Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 16: Wafuasi wa Kweli

14 min read

by Stephen Gibson


Kumfuata Yesu

► Je, inamaanisha nini kuwa mfuasi wa Yesu?

Baadhi ya watu hufikiri kwamba Mkristo ni mtu yeyote aliye mzuri. Wengie hufikiri kwamba kuwa Mkristo maana yake ni kuamini baadhi ya mambo fulani. Wengi wa watu hawa, imani hazileti tofauti yeyote ya maana kwenye maisha yao.

Watu wengine wako karibu na ukweli. Wanajua kwamba ni lazima kutakuwepo na kipindi cha kubadilika na au kuokoka, wakati mtu anapokuwa Mkristo. Wanaamini kwamba hali hii inatokea wakati mtu kwa kipindi fulani alipoamini kuwa alikuwa amesamehewa. Watu wengi wanaamini kwamba mtu aliyeokoka kwa ukweli ana uhakika wa mbingu hata kama akifanya jambo lolote baada ya kuokoka.

Ni ukweli dhahiri kwamba kuokoka ni lazima iwe jambo la kweli. Ni ukweli dhahiri kwamba msamaha unapatikana kwa neema kwa kukubaliana na imani. Ni ukweli dhahiri kwamba Mkristo anaishi kwa kumtii Mungu. Lakini hayo yote hayatoshi kumaanisha ndio kuwa mwanafunzi wa Yesu.

Tunaweza kuona ni nini kinachotokea wakati wa imani ikifanywa ndiyo kigezo pekee cha kuwa Mkristo—inatupeleka kwenye fundisho kwamba amri za Mungu siyo lazima kuzitii na au kufuatwa na Mkristo (antinomianism. Badala ya kuwa neema ya bure, inakuwa ni neema ya kubuniwa ambayo inajifanya kuhalalisha dhambi.

Makanisa ambayo yanatangaza neema ya kubuniwa yana watu wanaohudhuria katika ibada za kanisa lakini wanaishi kwenye dhambi za wazi kabisa. Wachungaji wao na viongozi wao wengine wanaishi maisha mazuri kuliko washirika wa makusanyiko yao lakini inawezekana pia wanaishi kwenye tabia za maovu. Wanasema siyo lazima kuishi kwenye utiifu wote kwa Mungu kwa sababu tumeokolewa kwa neema. Wamepoteza agizo lile Yesu alilolitoa kwa kanisa, ambalo ni kuwaweka watu kwenye utiifu wa maagizo yake Kristo. Kazi maalumu ya kanisa ni kuwageuza wenye dhambi wamrudie Mungu na kuwa watakatifu waabuduo Mungu, na kanisa halina sababu yeyote nzuri zaidi ya kulifanya lisiendelee kuwepo.

Hata makanisa ambayo yameshikilia msimamo wa umuhimu wa kumtii Mungu wana watu kadhaa ambao wako kwenye mrengo wa kimakosa. Wameyaweka maisha yao yakubaliane na matakwa ambayo wanaamini ni sahihi, lakini hawana ile roho ya kumfanania Kristo. Ni wakatili na wasiokuwa na msamaha. Hawawezi kutoa samahani yenye unyenyekevu na neema. Ni wepesi katika kuwahukumu watu wengine. Wana imani na baadhi ya watu wachache tu. Hawaonekani kuwa na mashaka na haki yao wenyewe. Wana majibu kwa kila jambo, na hawana heshima kwa yeyote anayeonekana kutofautiana au kutokukubaliana nao. Hawana mpango wala bidii yeyote ya kuwatafuta waliopotea, bali wana mipango na bidii ya kutetea maoni yao wenyewe. Wamejitosheleza wenyewe, na hawana mpango wa kubadilika.

Je, watu kama hawa kweli wanamjua Yesu na kutaka wamfanane naye?

Kuwa Mkristo inamaanisha ni kuwa mwanafunzi wa Yesu.

Je, inamaanisha nini kuwa mwanafunzi? Je, ni kumtii Kristo? Kwa hakika, angalao kwa kiwango kikubwa. Katika Agizo Kuu la Yesu mahali alipowaambia waende kila mahali wakawafanye mataifa kuwa wanafunzi, alisema, “na kuwafundisha kuyashika yote” (Mathayo 28:20).

Kutii maagizo ya Yesu hayo yote hayatoshi kumaanisha ndio kuwa mwanafunzi.

Wanafunzi wa rabi wa Kiyahudi walishiriki maisha yanayofanana na wao, siyo tu katika kujifunza mafundisho yao, bali pia na mitindo yao ya maisha. Walijifunza tabia zao na vipaumbele vyao.

Wakati Yesu alipowaita wanafunzi, akisema, “Njoo unifuate,”[1] hayo ndiyo aliyokuwa amemaanisha. Yesu bado hata wakati huu anawaita wanafunzi kupitia kwenye injili.

Je, inatokeaje mtu kuwa mwanafunzi?

[2]Kwanza, ni lazima uamini katika yeye—kama huwezi kuamini katika yeye, huna sababu ya kumfuata.

Unapaswa ubadili mwelekeo wako unakokwenda. Hakuna mtu yeyote anayeanza na kuwa mfuasi wa Yesu—tunaanza kwenda kwa njia zetu wenyewe. Unapaswa uamue kumfuata Yesu badala ya njia zako mwenyewe. Hiyo ina maana unaona kuna kitu kibaya kwa njia yako mwenyewe. Kumfuata Yesu kunaanza na toba – huwezi ukamfuata Yesu bila ya kuwa umejutia dhambi zako. Kama hujawa na majuto ya dhambi zako kwa kiwango cha kutosha kuachana nazo, bado utakuwa unaenda kwenye njia zako mwenyewe.

