► Soma Mathayo 19:16-22. Ni nini cha kukushangaza katika jibu la Yesu kwa mwanamume huyu? Kama ungesikia rafiki yako akitoa jibu hilo kwa mtu ambaye ameuliza ni kwa jinsi gani aurithi uzima wa milele, ungependa ueleze nini kwa huyo rafiki yako?
Jaribu kufikiria kwamba uko kwenye afya nzuri, lakini rafiki yako akaja kwako na kusema kwamba amenunua dawa ya tiba kwa ugonjwa fulani unaoweza kusababisha madhara ya kifo.[1] Ili kuweza kuinunua dawa hiyo, aliuza nyumba na vitu vyote alivyokuwa navyo. Aliinunua dawa hiyo ya tiba kwa ajili yako.
► Je, utasema nini kwa rafiki yako wakati akikupa zawadi yako hiyo?
Kwa vyovyote utamshukuru kwa ukarimu wake, lakini hutakuwa umeilewa hiyo zawadi. Kwa nini atumie gharama kubwa kiasi hicho kwa ajili ya kukununulia kitu ambacho huna hitaji nacho?
Sasa jaribu kufikiria tena taarifa nyingine tofauti. Umekuwa kwa daktari na ukakutwa una ugonjwa wenye madhara makubwa. Dawa kwa ajili ya tiba yake ni ya gharama kubwa, na huna namna yeyote ya kuweza kuilipia. Unaondoka kwenda nyumbani huku ukiwa unawaza kuhusu kifo, ukitambua kwamba familia yako itakukosa na kamwe hutakuwa na uwezo wa kutimiza kile ulichokuwa umetegemea katika maisha yako.
Kisha akajitokeza rafiki na kukuambia kwamba alitoa kila kitu alichokuwa nacho kwa ajili ya kukununulia hiyo dawa. Utaridhika na jambo hilo kwa sababu kwanza unaelewa hitaji lako. Zawadi yake ni uhai kwa ajili yako.
Sasa fikiria kuhusu majibu ya watu wa dunia wakati wanaposikia habari za injili. Neno injili lina maana ya “habari njema,” lakini watu wengi hawaelewi kwa nini ni habari njema.
Jaribu kufikiria kuhusu mtu aliyeitwa Petro. Marafiki zake wanamwambia kwamba, “Yesu alikufa msalabani kama dhabihu ili kwamba dhambi zako ziweze kusamehewa.”
Petro anafikiria, “Mimi siyo mtu mbaya. Mimi ni mzuri kwa marafiki zangu na kwa familia yangu. Kwa nini kuhitajike dhabihu kubwa kiasi hicho kwa ajili ya dhambi zangu? Kwa nini msamaha ni jambo muhimu kiasi hicho? Petro anaweza kukasirika kwamba rafiki yake anamfikiria ni mtu mbaya mtenda dhambi ambaye atahitaji kifo cha Yesu kwa ajili ya msamaha wake.
Biblia inatuambia kwamba watu wanakerwa na msalaba. Watu wanataka wapate njia ya kujihesabia haki wao wenyewe. Hawafikiri kwamba wanahitaji dhabihu ya Yesu, kwa hiyo msalaba unaonekana kama ni upumbavu kwao (1 Wakorintho 1:18).
Kama yalivyo maelezo kuhusiana na dawa ya tiba kwa ajili ya ugonjwa, watu hawakubaliani na msalaba kwa sababu hawaelewi ni kwa nini wanauhitaji.
Njia ya kibiblia ya kuwaandaa watu kwa ajili ya habri njema ni kuwaonyesha ni kwa nini wanahitaji injili. Wanapaswa kutambua kwamba wao ni watenda dhambi ambao muda siyo mrefu watahukumiwa na Mungu.
► Je, ni kwa nini mtu anapaswa kufurahi anaposikia injili?
[1]Wingi wa taarifa za somo hili zinawasilishwa na Ray Comfort kwenye mahubiri yake “Hell’s Best-Kept Secret” na kitabu chenye kichwa hiki hiki cha somo. Nyenzo nyingine zinapatikana kutoka katika http://www.livingwaters.com.
