Eric anapenda kuzungumzia kuhusu miaka ya awali ya kanisa lake. “Tulianza kwa kukutanika kwenye bustani ya kupumzikia, tukimkaribisha kila mtu tuliyemwona. Wakati wa kipindi cha baridi, tulikutanikia kwenye basi mbovu la zamani. Hatukuwa na vyumba vya maliwato. Baadaye, tulihamia katika ukumbi wa michezo ya mazoezi ya viungo kwa muda, kisha tukapangisha nafasi kwenye jengo moja la zamani la kanisa.”
Kanisa la Eric lilikuwa linakua katika miaka hiyo. Watu waliokuwa wamejitoa kwa ajili ya kanisa hawakuwa wamevutiwa na jengo la kanisa. Walikuwa wamevutiwa na kundi la watu.
Kwenye somo hili, tunapozungumzia kuhusu mpango wa kanisa, hatuzungumzii kuhusu jengo la kanisa. Makanisa mengi makubwa wanayo maelezo kuhusiana na jinsi walivyoanza wakiwa katika mazingira magumu.
Baadhi ya makanisa yanasema kwamba hayawezi kuwa kivutio kwa watu kwa sababu majengo yao hayaridhishi kwa uzuri. Ukweli ni kwamba wanakosa kitu kingine ambacho ni muhimu sana kuliko hata jengo.
Wakristo kila mahali hupenda kuwaalika watu wengine wahudhurie kwenye makanisa yao. Wana mategemeo kwamba wageni watalipenda kanisa na watakuwa wanapenda kuendelea kuhudhuria pamoja nao. Wanategemea kwamba wageni watakubaliana na injili.
► Je, wakati unapomwalika mtu kuhudhuria kwenye kanisa lako, mwaliko huo unamaanisha nini? Unatoa nini?
Hatuwakaribishi kuhudhuria kwenye ibada zetu kwa ajili ya mazoezi ya kidini, kana kwamba hilo litatimiza hitaji au kukamilisha wajibu. Hatuamini kwamba kwa kushiriki mila za kidini kutaleta ufanisi wowote kwa mtu ambaye siyo wa imani.
Hatutegemei kwamba wanajua kumwabudu Mungu wakati ambapo bado hawajabadilishwa na au hawajaokoka.
Tunategemea kwamba watapenda upendo wa watu walioko na watataka kuwa pamoja nao tena.
Tunategemea kwamba watakubaliana na injili.
Baadhi ya makanisa wanajaribu kutengeneza programu zao ziweze kuwavutia watu ambao hawana shauku ya kiroho. Wanategemea kwamba kama watu wataifurahia programu yao, watakuwa wanaendelea kuhudhuria kwenye ibada zao. Tatizo ni kwamba kama burudani itakuwa imefanikiwa, inakuwa na mvuto kwa watu wengi ambao hawana shauku iliyo sahihi. Kusanyiko linakuwa la vikundi mchanganyiko ikiwa ni pamoja na watu ambao hawana shauku ya kumwabudu Mungu bali kuburudika na burudani iliyopo katika kanisa. Viongozi wa ibada na wanamuziki wanakuwa ni waburudishaji. Hatimaye, unakuza viongozi wa ibada ambao hawapendi ibada. Kuabudu kunakuwa kumeharibiwa.
► Tafakari swali hili tena. Wakati unapomwalika mtu kuhudhuria katika kanisa lako, unakuwa unatoa nini? Unatakiwa uwe unatoa nini?
Jaribu kufikiria kuhusu mabadiliko makubwa yanayotokea kwa mtu anapokuwa amebadilishwa au kuokoka. Huachana na dini yake ya mwanzo, jambo ambalo linaweza kumtenga yeye na familia yake au marafiki zake. Anatubu dhambi zake, ikimaanisha kwamba atatengana na mambo mengi aliyokuwa amefikiria kwamba yangemfanya awe mtu wa kufurahia. Anajisalimisha kabisa maisha yake kwenye uongozi na mapenzi ya Mungu.
