Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 3: Dharura ya Uinjilisti

8 min read

by Stephen Gibson


Utangulizi

► Je, inawezekana mtu kuokoka bila ya kusikia injili? Je, kazi ya uinjilisti ina ulazima wowote?

Katika Maandiko tunapata huko mifano ya watu waliofikiwa na injili kwa neema ya Mungu bila ya mawasiliano yeyote kutoka Israeli au kanisa. Ayubu alikuwa mtu mwenye haki na alikataa mambo ya uovu hata kabla Musa hajatokea kuishi na kabla Maandiko hayajaandikwa. Baalam alikuwa mwenye uhusiano na Mungu, na alijulikana kama mwonaji aliyekuwa akipokea ujumbe kutoka kwa Mungu bila ya kuwa katika hali ya kupagawa. Abimeleki alifanya mambo mazuri zaidi ya haki kuliko Abrahamu, baada Abrahamu kufikiri, “yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa.” Warumi 1:21-32 inaelezea kuhusu wapagani au makafiri waliokuwa kwenye hali ya mkengeuko wa tabia; siyo kwa sababu walikuwa hawamjui Mungu, bali kwa sababu walikataa kile ambacho walikuwa wanakijua.[1]

"Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake” (Zaburi 25:14). Agano ni sharti la uhusiano wa Mungu na mwanadamu, ambalo linahitaji upatikanaji wa neema kwa sababu watu wote wametenda dhambi. Kama mtu akimheshimu Mungu kwa ukamilifu wote, Mungu atamwonyesha njia ya kuwa kwenye uhusiano na yeye.

Biblia inasema kwamba wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, isipokuwa Yesu (Matendo 4:12). Hata hivyo, watu waliokuwa wameokolewa wakati wa Agano la Kale hawalijui jina la Yesu. Waliiweka imani yao kwenye ahadi ya Mungu ili kupata wokovu na msamaha, na aliwapatia kupitia kwa Yesu. Kwa hali hiyo hiyo, watu ambao hawajawahi kulisikia jina la Yesu wanaweza wakamwamini Mungu kwa ajili ya wokovu wao, anaokuwa anautoa kupitia kwa Yesu.

Kwa hiyo, inamaanisha nini kwa kusema kwamba wokovu hauwezi kupatikana kupitia kwa mtu mwingine yeyote? Inamaanisha kwamba mtu hawezi akaokolewa kupitia mpango mwingine wa ukombozi. Inamaanisha pia kwamba mtu asiyejua habari za Yesu hapaswi kumkataa yeye kwa sababu kumkataa Yesu itakuwa ni kuukataa wokovu au kutazamia njia nyingine ya ukombozi.

Yesu alisema, “Mtu yeyote akiyafanya mapenzi yake, ataijua kweli.” Hii ni ahadi kwamba kama mtu atamtafuta Mungu kwa uaminifu, Mungu atamjulisha analopaswa kulijua. “Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu” (Yohana 1:9). Roho Mtakatifu huleta nuru ya Yesu hata kwa wale watu ambao hawajawahi kusikia habari zake.

Watu wengi wamepokea maono au ufunuo mwingine ambao uliwaleta kwa Mungu hata kabla hawajasikia habari njema za injili kutoka kwa mjumbe mwanadamu. Kwa mfano, kwa wakati wa sasa Waislamu wengi wanakubali kubadilika baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa Mungu

► Je, ulishawahi kusikia habari za mtu yeyote ambaye alipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Mungu kabla ya kuielewa injili sawasawa?

Kwa hiyo, tunaona kwamba inawezekana kwa mtu kumpata Mungu na hata kuweza kuokoka bila ya kusikia injili kutoka kwa wajumbe wa kibinadanu. Lakini bado, Biblia inaelezea injili kama ni ujumbe ambao kila mtu kwa umuhimu wake anatakiwa kuisikia.

[2]Kitabu cha Warumi kinaelezea umuhimu wa injili. Mtume alisema kwamba injili “ni uweza wa Mungu uletao wokovu” (Warumi 1:16). Alisema kwamba anawiwa na deni kwa kila mtu, ambalo ni kupeleka injili kwao (Warumi 1:14). Anajenga ukweli kwamba sisi tunahesabiwa haki na Mungu kwa kuamini tu ahadi yake ya kusamehe (Warumi 3:26, Warumi 5:1).

Kisha linajitokeza wazo la udharura. Anasema, “Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14). Akasema,”Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Mungu huitumia injili kutengeneza imani iokoayo kwa wasikiaji wake. Mahubiri ya injili ni njia ya kawaida ya Mungu anayoitumia katika kuwaokoa wenye dhambi.

Kama wanaweza kuokolewa pasipokuwa na mjumbe wa kuwapelekea ujumbe wa injili, ni kwa nini uwepo wa mjumbe ni muhimu sana?


[1]Ona pia Zaburi 19 na Warumi 10:18.
[2]

“Kwenye eneo kubwa la wazi la Kaskazini, nimekuwa mara nyingine nikiona wakati wa asubuhi moshi wa maelfu ya vijiji ambayo watu wake wako bila Kristo, bila Mungu, na bila ya mategemeo katika dunia.”

- Robert Moffat