(1) Kipange kikundi kiweze kukutana kila wiki, kama itawezekana. Wengine wanaweza wakahitaji msaada kwa ajili ya malezi ya watoto wao wachanga.
(2) Mtiririko wa vikao utakuwa kama ifauatavyo: (1) Muda wa kujifunza, kisha, (2) Kushirikishana mahitaji mbalimbali ya kuombea, kisha, (3) Maombi. 
Kama msingi mkuu wa kikundi ni kujifunza, muda wa kujifunza unaweza ukawa mrefu na sehemu nyingine zikawa fupi; lakini sehemu hizi tatu ni lazima zihusishwe. Kama kusudi la kikundi ni kwa ajili ya uwajibikaji wa kiroho, muda wa kujifunza utapaswa uwe mfupi, lakini watakuwa wanazo nyenzo nyingine za mafunzo ambazo wanajifunza.
Kama kikundi kina mambo binafsi ya kushirikishana na kujadiliana lakini hakuna vifaa vya masomo yeyote ya kujifunza, inawezekana kukawa na kutoelewana. Kikao kitatawaliwa na baadhi ya washiriki walio na haiba kuzidi wengine. Vifaa vya kujifunzia huwafanya watu wote washughulike zaidi na ukweli kuliko yale waliyo nayo kwenye mawazo yao.
(3) Anza na kumaliza kikao katika muda uliopangwa. 
Kama utaanza na kumaliza vikao kwa kuchelewa, wale wanaojali muda wao wataanza na wao kuja kwa kuchelewa au kukwepa baadhi ya vikao.
(4) Weka muda wa kusitisha kikundi. 
Washirika wa kikundi watahitaji kujua ni kwa muda gani wataendelea kuwepo kwenye kikundi. Kwa kawaida washirika wapya wasiruhusiwe kujiunga na kikundi baada ya kuwa kumefanyika vikao kadhaa, labda iwe kikunda kina mzunguko wa masomo kwa ajili ya waamini wapya. Kama kikundi kinajifunza mafunzo ya mzunguko ya mfululizo wingi wa masomo unaweza kuwa kipimo cha wiki ambazo wataweza kukutana. Kama wanakutana kwa ajili ya uwajibikaji wa kiroho, wanaweza wakajiwekea kiwango cha miezi sita. Wakifika mwisho, wataanda tena upya. Kwa wakati huo baadhi ya washirika katika kikundi wanaweza wakaondoka, na kikundi kinaweza kikafikiria tena aidha kuwaingiza au kutowaingiza washirika wapya kujiunga.
(5) Wakati wa kujifunza, sisitiza kuhusu kusudi linalobadilisha maisha badala ya maarifa kama maarifa. 
Mshirika wa kikundi atajihisi kwamba kikundi kinafaa kama atapata kitu cha kipekee cha kutumia katika Maisha yake binafsi kutoka katika mafundisho.
(6) Kufuatilia ahadi.
Kama mtu ameshirikishana tatizo lake kisha akakubali kuchukua hatua, uliza kwenye kikao kinachofuata endapo kama amefanya kama alivyoahidi kwamba atafanya.
(7) Kiongozi anapaswa kupatikana ili kukutana binafsi ili kutoa maelekezo ya kiroho. 
Washirika wengine mara nyingine wanaweza wakakaa pamoja kwa ajili ya kutiana moyo.
(8) Chagua eneo zuri la kufanyia kikao. 
Mahali pa kufanyia kikao pasiwe mahali rasmi lakini pawe ni eneo lenye mazingira ya nyumbani. Kikao kifanyike katika mazingira ya mkao wa mviringo kwa kadri inavyowezekana kusudi kila mshirika wa kikao aweze kumwona mwenzake usoni. Hali hii itamtia moyo mshiriki. Kikao kifanyike mahali ambapo hapatakuwa na usumbufu au vikwazo.
(9) Jenga tabia nzuri za kusikiliza. 
Ishara za kusikiliza vizuri ni kwa macho kukutana, kujieleza kwa hisia, kupuuzia usumbufu, na kuwa na mwitikio kwa ucheshi wa mnenaji na hisia zingine.
(10) Hakikisha hakuna mshirika wa kikundi ambaye kila siku ananyamaza bila kuongea chochote. 
Elekeza swali kwa mtu ambaye siyo mwongeaji sana katika kikao (“Charles, unafikirije kuhusu suala hili?”).
(11) Usimlazimishe mshirika wa kikundi kushirikisha kitu chake binafsi. 
Badala yake, tengeneza mazingira ambayo atajisikia huru kuongea. Jenga ujasiri wa mshirika wa kikundi kwa kumtazama machoni na kumpongeza kwa kile atakachosema.
