Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 17: Kuelekea Kukua Kiroho

12 min read

by Stephen Gibson


Huduma ya Kufundisha ya Kanisa

Wakati wa kipindi cha mtu kuokoka mabadiliko mengi hutokea. Mtu aliyebadilika na au kuokoka anakuwa na matamanio mapya na vipaumbele vipya—mabadiliko hayo ni makubwa sana kiasi kwamba Biblia inamwelezea huyu mtu kama “uzao mpya” (2 Wakorintho 5:17).

Lakini baadhi ya mambo huchukua muda kutokea. Mtu aliyebadilika na au kuokoka hawezi kuona kwa mara moja jinsi ya kutumia kanuni za Kikristo katika maeneo yote ya maisha yake. Atapaswa ajifunze hizo kanuni, na kisha aangalie jinsi ya kuzitumia.

Kunakuwepo pia na mchakato binafsi wa kukua kiroho. Mtu aliyebadilika na au kuokoka anakuwa ni “mtoto mchanga ndani ya Kristo.”

► Soma 1 Wakorintho 3:1-2. Je, kwa mujibu wa aya hizi, mtu aliyeokoka anafanana sana na nini?

► Soma Waebrania 5:13-14. Je, maziwa yanayozungumziwa katika aya hizi ni ya namna gani? Je, chakula kigumu ni nini? Je, tabia ya mtu anayekua kiroho ikoje?

Mapema kwenye kozi hii, tuliangalia kuhusu Agizo Kuu la Yesu ambalo alilitoa kwa kanisa. Tulipitie tena kwa mara nyingine.

► Soma Mathayo 28:18-20. Kwenye aya hii, je, ni jukumu gani Yesu alilolitoa zaidi ya uinjilisti?

Kabla ya kutoa Agizo Kuu, Yesu alitamka kwamba amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kisha akalipa kanisa jukumu la kuwaleta watu watakaokuwa watiifu kwenye mamlaka yake.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa wasihubiri tu injili, bali wafundishe pia na mambo yote ambayo alikuwa amewaamuru. Uinjilisti ni sehemu moja tu katika haya majukumu. Kuwafundisha watu waliookoka kutii maagizo yote ya Yesu ni mchakato wa ufuasi. Ubaya wa kushindwa kufanya ufuasi ni sawa na ule ule kama wa kushindwa kufanya uinjilisti.

Huduma ya ufundishaji ya kanisa ni kwa ajili ya kuwaleta waliookoka kwenye kukua kiroho.

Kwenye Waefeso tunaelezwa kwamba Mungu huwaita watu kwa ajili ya makusudi maalumu ya huduma kwa lengo la kuwajengea uwezo watu waliokoka ili wasiendelee kuwa watoto wachanga (Waefeso 4:11-14). Matokeo ya kufikia ukomavu wa kiroho wa utu uzima unatokana na uthabiti wa mafundisho ya imani.

Mchungaji ndiye mhusika mkuu wa huduma ya ufuasi. Paulo alimwambia Timotheo, “ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha” (1 Timotheo 4:13). Kimsingi hakuwa anarejelea kwa Timotheo kujifunza binafsi; alikuwa anazungumzia kuhusu huduma. Huduma ya Timotheo ilikuwa ni kuelekeza kwenye kusoma na kufafanua maandiko, kutoa mwelekeo wa kiroho, na kufundisha mafundisho ya imani ya Kikristo. Sifa mojawapo ya mchungaji ni kuwa na uwezo wa kufundisha (1 Timotheo 3:2).

Kwa kuwa kujifunza ni sehemu mjawapo ya mageuzo ya kiroho, kufundisha ni sehemu ya huduma ya ufuasi. Waalimu ni muhimu sana katika kanisa, na kanisa ni lazima liwe na wajibu wa kuwaendeleza waalimu.

"Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2 Timotheo 2:2). Maelekezo haya yalitolewa na Paulo kwa Timotheo, kutokea kwa mwinjilisti na mchungaji mzoefu kwenda kwa mtoa huduma mchanga. Paulo alikuwa na wasi wasi kama imani inaweza kuwa ya kuachizana kwa mahubiri peke yake. Watu binafsi watahitajika wapewe mafunzo kwa jitihada maalumu na wawe tayari kwa ajili ya kusaidia watu wengine. Kama mafunzo hayo hayataweza kukamilishwa kwa kuhubiriwa kwenye kusanyiko la washirika, “watu hawa waaminifu” watapaswa wahudumiwe kibinafsi au kwenye vikundi vidogo.

[1]Kuna mafundisho mengi yanayotakiwa kufundishwa. Je, mchungaji anao muda wa kuyafanya haya yote, hasa ikizingatiwa kwamba siyo kila mtu aliye na utayari wa kupokea maagizo yanayofanana kwa wakati mmoja? Lakini katika Waefeso 4:11 haijasemwa, "alimpa mchungaji" (mtu mmoja tu na jukumu moja tu). Badala yake, kuna majukumu mengi na watu kadhaa kwa ajili ya kuyafanya. Mungu anawaita waalimu, anawapa uwezo wa kufundisha, na anawawezesha kupitia katika kanisa kwa ajili ya huduma ya kufundisha.


[1]

“Lengo la awali la mpango wa Yesu lilikuwa ni kuwa na orodha ya watu ambao wangekuwa mashahidi wa maisha yake na ambao wangeubeba mzigo wa kazi yake baaada ya kuwa amerejea mbinguni kwa Baba.”

- Robert Coleman, The Master’s Plan