Kwa sababu ya mabadiliko makubwa yanayotokea wakati wa kubadilishwa na au kuokoka, mtu kwa kawaida hakubali kubadilishwa na au kuokoka bila ya kufikiria kuhusu jamii yake atakayoiacha na ile atakayoingia. Kama mtu atavutiwa na ushuhuda wa Mkristo binafsi, anataka kuona jamii ya waaminio ambayo yule Mkristo anaiwakilisha. Atataka aone ni kwa jinsi gani imani inatenda kazi kwa uhakika. Anakuwa na hisia kwamba ujumbe anaousikia tayari umeshatengeneza jamii ya waaminio ambayo ataingia kuwa nayo kama atabadilishwa na au kuokoka. Anakuwa kama anayejiuliza, “Liko wapi kundi la watu wanaouamini ujumbe huu na kuishi kama unavyonena? Itakuwaje kwangu mimi kuwepo kwenye kundi hilo?”
[1]Yesu alihubiri “injili ya ufalme” na mara kwa mara alizumgumzia kuhusu ufalme wa mbinguni. Alisema kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia (Luka 10:9). Watu wanaoingia kwenye ufalme wa Mungu wamekubaliana na uongozi wa Mungu, kuishi kwa mujibu wa sheria zake, na kushiriki maisha pamoja naye. Uaminifu wao kwa Mungu umewafanya wawe familia ya imani.
Kwa kuwa watu wanataka kuona familia ya imani iliyotokana na kuisikia injili, uinjilisti hauwezi kufanywa tu na watu binafsi wakiwashawishi watu wengine binafsi. Hiyo inamaanisha kwamba uwepo wa kanisa la mahali pamoja ni muhimu sana. Kanisa la mahali pamoja linatakiwa liwe la kuvutia kama familia ya imani.
► Je, ni kitu gani mtu atataka kuona kabla hajajiunga kwenye jamii ya imani?
Kanisa lina asili iliyoundwa na Mungu wajibu uliotolewa na Mungu. Kila kanisa la mahali pamoja linatakiwa lifanye vizuri itakavyowezekana kwenye viwango vya Mungu. Hatupaswi kuligeuza kanisa liwe kwa ajili ya shughuli nyingine kwa ajili ya kuvutia watu. Hatupaswi tujaribu kuliwasilisha kanisa kama kitu tofauti na jinsi lilivyo.
Kama kanisa litakamilisha kusudi ambalo Mungu amelitoa kwake, litawavutia watu sahihi ambao wataunda kikundi chenye kumaanisha.
“Yesu alikuwa amejenga muundo wa kanisa ambalo kwa wanafunzi wake lingeleta changamoto na ushindi juu ya mamlaka zote za kifo na Motoni. Ilianza kidogo kama punje ya haraladi, lakini ikakua kwa kimo na nguvu...“
- Robert Coleman, The Master’s Plan
Tabia za Kanisa la Mahali Linalovutia
(1) Washirika huonyesha kwamba uhusiano wao na Mungu ni wa uhalisia na unaotosheleza. Watu wasiookoka hawana uhusiano wowote na Mungu. Mtu atakapoona ni kwa jinsi gani maisha ya kuishi pamoja na Mungu yalivyo, ndipo atakapoona hitaji la kuwa na uhusiano naye. Washirika huonyesha hali hii kwa kutoa ushuhuda wa kufurahia kumjua Mungu na kuishi maisha ya kujikabidhi kabisa kwa Mungu. Kama mshirika atakuwa bado anaishi kwenye dhambi wakati anapokuwa hayupo kwenye kanisa, huyo anaonesha kwamba hajaridhika na Mungu.