Umuhimu wa Hukumu
Ukweli kwamba wenye dhambi watahukumiwa na kupewa adhabu ndiyo sababu ya muhimu ya mwenye dhambi kuwa na furaha ya kusikia injili.
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu (Waebrania 9:27).
Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu (Mathayo 12:36).
► Soma maelezo ya hukumu ya mwenye dhambi katika Ufunuo 20:12-15.
Hukumu ya mwisho ya wenye dhambi ndiyo sababu kuu ya msingi ya kila mwenye dhambi kuhitajika kuokoka.
Mungu ameagiza kila mtu atubu, “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki” (Matendo 17:30-31).
Kama mtu hawezi kuelewa kwamba dhambi yake inamweka kwenye hali mbaya, anakosa sababu muhimu sana ya kuhitaji wokovu.
► Je, ni nini kitakachomfanya mwenye dhambi ajitambue kwamba dhambi yake inamweka kwenye hali mbaya?
Matumizi ya Sheria
Watu wengi hawako katika hali ya kuitamani injili kwa sababu hawajioni wenyewe kwamba ni wenye hatia. Biblia inasema kwamba watu wengi wanajihesabia wenyewe kwamba ni watu wazuri (hawana hatia) (Mithali 20:6). Kama utamwuliza mtu yeyote kama yeye ni mtu mzuri, bila shaka atakujibu kwamba “ndiyo” na kuwa tayari kujitetea mwenyewe. Watu wengi wanafikiri kwamba dhambi zao siyo uovu, na kwamba watapaswa kuwiwa radhi. Watu kama hao kuwapa neema na msamaha hakuleti maana yeyote.
Mtu ni lazima ajiangalie mwenyewe kama mtenda dhambi na ajisikie mwenye hatia katika dhamira yake kabla hajajiona mwenye kuhitaji nema. Mungu ametoa sheria kuonyesha kuhusu dhambi.
Kwa kusema sheria hatumaanishi hususani taratibu za ibada za Agano la Kale ambazo ziliwaongoza watu kuabudu kwenye sinagogi. Pia hatuzungumzii kuhusu sheria zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya serikali ya Israeli, ambazo hazitumiki kwetu kwa njia inayofanana. Tunazungumzia kuhusu kipimo cha Mungu cha haki. Mfalme Daudi aliandika katika kitabu cha Zaburi 119 jinsi alivyokuwa ameipenda sheria ya Mungu kwa jinsi alivyokuwa anampenda Mungu, kwa sababu ilitoka katika tabia ya utakatifu ya Mungu mwenyewe.
Sheria ya Mungu inatuonyesha jinsi ya kuishi, na tuna hatia kwa kuikataa. Hakuna mtu atakayehesabiwa haki kwa kuishika sheria (Wagalatia 2:16, Warumi 3:20). kwa sababu kila mtu ametenda dhambi. Mtu anaitumia sheria vibaya kama atakuwa nafikiria kwamba kwa kujaribu kuifuata sheria atapata wokovu wake.
Sheria ya Mungu inayaongoza maisha yetu, (1 Wakorintho 9:21). lakini siyo njia ya wokovu wetu. Sheria haingeweza kutuleta sisi kwenye wokovu kwa sababu hatuna uwezo wa kutekeleza kwa ukamilifu mahitaji yake yote tangu kuzaliwa (Warumi 8:3, Wagalatia 3:21).
Sheria haipingani na injili kwenye mpango wa Mungu. Biblia inatuambia kwamba sheria inatumika kwa kusudi la kumfanya mwenye dhambi atambue hitaji lake la wokovu. Injili haijaivuruga sheria (Mathayo 5:17). au haijaifanya sheria isiwe na maana kwetu. Sheria inatumika kama maandalizi makamilifu kwa ajili ya injili, siyo kwa nyakati za kale tu bali hata sasa.
