya kiongozi. Wanapaswa kujua mapema kile wanachoweza kutarajia.
Kwa kawaida viongozi hawapaswi kuwashangaza watu kwa maamuzi yao. Ikiwa watu walioko kwenye shirika mara nyingi wanashtukizwa kwa mshangao kwa mambo ambayo viongozi wao wanayafanya, viongozi wanakuwa hawaelezei vizuri thamani zao na ni kwa jinsi gani wamepanga kuunga mkono uthamani wao. Matumaini katika shirika yanakuwa imara kama watu watajihisi kwamba maamuzi hayatafanywa kwa ghafla bila ya wao kuwa wameelimishwa wakayafahamu. Watashirikisha maono yao kama watapewa kuyajadili na kutoa ushawishi kabla ya kupitishwa yaanze kutumika.
Kiongozi anapaswa awape watu fursa ya kupatiwa taarifa zinazofanana zinazompa yeye motisha. Watu hawataweza kushirikishana malengo yao hadi wamepata motisha au kichocheo kinachotoka katika taarifa inayofanana.
[1]Stephen Covey, The Speed of Trust: The One Thing that Changes Everything (New York: Free Press, 2006), 213
Kuhudumia Wateja
► Je, kanisa lina wateja? Je, dhana ya kuhudumia wateja inatumika kwenye huduma?
► Mwanafunzi atapaswa kusoma 1 Petro 5:2-4 kwa ajili ya kikundi.
Mungu huwapa wachungaji wajibu wa kuwahudumia watu walioko katika kanisa. Tunapaswa tutambue mahitaji yao na kuwatunza au kuwachunga kama mchungaji wa kondoo anavyowatunza na kuwalisha kondoo wake.
Kama viongozi wa makanisa, tunapaswa tujifunze kanuni za kuwahudumia wateja – siyo kutokana na kipaumbele cha kufanikisha biashara, bali kutokana na kipaumbele cha kukidhi mahitaji ya watu. Kipaumbele chetu sisi ni kutimiza wajibu ambao Mungu ametupa.
Kila shirika – aidha liwe la kibiashara, huduma au aina nyingine yeyote – linakuwepo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu. Kwa hiyo, kila shirika linahitaji maono ya huduma yaliyo wazi. Baadhi ya kanuni hufanya kazi sawa kwenye biashara na au huduma
Maono na maadili ya huduma yanapaswa yawe wazi ili kila mtu katika shirika aweze kuweka fokasi yake kwenye kitu ambacho ni muhimu na atajua ni tabia gani ziazotegemewa au zinazotarajiwa.
Makampuni makubwa yanatambua kwamba wateja wao muhimu zaidi ni watu wao wenyewe: wafanyakazi na wasimamizi. Ikiwa viongozi watawajali watu wao na kuwatia moyo waweke akili zao kwenye kazi, watu watatoka nje kwenda kuwahudumia wateja. Uaminifu kwa mteja ni kile kitu unachopata wakati unapokuwa umetengeneza mazingira ya uhamasishaji kwa ajili ya watu wako.[1]
Watu wengi hukubaliana na huduma yenye ubora wa kiwango cha chini bila ya kulalamika kwa sababu hawatarajii iweze kuwa bora zaidi ya mahali ilipo. Hiyo haina maana kwamba wameridhika na huduma hiyo. Ikiwa katika hali hiyo iliyopo kutajitokeza chaguo lililo bora zaidi, watu watabadilika haraka kuingia kwenye hilo chaguo. Kwa hiyo, kiongozi hawezi akajidhania kwamba kila kitu kiko sawasawa au shwari kwa sababu tu watu hawalalamiki.
Ikiwa watu wanahama kutoka kwenye kanisa au shirika lingine lolote kwa sababu ya mambo yasiyo na maana au hata bila ya sababu yeyote, kuna ukosefu wa watu kutoridhika. Viongozi hawapaswi kungojea hadi wasikie malalamiko.
