John Maxwell alizungumza na mfanyabiashara ambaye kampuni yake ilinunua hoteli zilizoshindwa kuendeleza biashara na akaziandaa upya ili kuanza kupata faida. Maxwell aliuliza kama kuna kitendo chochote kimoja ambacho kampuni iliweza kufanya siku zote wakati waliponunua hoteli iliyoshindwa kibiashara. Yule mfanyabiashara alijibu, “Siku zote tunamfukuza meneja. Hatungojei kuona kama yeye ni meneja mzuri. Unakuta tayari tumeshajua kwamba yeye siyo meneja mzuri kwa sababu hoteli inashindwa kujiendesha kibiashara.”
Kama timu ya kitaaluma ya michezo ikishindwa, wenye hiyo timu hawatafuti wachezaji wapya tu; bali pia na mwalimu mpya wa timu. Shirika halitaweza kuwa na mafanikio likiwa na kiongozi mbaya.
Kiongozi wa kweli mzuri hatoi sababu za kujitetea kwa ajili ya shirika kushindwa kujiendesha. Kama shirika litashindwa, yeye ndiye aliyeshindwa.
► Je, kwa nini uongozi ni muhimu?
Eli alikuwa kuhani mkuu wa Israeli. Kwa kuwa hakukuwepo na mfalme, makabila yalikuwa hayajaungana kuwa chini ya serikali kuu moja. Kuhani mkuu alikuwa mtu mwenye nguvu aliyekuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika taifa.
Kwa bahati mbaya sana, Eli alikuwa kiongozi mdhaifu. Alikuwa na tabia ya binafsi nzuri, lakini hakuwa na uwezo wa kuongoza hata watoto wake mwenyewe kufanya haki. Watoto wake walikuwa waasherati, walikuwa wazembe kwenye mambo ya ibada, na wenye wivu wa mapato. Kwa sababu ya wao, watu wengi waliidharau ibada ya hekaluni (1 Samweli 2:12-17, 22, 29).
Eli alipaswa awaondoe watoto wake kutoka kwenye nafasi zao walizokuwa nazo, lakini matamanio yao yalikuwa ni muhimu zaidi kwake kuliko jukumu lake lilikokuwa limetengwa.
Eli alikuwa aliongoze taifa kwenye ibada ya kiroho na maisha matakatifu; lakini ushawishi wake ulisimama kwa watoto wake, badala ya kuueneza kwa taifa kupitia kwa watoto wake.
Sababu za Watu Kutofanya kile ambacho Walipaswa Kukifanya
(1) Hawajui kitu cha kufanya.
Hii inatokana na ukosefu wa kupewa taarifa. Kiongozi anapaswa atoe taarifa. Kama atakuwa hana ufahamu wote taarifa inayohitajika itolewe, anapaswa amtafute mtu mwingine wa kumsaidia.
(2) Hawajui wafanye namna gani.
Hii inatokana na ukosefu wa mafunzo. Kiongozi anaweza asiwe na Ustadi wa mambo yote yanayohitajika kwenye shirika, lakini anapaswa aandae mafunzo.
(3) Hawajui ni kwa nini wafanye hivyo.
Hii inatokana na ukosefu wa motisha. Wakati mwingine watu walioko kwenye shirika huwa hawaelewi malengo ya shirika. Au wakati mwingine huwa wanaelewa, lakini hawajali. Kiongozi anapaswa awasaidie watu kushirikishana katika malengo.
(4) Kuna matatizo ambayo yanawazuia kufanya hivyo.
Hii inatokana na ukosefu wa vifaa na mpangilio au mfumo. Kiongozi anapaswa awasaidie watu jinsi ya kutatua matatizo ambayo yanawazuia kutofanikiwa.
Orodha hii inatupa sababu nne za kawaida ambazo watu katika shirika wanashindwa kufanya kile ambacho walipaswa kukifanya. Sababu hizi nne zote zinaonyesha kushindwa kwa uongozi.
Wakati kiongozi anapolalamika kwamba watu wake hawataki kufanya kile ambacho walipaswa kukifanya, anatangaza kwamba yeye anashindwa kuongoza. Kwa mfano, mchungaji ambaye analalamika kwamba kanisa lake halifanyi uinjilisti tafakari maswali haya:
Je, niliwaeleza kwamba wanapaswa kufanya uinjilisti?
Je, niliwaonyesha jinsi ya kufanya uinjilisti (kwa kuwaonyesha wazi)?
Je, niliwapa motisha?
Je, niliwasaidia katika kupambana na matatizo ambayo yanawazuia kufanya uinjilisti?