Unatakiwa ujionee mwenyewe msamaha wake na uanze uhusiano na yeye. Unaanza kwa kumjua zaidi na utake kufanana yeye.

► Soma Mathayo 16:21-25.

Katika mazungumzo haya na wanafunzi wake, Yesu alielezea kuhusu ujio wa kifo chake. Petro alishtushwa na maneno ya Yesu. Petro hakuona kama kuteseka na kufa ni sahihi kabisa kwa Yesu. Alianza kubishana na Yesu, akijaribu kumtia moyo kukataa wazo la kifo.

Yesu alimkemea Petro na kumwambia kwamba hakuwa anaelewa mambo ya Mungu. Yesu alimwambia kwamba mtu yeyote akitaka kuwa mwanafunzi wake, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, na amfuate. Hii ilimaanisha kukubali kifo kwa nafsi. Kukemewa huku kulikuwa kinyume na tabia za asili za mwanadamu za ubinafsi, kujitosheleza mwenyewe, na kujitetea mwenyewe—mambo ambayo huzuia ufuasi wa kweli.

► Je, kwa nini nafsi ya binadamu hukinzana na ufuasi?

Wanafunzi hawakuona mateso na kifo kama kilikuwa ni stahili yao. Walikuwa bado hawajaelewa kwa ukamilifu ilimaanisha nini kumfuata yeye. Haikugharimu chochote wewe kusamehewa, lakini itakugharimu kila kitu ili kumfuata Kristo. Kumfuata yeye kunasababisha moyo kuendelea kutafuta, kuwa mnyenyekevu, na mabadiliko.

► Fafanua kauli hii, “Itakugharimu kila kitu ili kumfuata Kristo.”

Kuuchukua msalaba ni kukubaliana na aina ya kifo kwa ajili ya maisha ya milele pamoja na Mungu. Ni kifo cha nafsi, kifo cha uhuru wako mwenyewe. Siyo tu kukubali kwa nje, lakini inakwenda moja kwa moja hadi kwenye moyo. Ni unyenyekevu ambao Yesu ameelezea kama hitaji la kuingia kwenye ufalme wake.

Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa mwanzo, walio wengi leo hawaelewi inamaanisha nini kuwa mwanafunzi. Makanisa yanatangaza neema kwa wale watu ambao hawajatubu. Hali hiyo haiwezi kuleta watu waokoke kwenye barabara iliyo sahihi au kuwaandaa kwa kile kinachokuja. Ni tofauti sana kulinganisha na hali halisi ya kuishi ya Kikristo kwamba siyo barabara inayofanana.

Dietrich Bonhoeffer alikuwa mchungaji wa Kijerumani ambaye aliuawa na Adolph Hitler. Aliandika mistari hii kwenye kitabu chake kiitwacho The Cost of Discipleship (Gharama ya ufuasi).

Neema yenye gharama ni hazina iliyofichika katika shamba; kwa ajili yake mwanadamu atakwenda na kuuza vyote alivyo navyo kwa furaha. Ni lulu ya thamani sana kununua ambayo mfanyabiashara atauza mali zake zote. Ni sheria ya upendo ya Kristo, ambayo kwa ajili yake mwanadamu ataling’oa jicho lake linalomsababisha kuyumba; ni wito wa Yesu Kristo ambao mwanafunzi huachana na nyavu zake na kumfuata yeye…imani ya aina hiyo ni ya gharama sana kwa sababu inatutaka tufuate.

Kumfuata yeye ni kufanana naye. Ni kufa kwa nafsi kwa sababu yeye mwenyewe aliisalimisha kabisa nafsi yake. Siyo tu jambo la kuacha kufanya mambo fulani mabaya, bali kuachana nayo kwa sababu Yesu pia angeacha. Tunajaribu kufanya yale ambayo Yesu angeweza kufanya katika usafi wake, huruma, wema na msamaha.

Hatufanyi tu kile ambacho ni sahihi wakati mioyo yetu inapingana nacho. Tunataka mioyo yetu ifanane na moyo wake. Hakuwahi kumchukia mtu yeyote. Wako baadhi ya watu waliochagua kuwa maadui zake, lakini yeye hakuwa adui wa mtu yeyote. Hata pale alipokuwa juu ya msalaba alisamehe.

Wafuasi wake wa kweli siyo watu wa chuki au wenye inda. Wanafanya yaliyo mema kwa wale wanaowatendea mabaya. Wanabariki badala ya kulaani. Hawana kiwango cha kusamehe kwao. Wameamua kuachana na haki zao za binafsi na badala yake kutumika.

Hakuna mahali pa kwenda ukiacha jambo hili la kujisalimisha binafsi. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza—naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

► Je, tunawezaje kuwaita watu waokoke katika njia ambayo itawaandaa kwa ajili ya ufuasi?


[1]Mathayo 4:19, Mathayo 9:9, Mathayo 16:24, Mathayo 19:21, Yohana 1:43
[2]

“Yesu Kristo anasisitiza kuondoa kutoka katikati ya dunia chochote cha aina ya sanamu ambacho hapo awali kilimiliki, na yeye mwenyewe kuchukua mamlaka. Haya ni mabadiliko makubwa ya utii ambayo husababisha kubadilika na au kuokoka, au angalao mwanzo wake. Kisha mara moja Kristo amechukua nafasi yake sahihi, kila kitu kinaanza kuhama.”

- Lausanne Committee
for World Evangelization,
The Willowbank Report