(12) Jaribu kuuliza maswali watakayoweza kujibu ili kujenga ujasiri wao. 
Kama mtu atatoa jibu lisilo sahihi, jaribu kuthibitisha kitu kizuri kilichoko kwenye jibu lake kabla ya kufanyia tahakiki jibu lake.
(13) Jaribu kuthibitisha kila ushauri unaotolewa kabla ya kuanza kusahihisha
(14) Kama kuna mtu wa kuzungumza sana na kutaka kujibu kila swali, tafuta namna ya kumthibiti. 
Njia mojawapo ya kuweza kufanya hivyo ni kuelekeza maswali kwa baadhi ya washirika wengine wa kikundi waliopo. Au unaweza kuuliza, “Je, ninyi wengine mliobakia mnasemaje?” Kwenye majadiliano, unaweza ukasema, “Tusikilize kutoka kwa mtu mwingine ambaye hajaongea kabisa kuhusu jambo hilo.”
Kama bado mshirika huyo anaendelea kuongea sana, kiongozi anaweza kumwomba atoke naye nje ya eneo la kikao kwa mazungumzo. Anaweza akakuambia jambo kama hili, “Charles, wewe ni mtu unayefikiri kwa haraka na una uwezo wa kuingilia jambo lolote kwa haraka kwenye majadiliano, lakini ninajisikia kwamba wengine wetu hawataweza kushiriki kama tutajibu kila kitu kwa haraka. Je, unaweza kunisaidia kumfanya kila mmoja aweze kuhusika?”
(15) Usiruhusu washirka wengine wawili au watatu kuwa na vikao vyao vya chini chini huku wakipuuzia kikundi. 
Kama kuna mtu ambaye anataka aendelee na kubishania kuhusu jambo fulani, mwambie kwamba majadiliano yatakamilishwa baadaye nje ya kikao.
(16) Usiruhusu mtu mwingine aingilie kati ili awavuruge wasemaji wengine. 
Nyoosha mkono wako, na mzuie kwa dhati yule mtu anayeingilia kati kuvuruga, na ruhusu msemaji wa kwanza aendelee kuzungumza hadi kumaliza. Vinginevyo, majadiliano wakati wote yatakuwa yanatawaliwa na watu wachache wasiokuwa na maadili. Watu ambao hawana uthabiti wa mambo, watajisikia kufadhaishwa kwamba wanashindwa kumalizia sentesi zao katika majadiliano hayo.
(17) Sikiliza malalamiko. 
Lalamiko lolote linaweza kuonyesha tatizo ambalo linaweza kurekebishwa. Usipuuzie hali zinazojitokeza za kuonyesha kutoridhika. Kama mtu ataonyesha kutoridhika na kikao hicho cha kikundi, hataweza kuelewa kusudio, au inawezekana akawa na lalamiko sahihi na lenye sababu thabiti.
(18) Endapo mshirika wa kikundi anaonyesha uadui, kuchafua, ubishi, anaweza kuwa hakubaliani na malengo ya kikundi. 
Kikundi kinaweza kisifikie kuwa pale kilipokuwa kimekusudiwa. Zungumza na mtu huyu pembeni umsaidie aweze kuliona kusudi la kikundi.
(19) Kiongozi siyo lazima awe na jibu la kila tatizo. 
Dhima ya kiongozi siyo kuwa na jibu la kila tatizo bali ni kukiongoza kikundi kubeba mizigo yao katika maombi.
(20) Kuwa mtu mwenye uwezo wa kubadilisha mipango na mvumilivu wakati ratiba inapovurugika. 
Kumbuka kwamba matukio mengi katika maisha yetu ni sehemu ya mpango wa Mungu wa maendeleo kwa ajili yetu. Tatizo linaleta uwepo wa fursa nyingine.
(21) Kama mshirika wa kikao mara kwa mara atakuwa anataka akifanye kikao chote ni cha kushirikisha mahitaji yake, mpatie siku nyingine ya kumpa ushauri.
Vinginevyo, washirika wengine katika kikundi watajihisi kwamba wanapokonywa kikao chao. Usitoe fursa kwa kikundi kupoteza kusudi lake, labda iwe washirika wote wa kikundi wamekubaliana kwa pamoja kwamba kusudi hilo linapaswa libadilishwe.
(22) Usiruhusu majadiliano yawe ya kichochezi. 
Usitoe fursa kwa kikundi kuwa ni jukwaa la kutolea lawama dhidi ya kanisa la mahali pamoja na viongozi wa aina zote.
(23) Kumbuka kwamba ufanisi wa kikundi unategemea sana nguvu za Mungu zinazofanya kazi kupitia katika kikundi hicho.
Kikundi ni muundo tu wa kimaandiko ambao Mungu anautumia.