Kama majeshi ya kivita mawili yana ukubwa unaolingana na vifaa vinavyofanana, je, ni jeshi lipi litakaloweza kushinda? Jeshi ambalo lina jenerali bora ndilo litakaloweza kushinda.
Timu mbili za mpira zina wachezaji wenye vipaji vinavyofanana, Je, ni timu gani itakayoweza kumshinda mwingine? Timu iliyo na kocha bora ndiyo itakayoweza kushinda.
Changamoto ya Motisha
► Methali ya zamani inasema, “Kalamu ina nguvu zaidi kushinda upanga.” Unadhani hiyo inamaanisha nini?
Inamaanisha kamba nguvu iko kwenye wazo, ushawishi, na mawasiliano. Wazo lina ushawishi zaidi kuliko hata upanga. Neno “kalamu” linarejea kwenye mawasiliano kwa njia ya kuandika, lakini mawasiliano ya kuhamasisha ya aina yeyote yana nguvu zaidi kuliko kuwalazimisha watu wawe kinyume na mapenzi yao.
Ukijaribu kulazimisha watu, ni vigumu kuongeza ushawishi wako zaidi ya kuwepo kwako binafsi. Watu wanaolazimishwa hawawezi kufanya kazi kwa bidii. Hawajitolei nishati na mawazo yao katika kazi. Unaweza kufanikisha zaidi kwa kuhamasisha watu kuliko kwa kuwashurutisha. Wazo – dhana- vinaweza vikaenea na kushawishi mamilioni ya watu.
Vita Kuu ya Pili ni mfano wa nguvu iliyoko katika maneno. Vita Kuu ya Pili ilikuwa ni vita ya maneno, vita ya mawazo.
Kwa nini ilikuwa ni vita ya maneno? Adolf Hitler alikuwa msemaji mwenye nguvu. Aliweza kuwasilisha maono yake kwa ajili ya Ujerumani, na Wajerumani walimfanya kwa kiongozi wao. Aliweza kuwashawishi kwamba wao walikuwa ni mabingwa wa mbio ambao wangeweza kuitawala dunia. Hata baadhi ya makanisa walianza kumzungumzia kama yeye ni masihi na kusema kwamba Ujerumani ilikuwa ndiko ufalme wa Mungu. Hitler aliiongoza Ujerumani katika kutenda maovu ya kihistoria. Aliyafanya yote haya kwa nguvu ya maneno. Wakati mwingine watu hufikiri kwamba maneno hayawezi kuleta madhara, lakini maneno ya Hitler yaliuwa mamilioni ya watu.
Wakati Hitler alipokuwa anaongezeka kuwa na nguvu, baadhi ya watu nchini Uingereza walifikiri kwamba hakungeweza kuwepo na madhara yeyote kwao. Wakati ilipofikia wakati wa nchi kumchagua waziri mkuu mpya, baadhi ya wagombea waliwaahidi watu kwamba watakuwa na amani. Lakini Winston Churchill aliwaambia watu ukweli. Alisema, “Ninawapeni damu, jasho, na machozi yangu.” Aliweza kuchaguliwa kwa sababu alikabiliana na matatizo.
Hotuba za Churchill ziliiunganisha Uingereza katika kujilinda dhidi ya Ujerumani. Alisema, “Tutapigana baharini na angani. Tutapigana ufukweni kama watafika kwenye fukwe zetu. Tutawapiga kwenye kila barabara katika kila jiji. Hatutakubali kushindwa. Hatutakubali kujisalimisha.”
Kupitia hotuba zote hizi za Hitler na Churchill, tunaona nguvu iliyoko katika maneno. Kwa maana halisi ni kwamba kila vita, ni vita ya maneno.
► Elezea kuhusu taarifa kwamba kila vita ni vita ya maneno. Hii inatufahamisha nini kuhusiana na uongozi?
Wakati mwingine kiongozi hufikiri kwamba anaweza kupata msaada tu kwa kuulipia. Anafikiri kwamba watu wake watafanya mambo makubwa zaidi kama atawalipa zaidi. Kwa kawaida huo siyo ukweli. Watu hulisaidia shirika kwa sababu wanaliamini. Wanafanya kazi kwa juhudi kubwa kwa sababu wanashirikishana malengo.
