Ukumbusho kwa kiongozi wa darasa: Kwa kila kipengele cha Maandiko kilichorejelewa, ruhusu mtu mmoja asome, kisha mchukue mtu mwingine asome ufafanuzi wa kipengele. Acha nafasi kwa darasa lijadili kwa kifupi kila swali la majadiliano.
Vipengele vinavyofuata ni muhimu kwa injili. Inawezekana mtu kuokoka bila ya kuwa amevielewa kikamilifu. Hata hivyo, kupinga mojawapo ya kipengele chochote katika hivi kunaondoa msingi wa injili. Mtu au shirika ambalo linakataa au linapinga kipengele chochote katika hivi itasababisha kutengeneza injili nyingine, ikiwa ni pamoja na kuamini maana iliyo potofu ya wokovu.
Unaposhirikisha injili pamoja na mtu mwingine, vipengele kadhaa vitakuwa ni muhimu hasa kwa sababu ya makosa ambayo tayari anayaamini. Kwa mfano, kama anaamini kwamba wokovu unapatikana tu kupitia shirika au dini fulani, atakuwa ameamini kwamba mahitaji ya kuwa mwanachama wa shirika hilo au dini hiyo ni muhimu kwa ajili ya wokovu. Mtu huyu anahitajika ajue kwamba mtu binafsi hupokea msamaha na mwenyewe kuingia moja kwa moja kwenye uhusiano na Mungu.
(1) Mungu alimwumba mwanadamu kwa sura yake ili Mungu aweze kuwa na uhusiano na yeye (Mwanzo 1:27, Matendo 17:24-28).
Ukwli huu unaonyesha kusudi la maisha yetu na lengo la wokovu. Ukweli huu unapingana na dini ambazo haziamini katika Mungu mwenye sifa za kibinadamu. Ukweli huu unaonyesha tatizo halisi lililopo katika dunia; watu hawako kwenye uhusiano na Mungu.
► Je, itakuwaje kama mtu haamini kwamba Mungu anampenda?
(2) Wanadamu wa mwanzo walitenda dhambi na kutenganishwa na Mungu (Mwanzo 3:3-6).
Hii inaonesha asili ya dhambi na sababu kamili ya hali ya dunia ilivyo. Duniani ni mahali pa mateso na masikitiko kwa sababu ya dhambi. Bado kuna furaha na kusudi kwa sababu ya mpangilio wa Mungu, lakini dunia haiko kama vile Mungu alivyokuwa ameipangilia iwe.
► Je inakuwaje kama mtu hakuamini kwamba dhambi ndiyo tatizo halisi la ulimwengu wote?
(3) Kila mtu anazaliwa akiwa ametengwa na Mungu na kutomtii (Warumi 3:10, 23).
Kila mtu ni mwenye hatia kwa dhambi za kujitakia dhidi ya Mungu. Hakuna hata mtu mmoja ambaye siku zote amefanya yaliyo mema.
► Je, itakuwaje kama mtu atafikiria kwamba anaweza kujihesabia haki kwa mambo aliyoyafanya?
(4) Kila mtenda dhambi ambaye hataki kutafuta rehema atahukumiwa na Mungu na hukumu yake itakuwa ni adhabu ya milele (Waebrania 9:27, Warumi 14:12, Ufunuo 20:12).
Jambo hili linaonesha unyeti na umuhimu wa mtenda dhambi kwa ajili ya wokovu.
► Je, itakuwaje kama mtu hataamini kwamba kuna Mungu mwenye haki ambaye ana hasira kwa ajili ya dhambi zake?
(5) Mtu hawezi kufanya lolote kwa ajili ya kulipia dhambi zake alizozifanya dhidi ya Mungu (Warumi 3:20, Waefeso 2:4-9).
Matendo mema na karama haviwezi kutumika kama ni malipo kwa ajili ya dhambi kwa sababu dhambi ni dhidi ya Mungu wa milele ambaye kila kitu tayari ni mali yake.
► Je, itakuwaje kama mtu ataamini kwamba ana uwezo wa kujifanyia msamaha mwenyewe?
(6) Ni lazima kuwepo na msingi wa msamaha, kwa sababu dhambi ni jambo nyeti na Mungu ni mwenye haki (Warumi 3:25-26).
Mungu huwa anapenda kusamehe; lakini, kama atasamehe pasipokuwepo na msingi, dambi itaonekana ni jambo la kawaida na Mungu ataonekana kwamba siyo mwenye haki.
► Je, kwa nini kifo cha Yesu kilikuwa ni muhimu?
(7) Yesu, Mwana wa Mungu, aliishi maisha yasiyokuwa na dhambi na akafa kama dhabihu ili dhambi zetu ziweze kusamahewa (Yohana 3:16, Waumi 5:8-9).
