Kile ambacho kanisa linahitaji kwa wakati wa sasa siyo mashine zaidi au kitu kingine cha ziada, siyo mashirika mapya au ziada ya hayo, na siyo mbinu mpya, bali wanahitajika watu ambao Roho Mtakatifu anaweza akawatumia—watu wa maombi, watu wenye uwezo mkubwa kwenye maombi. Roho Mtakatifu hatiririki kupitia mbinu zilizopo, bali kupitia watu. Roho Mtakatifu haji juu ya mashine, bali juu ya watu. Roho Mtakatifu haachilii upako wake kwenye mipango, bali kwa watu—watu wa maombi.[1]
► Je, kuna kosa gani ambalo E. M. Bounds anajaribu kulisahihisha kupitia taarifa zilizoko hapo juu?
Kitendo cha maombi hutoa taarifa ya utegemezi kwa Mungu, Mtu ambaye anashughuli nyingi kwenye mambo yake hata akashindwa kuomba anafikiri kwamba kazi yake ni muhimu zaidi kuliko kazi ambayo Mungu ataifanya katika kujibu maombi yake.
Kwa kuwa sisi ni tegemezi kwa Roho Mtakatifu, maombi ni muhimu sana kwetu. Paulo aliwataka watu waombe kwa ajili ya kuieneza injili (2 Wathesalonike 3:1, Wakolosai 4:3, Waefeso 6:19).
[1]E. M. Bounds, Power through Prayer, Accessed from https://ccel.org/ccel/bounds/power/power.I_1.html on January 13, 2023
[1]► Tunajua kwamba maombi ni muhimu kwa mwamini. Je, kuna sababu gani chache za kuomba ambazo ni muhimu kwa mtu ambaye ni mwinjilisi?
Maombi ni muhimu kwa ajili ya mwinjilisti:
1. Mwinjilisti ni lazima awe hai kiroho. Maombi ndiyo pumzi ya roho. Mwinjilisti huwaongoza watu wengine kwenye uhusiano na Mungu ambao tayari yeye anao
2. Mwinjilisti hawezi akadumisha ari kwa ajili ya huduma bila ya kutumia muda wake na Mungu kwenye maombi. Bila ya maombi, mtu anayejaribu kufanya huduma ya uinjilisti atakuwa na motisha potofu (aidha wa kutafuta mafanikio binafsi au kufurahia mabishano).
3. Mwinjilisti ni lazima awe tegemezi kwa Mungu katika kumwonyesha mwenye dhambi kwamba ana hatia na aweze kumpa matamanio yatakayomwezesha kuokoka. Uinjilisti hautegemei nguvu za mwanadamu peke yake. Mwinjilisti anategemea kupata nguvu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Sababu za kufikirika za mwanadamu peke yake haziwezi kumfanya menye dhambi akubali kwamba ni mwenye hatia na atamani kumtafuta Mungu (Yohana 16:8, Yohana 6:24).
4. Mwinjilisti anamtegemea Mungu ili amsaidie kuhubiri Neno kwa ufanisi (Warumi 1:16, Isaya 55:11).
5. Mwinjilisti anahitaji uongozi wa Mungu katika huduma yake (Matendo 11:12).
[1]“Kama matamanio yako ya kusoma yanazidi matamanio yako ya roho za wengine, simama, na omba hadi mtamanio yako kwa ajili ya roho za wengine yatakapozidi matamanio yako ya kusoma.”
- William Smith,
(Mwanzilishi wa
Union Bible College)
Utekelezaji wa Maombi
Maisha Binafsi ya Maombi
Kila Mkristo anapaswa awe mwaminifu katika maombi ya kila siku, na umuhimu ni mkubwa zaidi kwa mtu ambaye anataka kuwa na ufanisi kwenye uinjilisti.
Anapaswa awe na muda wake maalumu kila siku ambao anautumia yeye peke yake na Mungu. Ikiwezekana, anatakiwa akae eneo la peke yake lisilokuwa na mwingiliano wa kitu chochote. Anaweza kuhitajika kuamka mapema sana ili aweze kuomba pasipo usumbufu kabla ya ratiba ya shughuli za kila siku haijaanza. Kama hawezi kufanya maombi yake maalumu katika muda wa mapema, anaweza kuchukua muda wa dakika chache kwenye mwanzo wa siku ili kuweza kuzungumza na Mungu.
Anapaswa asome baadhi ya maandiko kila siku na afanye tafakuri ya maandiko hayo, akiomba Mungu atimize ukweli uiloko katika Maandiko hayo kwenye maisha yake.