(2) Kanisa huwasilisha mafundisho ya imani ya kweli na pia kama masharti kwa ajili ya kuwa na uhusiano na Mungu. Tunafundisha mafundisho ya imani kwa sababu ni kweli, na siyo tu kwamba ni kweli. Fundisho la imani ni kitu ambacho tunahitaji kwa kuwa tunataka tukaishi pamoja na Mungu. Kama ambavyo ndoa ni uhusiano unaoambatana na ahadi za ndoa, uhusiano wetu na Mungu una ahadi zinazoambatana na kujitoa kabisa kwetu. Fundisho la imani linafafanua jinsi tunavyoishi kwenye uhusiano na Mungu.
(3) Kanisa linadhihirisha furaha ya kumwabudu Mungu. Furaha ya kuabudu katika ibada siyo sawa na furaha inayopatikana kwenye burudani. Watu ambao hawajui jinsi ya kumwabudu Mungu wa kweli hawana uwezo wa kuisikia furaha inayotokana na kumwabudu Mungu. Tumewekwa kwa ajili ya kuabudu; kwa hiyo, mtu ambaye hajaokoka anapoona ibada ya sifa inavyoleta furaha, yeye atakuwa na hitaji la kuipata.
(4) Washirika wa kanisa huonesha kusudi la maisha kwa ajili ya mtazamo wa maisha ya milele. Wakristo hawahitajiki kuwa na mashaka kama maisha yao yana umuhimu. Wkristo wanayo faraja na ujasiri katika nyakati ngumu za maisha. Watu ambao hawajaokoka wanajitahidi kutafuta kusudi la maisha, na hawajui jinsi ya kukabili kifo au uzima wa milele.
(5) Kanisa huonesha kipaumbele cha mahusiano, badala ya malengo ya ubinafsi. Kanisa halifanyi uinjilisti au kulea washirika wake kwa sababu za kujenga shirika lake. Watu wa dunia hudharau mahusino au hutumia mahusiano kwa ajili ya malengo ya ubinafsi.
(6) Ujumbe wa kanisa unatosheleza mahitaji ya ndani kabisa ya kiroho. Mtu mbaye hajaokoka huwa na kiu ya kiroho ambayo haiwezi ikatoshelezwa na kitu chochote kinachotolewa na ulimwengu huu. Mahubiri na mafundisho na ushauri vinavyofanyika katika kanisa vinapaswa vishabihiane na au viendane na mahitaji halisi ya watu.
(7) Kanisa ni mahali palipo na familia ya imani yenye upendo na inayowajali washirika wake. Vikundi vya aina nyingine vinaweza vikasaidia mahitaji ya wanachama wake, lakini ni Wakristo peke yake wenye uwezo wa kuwa na ushirika wa kweli wa Kikristo.
► Je, ni kwa njia gani maalumu ambazo kanisa linaweza likadhihirisha tabia hizi? Je, ni njia gani ambazo kanisa linapaswa lianze kufanya ili liweze kuonyesha vipaumbele vilivyo sahihi?
Kuliandaa Kanisa kwa ajili ya Uinjilisti
Kanisa linapaswa lihakikise kwamba programu zake na muundo wake unasaidia katika kutimiza lengo la umisheni kwa ajili ya huduma ya uinjilisti na ufuasi. Kila kitu ambacho kanisa linafanya kinapaswa kiende sambamba na kipaumbele hicho.
Kuwakaribisha Wageni
Kanisa linapaswa lijiandae kuwakaribisha wageni na kuwasaidia wajisikie wako vizuri. Watu wengine hawana mazoea na taratibu za kanisa. Wanapolitembelea kanisa, hawajui ni nini cha kutarajia. Hawajui ni nini kinatarajiwa kutoka kwao. Kwa muda wa dakika chache za kuwasili kwao katika kanisa, aidha watafurahia kwa kuja kwao, au wakajisikia ni afadhali wasingekuja. Kanisa linapaswa liandae watu mahususi watakaokuwa tayari kuwakaribisha wageni kanisani.
Kanisa halipaswi kuwatenga watu kwa ajili ya umaskini wao. Uvaaji unaotarajiwa watu wavae katika kanisa haupaswi uwatenganishe watu maskini walioko katika kanisa.
