Nguvu ya Kusadikisha
Kusadikisha kwa uhakika ni kuhusu ukweli. Mambo ya kusadikisha ni mambo thabiti ya imani yanayohusiana na uhalisi. Kusadikisha kunaongoza maamuzi yetu, kwa sababu mtu hutenda kama uwajibikaji katika kile anachoamini kwamba ni cha ukweli.
Kusadikisha hakurejei tu kwenye ukweli wa kidini. Ikiwa muuzaji anaamini kwamba bidhaa yake ni bora kabisa kuliko nyingine na kwamba inahitajika au inatakiwa na kila mtu, ana kusadikisha. Kusadikisha kutamfanya mtu huyo awe na uwezekano mkubwa wa kuwashawishi watu wengine.
Kundi la watu lilipotea jangwani. Wakazungumzia kuhusu hali yao na chaguzi zao. Mtu mmoja ni msadikishaji wa hali ya juu katika maelezo yake kuhusiana na hali yao. Mtu huyo akaweza kuwashawishi kwamba anajua ni jambo gani wanapaswa walifanye. Akawa kiongozi.
Kusadikisha unaweza ukawa mbaya. Mtu anaweza akaamini mambo ambayo siyo ya kweli. Hata usadikishaji mbaya unatoa mamlaka kwa kipindi cha muda fulani. Kwa mfano, kama mtu kwa makosa anaamini kwamba anajua upande wa kuelekea mahali fulani, watu wanaweza wakamfuata kwa sababu ya usadikishaji wake. Hatimaye watakuwa wamekataa tamaa, na ushawishi wake utapungua kwa kiasi kikubwa sana. Wana uwezekano mdogo sana wa kutoweza kumfuata tena.
Uongozi unategemea imani thabiti, kwa sababu kiongozi huwaongoza wengine kwa kuwaonyesha ukweli na kuwaonyesha mwitikio unaofaa kwa ukweli huo. Anasema, "Hivi ndivyo ilivyo, na hivi ndivyo tunavyopaswa kufanya.".
Ikiwa mtu yuko kwenye jengo lililofurika watu na akatambua kwamba jengo hilo linawaka moto, anajua kwamba kila mtu atahitaji kuusikia ukweli na kuchukua hatua kutokana na ukweli huo. Anao usadikishaji wa kushirikisha. Taarifa inahamasisha kitendo kutoka kwa kila mtu anayeiamini. Kwa sekunde chache sana, mtu huyo ni kiongozi kwa sababu anawashawishi kwa kuwasilisha usadikishaji wake. Hataendelea kuwa kiongozi hadi pia pale watakapoamini kwamba anajua kwa uhakika jambo ambalo wanapaswa walifanye. Uongozi wake unaishia pale usadikishaji wake utakapokoma.
Kwa Mkristo, ukweli wa Neno la Mungu na mapenzi yake kwetu unapaswa uwe ndiyo msingi katika kila eneo, na siyo tu kwa ajili ya mashirika ya huduma. Mkristo hapaswi kufanya biashara ambayo iko kinyume na Neno la Mungu.
Imani thabiti ni muhimu kwa uongozi imara. Fikiria kiongozi yeyote mashuhuri, iwe kutoka katika Maandiko au katika historia ya baadaye. Jaribu kumwazia bila imani thabiti, hata akiwa na uwezo mkubwa. Hata kama mtu ni mratibu mzuri na mwasilishaji mahiri, hawezi kuongoza kwa muda mrefu bila imani thabiti.
Kwa kila mmoja wa viongozi hawa kutoka katika historia, ruhusu mtu kutoka katika kikundi aelezee kuhusu kiongozi huyu, kisha uliza kikundi kijaribu kumfikiria huyo kiongozi kana kwamba hakuwa msadikishaji mwenye nguvu: Musa, Yoshua, Paulo, Martin Luther, Abraham Lincoln, Mahatma Gandhi, Winston Churchill, na Billy Graham. (Kila mmoja katika hawa alikuwa na ushawishi mkubwa sana, lakini siyo wote waliokuwa viongozi wa Kikristo.)
Kusadikisha, na siyo mafanikio, kunapaswa kuwe ndiyo uendeshaji mkuu wa Kiongozi. Analazimika kufanikiwa kwa sababu ya kusadikisha ukweli. Kwa hiyo, kamwe hatakubali kuwa na mwafaka au makubaliano ya kuulegeza usadikishaji wa ukweli kwa ajili ya mafanikio.
Kusadikisha hakupaswi kuwe ni kwa muda au kujifanya. Kama mtu yuko tayari kubadili usadikishaji wa mambo ya ukweli kwa sababu ya kukodishwa au kulipwa ili kuwakilisha imani zilizo tofauti au kinyume, hawezi akawa kiongozi mwenye nguvu.
Kiongozi anapaswa afahamke na ajulikane kwa ajili ya mapenzi yake ya kupenda ukweli. Kwa kuwa anaongozwa na usadikishaji, siku zote atataka kujua ni lipi jambo la ukweli. Atakuwa tayari kusahihishwa kuliko aendelee kuamini kitu ambacho hakina ukweli
Imani thabiti humfanya mtu kuwa mwenye nguvu zaidi kuliko ambavyo haiba yake ingeweza kumwezesha. Hata mtu anayechukia makabiliano, mabishano, na ukosoaji anaweza kuwa kiongozi kwa sababu ana imani thabiti.
Imani pia humfanya mtu afanye kazi katika kiwango cha juu cha akili kuliko ambavyo angeweza bila hiyo. Kwa "uwezo wa kiakili wa imani," maamuzi mengi hufanywa kwa silika kwa sababu machaguzi fulani hayastahili kuzingatiwa. Hii inamwezesha mtu kuona kilicho sahihi kwa haraka zaidi. Kama ilivyo kwa maarifa au hekima, mtu asiye na imani thabiti ni mpumbavu.
► Je, ni kiongozi gani maarufu unayemjua wewe mwenyewe binafsi? Ni kwa jinsi gani usadikishaji umemsaidia katika kupata nguvu kwenye uongozi wake?
Danieli na baadhi ya Wayahudi walikuwa katika mafunzo ya uongozi kwenye ufalme wa nchi ya kigeni. Ilikuwa ni jambo la muhimu kwake aweze kufanya vizuri na kumfurahisha mkurugenzi wake wa mafunzo, lakini usadikishaji wake ulijaribiwa wakati alipotambua kwamba chakula kile walichotakiwa kukitumia hakikuwa ni kizuri kutumiwa na Myahudi. Watu wengi kwenye hali inayofanana na hiyo hufikia kuafikiana katika kulegeza masharti ya usadikishaji wao kama itaonekana kwao kwamba usadikishaji huo utawashushia hadhi zao.
Mkurugenzi wa mafunzo tayari alishagundua kwamba Danieli alikuwa na roho bora sana. Danieli alimwendea kwa busara sana, kwa unyenyekevu, na akapendekeza watumie kitu kingine mbadala ambacho hakitasababisha kumweka hatarini mkurugenzi. Mungu aliheshimu uaminifu wa Danieli na akampatia mafanikio makubwa sana (Danieli 1:8-15).