Huwezi kuwa na kazi yenye thamani kubwa isipokuwa kama kila mtu atafanya kazi kuelekea uelewa mzuri na ushirikishwaji wa malengo. Lakini hiyo haitoshi. Inategemea ni kwa jinsi gani utafikia kwenye lengo. Ni lazima uongozwe na maadili. Kwa pamoja unapaswa ujivunie kuhusu lengo na jinsi ulivyofika pale kwenye hilo lengo.[1]
► Inamaanisha nini kusema kwamba unapaswa ujivunie kuhusu lengo na jinsi ulivyofika pale kwenye hilo lengo?
Mfanyabiashara hatatengeneza kampuni kubwa kwa kuwalipa tu wafanyakazi wake. Lazima awaongoze kwa malengo na maadili. Ikiwa pesa pekee ndizo zina maana, watu hawatafanya kazi kwa ajili ya malengo ya biashara. Hawatathamini ubora na hawatajivunia kazi yao.
[2]Mambo muhimu zaidi hayafanyiwi kwa ajili ya fedha. Jaribu kufikiria mambo ambayo watu wanayafanya kwa ajili ya familia zao na watoto wao. Hawafanyi mambo hayo kwa sababu ya fedha, bali kwa sababu ya mambo muhimu makubwa ya manufaa. Watu huongozwa na maadili yao.
Kwenye huduma, Ustadi wa uongozi ni bora zaidi kuliko kwenye biashara ya dunia, kwa sababu watendakazi katika huduma ya kanisa wengi ni wa kujitolea. Kiongozi hawezi akatoa motisha kwa ajili ya kazi ya kulipia kwa walio wengi wao. Watu wanaosaidia katika shughuli za kanisa wanafanya hivyo kwa sababu wanaliamini kanisa. Kama kanisa litakuwa halipati msaada wa mtaa kifedha na nishati, kiongozi atakuwa ameshindwa.
► Je, watu wanaotoa msaada kwenye kanisa lako ni kina nani? Je, kwanini wanafanya hivyo?
Wajibu wa kiongozi umefafanuliwa kwa muhtasari kwa njia hii:
Wafanye watu wajue ni kwa nini kazi ni ya thamani kubwa. Fanya maamuzi ya unakotaka uelekeze. Hakikisha kwamba timu yako inashirikishwa kuhusu lengo linalotakiwa. Weka tayari rasilimali zinazohitajika. Wakague wote watakaosimamia maamuzi. Kwa pamoja hakikisha unao msaada unaohitajika kutoka ndani na nje ya shirika. Elekeza jicho lako kwenye mambo ya baadaye ili kuepukana na matatizo na kuwa tayari kuubadili mwelekeo.[3]
[1]Ken Blanchard and Sheldon Bowles, Gung Ho: Turn on the People in Any Organization (New York: William Morrow, 1997), 38
“Kuwa na mishughuliko mingi haimaanishi siku zote kwamba ndiyo kazi halisi. Makusudi makubwa ya kazi ni uzalishaji au ukamilishaji, na aidha kwa ajili ya hii miisho ni lazima kuwepo na wazo tangulizi, mfumo, upangaji, uchunguzi, na kusudi la kweli, pamoja na kutoa jasho.”
Kama mtu anao ustadi kwenye aina fulani ya kazi lakini akawa hana ustadi katika uongozi, atakuwa anafanya kazi mwenyewe au atakuwa chini ya maelekezo ya mtu mwingine. Lakini mtu ambaye ana kiwango cha juu cha ustadi wa kazi na pia akawa anao uwezo wa uongozi atakuwa ana uwezo wa kuwaongoza watu wengine na kukamilisha mambo makubwa zaidi.
Mtume Paulo Alianzisha mtandao kwa ajili ya makanisa kwenye miji mikubwa. Alichagua viongozi kwenye kila eneo, kwa sababu alijua kwamba viongozi wengi walikuwa wanahitajika kwa ajili ya kanisa kuweza kukua kila mahali.
Paulo alitoa mafunzo kwa baadhi ya watu kwa kuwachukua na kutembea nao katika safari zake za umisionari. (Matendo 16:3, Matendo 19:22). Paulo alisisitiza hitaji endelevu la kuwaendeleza viongozi. Alimwambia Timotheo kuwatafuta watu ambao watakuwa na uwezo wa kuwafundisha watu wengine (2 Timotheo 2:2).
Fundi mchundo mwenye uwezo wa uongozi anaweza akawa na mambo mengine ya kufanya na mafundi michundo wenzake wanaofanya kazi kwa ajili yake. Kama yeye siyo kiongozi, atakuwa anafanya kazi mwenyewe au kwa ajili ya mtu mwingine.
