Kanisa la Kiinjili ni kanisa ambalo hufundisha injili ya kimaandiko kuhusiana na wokovu kwa neema peke yake na kwa kupitia imani peke yake. Hakuna matendo yeyote mema ya kibinadamu yaliyoongezwa kwenye upatanisho wa Mungu na binadamu kwa maisha na kifo cha Kristo ambayo yanaweza kutusaidia sisi kustahili wokovu.
Kutangaza injili ya kweli ni kipaumbele cha kwanza cha kanisa la kiinjili kwa sababu watu ambao huiamini injili wanajua kwamba ni jambo muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Injili ni hazina maalumu iliyokabidhiwa kwa kanisa na Mungu kwa minajili ya kuushirikisha ulimwengu.
Kuna tabia ambazo zinafanana baina ya makanisa mengi ya kiinjili. Tabia hizi zimeorodheshwa katia aya chache zifuatazo.
1. Watu wa injili huamini katika mamlaka kamili ya Biblia. Kukataa mamlaka kamili ya Biblia ni kuifanya injili iwe ya hoja nyingi.
2. Watu wa injili (evangelicals) huamini katika historia, na imani za msingi za Ukristo. Kuzikataa imani hizi ni kukinzana na injili. Kwa mfano, madhehebu yanayokataa uungu wa Yesu yanakataa pia kwamba kazi ya upatanisho wa Mungu na binadamu kwa maisha na kifo cha Kristo siyo toshelevu kwa ajili ya wokovu na badala yake hufundisha injili ya matendo.
3. Makanisa ya Kiinjili husisitiza uzoefu binafsi wa kiroho. Tabia hii ipo kwa sababu wanaamini katika mabadiliko ya mtu binafsi na imani thabiti. Kwa sababu ya kuamini huku, watu wa injili husisitiza uinjilisti kwa watu wasioamini na mabadiliko ya kiroho kwa walioamini.
► Je, kanisa lako linaelezaje kuhusu tabia hizi? Je, kunazo tabia nyingine zinazoonyesha kwamba injili ni kipaumbele?
Kiini cha Injili
Injili ndio iipayo kanisa dira ya umisheni. Kanisa ambalo kwake injili siyo kipaumbele cha kwanza limesahau kazi ya umisheni iliyotolewa na Mungu.
Tumejifunza kuhusu agizo Kuu la Kristo lililotolewa katika Mathayo 28:18-20. Ni nini msingi mkuu wa umisheni wa kanisa?
[1]Injili hutengeneza kanisa mahali popote inapohubiriwa. Kanisa la kweli kwa mujibu wa historia hupatikana mahali ambapo injili inahubiriwa. Urithi wa kanisa tangu wakati wa mitume hauko kwenye uendelezaji wa taasisi, bali katika uendelezaji wa kuhubiri injili kwa imani.
Taasisi zozote zilizoanzishwa na kanisa zinapaswa zihudumu kwenye kipaumbele cha injili. Kwa mfano, ratiba ya kufundisha wachungaji inapaswa iendane na kuwaandaa katika kuliongoza kanisa kwenye kutimiza umisheni wake kwa ajili ya uinjilisti na ufuasi.
Taasisi zina tabia ya kujitengeneza zenyewe ziendelee kuwepo na kusahau umisheni wao wa asili. Msisitizo mpya unavyozidi kufanywa kwa ajili ya injili siku zote kunasababisha kufanyika kwa mabadiliko mapya kwenye taasisi.
Kanisa hukuza taratibu za imani, aina za kuabudu, maisha ya Kikristo na sera ya kanisa; lakini msisitizo mpya unavyozidi kufanywa kwa ajili ya injili kunasababisha kufanyika kwa mabadiliko ya taratibu husika.
“Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Kristo Bwana na umisheni wa kanisa kwa ajili ya dunia. Hii inajitokeza wazi wazi katika maelezo ya Mathayo kuhusiana na Agizo kuu la Kristo. Liko dhahiri kwa sababu mamlaka yote mbinguni na duniani yametolewa na Mungu Baba kwa Mwanae kwamba kanisa lina wajibu wa kuwafanya mataifa wote kuwa wanafunzi wake.”
- J. Herbert Kane, “The Work of Evangelism”
Mifano ya Kupoteza Kipaumbele cha Injili
Mfano 1
Wakati kanisa linafanya kazi ya kutimiza umisheni wa uinjlisti, ni muhimu kutengeneza mipango, kuandaa timu za kazi, kutengeneza ratiba mbalimbali na kutafuta misaada. Kanisa linaanzisha taasisi za kutumika kwa makusudi ya kuwajibika kivitendo. Mara nyingi, taasisi huundwa wakati wa uamsho wa kiroho wakati watu wanapokuwa wamejikabidhi kutumika kabisa, na kanisa linakuwa limehamasika katika kutimiza umisheni wake.