“Sheria (torati) imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo,” (Wagalatia 3:24). Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kulikuwa na kipindi ambacho sheria ilishapita , na kwa sasa kuna kipindi cha neema. Ukweli ni kwamba kila mtu ni lazima atakutana na sheria ya Mungu na atatambua kwamba anahesabika mwenye hatia kabla hajaelewa kuhusu neema. Mtume Paulo alisema, “Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria” (Warumi 7:7).
Paulo alisema kwamba sheria imetolewa ili wenye dhambi waonyeshwe kwamba wana hatia na hawawezi kujitetea; kwa sababu, kwa sheria watu hutambua kwamba wao ni watenda dhambi (Warumi 3:19-20). Kila mtu yuko “chini ya sheria” na kufanywa mwenye hatia na hiyo sheria hadi atakapokuwa ameokoka.
Injili huwa siyo habari njema kwa mtu ambaye hataki kujua kwamba dhambi yake imemweka mahali pabaya. Injili ni habari njema kwa mtu anayeelewa kwamba yeye ni mwenye hatia na hivi punde atakutana na hukumu ya Mungu.
► Soma Luka 18:10-14. Kama angetokea mtu akamweleza yule Farisayo kwamba bila ya gharama yeyote anaweza akasamehewa kwa neema ya Mungu, angewezaje kujibu hili?
Kosa la makanisa ya leo ya ki-injili (evangelicals).
[1]Leo makanisa ya kiinjili mengi hawataki kuwekea mkazo kila mtu ni mwenye hatia kutokana na dhambi na anastahili adhabu ya Mungu.
Hawataki kuwaambia watu kwamba wao ni watu wabaya.
Wanataka kuzungumzia mambo chanya tu badala ya hasi.
Wanataka kutoa manufaa ya haraka ya wokovu, badala ya manufaa ya milele, kwa sababu wanazungumza na watu ambao wameweka mtazamo wao kwenye mambo ya dunia hii.
Wanachukulia kwamba sheria ya Mungu ni jambo baya, ni adui wa wokovu, na ni muhimu tu kwa watu ambao wanataka waokoke kwa matendo yao. Biblia inasema kwamba sheria ni nzuri na takatifu; (Warumi 7:12-14). mtu anayetaka kumpendeza Mungu atajaribu kufuata maelekezo ya Mungu katika maisha yake yote (Zaburi 119:1-8).
Wanadhani kipimo cha Mungu haiwezekani na hakiingii akilini, na kwamba hupaswi kujilaumu kwa ajili ya dhambi zako.
Tatizo ni kwamba kama mtu kwa uhakika siyo mwenye hatia, hawezi akatubu. Hawezi akajutia kwa yale anayotenda labda iwe anajua kwamba amechagua mwenyewe kutenda uovu. Kama mtu haamini kuwa yeye ni mwenye dhambi pale anapoomba msamaha, kwa ukweli ni sawa tu na kuomba Mungu akubaliane na makosa yake ya kibinadamu.
Ukweli ni kwamba wenye dhambi hawahesabiwi kuwa na hatia kwa ajili ya kuzaliwa na asili ya dhambi. Wanahesabiwa kuwa wana hatia kwa matendo na mienendo yao ya dhambi wanayofanya kwa hiari yao wnyewe ambayo ni uasi dhidi ya Mungu (Yuda 15).
Watu wengi wanaamini kwamba Mungu ni wa upendo na mwenye kusamehe, lakini hawatambui pia kwamba ni Mungu anayehukumu kwa haki. Wanategemea kwamba endapo itatokea wakakutana na Mungu, atawasamehe hata kama kamwe hawakuwahi kutubu. Injili isiyokuwa kamili ambayo waiiisikia imewafanya wawe watu wa kuridhika sana katika dhambi zao.
Makanisa mengi ya ki-injili leo hii yanasisitiza kwamba kama mtu anakuwa Mkristo, atakuwa na maisha yenye furaha zaidi. Wanasema kwamba dhambi haimridhishi mtu, lakini Mungu anafanya hivyo. Wanasema kwamba mtu atapokea upendo, amani, na furaha. Wanasma kwamba Mungu anao mpango wa ajabu kwa ajili ya maisha ya kila mtu, na kwamba mpango huo utatimilika kama mtu ataokoka.