Alex anajua jinsi ya kufanya aina zote za kazi za ujenzi kwenye majumba. Anafanya kazi vizuri sana na ni mwaminifu. Wateja wake humtambulisha kwa watu wengine, na siku zote anakuwa ana kazi inayomsubiri akaifanye. Alex hana wafanyakazi aliowaajiri kwa sababu anajua jinsi ya kufanya kila kitu na hataki kumtumia mtu mwingine ambaye anaweza asiifanye kazi yake kama yeye mwenyewe anayotaka. Kwa kuwa Alex siyo kiongozi. Kazi yake kamwe haitakaa ipanuke kuwa kubwa zaidi kazi anayoweza kuifanya yeye mwenyewe.
Ustadi wa uongozi huzidisha thamani ya uwezo mwingine alio nao mtu. Mtu aliye na utendaji mahiri wa hali ya juu kwenye eneo lolote anaweza akajiongezea umuhimu wake kwa kuongeza ustadi wake wa uongozi.
Kuaminika kwa Kiongozi
Kiongozi wa kuaminika huwapa watu wake kile wanachohitaji katika kufanikiwa. Kiongozi hutengeneza mazingira ya mafanikio yao. Wanahitaji wajue kwamba atatekeleza majukumu yake ili na wao waweze kutekeleza majukumu yao.
Kama kiongozi atakuwa siyo mtu wa kuaminika, watu hawawezi kufikia malengo ya shirika lao, kwa hiyo wanabadilika kwa kuacha kutekeleza malengo yao. Kiongozi ambaye siyo mtu wa kuaminika mara kwa mara huwa anawaeleza watu wake ni kwa nini hakuweza kufanya na kufikia matarajio ya mategemeo yao.
Kiongozi hapaswi kuwa mtu asiyekuwa tayari kwa ajili ya matatizo. Anahitajika kupanga kwa ajili ya muingiliano na vizuizi vyote na kuwa tayari kukabiliana nayo. Kiongozi anajua kwamba mara zote mambo huwa yanabadilika. Anatambua kwamba mabadiliko yeyote yanaweza kuzua matatizo mapya, kwa hiyo anapaswa kujiandaa. Watu wengine wanaweza wakajichukulia watakavyo hali mbalimbali kama zinavyojitokeza, lakini kiongozi ni lazima awe tayari kuendelea kuongoza.
Musa alikuwa msimamizi wa wafanyakazi wa ujenzi. Mkaguzi wake alimwambia kwamba baadhi ya kuta zilihitajika ziwe zimejengwa hadi kufikia mwisho wa siku, kwa hiyo Musa naye akawaeleza wafanyakazi wake. Hata hivyo, vifaa vya ujenzi havikufika kwa sababu mkaguzi alisahau kuvituma. Musa akawaeleza wale wafanyakazi kwamba lengo lao halitakuwa limefikiwa. Baada ya hali kama hiyo kuwa inatokea mara kadhaa, ilikuwa ni vigumu kwa Musa kuweza kuwaeleza wafanyakazi wake kwamba wanapaswa watekeleze jukumu kwa haraka.
Esta alikuwa mwalimu wa shule. Siku moja alifika shuleni na mkuu wa shule akamwambia kwamba darasa lake litatumiwa na kikundi kingine katika siku hiyo. Esta hakuwa amejitayarisha kufundisha katika mahali pengine na hakuwa na muda wa kutosha wa kuhamisha vitu alivyovihitaji kutoka katika darasa hilo.
Uongozi katika Huduma
Biblia inatueleza kwamba Mungu alitoa watu wengine kuwa mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu (Waefeso 4:11-12). Mungu pia aliwapa uwezo uliokuwa unahitajika.
Wito wa Mungu unampa mtu nafasi ya kuongoza, lakini siyo dhamana ya mafanikio. Kama tabia ya mtu inampunguzia ushawishi wake badala ya kumwongezea, hawezi akawa na mafanikio.
Angalia majukumu ya huduma yaliyoko kwenye Waefeso 4:11. Je, ni kwa jinsi gani mwinjilisti anaweza kufanikiwa kama watu watakuwa wanafikiria kwamba hawawezi kumwamini? Je, ni kwa jinsi gani mwalimu ataweza kufanikiwa kama watu watajua kwamba alifundisha mambo yaliyokuwa makosa? Je, mchungaji anawezaje kufanikiwa kama watu watagundua kwamba alikuwa anataka tu kujinufaisha kutoka kwao?
Bila kuwepo na ushawishi, mtu hawezi akafanikiwa katika huduma. Majukumu haya ya huduma ni majukumu ya uongozi, kwa sababu yanategemea uwepo wa ushawishi.