Uwepo wa taasisi ni muhimu. Taasisi kimsingi ni muundo wa muda mrefu wa watu na rasilimali. Bila kuwepo kwa taasisi, hakutakuwepo na majengo ya makanisa, hakutakuwepo na huduma za nje za kimataifa, hakutakuwepo na uchapishaji wa Biblia au aina nyingine za Maandiko mbalimbali, hakutakwepo na mashule ya Kikristo au ratiba za mafunzo ya elimu, na hakutakuwepo na msaada wa kifedha kwa ajili ya huduma. Hata kanisa la mahali pamoja ni taasisi ambayo haipo hadi kikundi cha watu kitakapojitolea kuwepo kwa ajili yake.
Endapo taasisi itafanikiwa, inaweza kuwa kubwa, kwa wingi wa watu na bajeti kubwa. Kuhakikisha taasisi inaendelea kuwepo kunahitaji nguvu nyingi na gharama za matumizi. Mara nyingine watu wanaofanya kazi kwenye taasisi huanza kujisisikia kwamba jukumu la kuijenga hiyo taasisi ni kipaumbele cha kwanza. Wanafikiri kazi yao ni kuiwezesha taasisi izidi kuendelea kuliko kutimiza lengo la awali la umisheni la taasisi.
Ingawaje uwepo wa taasisi ni muhimu, ni lazima mara kwa mara zifanyiwe tathmini na mabadiliko kutokana na kipaumbele cha injili.
Mfano 2
Kwa kuwa huduma ina uwezekano mkubwa wa kuingiza fedha, baadhi ya watu wameanzisha huduma kama biashara. Siyo vibaya kwa huduma kuuza vitu kwa ajili ya kusaidia gharama za uendeshaji, na pia siyo vibaya kwa huduma kuangalia vianzo vingine vya msaada wa kifedha. Hata hivyo, kama mtu anavutiwa zaidi na mapato ya fedha kuliko kipaumbele cha injili, kusudio la moyo wake limepotoka na kazi yake haimpendezi Mungu (1 Petro 5:1-2, 2 Petro 2:3).
Simoni alikuwa mtu aliyekuwa anataka apate karama ya kiroho ili aweze kuwa mtu mkubwa mwenye hadhi na faida ya kifedha, lakini mtume alimwambia kwamba moyo wake umepotoka (Matendo 8:18-23).
► Je, kuna kitu gani potofu katika hali ya mchungaji anayejaribu kuliuza kanisa lake? Je, kuna kitu gani potofu katika ufahamu wake kuhusu kanisa ni nini?
Mfano 3
Hii ni mchanganyiko wa Ukristo na imani zinazojichanganya na mapokeo kutoka katika dini nyingine. Mfano wake katika nyakati za Agano Jipya ni dini ya Kisamaria. Wageni waliokuwa wakiabudu sanamu waliingia katika taifa la Israeli wakachanganya dini ya wana wa Israeli na sanamu; Yesu akasema kwamba hawajui walichokuwa wanakiabudu (Yohana 4:22).
Mfano, mwingine ni kutoka katika historia ya Haiti. Wakati nchi ya Haiti ilipokuwa koloni la Mfaransa, watumwa kutoka Afrika walitakiwa kuwa wakristo. Walichanganya dini zao za awali na Ukatoliki. Watu wengi wa Haiti hadi leo wanashiriki Voodoo, ambayo ni ibada ya maroho, lakini wakitumia alama za Ukristo na majina ya watakatifu wa kikristo.
Mara nyingine mchanganyo huu wa imani hutokea kwa sababu Ukristo uliambatana na taifa lililokuwa linamilikiwa na taifa lingine. Watu walikuwa wanataka kuliridhisha taifa lililokuwa chini ya umiliki wao, kwa hiyo walikubaliana na mila zao za kidini lakini wakizilinda imani zao za mwanzo.
► Je, umeshawahi kuona mifano gani ya michanganyiko kati ya Ukristo na dini nyingine?
Malengo ya kidunia yanaweza kusababisha kuwepo na michanganyo Kama watu watafikiri kwamba kuikubali injili kutawaletea mafanikio ya kifedha, ushawishi wa kisiasa, au upendeleo kutoka kwa watu wenye ushawishi, wanaweza kukubaliana na mwonekano wowote wa Ukristo bila hata ya kuwa wamebadilika kiukweli. Kisha wataendelea kufuata imani zao za zamani na mapokeo yao lakini wakiziita kwa maneno ya Kikristo. Inakuwa ni vizuri zaidi wakati kanisa linapofanya uinjilisti lisitoe vitu ambavyo vinaweza kusababisha watu wakavipokea kwa malengo potofu.
