Huduma Ya Uongozi
Huduma Ya Uongozi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 13: Kuwaendeleza Viongozi

15 min read

by Stephen Gibson


Kujifunza Kuwaongoza Viongozi

Viongozi wengi wana ushawishi wenye msingi wake kwenye haiba kubwa, ambayo haiendi mbali zaidi ya mwonekano wao binafsi. Wao binafsi ndio wanaoelekeza kila kitu kinachotokea kwenye shirika, Hawatengenezi mfumo wa uongozi na wanaonekana kutoweza kuwatayarisha viongozi ambao wataunga mkono maono yaliyoshirikishwa. Wakati mwingine wanaonekana kama ni viongozi wenye nguvu sana kwa sababu ya kuwa na uthibiti mkubwa kwenye shirika lao, lakini shirika lao haliwezi kuendelea kukua juu ya kiwango fulani.

Shirika haliwezi likaendelea hadi pale viongozi wao watakapokuwa wamejiendeleza. Shirika hufikia kikomo chake wakati viongozi nao wanapokuwa wamefika kwenye ukomo wao. Shirika haliwezi likajiongeza katika viwango vyake kutokea pale lilipo hadi viongozi wake watakapotafuta njia za kujiendeleza wao wenyewe.

Kiongozi aliyekuwa kijana alipata nafasi ya kushika madaraka ya kuongoza taifa. Alitaka ashikilie madaraka yote ya kuongoza nchi na ahakikishe kwamba hakuna mtu atakayeshindana naye. Kujifunza jinsi ya kufanya hivyo, alikwenda kumtembelea kiongozi mmoja wa zamani au mstaafu ambaye aliwahi kuwa dikteta kwenye uongozi wa taifa lake kwa muda mrefu. Aliuliza, “Je, utahakikishaje kwamba kamwe hakuna mtu yeyote atakayejitokeza kutaka kuja kuchukua madaraka yako?” Walikuwa wanatembea pamoja kwenye bustani mahali ambapo magugu yalikuwa yameota. Dikteta yule wa zamani au mstaafu alikuwa na henzirani au ufito wa mwanzi, na walipokuwa wanatembea kupitia katika yale magugu, yule dikteta aling’oa gugu moja lililokuwa limerefuka kuliko magugu yote mahali pale. Baada ya kuangalia kwa dakika kadhaa, yule kiongozi kijana akamwambia, “Nimekuelewa.”

Baadhi ya viongozi huwa hawapendi kuwa na wasaidizi ambao wana mawazo mapana na uwezo wa uongozi. Viongozi hawa wanataka tu wawe na watu ambao watafuata maelekezo yao tu.

Viongozi wanaojitafutia maslahi binafsi, ambao wamelewa madaraka, kutambuliwa, na wanaogopa kupoteza nyadhifa zao, hawana uwezekano wa kutumia muda au juhudi yoyote kuwafundisha warithi wao.[1]

Viongozi hawa huunda mazingira ambamo viongozi wapya hawaendelei. Kunakuwa na kiongozi mmoja tu na wasaidizi wake. Shirika halitengenezi idara na mipango inayohitaji viongozi wa ziada. Vijana wenye vipaji vya uongozi mara nyingi huondoka kwenye shirika hilo kutafuta mahali penye fursa.

Viongozi wapya wanahitajika kwa makusudi makuu mawili: (1) Kuandaa nafasi za uongozi kwa ajili ya wakati ujao. (2) Kupanua shirika.

Herode Mkuu alikuwa mtawala wa nchi ya Yuda, akiwa ameteuliwa na watawala wa Kirumi. Hakuwa Myahudi, na takribani watu wengi katika nchi ile hawakuwa wamependa awe mtawala wao. Kila wakati alikuwa mtu wa wasiwasi na mashaka kwamba watu walikuwa wanataka kumwondoa asiwe mfalme. Aliwauwa baadhi ya wake zake na watoto wake kwa sababu aliwahisi kwamba wanataka kumwondoa kwenye ufalme. Hakutaka kumpa mafunzo mtu yeyote kwa ajili ya kurithi nafasi ya kuwa mfalme. Baada ya kifo chake, mtoto wake alifanywa kuwa mfalme lakini hakuweza kuimudu kazi yake vizuri, hivyo akaondolewa kwenye ufalme na Warumi. Warumi wakamweka mtu mwingine kuwa Gavana juu ya Yuda, na Yuda kamwe haikuja kuwa tena na mfalme mwingine.

