Huduma Ya Uongozi
Huduma Ya Uongozi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 5: Uongozi wa Utumishi

14 min read

by Stephen Gibson


Mfano wa Kufuata wa Uongozi Uliotukuka

Karamu ya mwisho ambayo Yesu alikula akiwa na wanafunzi wake ilikuwa ni sherehe ya Pasaka. Ilikuwa ni jambo la jadi kwamba kwenye karamu iliyoandaliwa rasmi mtumishi atatawadha miguu ya wageni waliopo. Kazi hii kwa kawaida alikuwa anapewa aifanye mtumishi wa hali ya chini sana kuliko wote waliopo.

Kwenye karamu hii, Yesu peke yake na wanafunzi wake ndio waliokuwepo mahali pale. Mwanzoni, hakuna mtu aliyefanya kazi ya kutawadha miguu. Hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyejitolea kwa ajili ya kuifanya kazi hii kwa sababu hawakuwa wanataka kuwa kwenye nafasi ya mtumishi wa hali ya chini sana. Kila mmoja alikuwa bado anategemea kuwa kwenye nafasi ya juu katika ufalme mpya.

Tunaweza tukafikiria kwamba labda Petro alimwambia Yohana kwa polepole, “Mtu anahitajika kufanya kazi ya kutawadha miguu; unatakiwa ukaifanye wewe.” Labda Yohana alijibu, “Hapana, mimi siwezi nikaifanya kazi hiyo; Yakobo anatakiwa aifanye.” Hakuna hata mmoja wao miongoni mwao aliyekuwa tayari kuifanya kazi hiyo iliyokuwa ni jukumu la mtumishi wa hali ya chini sana. Pale mwishoni mwa karamu, Yesu alisimama, akachukua maji na taulo, akaanza kuifanya kazi hiyo. Kwa hakika baadaye wanafunzi walishikwa na aibu.

Petro alikataa kumruhusu Yesu amtawadhe miguu yake mwanzoni, akisema kwamba alimheshimu Yesu sana hivyo asingeweza kumruhusu afanye kazi ya chini kama hiyo. Yesu akamwambia Petro, “Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.” Alikuwa anatumia kazi hiyo ndogo sana kuwakilisha kusudi kubwa la mwili wa Kristo. Kwa wakati mwingine alisema, “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mathayo 20:28). Huduma aliyoitoa pamoja na kifo chake ilidhihirishwa kwa matendo yake mengi ya huduma, ikiwa ni pamoja na kuwaosha miguu wanafunzi siku hiyo. Kama mtu hataikubali huduma ya Yesu, huyo mtu siyo sehemu ya ufalme wa Yesu.

Baadaye Yesu alisema, “Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? Akawaeleza kwamba katika utaratibu wa kidunia, kiongozi anategemea ahudumiwe. Lakini kwenye ufalme wa Mungu, uongozi ni huduma.

Matazamo sahihi wa uongozi ni huduma kwa watu wote. Mtu anayezingatia mahitaji ya watu na akapata nafasi ya kuhudumia mahitaji hayo ataweza kuwa kiongozi. Watu wanataka kiongozi ambaye anawajali na mwenye uwezo wa kushughulikia mahitaji yao. Watu wako na hiari ya kukabidhi mamlaka kwa mtu ambaye atayatumia mamlaka kwa ajili ya mustakabali wao.

Kundi la wanajeshi walikuwa wanajenga nyumba zenye kutumia magogo. Walikuwa wanajitahidi kuinua gogo lililokuwa zito sana, na sajini wao alikuwa anawapaazia sauti kwa nguvu. Mtu mmoja alikuwa anapita karibu nao na akasimama akiwaangalia. Akamwambia yule sajini, “Kwa nini huwapi msaada? Yule sajini akajibu kwa hasira, “Mimi ni sajini.”

Yule mpita njia akaungana na wale wanajeshi na akawasaidia katika kuliinua lile gogo, kisha akafungua koti lake alilokuwa amelivaa akaonyesha nguo zake za kijeshi alizokuwa amevaa. Akasema, “Mimi ni jenerali.” Huyu alikuwa ndiye Jenerali George Washington, ambaye baadaye alikuja kuwa raisi wa Marekani.

Hata kwenye utaratibu wa kidunia, hamu ya kutumika huleta kuinuliwa. Hali hii hutambulika kwenye baadhi ya vyeo. Kwa mfano, nafasi ya juu katika serikali ya Uingereza ni Waziri Mkuu, ambalo kwa maana iliyo wazi ni “mtumishi wa kwanza.” Viongozi mashuhuri katika historia wamekuwa ni wale ambao wamekuwa wakitumika kwa ajili ya mahitaji ya watu. Viongozi wa dunia siyo wakati wote wanawahudumia watu kwa nia sahihi, lakini mfuasi wa Yesu atapaswa kipekee awe na moyo wenye kutamani kutumika.

Mkuu wa chou alifika ofisini kwake akiwa na mifuko kadhaa. Alipomwambia mwanafunzi mmoja amsaidie, yule mwanafunzi alimjibu, “Mimi siyo mtumishi.” Mara mwanafunzi mwingine akasema, “Ninaweza nikakusaidia; Mimi ni mtumishi. Miaka mingi baadaye ikapita, yule mwanafunzi wa pili aliyetoa msaada alikuja kuwa Mkuu wa kile chuo.