Ni vyema kuorodhesha mambo ambayo tunapaswa kuyaombea. Vinginevyo, inawezekana tusikumbuke baadhi ya mambo muhimu ya kuombea. Tunatakiwa tuwe tunaomba kwa ajili ya injili ienee duniani kote, hasa katika nchi ambazo Wakristo wako kwenye mateso. Tunatakiwa tuwe tunaomba kwa ajili ya mafanikio ya injili katika nchi yetu wenyewe. Tunatakiwa tuwe tunaomba kwamba kanisa likamilishe mpango wa Mungu wa umisheni kwa ajili ya jamii yetu. Tunatakiwa tuwe tunaomba kwamba Mungu atusaidie binafsi katika kushirikisha injili kwa ufanisi mkubwa.
Orodha pia inamsaidia mtu katika nyakati ambazo ana matatizo endelevu yaliyombana.
Siyo muhimu kutumia orodha ya maombi kila wakati unapokuwa unaomba. Mara nyingine unajisikia kuomba kwa ajili ya mambo fulani, na una uwezo wa kuyakumbuka bila ya kuwa na orodha ya maombi.
► Je, ni mambo gani mengine yanapaswa yawe kwenye orodha ya maombi?
Orodha ya Majina kwa ajili ya Maombi
Orodhesha majina ya watu kumi ambao unajua wanahitaji waokoke. Watu hawa wawe ni wale ambao mara nyingi uko pamoja nao. Jihusishe katika kuwaombea kila siku. Kama Mungu atafungua nafasi zungumza nao; kama hakuna nafasi ya kuzungumza nao, endelea kuwaombea. Kwa mujibu wa ushuhuda wa watu wengine ambao waliwahi kufanya hivyo, kama utafanya hili, kabla ya mwaka mmoja kupita baadhi ya hao watu watakuwa wameokoka.
Wabia wa Maombi
Ni vyema kwa Mkristo kuwa na rafiki ambaye atakuwa akishirikiana naye katika maombi mara kwa mara. Watapaswa washirikishe mahitaji na ushindi kwa pamoja. Wanaweza wakakutana kila wiki, au mara nyingi zaidi.
Kwa njia hii mume na mke wanaweza kushirikiana kuomba pamoja; lakini ni jambo jema zaidi kwa mwanamume kuwa na mwenzake wa kiume katika maombi, na mke akawa na mwanamke mwenzake wa kuomba naye kama mbia wake wa maombi.
► Je, ni uzoefu gani walio nao washiriki darasani katika kuwa na wabia wa maombi?
Matembezi kwa ajili ya Maombi
Kutembea katika maombi kunaweza kufanyika kwa sababu ya huduma kujisikia inawajibika kwa ajili ya majirani wanaowazunguka. Kikundi au watu binafsi wanaweza kuwa wanatembea kwenye eneo husika wakiwa wanaomba kwa ajili ya mahitaji ya eneo hilo. Maombi yanaweza kuwa ni ya kimya kimya. Wanaweza kuzungumza na watu wanaokutana nao, lakini kusudi la msingi la matembezi hayo ni maombi. Matembezi kwa ajili ya maombi yanaweza yakafanyika mwanzoni mwa huduma katika eneo husika au yanaweza yakafanyika baadaye.
Kituo cha Maombi
Baadhi ya makanisa yameanzisha vituo vya maombi vya muda kwenye maeneo ya wazi ambayo watu wengi wanapita. Wanaweka hapo ishara inayosema “Kituo cha Maombi” na wanajitolea kuomba na watu wanaopita eneo hilo. Wanauliza, “Je, unalo hitaji ambalo ungetaka mimi niombe kwa ajili yake?” Onyesha kuwa mtu unayehusika na mahitaji ya watu na siyo kuanza mabishano. Mara nyingi huwa wanapata nafasi ya kushiriki injili.
► Je, ni eneo gani linafaa kwa ajili kuweka kituo cha maombi katika eneo lako?
“Watu ambao kwenye mabega yao yalibeba wajibu wa msingi wa kuifanya dunia iwe ya Kikristo walikuja kwa Yesu wakiwa na ombi moja kuu. Hawakusema, ‘Bwana, tufundishe kuhubiri,’ au ‘Bwana, tufundishe jinsi ya kufanya miujiza,’ au ‘Bwana, tufundishe jinsi ya kuwa na hekima’ lakini walisema, ‘Bwana tufundishe jinsi ya kuomba.’”