Ahadi hizi inawezekana zisieleweke. Mungu hutoa upendo wake na amani, lakini kutakuwepo na mgogoro kwa watu ambao wanamkataa Mungu (Mathayo 10:34-36). Anatoa furaha, lakini wakati huo huo panaweza kuwepo na mateso (1 Wathesalonike 1:6). Ana mpango kwa kila mtu, lakini Mkristo anaweza akakutana na mazingira magumu na mambo makubwa yaletayo huzuni (2 Wakorintho 11:24-27). Kama mtu ataamua kuwa Mkristo kwa sababu ya kudhania kwamba maisha yake yatakuwa mazuri zaidi, anaweza akakatishwa tamaa sana. Watu wengine wanapata mateso makubwa sana kwa sababu tu wao ni Wakristo.
Kama Wakristo, tunaelewa kwamba maisha pamoja na Mungu ni mazuri sana, hata kama tunateseka katika mazingira magumu. Tunaweza kusema kwamba kumtumikia Mungu ni maisha mazuri sana. Hata hivyo, watu wengi ambao hawajaokoka hawana wazo sahihi kwamba maisha mazuri sana ni nini. Kama utawauliza kutoa ufafanuzi wa maisha mazuri sana watakujibu kwa kuzungumzia afya, fedha, uhuru, amani, na hali nyingine nzuri. Hawatakuwa wanaelewa kwamba Mkristo anayeumizwa kwa mateso na kuteseka anamaisha mazuri sana. Kwa hiyo, kama utamweleza mwenye dhambi kwamba kama akiwa Mkristo atakuwa na maisha mazuri sana, inawezekana asielewe kitu unachomwahidi.
Kuna tatizo lingine la ufahamu potofu wa injili. Mtu anaweza akaukubali ujumbe bila ya kujikagua mwenyewe kama ni mwenye dhambi anayestahili kuhukumiwa. Kwa sababu haoni uzito na madhara ya dhambi, kwa ukweli hatubu. Hatafuti wokovu wa kuachana na dhambi, bali kwa ajili ya manufaa mengine. Anaweza akafikiri kwamba ameokoka wakati kiuhalisia sivyo alivyo.
Hawezi pia hata kupokea manufaa ya kweli ya wokovu kwa ajili ya maisha yake, kwa sababu hajaokoka. Anajaribu kwa muda mfupi kisha anaacha kwa kukata tamaa.
Matokeo mabaya zaidi ya injili potofu ni kwamba mtu aliyekuwa amekata tamaa ana uwezekano mkubwa wa kutokubaliana na injili ya kweli katika siku za baadaye.
Kwa muhtasari, matatizo yanayotokana na injili ya maisha mazuri sana ni kama yafuatayo:
1. Inatoa ahadi ambazo Mungu hajawahi kuahidi.
2. Haieleweki kwa mwenye dhambi.
3. Mtu hataweza kuwa amebadilika kiukweli.
4. Hatapata manufaa aliyokuwa anategemea.
5. Ana uwezekano mkubwa wa kutokubaliana na injili ya kweli katika siku za baadaye.
► Soma Matendo 14:21-23. Je, ni kitu gani mitume walichowaambia waumini wapya wategemee?
Yesu aliwaonya wanafunzi wake kwamba watu watawachukia kwa sababu ya imani yao katika Kristo. Aliwaambia hawatakuwa wameokoka hadi hapo watakapokuwa wamevumilia hadi mwisho. Waandishi watatu miongoni mwa waandishi wa injili waliandika haya maneno (Mathayo 10:22, Marko 13:13, Luka 21:17). Wengi wa mitume wa kwanza walikufa kwa ajili ya Kristo.
Mamilioni ya Wakristo wameshauawa kwa ajili ya imani yao. Hili siyo tatizo kwa ajili ya zamani tu. Zaidi ya nusu ya wafia imani waliuawa katika karne ya 20.