Kanisa linapaswa liwe tayari kutoa huduma kwa watoto ambao huja bila wazazi wao. Watu wachaguliwe na wapewe mafunzo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia watoto wanaohudhuria katika kanisa.
Mgeni anapaswa aalikwe kuhudhuria kwenye kusanyiko la kikundi kidogo au kusanyiko la seli za nyumbani ambako anaweza kujifunza zaidi na kuuliza maswali.
Kuwafikia Watu wa Nje
Jukumu la kwanza la kanisa ni kulichunga kusanyiko la washirika ambao wamejitoa kabisa kwa ajili ya kanisa. Hata hivyo, kanisa siku zote linapaswa liwe linawafikia majirani na watu wengine walioko nje ya kanisa. Kanisa ni lazima liwe na shughuli za kufanya ambazo watahakikisha kwamba watu walioko nje ya kanisa wataona majukumu mbalimbali yanayofanywa na kanisa na hata kuweza kuisikia injili. Baadhi ya shughuli hizi zinaweza kuwa za kujitokeza. Inawapasa viongozi kupanga shughuli zingine vile vile. Washirika walio na uwezo wanapaswa waalikwe na kupewa mafunzo yanayohusiana na hizi shughuli za nje za kanisa.
Kanisa linapaswa litafute njia za kushughulikia mahitaji ya majirani wanaowazunguka. Kipaumbele siku zote kiwe ni kuonyesha upendo wa Mungu na kudhihirisha kanuni za kibiblia.
Huduma ya Kikundi cha Seli
Wakati mtu anapokuwa ameokoka hapaswi tu kukaribishwa kwenye huduma za ibada. Anapaswa aalikwe kwenye mpango wa haraka wa ufuasi. Jambo hili linaweza kuanza kwa kuwepo na ziara za binafsi zitakazofanywa na mchungaji. Mtu huyu pia anaweza kualikwa kwenye huduma za vikundi vya seli za nyumbani zinazokutana kila wiki.
Kwa kawaida kanisa lenye afya na ustawi huwa na aina ya vikundi vidogo mabimbali ambako maisha ya kiroho yanasimamiwa. Hivi vikundi vidogo vinaweza vikawa ni nyumba za kanisa, madarasa ya shule za Jumapili, au vikundi vya aina nyingine. Uwajibikaji wa kiroho na mabadiliko ya maisha kwa kawaida hutokea kwenye vikundi vidogo. Viongozi wa kanisa wanapaswa wahakikishe kwamba vikundi vidogo vinakuwepo ambavyo vitakamilisha malengo haya. Kama taratibu zilizopo na au miundo iliyopo ndani ya kanisa haviwezeshi kuwepo kwa maisha ya kiroho, mabailiko yatahitajika.
Uanachama Unaoonekana
Watu wanaotaka kuwa washirika wa kanisa wanataka hasa kujua kushiriki kikamilifu kutamaanisha nini. Baadhi ya makanisa wanadai kutokuwa na muundo wa uanachama, lakini kila kanisa lina jinsi ya kujua washiriki ni kina nani. Kila mtu huwa anahitaji kujua watu wanaoshiriki katika kanisa ni watu wa aina gani.
Kila mtu anapaswa kujua ni mambo gani yanayohitajika kwa ajili ya uanachama. Mahitaji na maelezo ya mchakato wa kuwa mwanachama wa kanisa inabidi yachapishwe.
Mtu aliyebadika na au kuokoka aliye tayari kujikabidhi katika kanisa anapaswa awe tayari mara moja kulisaidia kanisa. Hali hiyo haimaanshi kwamba atapaswa apewe aina fulani ya nafasi au majukumu ya uongozi. Ni muhimu kwake ajue kwamba yeye ni sehemu ya kanisa.