Baadhi ya Dhana potofu kuhusu Uongozi
Baada ya kusoma kila pointi na kabla ya kutoa maelezo, uliza, “Ni kitu gani kilicho potofu katika dhana hii?”
(1) Kiongozi ni mtu ambaye anatumikiwa na watu wengine.
Kiongozi ni mtu ambaye hutafuta njia ya kukidhi mahitaji kwa ajili ya kikundi. Hiyo ndiyo sababu wanamkubali yeye kama kiongozi. Yesu alisema kwamba kiongozi ni mtu anayetumikia wengine. Alisema kwamba mtu aliye mkuu ni mtumishi wa watu wote. Kiongozi husalimisha maslahi yake mwenyewe kwa ajili ya watu wengine.
(2) Kiongozi wa huduma ni mtu wa kiroho na kimungu zaidi kuliko wafuasi wake.
Ukweli ni kwamba makanisa mengi yana wanachama ambao ni wa kimungu zaidi kuliko hata mchungaji wao. Uwezo wa uongozi hauthibitishi kuwa mtu ni wa kiroho.
(3) Kupanda hadhi katika uongozi wa huduma kunategemea juhudi za mtu binafsi.
Majaribio ya mwanadamu ya kupanda hadhi kwa kawaida hayafanyi kazi inavyotakiwa. Tunapaswa tufanye vizuri kwa kadri inavyowezekana katika majukumu yetu na kumwamini Mungu kwamba atatuweka kwenye sehemu sahihi. Kamwe usifanye kitu ambacho hakitampa Mungu heshima katika majaribio yako ya kuwa kwenye nafasi ya uongozi. Kama huwezi kufika kwenye nafasi hiyo kwa kumheshimu Mungu, hustahili kuwepo kwenye nafasi hiyo.
Viongozi waliochaguliwa na Mungu mara nyingi ni watu ambao walikuwa hawatafuti kuwa kwenye nafasi za uongozi. John Chrysostom alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Constantinople katika mwaka wa 397 B.K. Mwanzoni kabisa aliikataa nafasi hiyo kwa sababu alikuwa anafikiri kwamba hana sifa za kuwa kwenye nafasi kama hiyo. Baadaye, aliandika kuhusu tabia halisi inayohitajika katika nafasi za huduma. Alisema kama mtu akikataa kwenda kulisha ng’ombe halitakuwa jambo la kushangaza kwa sababu nafasi yenyewe ni ya hali ya chini. Kama mtu akikataa kuwa mfalme, kimsingi huenda akawa anawaza kwamba nafasi hiyo ni ya juu sana kwake. Kama mtu akikataa nafasi ya huduma, inawezekana ikawa ni kwa sababu kadhaa, kutegemea kwamba aidha anafikiri huduma hiyo ni ya juu sana au ni ya chini sana kwake.[1]
Ruhusu baadhi ya wanafunzi washirikishane kuhusu ni kwa jinsi gani wanategemea kubadilisha malengo au matendo yao kutokana na somo hili.
1. Kama shirika litakuwa linashindwa, kiongozi wake ndiye anayeshindwa.
2. Mafunzo na Motisha ni majukumu ya uongozi.
3. Watu hupenda kujivunia kuhusu malengo yao na jinsi walivyoyafikia.
4. Ustadi wa uongozi huongeza thamani ya uwezo mwingine wa mtu.
5. Kuaminika kwa kiongozi ni kipimo cha kuaminika kwa shirika.
Kazi za Kufanya Somo la 3
1. Andika aya inayotoa muhtasari wa dhana ya kubadilisha maisha kutoka katika somo hili. Elezea kwa nini ni muhimu. Je, ni jambo gani zuri linaloweza kufanywa? Je, ni madhara gani yanayoweza kujitokeza kwa kutojua?
2. Elezea ni kwa jinsi gani unavyoweza kutumia kanuni zilizoko katika somo hili kwenye maisha yako mwenyewe. Je, ni kwa jinsi gani somo hili linabadilisha malengo yako? Je, ni kwa jinsi gani umejipanga kubadilisha matendo yako?
3. Fanya kukariri Taarifa Tano kwa Muhtasari zilizoko katika somo la 3. Kuwa tayari kuziandika bila ya kunakili kutoka katika kumbukumbu za ufahamu wako mwanzoni mwa kipindi kinachofuata cha darasa.
4. Kabla ya kipindi kinachofuata cha darasa soma 1 Wafalme 19:19-21 na 2 Wafalme 2:1-15 na andika kuhusu mabadiliko ya uongozi kuwa nabii mpya.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.