Mafanikio ya muda mfupi bila ya kuwepo na mrithi ni maanguko ya muda mrefu. Kama shirika halitaendelea kufanya vizuri baada ya kiongozi kuwa ameshindwa, atakuwa hakukamilisha majukumu yake yote kwa ukamilifu.

Mtu huandaliwa kwa ajili ya nafasi ya juu ya uongozi siyo tu kwa ajili ya kumsaidia kiongozi mkuu, bali kwa ajili ya kutumika kama kiongozi. Kiongozi mkuu ni lazima awe tayari kuwa na viongozi wanaonyesha kuendelea kwenye shirika lake: viongozi ambao wana mawazo, wanaochukua hatua, na wenye uwezo wa kufanya maamuzi mbalimbali.

Viongozi wapya ni lazima waendelezwe kwa ajili ya kukua kwa shirika. Shirika haliwezi likaendeleza programu mpya au kupanuka bila ya kuwepo na ongezeko la viongozi.

[2]Ni muhimu kuwa na fursa kwa viongozi watarajiwa. Ikiwa shirika lina nyadhifa chache tu za uongozi na haliwezi kuongeza zingine, haliwezi kupanuka wala kuwahifadhi viongozi wenye uwezo tarajiwa. Kwa mfano, kanisa lenye afya lina watu wanaojihusisha zaidi na wanaotamani kuanzisha huduma mpya. Ikiwa hawapewi nafasi ya kuongoza, kanisa halitakua kama inavyostahili.

Kushindwa kuwaendeleza viongozi wengi kutasababisha maamuzi yote yatoke kwa kiongozi mkuu peke yake. Kwa kiongozi anakuwa na mipaka yake, watu watakuwa wanamngojea yeye kwa muda wao mwingi.

Musa alikuwa kwenye nafasi mpya ya uongozi baada ya kuwaongoza wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri. Watu walikuwa wanakuja kwake kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa migogoro iliyokuwa ikitokea kati yao. Kulikuwepo na migogoro mingi kwa sababu kulikuwa na watu wengi sana kwenye eneo jipya ambalo lilikuwa halina sheria zilizokuwa zimewekwa au hakukuwepo na mifano ya kuiga. Yethro alimtembelea Musa na akaona kwamba Musa alikuwa anatumia muda wake mwingi kila siku katika kutatua migogoro ya watu. Yethro alimshauri aanzishe waamuzi kwenye ngazi tofauti za watu kwa ajili ya kuamua mashauri yaliyokuwa mengi. Kitendo hiki kilianzisha uwepo wa viongozi wengi waliokuwa na mamlaka kamili.

Kiongozi anayeelekeza fokasi yake katika kuwavutia wafuasi wake kwa kawaida huwa amekosa msaada wa uongozi. Shirika linaweza likaongeza wafuasi, au linaweza likazalisha maradufu wafuasi kwa kuwavutia na kuwaendeleza viongozi.

Kuwaendeleza viongozi siyo wajibu wa kiongozi mkuu peke yake. Kila kiongozi kwenye shirika, katika ngazi yeyote, anapaswa kusaidia katika kuwaendeleza watu wanaomzunguka kwa kuwashauri na kuwashirikisha majukumu yaliyopo.

► Kwa nini shirika lenye nguvu na linalokua linahitaji viongozi wengi?


[1]Ken Blanchard and Phil Hodges, The Servant Leader: Transforming Your Heart, Head, Hands, and Habits (Nashville: Thomas Nelson, 2003), 18
[2]

“Acha yeyote aliyeko kwenye mamlaka aingize swali hili jepesi kwenye kichwa chake, siyo ‘Ni kwa jinsi gani mimi ninaweza kufanya hiki kitu sahihi mwenyewe, lakini ‘Ni kwa jinsi gani ninaweza kuhudumu kwa ajili ya hiki kitu sahihi kiweze kufanyika kila wakati?’”

- Florence Nightingale