Uwajibikaji wa Haraka kwa Watu Wapya Waliobadilika na au Kuokoka
Ufuasi huanzia pale mtu anapokuwa amebadilika na au ameokoka. Mtu aliyebadilika na au kuokoka anakuwa na mahitaji kadhaa ya haraka. Kuendelea kwenye uhusiano na Mungu ambo ndio tu umeanza, anahitaji kujua jinsi ya kuomba na kusoma Biblia. Pia anahitaji jamii mpya ya marafiki wa sababu kwa vyovyote atawapoteza marafiki wake wengi wa zamani. Atahitaji apate mwongozo katika mambo mengi ya mtindo wa maisha.
Kanisa linapaswa lianzishe mara moja huduma ya ufuasi kwa mtu mpya aliyebadilika na au kuokoka. Mara moja haina maana ya Jumapili inayofuata. Inamaanisha kwamba mara tu anapokuwa anainua kichwa chake kutoka kwenye maombi kwa ajili ya kuokoka. Mtu mmoja ni lazima achukue wajibu wa mawasilino ya kila siku na huyu mtu mpya aliyeamua kubadilika na au kuokoka angalao kwenye wiki yote ya mwanzo. Atapaswa aweze kukutana na Wakristo wengine katika kanisa la mahali pamoja. Atapaswa awe na nafasi za kujadili kuhusu mabadiliko yanayotokea kwake na aulize maswali.
Huyu mtu mpya aliyeamua kubadilika na au kuokoka atapaswa aalikwe na ajiunge kwenye kikundi kidogo ambacho anaweza akauliza maswali na kutiwa moyo. Ikiwezekana, atapaswa atambulishwe kwa washirika wengine kadhaa kwenye kikundi katika siku za mwanzo kabla ya kikao cha kwanza atakochohudhuria kwenye kikundi. Baadhi ya washiriki katika kikundi wanaweza wakampigia simu kabla ya kuanza kwa kikao kwa ajili ya kuendelea kumwonyesha urafiki pamoja naye na kumkaribisha ahudhurie kwenye kikao cha kikundi. Hali hii itaanza kumjengea hisia za kujisikia yuko na anahusika katika jamii.
Mtu mpya aliyeamua kubadilika na au kuokoka atapaswa kujiunga na kikundi kwenye kikao kitakachofuata. Masomo yatafanyika kwa mzunguko ili kwamba mshiriki katika kikundi aweze kuingizwa wakati wowote. Kwa njia hii mtu mpya aliyeamua kubadilika na au kuokoka anapata msaada wa kikundi mara moja. Washiriki huhitimu kozi kibinafsi wanapokuwa wamemaliza masomo yote.
Kujali Mahitaji
Kanisa ni lazima liweze kujali mahitaji ya kifedha ya watu wa kusanyiko lake. Mahitaji mengi yatatimizwa na watu kusaidia watu wengine kwenye kusanyiko la kanisa bila ya kuhusisha kuongozwa na viongozi wa kanisa. Kama watu wengi katika kanisa hawaoni kujisikia kwa ajili ya kusaidia watu wengine, bado watakuwa hawajatengeneza kanisa lenye ukomavu.
Kanisa linatakiwa liwe na mashemasi ambao watakuwa wanahakikisha kwamba mahiaji yanatambulika. Kanisa katika kitabu cha Matendo kilichagua mashemasi wa kwanza kwa ajili ya kusudi hili.
Kujali mahitaji ni muhimu kwa ajili ya umisheni wa injili. Watu ni lazima wawe na umakini wa kuangalia kwamba kanisa ni familia ya waaminio ambao washiriki hujali kwa ajili ya mtu mwingine.
Kazi ya Kufanya
Jaribu kufikiria kanisa linalotenda mambo yote tuliyozungumzia katika somo hili. Andika kuhusu mtu wa kufikirika ambaye hutembelea kanisa, akaamua kubadilika na au kuokoka, na akawa mshirka anayejitoa kwa kanisa. Elezea hali yote jinsi ilivyotokea.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.