Kwa kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, dhabihu yake ina thamani ya milele na inatoa msingi wa msamaha kwa mtu yeyote katika ulimwengu huu. Kama angekuwa ni mwanadamu wa kawaida tu, dhabihu yake ingekuwa na thamani ndogo sana yenye mwisho. Damu ya Yesu inawakilisha maisha yake yaliyotolewa kwa ajili yetu. Bila ya damu yake hakungekuwepo na wokovu (Waebrania 9:22). Kama hangekuwa ni Mungu, hangeweza kutuokoa kabisa; na, tungekuwa tunatafuta bila mafanikio, njia nyingine ya kupata wokovu.
► Je, ni kwa nini baadhi ya dini zinafikiri kwamba watu ni lazima waokolewe kwa njia ya matendo?
(8) Yesu alifufuka kimwili kutoka katika wafu, akithibitisha utambulisho wake kama Mwana wa Mungu na akidhihirisha uwezo wake wa kutoa uzima wa milele (Yohana 20:24-28, Ufunuo 1:18).
Madhehebu yanayokataa kwamba Yesu hakufufuka, kwa kawaida pia yanakataa uungu wake na utoshelevu wa dhabihu yake kwa ajili ya wokovu. Kisha, wanaanzisha njia nyingine ya wokovu.
► Je, Ni mambo gani tunayoyajua kwa sababu ya Yesu kafufuka kutoka kwa wafu?
(9) Dhabihu ya Yesu inatosha kwa ajili ya msamaha wa dhambi zote (1 Yohana 1:9, 1 Yohana 2:2).
Kama mtu ataukataa ukweli huu, ataamini injili ya matendo. Dini nyingi zinaamini ujumbe wa jinsi ambavyo mtu anaweza kuupata wokovu kiasi fulani. Hali hii inawaweka watu kuwa chini ya utawala wa shirika la kidini linalowaambia kitu cha kufanya ili waweze kuokoka.
► Je, kwa nini watu wengine wanafikiri kwamba hawawezi kuokoka bila ya shirika lao la kidini?
(10) Mungu husamehe kila mtu ambaye anakiri kwamba ni mwenye dhambi, anayetubu dhambi zake,na anayeamini katika ahadi ya Baba ya kusamehe (Marko 1:15, 1 Yohana 1:9).
Hakuna shirika lolote la kibinadamu lenye haki ya kuongeza chochote kwenye mahitaji ya wokovu au kutoa njia nyingine mbadala ya wokovu.
►Je, ni aina gani ya mtu ana haki ya kuamini kwamba ameokoka?
(11) Toba maana yake ni mtu kujutia dhambi zake na kutaka kwa hiari kuachana na dhambi zake (Isaya 55:7; Ezekieli 18:30; Ezekieli 33:9-16; Mathayo 3:8).
Toba haimaanishi kwamba ni lazima mtu ayafanye maisha yake yawe makamilifu kabla Mungu hajaweza kumkubali; ni Mungu peke yake mwenye uwezo wa kumtoa mwenye dhambi kutoka katika nguvu ya dhambi zake. Toba inamaanisha kwamba mwenye dhambi amejutia dhambi zake na kutaka kwa hiari kuachana na dhambi zake. Kama mtu hataki kuachana na dhambi zake kwa hiari yake, haiwezekani kuokoka. Kama mtu bado anaishi kwenye dhambi kwa makusudi, bado hajaokoka.
► Je, kwa nini toba ni muhimu?
(12) Mwenye dhambi aliyetubu na kuamini hupokea msamaha wakati anapokuwa anaomba kwa Mungu na kumsihi Mungu amsamehe (Warumi 10:13, Matendo 2:21).
Kila mtu anacho kibali cha kupokea moja kwa moja huruma ya Mungu kwa sababu ya Yesu. Hakuna taasisi au wakala ambaye ni muhimu kwa ajili ya mtu kupokea msamaha wa Mungu. Mtu hupokea msamaha wake yeye mwenyewe na kuanza uhusiano wa moja kwa moja pamoja na Mungu.
► Je, tunawezaje kujua kama mtu anaweza kufanyika kuwa Mkristo katika kipindi fulani cha muda?
Kazi za Kufanya
(1) Katika aya chache, elezea ni kwa jinsi gani kipengele kimoja au viwili miongoni mwa hivi vilikuwa ni muhimu sana wakati wa kubadilishwa kwako.
(2) Chagua dhehebu moja au dini moja isiyokuwa ya Kikristo kwa ajili ya kufanyia utafiti. Kwenye kurasa 2-3, fafanua jinsi wanavyokataa baadhi ya vipengele muhimu vya injili. Elezea kuhusu injili potofu wanayohubiri na onyesha ni kwa jinsi gani imejikita katika imani za uongo. Fafanua ni kwa jinsi gani utaweza kuwapa ushahidi wa kibiblia kwa ajili ya ukweli.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.