Kama mtu atabadilika kwa sababu ya ahadi ya wokovu bila ya ahadi ya maisha mazuri, hatakata tamaa kwa sababu ya maisha magumu. Atakuwa tayari kuhimili majaribu kwa ajili ya wokovu wa milele. Majaribu hufanya wokovu kwa mtu huyu kuwa kitu cha thamani sana kwake.
“Kubadilika kunahusisha kutengana kikamilifu na mambo ya zamani ambayo huitwa yamekufa. Sisi tumesulubiwa pamoja na Yesu. Kupitia katika msalaba wake, tumekufa kwa mambo maovu ya dunia, matarajio yake na vipimo vyake vyote.”
- Kamati ya Dunia ya Uinjilishaji ya Lausanne, Taarifa yaWillowbank
Kuonyesha Upendo
► Soma 2 Timotheo 2:24-26. Je, aya hizi zinatueleza nini kuhusu tabia ya mwinjilisti?
Mwinjilisti hapaswi kuwa mtu anayeonekana kupambana na watu anaowafanyia huduma ya uinjilisti. Shetani ni adui, na wenye dhambi ni mateka wa shetani. Tunapaswa tueleze ukweli kwa upole. Kusudi letu ni kuwasaidia, na siyo kuwashinda kwa mashindano. Maneno yanayotumika katika kifungu hiki yanahusisha pamoja na upole, unyenyekevu, na uvumilivu.
► Soma Tito 3:2-5. Kifungu hiki kinaseme nini kuhusiana na mwenendo wa mwinjilisti?
Tunapaswa tukumbuke kwamba bila ya neema ya Mungu, tutakuwa kama watu wa kidunia. Mungu alikuja kwetu siyo pamoja na hukumu, bali alikuja kwetu kwa upole na upendo.
Mwinjisti hapaswi kuwa na hasira na mwenye dhambi, bali dhidi ya dhambi na Shetani. Hapaswi kuwa mkali. Hapashwi kufurahia katika kutafuta makosa yao, lakini anapaswa kuwajibika kwa ajili ya wokovu wao.
Tumejifunza kwamba hatupaswi kuonyesha upendo kwa mwenye dhambi kwa kuahidi ahadi ambazo Mungu hakuwahi kuahidi. Hatupaswi kuonyesha matendo ya huruma kana kwamba matatizo yao ya maisha ni ya muhimu zaidi kuliko hatima yao ya milele.
Yesu alikamilisha unabii kwamba Masihi hangelikuwa mtu wa vurugu, bali mpole, na hangekuwa mtu wa kumuumiza mtu ambaye amejeruhiwa na dhambi (Mathayo 12:19-20).
► Je, ni kwa njia gani tunaweza kudhihirisha upendo wa Mungu wakati tunapofanya uinjilisti?
Uinjilisti wa Kibiblia
Mtazamo wa kibiblia katika uinjilisi ni kutumia sheria ya Mungu katika kuwaandaa watu waipokee injili. Sheria inawahukumu wenye dhambi na kuwaonyesha kwamba watahukumiwa endapo hawatatafuta kusamehewa.
Yohana Mbatizaji alihubiri kwamba watu wanapaswa kutubu kwa ajili ya maandalizi ya ujio wa Bwana na ili kuepukana na hukumu (Mathayo 3:1-12).
Yesu alihubiri mara nyingi kuhusu hukumu na moton. Alitoa neema kwa wale waliojutia kuhusu dhambi zao.
► Soma Luka 7:36-50. Je, ni aina gani ya mtu anayepaswa kupewa msamaha?
Hatuoni mahali popote katika huduma ya Yesu kwamba alitoa msamaha kwa watu ambao hawakuwa wamejutia dhambi zao. Alionya watu kuhusu uwepo wa hukumu. Baada ya kuonyesha maafa ambapo watu wengi waliuawa, Yesu aliuambia umati wa watu kwamba wote wataangamia kama hawatatubu (Luka 13:1-5).