Ukristo unaonekana kama ni dini ya kigeni wakati injili ilipoletwa na wamishenari wa kigeni. Hata hivyo, ni muhimu kwa Ukristo kuingizwa katika kila mila na kuchukua nafasi ya aina ile iliyoko katika mila hiyo. Haipaswi kuonekana kama ni dini ya kigeni. Hata hivyo, ni muhimu kwa wamishenari na wainjilisti kutambua kuna nini kwa kina kwenye mila ambayo haiwezi kuingiliana na Ukristo. Utambuzi huu ni mchakato ambao ni lazima upate msaada wa Wakrirsto wenyeji na hauwezi kumalizika kwa haraka.
Mfano 4
Mara nyingine dini hufikiriwa kama ni dini iliyoanzishwa kwa ajili ya taifa. Kwa mfano, kwenye baadhi ya mataifa, watu wengi ni Waislamu. Kwenye mataifa mengine, watu wengi wanajinasibu wenyewe kwamba ni Wakatoliki. Watu wengi hawafuati kwa ukweli kabisa viwango vya uadilifu vya dini yao na mara chache sana hutendea kazi mila zo za kidini; lakini wanasema kwamba wao ni wafuasi wa dini hiyo.
Watu wengi wanajiita Wakristo kwa sababu katika mitazamo yao katika jamii watu wote wazuri wanachukuliwa kama ni Wakristo. Kiuhalisia huwa hawajatubu. Wanafuata viwango vyao wenyewe vya uadilifu.
Injili ni wito wa kufikia kwenye toba na kujikabidhi kabisa kwa Kristo. Yesu alisema kwamba mtu hawezi akawa mwanafunzi wake hadi awe amejikana mwenyewe na awe mfuasi wake wa kweli (Luka 9:23).
Tafsiri ya kuwa Mkristo haiwezi ikafanywa kwa kupendwa katika jamii ya watenda dhambi. Hali ya kawaida ya uadilifu ya jamii siku zote iko chini ya kiwango cha uadilifu cha Ukristo, na Mkristo anahitilafiana kabisa na dunia.
► Je, ni kwa jinsi gani Ukristo unaopendwa bila toba mara nyingi unaonekana mara nying katika jamii yako?
Mfano 5
Hatuwezi tukategemea kuona kwamba Wakristo wote wakubaliane katika imani zote. Kuna tofauti miongoni mwa Wakristo, ingawaje wanakubaliana na Biblia kama mamlaka yao kwa ajili ya imani.
Mara nyingine makanisa huwekea mkazo zaidi kwenye imani ambazo zinawatofautisha wao na makanisa mengine, lakini imani hizo siyo muhimu kama imani za msingi za Ukristo. Kanisa haliwezi likasema kwamba makanisa mengine siyo ya Wakristo wa kweli, kama makanisa hayo yanafundisha injili ya msingi.
Kanisa halipaswi kuanzisha utambulisho wake wenyewe kwa kupigana na makanisa mengine. Linapaswa lijitambulishe kwanza kwa njia ya injili, kisha kwa kujenga ushirika wa kikundi cha watu waliojikabidhi kabisa.
► Je, ni kwa misingi gani kanisa linapaswa likubali kanisa lingine kuwa ni la kweli la Kikristo?
Mfano 6
Hata imani ya ukweli inaweza ikawekewa msisitizo sana kiasi kwamba ikaonekana kuhitilafiana na ukweli mwingine. Kwa kuwekea msisitizo wa rehema, kanisa linaweza kuonekana likipunguza kiwango cha uhitaji wa utii kwa Mungu. Kwa kuwekea msisitizo katika kusaidia na kuombea watu kuokoka kunaweza kufanya kusahau mchakato wa kufanya wafuasi. Wakati wa kuweka msisitizo wa uaminifu wa Mungu kwa mtu aliyerudi nyuma kiimani, kanisa linaweza likashindwa kuonya kuhusu hatari ya kuasi imani. Wakati wa kuheshimu karama za kiroho, kanisa linaweza kupuuza undani wa mambo ya kiroho na tabia ya Mkristo.
Hitilafu ya Imani hujitokeza kwa muda fulani na inakuwa na athari za muda mrefu. Fundisho lolote ambalo (1) linasababisha kutoonesha kujali kuhusu suala la dhambi, (2) linapoteza uhakika wa wokovu, (3) linaloongeza ugumu wa ziada katika njia ambayo mtu angeweza kukubaliana na injili, au (4) linaficha usahihi wa injili, hiyo ndio hitilafu ya imani.