Ubora ulio thabiti unahitaji programu ya mafunzo na uboreshaji wa mara kwa mara. Msimamo ni muhimu kwa sababu kama utajenga matarajio makubwa lakini ukashindwa kukamilisha matarajio hayo, watu watakuwa wamekatishwa tamaa.
Huduma huanza na urafiki wa kawaida. Kuwa na urafiki na mtu inamaanisha ni kumthamini kama mtu, na siyo tu kama kukutana kibiashara. Unapokuwa unazungumza nao kuhusu jambo lolote ambalo halihusiani na manunuzi, wanajisikia kwamba wanaingiliana na wewe kwa njia ya kirafiki.
Zaidi ya kuwa rafiki, weka tahadhari kwa mahitaji ya watu. Jaribu kuona hitaji na usaidie katika njia ya kipekee zaidi ya huduma ya kawaida.
Ni jambo lililo wazi kwamba shirika haliwezi kutoa kila kitu ka ajili ya kila mtu, lakini linapaswa lihudumie baadhi ya mahitaji katika njia isiyokuwa ya kawaida.
Tafakari:
Je, ni aina gani ya watu unaotaka kuwavutia?
Je, unataka ukamilishe kitu gani?
Je ni mahitaji gani unayopaswa uyatoe?
Kiongozi anapaswa afikirie huduma kamili itakuwaje, kisha aendeleze na kurekebisha ufahamu wake kwa kuzungumza na watu anaowahudumia.
► Tafakari kuhusu shirika lako. Ni aina gani ya watu unataka kuwavutia? Ni mahitaji ya nani unapaswa kutimiza?
► Tafakari kuhusu aina ya watu ambao walishawahi kuhudumiwa na shirika lako. Je, ni kitu gani wanachokitafuta wanapokuwa wamekuja kwako? Ni kitu gani unachoweza kuwapa kinachozidi matarajio yao?
Ruhusu baadhi ya wanafunzi washirikishane kuhusu ni kwa jinsi gani wanategemea kubadilisha malengo au matendo yao kutokana na somo hili.
[1]Ken Blanchard, Kathy Cuff, and Vicki Halsey, Legendary Service: The Key is to Care (New York: McGraw-Hill, 2014), 5
Muhtasari wa Taarifa Tano.
1. Watu hufanya kazi kwa ufanisi zaidi wanapojisikia kuwa na dhamira binafsi kwa shirika.
2. Kiongozi anapaswa atumie muda wake katika kukuza viwango vya ushiriki wa watu wake.
3. Kama watu kwenye shirika hawatoi na kufanya kle kinachohitajika kufanywa, hawawezi kujisikia kuhusiana.
4. Kiongozi anapaswa awe na namna ya kukaribisha malalamiko na taarifa zilizo hasi.
5. Kwa kawaida viongozi hawapaswi kuwashutua na kuwashangaza watu kwa maamuzi yao.
Kazi za Kufanya Somo la 9
1. Andika aya inayotoa muhtasari wa dhana ya kubadilisha maisha kutoka katika somo hili. Elezea kwa nini ni muhimu. Je, ni jambo gani zuri linaloweza kufanywa? Je, ni madhara gani yanayoweza kujitokeza kwa kutojua?
2. Elezea ni kwa jinsi gani unavyoweza kutumia kanuni zilizoko katika somo hili kwenye maisha yako mwenyewe. Je, ni kwa jinsi gani somo hili linabadilisha malengo yako? Je, ni kwa jinsi gani umejipanga kubadilisha matendo yako?
3. Fanya kukariri Taarifa Tano kwa Muhtasari zilizoko katika somo la 9. Kuwa tayari kuziandika bila ya kunakili kutoka katika kumbukumbu za ufahamu wako mwanzoni mwa kipindi kinachofuata cha darasa.
4. Kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa, soma 1 Wakorintho 12.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.