Yesu alitoa mfano wa mtoza ushuru na Mfarisayo walioomba maombi tofauti. Mtoza ushru alijutia makosa yake na akapokea msamaha. Mfarisayo alijaribu kujiinua na kujiridhisha mwenyewe kwamba siyo mtenda dhambi. Haingekuwa na maana yeyote kutoa msamaha kwa Mfarisayo kwa sababu hakuwa anaamini kama aliuhitaji huo msamaha.
Mtume Petro alihubiri ahadi ya maisha ya uzima wa milele na akawataka watu kutubu ili wapokee msamaha (Matendo 2:38, Matendo 3:19, Matendo 5:31).
Stepheno, akiwa anahubiri kwa watawala wa Kiyahudi, hakutamka neema juu yao, bali aliwashutumu kwa kumkataa Mungu na kuvunja sheria yake (Matendo 7:51-53).
Paulo alihubiri kwamba watu wanapaswa kutubu kwa sababu Mungu hatakuwa na msamaha juu ya dhambi (Matendo 17:30-31).
Siyo jambo baya kuzungumzia kuhusu furaha na baraka zinazotokana na mtu kuwa Mkristo; lakini mbinu ya msingi ya wainjilisti katika Biblia ilikuwa ni kuhubiri hadi kumleta mtu ajisikie kwamba ni mwenye kuhitaji msamaha, akipokea wokovu badala ya hukumu.
► Soma 2 Wakorintho 5:11. Je, Mtume alisema nini kwa ajili ya kushawishi?
► Soma Matendo 24:25. Je, mtume Paulo alisema nini kuhusu Feliki? Je, Feliki aligusikaje?
Mfano wa Uinjilisti wa Kibiblia
Andrea alikuwa akisambaza mialiko ya kuja kanisani wakati alipokutana na Petro.
Petro: Silihitaji kanisa.
Andrea: Biblia inaema kwamba kila mtu atasimama mbele ya Mungu kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi zake. Je, unafikiri kwamba Mungu atakukubali wewe kwa jinsi ulivyo?
Petro: Ndiyo, Ninafikiria hivyo.
Andrea: Wewe ni mtu mzuri?
Petro: Ndiyo, nadhani ndivyo nilivyo.
Andrea: Inawezekana ni mzuri ukilinganishwa na watu wengine. Inawezekana ni mzuri kwa marafiki zako na familia yako. Lakini, je, unajua viwango ambavyo Mungu anavitumia? Biblia inatueleza sisi jinsi Mungu anavyohukumu wenye haki na wasiokuwa na haki. Kwa mfano, sehemu ya sheria zake inaitwa Amri Kumi za Mungu. Je, wewe unazijua Amri Kumi za Mungu?
Petro: Baadhi yake.
Andrea: Kwa mfano, amri moja inasema, “Usiseme uongo.” Je, katika maisha yako hujawahi kamwe kusema jambo lolote ambalo halikuwa la ukweli?
Petro: Hakika ndiyo, kila mtu amewahi kufanya hivyo kwa wakati fulani.
Andrea: Lakini kusema uongo ni kuvunja amri ya Mungu. Amri nyingine inasema usiibe. Je, ulishawahi kuiba kitu chochote?
Petro: Vitu vidogo vidogo sana, na sijawahi kumfanya mtu akaumizwa kwa kuiba vitu hivyo kutoka kwake.
Andrea: Lakini Mungu hatuachii sisi tuamue kitu cha kuiba. Amri yake ni kwamba tusiibe. Amri nyingine ni kwamba tusilitaje jina la Bwana Mungu wetu bure, kulitaja bila kuonyesha unyenyekevu na heshima, au kulitumia kama neno la kulaani.
[Kila amri kutoka katika hizo Amri kumi za Mungu, zinaweza kutumika, lakini zote hazipaswi kutumika katika mazungumzo ya aina moja. Kuna mifano hapa chini.]
Mungu anatuambia sisi kwamba tusiwe wazinzi, na Yesu akasema kwamba kumwangalia mwanamke kwa matamanio ni kufanya uzinzi ndani ya moyo wako.