Uamsho wa kihistoria na Matengenezo ya Kanisa
Wakati mwingine katika historia ya kanisa injili ilionekana kusahauliwa na taasisi zilizokuwa maarufu. Makosa yaliyokuwepo kama ya kujiimarisha zaidi kwa taasisi, michanganyo, na hitilafu ya imani kulijidhihirisha wazi zaidi kuliko injili. Viongozi walipaswa kuwa mifano ya viongozi wa kiroho, lakini walionekana kuwa wanaoonyesha mtazamo potofu, tabia potofu na kupenda sana mambo ya kidunia.
Mara nyingine Mungu amekuwa akituma uamsho mkubwa sana kwa kanisa. Uamsho wenye matokeo mapana na ya muda mrefu uko katika vipengele vitatu.
1. Kunakuwepo na matengenezo ya kitheolojia, wakati ukweli wa kiroho uliopuuzwa unaporejeshwa tena kwa upya.
2. Kunakuwepo na uhuishwaji mpya wa kiroho, pamoja na maombi kwa wingi, kuabudu kwa hamasa kali, na mabadiliko ya watu kwa wingi.
3. Kunakuwepo na mbinu mpya za huduma, wakati kanisa linapata njia mpya za kufanya uinjilisti na uanafunzi.
Matengenezo ya Kiprotestanti (yaliyofanyika katika Bara lote la Ulaya katika miaka ya 1500) yalikuwa ni kufufua upya injili ya wokovu kwa njia ya neema peke yake na kwa imani peke yake. Maelfu ya watu walibadilika. Maandiko yalitafsiriwa katika lugha mbalimbali na kutawanywa katika maeneo yote husika.
Waanabaptisti (katika Bara lote la Ulaya kwenye miaka ya 1500 na baadaye) walikuwa watu waliohusika sana kwa sababu wafuasi wengi wakati wa matengenezo walidhania kwamba kuamini imani sahihi kulikuwa kunatosha kwa ajili ya wokovu. Watu wengi walikiri kuupokea ukweli wa injili lakini walikuwa hawajawahi kupata uzoefu wa mabadiliko. Wanabaptisti walisisitiza kuhusu mabadiliko ya mtu binafsi.
Watu waliokuwa na uchaji wa Mungu (mwishoni mwa miaka ya 1600 nchini Ujerumani) walikuwa watu waliotambua umuhimu wa kufanya ufuasi. Walianzisha vikundi vidogo vya huduma na mifumo ya kufundisha waamini kwa ajili ya ukuaji wa Mkristo.
Uamsho wa Wamethodisti (mwishoni mwa miaka ya 1700 nchini Uingereza) kulianza na huduma ya John Wesley. Wengi wa makasisi wa Kanisa la Uingereza walipinga kuwepo kwa uwezekano wa uhakika wa wokovu kwa mtu binafsi. Wesley alihubiri kwamba kila mtu anaweza akajijua kwamba anayo imani iliyo hai ndani ya Kristo na uhakika wa wokovu kutoka kwa Roho Mtakatifu.
► Je, ni ukweli gani mkubwa unaohitaji kuwekea msisitizo katika jamii yako?
Hitimisho
Taasisi nyingi za Kikristo, ndogo na kubwa (ikiwa na pamoja na makanisa ya mahali pamoja), yalianza na kujihusisha katika kipaumbele cha injili. Baada ya muda mrefu, mengi ya makanisa hayo yalibadilika na kugeuka kutoka katika kipaumbele hicho.
Ili kufufua upya ufanisi wa kanisa, hatuhitaji imani mpya za ajabu au mafunuo mapya. Tunachohitaji ni urejeshwaji wa kanuni ya kiinjili ya kipaumbele cha injili.
Mtihani
Utaanza kipindi cha darasa kitakachofuata kwa kufanya mtihani unaohusiana na somo la 5. Jifunze maswali ya mtihani kwa uangalifu kwa ajili ya maandalizi.
(1) Je, kuna tabia ngapi tatu za makanisa ya kiinjili?
(2) Je, kuna njia ngapi sita ambazo kanisa linaweza kupoteza kipaumbele cha injili?
(3) Je, kuna ishara ngapi nne kwamba imani ina hitilafu?
(4) Je, ni mambo gani matatu ya uamsho wa muda mrefu?
(5) Andika taarifa ya ukweli kuhusiana na kila kimoja kinachofuata hapa:
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.