- Billy Graham
Maombi ya Kibiblia
Maombi aliyoomba Yesu pamoja na mitume yanatuonyesha kwamba tunapaswa kuomba, kwa sababu tunajua kwamba waliomba katika mapenzi ya Mungu. Hapa kuna mifano mitatu:
Sala ya Bwana: Katika Mathayo 6:9-13, Yesu alitoa mfumo wa maombi kwa wanafunzi wake. Tunapaswa tuombe kwa maneno haya, lakini pia tunapaswa tuombe kwa ujumla pamoja na vipaumbele hivi.
Maombi ya Paulo kwa Waefeso: Katika Waefeso 3:14-19, Paulo aliomba kwa ajili ya kufanywa imara kwa waamini. Tunapaswa tuombe maombi hayo hayo kwa ajili yetu wenyewe na watu wengine.
Maombi ya Mavuno: Katika Mathayo 9:36-38, Yesu alitaka wanafunzi wake kushirikisha huruma zake kwa wenye dhambi na kuomba kwamba Mungu atume watendakazi kwenye mavuno ya kiroho
Utekelezaji wa Kufunga
Kufunga ina maana ya kuweka mtazamo wetu kwenye mambo ya kiroho na ya milele, mbali na mambo ya kimwili na yale ya muda mfupi yanayopita. Kufunga kunadhihirisha kwamba mambo ya kiroho na ya milele ni muhimu zaidi kuliko mambo ya kimwili na yale ya muda yanayopita. Hii ni njia mojawapo ya kuimarisha imani yetu.
► Je, Ni kwa jinsi gani kufunga kuna tofauti na mtu anayejitesa kwa njaa ili kumshawishi Mungu amtendee jambo fulani?
Mifano ya Kimaandiko kuhusiana na Kufunga
Hii ni mifano iliyo kwenye kumbukumbu za Maandiko katika nyakati ambazo mtu alikuwa na dhamira kubwa ya Mungu kuingilia kati katika maisha yake ambayo ilimsukuma kufunga. Mifano hii imechaguliwa miongoni mwa mifano mingi ya kurejelea katika Maandiko ili tu kuonyesha kwamba Biblia kwa kawaida hupendelea kuzungumzia kuhusu kufunga. Katika Maandiko, mara nyingi yametajwa kama sehemu ya maelezo ya ni kwa nini Mungu aliingilia kati.
► Soma mojawapo ya haya Maandiko kuhusiana na kufunga na wajadili mazingira yaliyoelezwa katika kifungu hicho.
Maandiko
Matokeo ya Kusali na Kufunga
2 Mambo ya Nyakati 20
Kufunga kwa taifa zima kulileta ushindi kwenye vita.
Ezra 8:21
Ezra alifunga na kuomba ili kuomba ulinzi wa Mungu kutoka katika hatari.
Esta 4:16
Wayahudi walifunga kwa ajili ya Mungu kuingilia kati katika mpango uliokuwa umeandaliwa wa kuwaangamiza kwa mauaji ya kimbari.
Yona 3:5-9
Ninawi walifunga kwa ajili ya kuomba rehema ya Mungu.
Waamuzi 20:26
Israeli ilifunga kwa ajili ya kupata mwongozo wa Mungu katika vita.
1 Samweli 7:6
Israeli ilifunga kwa ajili ya msamaha na ukombozi.
Nehemia 1:4
Nehemia alifunga kwa ajili ya kumwomba Mungu awawezeshe kulijenga jiji kwa upya tena.
Danieli 9:3
Danieli alifunga kwa ajili ya ukombozi wa Israeli kutoka utumwani.
Yoeli 2:12
Kufunga kuliitishwa kulikoambatana na kuomba masamaha na kuepukana na hukumu.
Mathayo 4:2
Yesu alifunga kwa siku arobaini (40) kwa ajili ya maandalizi ya huduma yake hapa duniani.
Luka 2:37
Anna alikuwa nabii wa kike aliyeutumia muda wake mwingi katika kufunga na kuomba.
Matendo 10:30
Kornelio alikuwa katika hali ya kufunga wakati alipopokea ujumbe kutoka kwa Mungu.
Matendo 13:2-3
Wakiwa katika kufunga, kanisa liliagizwa na Mungu litume wamishenari.
Matendo 27:21
Paulo alifunga na kuomba katika nyakati za migogoro.
Maelekezo ya Yesu
Yesu alisema kwamba wanafunzi watapaswa kufunga wakati atakapokuwa hayupo tena pamoja nao kimwili (Mathayo 9:15, Luka 5:33-35). Aliwaelekeza njia sahihi ya kufunga. Alisema kwamba kufunga kusingepaswa kuwe ni onyesho la watu wengine kuona.