Mungu alisema tusiue, na Yesu akasema kumchukia mtu mwingine ni sawa na kuua ndani ya moyo.
Mungu anatuambia sisi kwamba tuikumbuke Siku ya Bwana na kuitakasa. Je, umekuwa ukiitakasa Siku ya Bwana kila wiki?
Mungu anatuambia sisi kwamba tusitamani mali za wengine, tusifikiri kwamba mali na vitu vingine vitatufanya sisi tuwe na furaha badala ya Mungu, tukitamani kuwa tungekuwa na vitu walivyo navyo watu wengine.
Mungu anatuambia sisi kwamba tusiwe na miungu mingine, tusiruhusu kufanya kitu chochote kuwa chenye umuhimu kuliko yeye Mungu, ikimaanisha kwamba haturuhusu kitu chochote kituweke mbali na kumtii na kumwabudu Mungu kama anavyostahili.
[Baada ya kutumia amri kadhaa kuonyesha kwamba mwenye dhambi ana hatia, ndipo tunaenda kwenye hitimisho.]
Andrea: Kama leo hii Mungu atakuhukumu, hutafaulu. Utakuwa mwenye hatia kwa viwango vyake. Je, utataka kujua jinsi ya kupata msamaha ili kwamba usiwe na hofu ya hukumu ya Mungu?
[Kisha, mwinjilisti anaweza kumshirikisha injili na kumwalika mwenye dhambi kwenye hatua nyingine ya kuomba naye.]
► Wanafunzi wawili watapaswa kuonyesha mazungumzo ambayo mmoja anawakilisha injili kwa kutumia Amri kumi za Mungu. Kikundi kinaweza kujadili kuhusu onyesho lao. Wanafunzi watapaswa kugawanyika kwenye vikundi vya watu wawili wawili kwa ajili ya kufanya mazoezi ya jinsi ya kuwasilisha injili.
► Je, utajuaje kwamba uwasilishwaji wa injili ulikuwa wa mafanikio?
Ni wazi kwamba mtu anapochagua kutubu na kuokoka baada ya uwasilishaji wetu wa injili, tunajua kwa uhakika kwamba ulikuwa wa mafanikio. Lakini, hicho siyo kipimo pekee cha mafanikio. Mungu ndiye anayehusika katika kuharakisha ukweli ukae ndani ya moyo wa mtu. Kama uliwasilisha injili kwa njia ambayo msikilizaji alikuelewa, ulikamilisha jambo fulani la muhimu sana hata kama kamwe hukuona matokeo. Kama atajisikia kwamba una mzigo juu yake na una nia ya kutaka kumsaidia, jambo hilo ni jema pia. Kama alikuwa mwenye hasira au mizaha, hiyo haina maana kwamba umeshindwa hasa zaidi kama alikasirika kwa ukweli aliousikia kutoka kwako. Mungu huheshimiwa kwa ujumbe wa injli; wakati unapouwakilisha, una mafanikio katika jambo fulani muhimu.
Ukumbusho kwa Kiongozi wa Darasa
Hii ni njia yenye ufanisi sana kwenye kuwasilisha injili. Ni muhimu kwa sababu wanafunzi hujifunza kuitumia. Kwenye darasa lako linalofuata, wape wanafunzi muda wa kuelezea uzoefu wao wakati watakapokuwa wakishirikisha injili kwa kutumia mbinu hii. Wape nafasi ya kutiana moyo na kushauri kila mmoja na mwenzake. Itakuwa ni jambo la busara sana kuchukua kipindi kizima kwa njia hii na kungojea hadi wakati mwingine wa kwenda kwenye somo linalofuata.
Kazi ya Kufanya
Wasilisha injili kwa angalao watu watatu kwa kutumia ile njia ya Andrea katika somo hili. Andika aya moja yenye kuelezea kila mazungumzo yanayofanyika. Jiandae kuelezea kuhusu hili kwenye kipindi cha darasa kitakachofuata.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.