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi (Mathayo 6:16-18).
Mifano ya Kihistoria kuhusiana na Kufunga
Baadhi ya waamini katika kanisa la kwanza walifunga kwa kutokula mlo mmoja kila Jumatano na Ijumaa ya wiki, mbali na siku za kufunga zilizokuwa zimeratibiwa katika mwaka. Martin Luther, John Calvin, John Knox, Jonathan Edwards, Charles Finney, na D. L. Moody wote kwa pamoja walifunga sana. Kila uamsho uliokuwa na mwisho mwema wa mafanikio muhimu ulianza kwa maombi na kufunga.
► Je, ni watu gani unaowajua ambao walishawahi kupata matokeo mazuri kutokana na kufunga?
Udhaifu wa Kanisa la Sasa
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba walikuwa wameshindwa kumsaidia mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo kwa sabau ya kutokuamini kwao. Kisha baadaye akasema, "Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga” (Mathayo 17:21). Alimaanisha kwamba maombi na kufunga ndio njia ya kuimarisha imani; Na, kwa hiyo, ndiyo tiba ya kutoamini. Hakumaanisha kwamba wanafunzi wataanza tu kufunga wakati kunapojitokeza mgogoro; alimaanisha kwamba maombi na kufunga mara kwa mara kunapaswa kuwe ni sehemu ya maisha yao, ili waweze kuwa na imani inayohitajika kwa ajili ya kukabiliana na migogoro.
Tukitafakari kutokana na maneno ya Yesu na kutokana na mifano mingi ya kimaandiko na kihistoria, tunaweza tukatengeneza umbo la mchoro wa baraka zetu zinazopatikana kwetu kwa kuwa na mchoro wa pembe tatu iliyogawanyika katika viwango (ngazi) kadhaa. Viwango vya chini vya baraka vinaweza kupatikana kutokana na kiwango cha imani tuliyofikia katka maombi peke yake. Viwango vya juu vya baraka vitapatikana tu kutoka kwenye imani iliyofikiwa kupitia katika maombi na kufunga kwa tukiwa pamoja.
Jinsi ya Kufunga kwa Usahihi
Changanya kwa pamoja maombi na kufunga ili kwamba kufunga kusiwe tu ni kitendo cha nje, bali kufanywa upya kiroho na kufanya imani yao kuwa endelevu.
Funga kwa madhumuni ya kumtukuza Mungu na siyo kwa ajili ya majivuno.
Wakati unapokuwa unaomba na kufunga, tafuta mapenzi ya Mungu kuhusiana na hitaji lako.
Usifanye utiifu kuwa ni mbadala wa kufunga.
Usiuumize mwili wako.
► Jadili tendo la kufunga na kuomba vitakavyoweza kufanyika kwa pamoja.
Usalama wa Kufunga
Kufunga haina madhara ya afya kama ikifanywa kwa njia iliyo sahihi. Kwa kweli, kuna faida nyingi za kiafya zinazoambatana na kufunga mara kwa mara.
Kunywa maji wakati wa kufunga. Usifunge kunywa maji.
Anza kwa kufunga mara moja. Hatua kwa hatua ongeza vipindi virefu zaidi vya kufunga. Kuwa na wiki moja la kutumia chakula kikawaida kati ya siku moja ya kufunga au zaidi.
Vipndi vya kichefuchefu na maumivu ya kichwa ni jambo la kawaida kwa watu ambao hawana uzoefu wa kufunga. Kama mtu alie na afya njema akifunga mara kwa mara, hataweza kuwa na dalili hizo baada ya siku chache za mwanzo. Ladha mbaya kwenye mdomo na harufu mbaya huja wakati wa kupumua kwa sababu mwili unatoa sumu zilizoko kama uchafu.
Kwenye ufungaji wa muda mrefu, wingi wa dalili za kutojisikia vizuri hutoweka baada ya siku chache.
Unapotoka katika kumaliza mfungo wa muda mrefu anza kwa kutumia juisi, kisha chakula chepesi.
Kazi za Kufanya
(1) Fikiria ni nini utakachofanya katika kuendeleza uzoefu wako mwenyewe wa maombi. Chagua muda na kiwango cha muda utakachokitoa kwa ajili ya maombi ya kila siku. Fikiria kuandaa ratiba yako ya kufunga mara kwa mara.
(2) Soma vifungu viwili vya Maandiko kutoka katika vifungu vya kufunga. Andika aya moja nzuri kwa kila aya, ukielezea mazingira na matokeo ya kufunga.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.